Ulitaka avae sare za chadema au Cuf, au yale magwanda ya kijeshi, Kaunda suti kwenye kikao Cha chama cha CCM,
Hizo ni code za mavazi na ilitakiwa wavae hivyo kama wao waliona kuna tija kukamilisha Jukumu lao la ulinzi .
Swala la ulinzi ni kubwa na ni Pana sana kwamba hapo alikuwa anamlinda Raisi ambae pia ni Mwenyekiti wa chama.
Ata mbowe,Seif, dovutwa, siku mmoja wapo akiwa Raisi siku akienda kwenye kikao cha chama basi walinzi nao watapaswa kuvaa kichama kama wataona kuna tija ya kufanya hivyo ili tu kumuweka salama mlindwaji na wao kutokutambulika kirahisi.
Ukitaka isiwe hivyo basi Vinginevyo Katiba itamke Rasmi kwamba Rais wa JMT hatakiwi kuwa kiongozi wa chama cha siasa abakie kuwa ni mwanachama tu na kiongozi wa Taifa.