Dereva aliyeuawa azikwa Dar
Na Muhibu Said
MAZISHI ya dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), anayedaiwa kuuawa kwa risasi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwano Ditopile Mzuzuri, jana yalitawaliwa na simanzi na vurugu zilizosababisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujeruhiwa usoni kwa jiwe.
Askari huyo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, alikumbwa na mkasa huo baada ya vijana wenye hasira waliokuwa katika barabara ya Kawe wakikusanya michango ya mazishi ya marehemu, kulishambulia kwa mawe na viatu gari la jeshi aina ya Range Rover alilokuwa amepanda askari huyo na mwenzake.
Vijana hao, wakiwamo madereva na makondakta wa daladala, walilishambulia gari hilo baada ya askari huyo na mwenzake, kutaka kumkamata dereva wa daladala aliyedaiwa kutaka kusababisha ajali katika barabara hiyo.
Tukio hilo lilitokea saa 7.30 mchana katika eneo la Kawe Mzimuni, karibu na nyumbani kwa marehemu na kusababisha tafrani iliyodumu kwa takriban dakika tano.
Baada ya kulituhumu kutaka kusababisha ajali hiyo, askari hao kwa kutumia gari lao, walilifukuza daladala hilo na walipofika katika eneo hilo, walilitangulia kwa mbele na kulizuia.
Kitendo hicho, kilionekana kuwachukiza vijana hao ambao waliamua kulizingira gari hilo na kulishambulia kwa ngumi, mawe na viatu.
Kutokana na kuelemewa na vurugu hiyo, dereva wa gari hilo la jeshi aliliondoa gari hilo kwa kasi katika eneo hilo na askari aliyejeruhiwa, alivua kofia yake na kuitumia kama kitambaa kufuta damu zilizokuwa zikichirizika usoni.
Mbali na tukio hilo, wakati mwili wa marehemu ukifanyiwa ibada katika Msikiti wa Shamsia, Kawe, vijana hao walifunga barabara na kuanza kukimbia mchakamchaka huku wakiimba nyimbo wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuikejeli serikiali.
Vijana hao ambao waligawanyika katika makundi mawili, moja likikusanya michango ya mazishi kutoka kwa madereva wa magari yaliyokuwa yakipita katika njia hiyo na lingine likiimba.
Hali hiyo iliwafanya askari polisi waliobeba silaha kufanya kazi ya ziada kuwadhibiti vijana hao wasilete vurugu katika mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Maringo.
Zaidi ya Sh300,000, zikiwamo Sh100,000 zilizotolewa na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, zilitangazwa kukusanywa katika mazishi hayo.
Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani saa 8.30 katika gari la polisi aina ya Land Rover Defender na kuagwa na ndugu, jamaa, marafiki na majirani kabla ya kupelekwa katika msikiti huo kwa ajili ya sala.
Mbali na Mrema, viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo, ni Naibu Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mtoro, Sheikh Khalifa Khamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva na Makondakta Mkoa wa Dar es Salaam (Uwamadar), Shukuru Mlawa na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow.
Kamanda Rwambow aliwataka ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa watulivu katika kipindi cha msiba na kuwaahidi kuwa polisi inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha haki inapatikana.
"Watu wasivuruge azma hiyo, mshitakiwa kishafikishwa mahakamani na amepelekwa gerezani. Kiutaratibu hatutakiwi kuzungumzia kitu kilichopo mahakamani, kitatuharibia kupata haki yetu, kwa mfano hayo mabango hayatusaidii kitu, naomba tuviamini vyombo vya serikali," alisema Rwambow.