Kichuguu,
Mkuu nakueleweni nyote isipokuwa nasimama upande wa pili kuona kama sisi tunao ushahidi tosha wa kumsimamisha Mkapa mahakamani. Chukulia tu kwamba mimi ni mwajiriwa upande wa utetezi kumwakilisha Mkapa ktk hoja za hapa lakini haina maana namuunga mkono ama siamini kwamba hakuhusika na hujuma za uchumi wa nchi yetu.
Mkuu nachokiona hapa kulingana na hoja zilizotangulia ni matokeo ya kile tulichokiona Mkapa kisha simamisha. Sawa na muuza unga aliyejenga nyumba lakini hata siku moja hajakamatwa na unga.. Hiyo nyumba sio ushahidi wa kuuza unga na hata kama tukifanya uchunguzi biashara yake ya kuuza nguo za India au Pakistan inaweza kuvunja tuhuma zote halali..Kinachotakiwa ni ushahidi zaidi, uchunguzi zaidi na pengine Kikwete anayafanya haya bila wananchi kufahamu.. unajua tena FBI..
Pamoja nayote haya, hakuna hata mmoja wetu anayefahamu mali za Mkapa zilipatikana kwa njia gani zaidi ya kusema haramu.. je alifanya nini kinyume cha sheria hadi tuite haramu....No one knows!
Pili, discussion yote hii ni ktk kutafuta njia za kumshitaki Mkapa kama rais mstaafu na sio Mkapa.. Huo ndio msisitizo wangu na ndio sababu sote tumetazama katiba kama inamlinda, laa sivyo sioni sababu ya kutazama katiba ikiwa yeye ni Mkapa na binadamu kama sisi...Ndani ya katiba kuna kipengele hicho kinachomhusu rais peke yake tofauti na sheria nyingine zinazowahusu watu wote...Mimi na wewe hatuwezi kuwa impeached isipokuwa kiongozi wa nchi na sio Mkapa..sheria ipo kwa WHO is he/she hilo jina imetokea tu kuwa jina lake linaitwa Mkapa.
Viongozi wa Kiafrika ni Miungu na sheria zilizowekwa zimeambatana na Azimio linalomruhusu wala sio yeye pekee yake.. Viongozi wote wa chama wamenufaika na madaraka tuliyowakabidhi. waziri wa Utalii walifungua ofisi za Utalii, Kilimo walinunua mashamba, Afya wakafungua mahospital, Elimu wkafungua mashule lakini wote wametumia ujanja ujanja kuweza kuficha madhambi yao na kisheria inakuwa kazi sana kuwabana wote kwa sababu kwanza hilo Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu Conflict of interest..na haikuwa dhambi kama ilivyokuwa Takrima ktk uchaguzi uliopita..
Sasa ikiwa leo hii tukiondoa takrima na kuiharamisha Je, tunaweza kutumia sheria hiyo mpya kuwahukumu viongozi waliopita ktk uchaguzi wa 2005..kisheria sidhani!
Ndio maana msisitizo wangu ni kujaribu kuwaonyesha nyote kwamba kuhusiana na Mkapa tumesha liwa wakuu zangu. hakuna mtu humu JF ambaye atafurahi sana kuona Mjomba katinga Kisutu ama mahakama yoyote zaidi yangu... nina usongo na mtu yule isipokuwa nikitazama possibility kisheria sioni ndani kabisa zaidi ya kuwepo Mageuzi/Mapinduzi ya utawala...
Kikatiba, he is above the law wajomba!