Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mrefu,
hata huyo Bush sio lazima Obama amshtaki ila wananchi kwa kupitia wajumbe wao wanaweza kutaka Bush asimamishwe mahakamani aidha kwa mauaji ama hasara aliyoipatia taifa lake...hatuwezi kusema haiwezekani isipokuwa hadi sasa hivi Bush anaonekana kuwa kiongozi aliyetumia maamuzi mabaya, hakuna hujuma yaani maamuzi ya makusudi kuliweka Taifa ktk hali iliyopo..Kuna wakati baadhi ya viongozi marekani walitamka uwezekano wa kumweka Bush kitimoto lakini navyofahamu swala zima la Uongozi wa Bush litakufa tu...
Na kama itatokea hivyo ni lazima kuna commmission itaundwa kutazama mabaya hayo na kama kweli alitumia makusudi kuua ama kuliweka Taifa ktk hali mbaya kisha mahakama maalum italishughulikia hilo... Tumemuona Saadam na wengine wengi tu wakifungul;iwa mashtaka.
Swala la Mkapa ni zito kuliko tunavyofikiria na pengine ndio maana viongozi wa CCM wanasema hapatakalika..Kila mmoja wao alihusika kwa njia moja ama nyingine kujitajirisha kutokana na RUKSA ya Azimio la Zanzibar ambalo lilitazama upande ktk swala la Conflict of Interest...
Hakuna binadamu hata mmoja anaweza kuwa kiongozi, kisheria karuhusiwa kufanya biashara lakini akaacha kutumia mwanya huo kujitajirisha..
 
Marais wawili wa Jamhuri ya Korea waliokuwa wamtumia mdaraka yao vibaya na kusababisha maafa walishitakiwa na kuhukumiwa mika kadhaa baada ya kustaafu.Ni mfano mzuri wa kuonesha utawala bora na kuiweka nchi katika utulivu.
 
Mzee, hapa huna ujanja!

2008-12-03 18:53:01
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili huenda rais mstaafu wa awamu ya tatu, Bwana Benjamini Mkapa, akajikuta akiwekwa pabaya kufuatia mazali anayodaiwa kuyafanya yeye mwenyewe ama baadhi ya watendaji wake wakati wa utalawala wake, kuanza kubumbuluka moja baada ya jingine.

Baadhi ya watu wamedai kuwa kwa mwamko walio nao Watanzania hivi sasa wa kutaka kila aliyeboronga, abebeshwe msalaba wake, Mzee Mkapa, hana ujanja kabisa.

Baadhi ya waliozungumzia suala hilo ni Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Mheshimiwa Philemon Ndesamburo, ambaye amesema rais huyo mstaafu, hana namna ya kukwepa tuhuma na hivyo ni lazima apandishwe kizimbani ili sheria itwae mkondo wake.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Mheshimiwa Ndesamburo amesema kwa nafasi yake ya urais, Mkapa alikuwa ndiye kinara wa vikao mbalimbali vya mawaziri wake.

Akasema kwa sababu hiyo, Mkapa alijua mambo mengi yaliyofanywa na wasaidizi wake na kamwe hawezi kukwepa tuhuma za kulisababishia hasara taifa kwa sababu aliviacha vifanyike au yeye mwenyewe alivifanya.

``Yeye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Cabinet (baraza la mawaziri)... na maamuzi mengi yalifanyika kwa maelekezo yake.

Kwa sababu hiyo, hana ujanja wa kukwepa tuhuma na hivyo anapaswa kuunganishwa kwenye kesi za watendaji wake na yeye vilevile akapandishwa kizimbani,`` akasema Mheshimiwa Ndesamburo.

``Yapo mambo mengi ya kifisadi yamefanyika wakati wa utawala wa Mkapa... sasa hana namna ya kukwepa. Na yeye anapaswa kusimamaishwa kizimbani kama ambavyo sasa imeanza kufanyika kwa wasaidizi wake,`` akaongeza Mheshimiwa Ndesamburo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema suala la Mkapa kutakiwa na yeye apelekwe kizimbani halina mjadala.

Akifafanua zaidi, Prof. Lipumba amesema enzi za utawala wa Mkapa, mambo mengi ya kifisadi yamefanyika na kwa sababu hiyo, anastahili kuburuzwa kizimbani ili akajibu tuhuma.

``Yapo mambo mengine yalifanywa na wasaidizi wake huku yeye akiyaacha kwa namna inayotia shaka kuwa kwa vyovyote vile, naye alinufaika kwa namna moja au nyingine,`` akasema.

Akaongeza kuwa masuala ya ufisadi wa kwenye EPA, ununuzi wa rada, migodi ya Meremeta Gold, Tangold na mengine mengi yamefanyika chini ya Mkapa.

Aidha, Prof. Lipumba akaongeza kuwa mamabo mengine yalifanywa na Mkapa mwenyewe na kwa sababu hiyo, sasa hana ujanja wa kukwepa tuhuma za kumfikisha kortini ambazo ziko nyingi mno.

``Yeye Mkapa hawezi kukwepa tuhuma za kuhusika katika uuzwaji holela wa majumba ya Serikali... yote hayo ni ufujaji wa mali za umma na yanatosha kumfanya astahili kusimamishwa kizimbani ili akajibu mashtaka,`` akasema.

SOURCE: Alasiri
 
Hili LiMkapa lipandishwe kizimbani tu. Hakuna cha kinga wala nini.
Kwani lenyewe ni linani hadi liwe na kinga..ala!! Kama halina makosa basi mahakama ya sheria itaamua. Kamata hili limtu na fungulia mashitaka.
 
Hiyo kinga wananchi wanaweza kuitoa kama Kikwete akiiing'ang'ania.
Ni rahisi sana kutoa kinga kwa wezi na wahujumu.wakati ukifika tutamtoa kinga na adhabu itatolewa kulingana na makosa yake, ni aheri atolewe kinga na wezi wenzeke kuliko atolewe kinga na masikini wenye njaa na uchungu.
 
Very poor and one sided journalism.. kwanini amehoji viongozi wa upinzani tuu japokuwa the point is valid lakini it shows gross bias. Japokuwa tutafurahi Mkapa akiwa stripped of the fake iimmunity that he really doesnt have (for acts committed by him in office but unrelated to the Presidential office) na kufunguliwa criminal charges for all the wrong he did.. Tanzania itakuwa a much better Tanzania siku za kesho... Lakini this article is cheap..
 
Naombeni wana JF wanaojua mali za hao wakulu watutajie ili tuone ni kwa jinsi gani wamejilimbikizia mali.
 
Nijuavyo ni kuwa mali za Mama zinauzwa kwa speed ya mwanga. Moja ya makampuni ya majumba Knightfranks inahusika na zoezi hilo. Sasa sijui hizo fedha zitapelekwa katika shughuli za kijamii ama account za Geneva.....

Tanzanianjema
 
Nilipoweka thread hii nilidhani kuwa wana JF watakuwa habari kuhusu mali hizi. Lakini kwa mshangao wangu KIMYAAAAAAAAAAAAA. so, we don't dare to talk openly.
 
Congo kama watu hawana data unataka waropoke Hovyo...?....otherwise fanya utafiti wako..then leta data...hapo..utapata wachangiaji...ukitaka kulazimisha mada zako zijadiliwe utatutia mtihani....!!!
 
Jinsi kila kitu kinavyosambaratika na kuangamia, uharamia, uzembe, ukosefu uadilifu, kukosa uungwana na utu, hujuma, wizi, ufisadi na dhuluma zikiongezeka, vifole vyote vinabidi vimnyokee mtu mmoja, Benjamin William Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndiyo, Mchungaji kanena msilishangae. Ndiyo, Mchungaji kanena pamoja na kumshikia bango Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuwa mgumu kufanya maamuzi mazito kuisafisha nchi yetu, lakini badala ya kuendelea kumwagia Kikwete lawama, Mchungaji anasema, turudi kwa yule aliyekuwa madarakani kabla ya Kikwete.

Wengine wenu mtadai turudi nyuma kwa Mzeee Mwinyi hata kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mimi nasema hapana, tunaanzia na Mkapa wala si kulitafakari Azimio la Zanzibar bali ni utendaji kazi wa Serikali ya Mkapa na uongozi wake Serikalini, Chama cha Mapinduzi na Taifa zima.

Nilipoandika mada kuhusu Andrew, Omari, Cornell na Robert, niliwataja wakuu wa mambo ya sheria na dola, usalama wa Taifa na nchi, katiba na haki na kuwatuhumu kuwa wao katika nyadhifa zao na wakati wa uongozi wao, Tanzania iligeuka kuwa dangulo na handaki la kila aina ya uharamia kuliibia Taifa wazi wazi bila woga wala aibu.

Kikwete katuambia, tumuache "Mzee Mkapa" astaafu kwa amani, mimi nasema hapana, hatuwezi kuendelea mbele bila Mkapa kufikishwa kizimbani na kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kulilinda Taifa kutoka maadui na uhalifu na mbaya zaidi kuliingizia Taifa hasara.

Simtuhumu Mkapa kwa wizi, bali nalisema wazi kuwa ndani ya utawala wa Mkapa wa miaka 10, makovu na majeraha tunayoyaona leo hii ya uhujumu na ufisadi, yalianzia nyakati hizo, michubuko na mikwaruzo ilifanyika nyakati hizo na tulichobakishiwa ni uozo ambao unatambaa kama algae na fungi.

  • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
  • Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
  • Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
  • Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato.
  • Sheria na Katiba: kuendelea kuwepo kwa sheria na mambo mabovu katika sheria na katiba ambayo yameondoa kabisa mihimili ya Bunge na Mahakama kuwa na nguvu za kikatiba na mamlaka kuihakiki Serikali kuu.
  • Uchumi wa nchi, kudorora kwa uchumi kwa hali halisi ya uzalishaji mali, kudumaa kwa kilimo na kukimbilia utegemezi wa kuagiza chakula, kupungua uzalishaji mali kutokana na kosekana kwa umeme, maji, barabara nzuri.
  • Elimu na Afya: kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania kwa kuruhusu matakwa binafsi ya watu wachache waamue kubadili mfumo wa Elimu bila kupata ushauri wa wataalamu wa Elimu. Afya kuendelea kudorora huku kukiwa na uhaba mkubwawa vifaa, madawa na wataalamu wa afya.
  • Uongozi mbovu; kukosekana kabisa kwa uwajibikaji ndani ya serikali ambako kumezaa tabaka la viongozi wa Serikali na Mashirika ambao wanajiona ni Miungu wasio na makosa (Mattaka, Chenge n.k). Kukosekana na Sauti ya kuheshimiwa kuliongoza Taifa.
Pamoja na yale machache tuliyoyashuhudia ambayo tunayaona kuwa ni chanya, kama kufutiwa madeni yetu na harakati za kuendeleza Mkukuta na Mkurubita, lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa kama kweli Mkapa aliacha misingi imara, basi pamoja na Kikwete kujenga baraka la mawaziri kubwa na la kifahari, uchumi na pato la Taifa lisingeporomoka jinsi lilivyoporomoka kwa haraka.

Ni wajibu wetu wote kama taifa kuwajibika na kuchapa kazi ili kulikwamua Taifa kiuchumi ili kuwepo na elimu na afya bora, ajira na tumaini la kuwa Taifa linalojitegema, lakini kinara, kiranja mkuu ambaye alitutukana kuwa tuna wivu wa kike na ni wavivu, matusi na lawama za Taifa kushindwa kusonga mbele zinarudi kwake na si mtu mwingine.

Ni haki yetu kama Wananchi, kutaka Mkapa awajibishwe kwa kuvurunda kazi. Hata pamoja na kuwa hawezi kupigiwa kura tena, lakini anapaswa afikishwe mahakamani kwa uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Suala la Kinga ni la kitoto na linaendelea kulea uozo, ujuvi na ubabe wa kutishana na kulindana.

Atakapofikishwa Mkapa mahakamani, hata kina Rostam, Lowassa, Chenge na wengine watabaini kuwa Watanzania, hatutaki mchezo. Kila mwenye ndoto ya Ufisadi, Uzembe, utumiaji vibaya madaraka, uvivu na kukosa kuwajibika ama itabidi atafute nchi nyingine ahamie au anyooke na kuanza kuishi kama Mtanzania Mzalendo.

Kura zile za Tsunami hazikuwa za kutuletea Ze Comedy! Bwana Kikwete nakuomba fanya kazi yako, ondoa magugu, visiki na viwavi jeshi walio ndani ya Serikali na Chama chako.

Jaruzelski, pamoja na yote aliyofanya kwa madai ya kutumia madaraka au kwa mujibu wa sheria, leo hii yuko mahakamani kujibu mashitaka. Kila kona dunia hii, kiongozi aliyebainika alifanya kosa anavuliwa kinga na kufikishwa mahakamani, kama rafiki yetu Chiluba alivyofanyiwa.

Hivyo basi, tupaze sauti zetu kwa nguvu tukimtaka Kikwete amfunge paka kengele.

Rais Kikwete, nakuomba usicheze nalenale, ushamfikisha Mramba, Yona na Mgonja, tunamtaka Lowassa, Rostam na zaidi ya yote, tunamtaka Mkapa.

La sivyo, unatupa kazi moja, nikinukuu maneno ya mmoja wa viongozi wa chama cha wafanya kazi Ugiriki walipofanya fujo kutokana na Polisi kuua mtoto mdogo "It is very simple, we want the government to fall". Sentenzo hiyo ilitolewa kwa ghadhabu kwa Serikali kushindwa kufanya kazi yake ipaswavyo.

Ukishindwa kufanya kweli, basi nasi kwetu itakua "it is very simple, we want the government to fall" na kweli kwa kiapo cha kilio cha machungu Serikali yako itashindwa na kuanguka yenyewe. Usitufikishe hapo kwenye mchanga tukakuchukia na kugotesha meli yetu na kutoa kauli hiyo ya kutakia maangamizo ya Serikali yako.

Ili tuendelee mbele, fungua kesi, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Benjamin William Mkapa.
 
Tuko pamoja mkuu Kishoka, mimi naamini Mkapa ndiye aliyeweka misingi ya Ufisadi katika nchi yetu founder of grand corruption in this country) na pamoja na hayo uliyosema, mengineyo ni:-

1. Kujimilikisha mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira
2. Kufanya biashara akiwa Ikulu na kuondoa utakatifu wa Ikulu
3. Kushindwa kuteleza makubalianao ya mwafaka wa Zanziba waliyotia saini wao wenyewe.

Naamini kuwa isku ambapo kinga yake itaondolewa na kufikishwa mahakamani tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana na tutarejea kwenye miiko ya uongozi kwa vitendo pia itapunguza mbio za wanasiasa uchwala ambao siku zote wanaiota Ikulu.
 
Niliwahi kuzungumza siku nyingi sana hapa kijiweni kuwa Mkapa ndiye aliyeharibu nchi yetu. Aliuza raslimali zetu zote kwa faida yake pamoja na jamaa na marafiki zake tu. Akajenga msingi wa aina maalum ya ufisadi kuzidi ule uliozoeleka wa Nigeria. Wafanyabiashara za halali waliofanya biashara zao kwa siku nyingi sana wakaachwa nyuma sana na wafanyabiashara walitoka kwenye siasa au walioingia kwenye siasa au waliokuwa na connection na wanasiasa.

Adhabu ya mtu aliyeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana akayatumia vibaya kwa kujinufaisha binafsi inatakiwa iwe ni kubwa sana, sawa na ile ya kuua kwa kukusudia!!!
 
Ni haki yetu kama Wananchi, kutaka Mkapa awajibishwe kwa kuvurunda kazi. Hata pamoja na kuwa hawezi kupigiwa kura tena, lakini anapaswa afikishwe mahakamani kwa uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Mkuu Rev,

- Heshima mbele, hapa tupo ukurasa mmoja mkuu. Ukweli ni kwamba kama kweli sheria ikichukua mkondo wake na haki kwa wananchi kutendeka, basi huwezi kuwapata Yona na Mramba wakiwa na hatia against sisi wananchi bila ya kumjumuisha Mkapa, au Sumaye, hilo liko wazi na ninaamini kwamba hata wanaohusika wako macho hapo na wanajua,

- In private sasa hivi Mkapa anasema kuwa kuna ya kwake, lakini mengi sio ya kwake, sasa aburuzwe Keko mara moja kupitia pale Kisutu, ili atuambie taifa yapi ya kwake na yapi sio yake, halafu hizi kesi za mafisadi kama zilivyoanza zifanyike hivi hivi kwa uwazi tusikie yote, maana najua utafika wakati watazihamisha na zitafanyika kawa siri.
 
Mkapa should be the most wanted,issue zote zinazomshuhulisha bwana kikwete chazo chake ni Mkapa.tatizo kikwete amekuwa mgumu kutoa maamuzi.
 
- Muungwana anatakiwa kubanwa na ukweli, baada ya kuongea sana na mapilato in private, ukweli ni kwamba akibanwa na ukweli huwa hana ubishi kuamua sasa dawa ni pressure tu kutoka kwa sisi wananchi na wanaohusika kisheria, akipewa ukweli huwa hana shida ku-act!

- Maana ahata hawa wanaotinga sasa Kisutu, nasikia siku alipoonyeshwa ukweli wa ushahidi kisheria, alitaka wakamatwe wote mara moja lakini kwa kuogopa uwezo wetu mdogo wa kuweza kuwashughulikia kwa wakati mmoja mafisadi wote, ndio akashauriwa kuwaambia warudishe pesa kwanza wenyewe.
 
Haya makosa yote yalifanywa wakati wa Mkapa....yeye pamoja na watu wake wa karibu 'inner circle' wawajibike, watanzania wanateseka kutokana na uzembe na wizi wa watu wachache.
 
Kikwete anaweza kuwa ni mdhaifu kufany amaamuzi na kuchukua hatua, lakini tunayoyaona yanalipuka sasa hivi, chanzo chake si awamu ya nne, bali ni awamu ya Tatu.

Pamoja na kuwa Azimio la Zanzibar lilifungulia "mbwa", lakini kujiamini kwa viongozi kujifanyia mambo holela hakukutokea mpaka Mkapa alipoingia madarakani.

Mfano, kwa nini alikubali mkataba wa IPTL usainiwe kisa kushinikizwa na Rais wa Malaysia? Kwa nini hakusimama kidete na kufuata ushauri wa Antony Rutabanzibwa na kuliambia baraza lake la mawaziri na huyo Rais wa Malaysia kuwa Tanzania na Tanesco hazitapata manufaa yeyote kwa huo mkataba?

Ilikuwaje mwaka 1997 alimkubalia Jenerali Robert Mboma mkuu wa majeshi kuiingiza JWTZ katika biashara ya kuchimba madini kwa kuidhinisha kuanzishwa kwa Meremeta?

Uchaguzi mkuu wa Zanzibar 2000 na mauaji Pemba, kwa nini hakumwajibisha mahita kutokana na vifo vilivyotokea na hata kuishia kuwafanya Wapemba wakimbie nchi yao na kwenda Kenya?

Mauaji ya Mwembechai, ikiwa raia walikuwa na mgomo na kulalamika mambo wanayohisi kuwa ni dhuluma au unyanyasaji, kwa nini alituma Jeshi na si kuwaita viongozi wa watu hawa wakae chini na kuongea kiungwana?

Kwa niliyoyasikia, Mkapa alikuwa na kiburi na ujeuri wa kujifanyia alilotaka bila hata kushirikisha Baraza la Mawaziri au Kamati Kuu ya CCM.

Mbaya zaidi ni ile habari inayosemekana alitamka waziwazi kuwa alikuwa akimhusudu sana Daniel Arap Moi na jinsi alivyojijenga na familia yake kwa kufanya biashara Ikulu.

Mkapa pia anasifika kuwa na chuki mbaya. Alitoa kiapo kuwa hawezi kumachia "mwarabu" Salim awe Rais wa Tanzania kutokana na ugomvi wao wa miaka mingi ambao ulitokea wakati Salim akiwa Naibu Waziri Mkuu.

Ama alitoa kiapo na kukasirika kwa nini Malecela na Mwandosya waliamua kugombea urais 2005 bila kupata kibali chake.

Kinakera zaidi kusikia alivyotumia Ikulu kujinufisha. ANBEN, Kiwira, ardhi, nyumba, Benki M na vitu vingine vingi ambavyo vilifanywa kwa faida yake na familia yake, kwa kutumia wadhifa wake kujinufaisha na kujipendelea.

Kinachosikitisha zaidi, ni kule kushindwa kwake kutumia madaraka kuzima ufidhuli uliokuwa unatokea ndani ya Serikali yake kwa kutumia dola. Ikiwa Chenge, Mahita, Apson na Mboma walitumia mirija kuinyonya Taifa na kutuweka mateka, Rais wetu alikuwa wapi?

Kiapo chake Desemba 1995 na Desemba 2000 vilikuwa na maana gani kama alishindwa kulitumika Taifa kwa dhati na kuishia kutumikia matakwa ya watu wachache kwa manufaa yao na si kwa manufaa ya Taifa?
 
Tumechoka na maneno yenu. Mambo mangapi mazuri Mkapa ameifanyia Tanzania? Ila kwa vile mmeumbwa kuona mabaya tu hamtaki kuyakumbuka mazuri. Waulizeni awamu ya nne ile jeuri ya kuunda baraza la utitiri wa mawaziri waliipata wapi?

Halafu kwa nini mumuone Mkapa tu? Mbona hamzungumzii ufisadi alioufanya Mwinyi na mama siti awamu ya pili? Mbona hampigi kelele na wao wafikishwe kwenye mkono wa sheria?
Au bado mna wivu wa kike kwavile aliwaambia ni wavivu wa kufikiri?
 
Back
Top Bottom