Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.

See the bold? Mkapa kuna deals alizifanya kama Benjamin William Mkapa, hizi ndizo hazina kinga.
 
Apart from all contradiction, hakuna sub-section inayo ipa bunge uwezo wa kuondoa hiyo kinga either kwa rais aliyepo madarakani au aliye staafu?
 
Apart from all contradiction, hakuna sub-section inayo ipa bunge uwezo wa kuondoa hiyo kinga either kwa rais aliyepo madarakani au aliye staafu?

August,

Hapo juu kifungu kimeacha mwanya kumshitaki rais mstaafu aliyefanya makosa yaliyo nje ya capacity yake ya urais (kama kufungua kampuni dubious under the capacity of citizen Mkapa, not president Mkapa, which is exactly what Mkapa did)
 
Apart from all contradiction, hakuna sub-section inayo ipa bunge uwezo wa kuondoa hiyo kinga either kwa rais aliyepo madarakani au aliye staafu?

Bunge likimtoa madarakani kwa mashitaka Bungeni, Rais atakuwa hana kinga ya mashitaka mahakamani.

Katiba ya Jamhuri

46.(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki...

46A(10) yasema:

Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
 
August,

Hapo juu kifungu kimeacha mwanya kumshitaki rais mstaafu aliyefanya makosa yaliyo nje ya capacity yake ya urais (kama kufungua kampuni dubious under the capacity of citizen Mkapa, not president Mkapa, which is exactly what Mkapa did)

Nimekiona hicho kitundu, lakini wenzetu DPP na wenzake wanajifanya hawalioni hicho kifungu, hivyo wanataka tundu kubwa , ndio maana nikawa naangalia uwezekano wakuwaongezea hilo tundu la kumshtaki mstaafu wetu Che Nkapa
 
Bunge likimtoa madarakani kwa mashitaka Bungeni, Rais atakuwa hana kinga ya mashitaka mahakamani.

Katiba ya Jamhuri

46.(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki...

46A(10) yasema:

Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
Kuhani,
Je, katiba inasemaje kuhusu former President? Zambia walitumia utaratibu gani kumfikisha Chiluba hatiani?
 
Nimekiona hicho kitundu, lakini wenzetu DPP na wenzake wanajifanya hawalioni hicho kifungu, hivyo wanataka tundu kubwa , ndio maana nikawa naangalia uwezekano wakuwaongezea hilo tundu la kumshtaki mstaafu wetu Che Nkapa
Kama DPP na ofisi ya AG wameshindwa kumhusisha Yona na kashifa ya Kiwira unategemea akatafsiri hicho kifungu dhidi ya BWM? It'll be like walking while dream
 
Je, katiba inasemaje kuhusu former President?

Jasusi,

Rais mstaafu hawezi kushtakiwa kwa "jambo lolote alilofanya yeye kama Rais," isipokuwa kama aliondolewa kwenye Urais na Bunge (impeachment). Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 46 (3) na 46A (10) ya Katiba kama ilivyowekwa hapo juu.

Kumbuka, lakini, kujimilikisha migodi pamoja na Waziri wa Madini kwa idhini ya Waziri wa Madini au kufungua biashara kwa anwani ya Ikulu ni ufisadi ambao hauna kinga kwa sababu hakutenda mambo hayo kama Rais. Hii ilikuwa ni miradi-fisadi binafsi ya Ben Mkapa, mkewe Anna, Daniel Yona na watoto.

Zambia walitumia utaratibu gani kumfikisha Chiluba hatiani?

Tofauti na yetu, Katiba ya Zambia inalipa Bunge nguvu ya kuondoa kinga ya Rais Mstaafu. Hivyo waliondoa kinga dhidi ya Chiluba ambae, kama Ben Mkapa, alikuwa na shutuma nzito za ufisadi baada ya kustaafu.

Zambia Constitution, 1991, Article 43 (3)
Protection of President in Respect of Legal Proceedings

No person who has held, but no longer holds, the office of President shall be charged with a criminal offence or be amenable to the criminal jurisdiction of any court in respect of any act done or omitted to be done by him in his personal capacity while he held office of President, unless the National Assembly has, by resolution, determined that such proceedings would not be contrary to the interests of the State.
 
Kikatiba hakuna sheria ya kumshtaki Mkapa zaidi ya mtu mmoja katili na Dikteta ambaye kaamua kufanya yale yasiyowezekana ikiwa ni pamoja na kuibadikisha Katiba kwa nguvu ya dola yake!..
Ndio maana nikasema badala ya kumtazama Mkapa nadhani kisheria kwa Mkewe inawezekana na kama huyu ataingizwa mahakamani basi Mkapa ndio kesha..Kimaisha ni pigo kubwa kuliko yeye mwenyewe!
 
Mkandara:

Pindua nchi, baadaye wapige makonzi viongozi wote waliboronga. Afu rudisha tena nchi kwenye utawala wa kiraia.
 
Nilikuwa nasoma Katiba tena, sikuona kipengele chochote cha katiba kinachosema Mkapa hawezi kushitakiwa katakata. Katiba inasema kuwa hawezi kushitakiwa kwa makosa yatokanayo na utekelezaji wa majukumu yake kwa niaba ya Jamhuri, lakini kinga hiyo haisemi kuwa asishitakiwe kwa kutumia madaraka yake kwa manufaa yake binafsi yasiyo ya Jamhuri. Bado anaweza kushitakiwa kama mmoja wa wakurugenzi wa ANBEN kwa kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.
 
Kuhani,
Ni kweli katiba inasema nini cha kufanya ili kumshtaki mtu akitimiza majukumu ya Urais. Je kama alifanya madudu kama mtu binafsi ndo inakuwaje?

Tatizo tulilonalo ni kuwa mambo mengi ya Mkapa aliyafanya kama Mkapa na si Rais Mkapa. Kwa mfano, kama dili la Kiwira lingekuwa limefanywa na Rais Mkapa, tusingekuwa tunalalamika sana kwani Kiwira ingekuwa bado chini ya serikali. Lakini alitumia madaraka yake (na Yona) kujiuzia machimbo haya na hili, binafsi naona kuwa pamoja na kutumia vibaya madaraka na conflict of interest, ni jambo la kufedhehesha Urais.
 
Kichuguu,
Tazama Azimio la Zanzibar... maslahi binafsi kwa viongozi ni ruksa..
 
Jamani si jk katika hili alishajibu kwamba hawezi kumshitaki kwa sababu nchi haitakalika? au mimi ndiye nimesahau nini?
 
Kichuguu,
Tazama Azimio la Zanzibar... maslahi binafsi kwa viongozi ni ruksa..
Azimio lile linahalalisha kiongozi kufanya biashara, lakini halihalalishi kiongozi kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; kupata mali kwa njia ya udanganyifu ni kosa la jinai.
 
Kichuguu,
Azimio lile linahalalisha kiongozi kufanya biashara, lakini halihalalishi kiongozi kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; kupata mali kwa njia ya udanganyifu ni kosa la jinai.
Nakubaliana na wewe isipokuwa unaweza kutupa ushahidi wa huo udanganyifu uliotumika!.. maanake hapa ndipo tunapokwama kisheria. Inawezekana kabisa kuwa Mkapa aliweza kujilimbikiza mali (udanganyifu) kwa kutumia kiti cha Ikulu, hili ni kosa nje ya kanuni za uongozi na sidhani kama sheria inamkinga...hakuna sheria inayoweka kinga dhidi ya Utawala bora - Kitu muhimu ni kuweza ku prove that na ipingane na Azimio la Zanzibar...
 
Ndiyo maana tunataka achunguzwe kwa mujibu wa sheria, asikingweakingwe na kivuli cha katiba; tunataka tujue ukweli kuhusu alivyojipatia mradi ule na contract ya kulipwa na TANESCO kwa miaka 20.
 
Ndiyo maana tunataka achunguzwe kwa mujibu wa sheria, asikingweakingwe na kivuli cha katiba; tunataka tujue ukweli kuhusu alivyojipatia mradi ule na contract ya kulipwa na TANESCO kwa miaka 20.

- Ndio maana tunaamini kwamba Kikwete kwa kuwafikisha kwenye sheria mawaziiri wawili wa zamani wa Mkapa, amejiletea mtihani mzito sana, kwa sababu hataweza ku-draw the line tena sasa wananchi tutataka sheria iende mpaka mwisho, na hapo ndio tutajua kama ni kweli au kampeni za 2010, lakini naamini amedhamiria kufanya kweli na Mkapa atafikiwa tu soon, hilo halina ubishi just the matter of time!
 
Kichuguu,
Mkuu tatizo la sheria sio swala la sisi kujua alivyoupata mradi wa Tanesco ama mingineyo isipokuwa inatutaka sisi kutoa ushahidi against yeye tukisha fanya uchunguzi wa njia zilizotumika..Mkapa hana haja ya kuzitoa hizo njia unless sisi tuwe na ushahidi kwanza kuthibitisha kwamba alikiuka sheria..
Sasa kama kuna mmoja wetu anazo hizo njia haramu zilizotumika nadhani itakuwa mwanzo mzuri..
Kama ningekuwa mimi na sii mwana CCM ningesema weka ndani itajulikana baadaye! lakini Kikwete sio Dikteta anatafuta haki na kuna hatari kubwa kama hatachukua hatua za Kisheria kuna watu nyuma ya huyu jamaa na wenzake wanaweza kuzua balaa ya kwa kutumia Udini, sasa hivi tu kuna watu wanaamini swala la Yona na Mramba limesababishwa na Kisasi..
tatizo wote tunajua Yona na Mramba walitumia vibaya madaraka yao na kujilimbikiza mali lakini hatuna ushahidi tosha zaidi ya kutumia hoja ya walitumia vibaya madaraka yao!..
 
Mwizi ni mwizi tu..Anaweza akatumia madaraka ama silaha ama udanganyifu...Njia ni nyingi tu...Nilipokuja bongo mara ya mwisho nilikuwa nasikia ni "Wizi wa kalamu"
Sheria ni msumeno...Sasa kama hao wanaodai hawaoni ni kivipi watakutwa na makosa...Then hizo mali za wananchi walizopora zifuatiliwe halafu tuone kama hakuna atakeyesema ni zake.
Kwani hakuna asiyeweza ku "Trace?" Kwamba ile miradi ambayo ilimilikiwa na serikali sasa iko mikononi mwa watu flani flani wakiwemo viongozi?
Kwamba ubinafsishaji ulikuwa technically ujambazi?
Binafsi siamini kama watanzania watakubaliana na changa la macho kama lipo kwasababu ufisadi si hadithi za kufikirika bali ni reality...Wananchi wanaiona na vijimaneno haviwezi kuubadili ukweli halisi ambao mwananchi wa kawaida anauona kwenye maisha yake ya kila siku...Kuanzia mkulima,mfanyakazi na wanafunzi...Jamii kwa ujumla imeguswa na ujambazi huu ambao eti unasemekeana hauna lugha ya kuwafanya watiwe hatiani.
 
Back
Top Bottom