Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Ukisikiliza hotuba ya Mwl, iliyopo kwanye nukt77.blogspot, hatuwezi kukosa sababu za kumshtaki Mkapa, kwanza nia ya kumshtaki tunayo, sababu za kumshtaki tunazo, tunachokosa ni utashi .
Mojawapo wa mambo aliyo ongea Mwl, ni kwamba tunataka kiongozi, atakaue aapa lkulinda na kuitetea katiba, na si kufuata ushauri ......, ili akikosea tuweze kumshtaki.
 
Kwa mealezo zaidi soma na changanueni sehemu hii ya katiba ya Jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 ibara ya 43 hadi 46B juu ya rais. Sioni mwanga sana kwamba ana kinga hapo labda wanasheria au wanakatiba wafafanue zaidi


Masharti ya kazi
ya Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9

43.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na
atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au
posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo
hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho,
vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais
havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Madaraka ya
kutangaza vita
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib.14


44.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
lililotolewa na Rais.

Uwezo wa
kutoa msamaha
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9


45.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na
hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza
kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa
masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu
yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa
lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au
asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote
kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

36
aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au
kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza,
au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia
ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka
yake kwa mujibu wa ibara hii.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa
na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa
Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo
yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania
Bara kwa mujibu wa sheria.

Kinga dhidi ya
mashataka ya
na madai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.20 ib…


46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
37
Bunge laweza
kumshtaki Rais
Sheria ya 1992
Na.20 ib.8
Sheria ya 1995
Na.12 ib.4


46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-
Sheria ya …. (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
38
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
39
Wajibu wa
viongozi wakuu
wa vyombo vya
mamlaka ya
utendaji
kudumisha
Muungano
Sheria ya 1995
Na.12 ib.5


46B.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika
ibara ya 28 ya Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vyenye
mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano vilivyotajwa
katika, ibara ya 4 ya Katiba hii, watawajibika, kila mmoja wao
katika kutekeleza madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii
au Katiba ya Zanzibar, 1984, kuhakikisha kuwa analinda
kuimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila
mmojwawapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlaka
ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano kabla ya kushika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea na
kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hii:-
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar, na
(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
 
Someni between lines sasa acheni ubishi. Sehemu yeyote ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania semeni nitawapatieni mchambue na sii kuongea kama kijiweni. We are elites atiii!!!
 
Kama nimeelewa vizuri sehemu hiyo ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 kuhusiana na rais, naona aliye na kinga tena kiduchu ni rais aliye madarakani na bado sioni ikiwa aliye madarakani ana kinga isiyo mia kwa mia then how about the mstaafu. Should I betray myself kuwa hana kinga? Kwa kuwa hamna pahala panaposema BOLD kuwa na kinga! Narudia na kurudia sipaoni kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania panapotetea uozo namna hiyo. Remember katiba hii ni biblia takatifu ya nchi na serikali yetu na kamwe isingeweza kutoa mwanya huo. Niseme tu sijaona kinga dhidi ya rais mstaafu eg. mkapa katika katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 na kwa kuwa katiba ni sheria mama na nyingine zote zatokana na misingi ya katiba sidhani ipo yeyote derived from katiba ambayo itapingana na katiba otherwise .......convinced otherwise I do not see the immunity
 
TANZANIA: Zanzibar Election Massacres Documented

Human Rights Watch: April 9, 2002

Tanzanian security forces committed gross abuses, killing at least thirty-five people and wounding more than 600 others, when they ruthlessly suppressed opposition demonstrations in Zanzibar more than one year ago, Human Rights Watch charged in a new report released today. Human Rights Watch said that none of those responsible for the abuses at the end of January 2001, including shootings of demonstrators, beatings and sexual abuse, had yet been held to account."Not until a year after these shocking events did the Tanzanian government appoint a commission of inquiry,” said Peter Takirambudde, executive director of the Africa division at Human Rights Watch. “We welcome that decision, but urge the commission to move quickly to gather the evidence necessary to bring those responsible to justice. We hope that our report will help them get to the truth.”

The report, “'The Bullets Were Raining’ – The January 2001 Attack on Peaceful Demonstrators in Zanzibar,” details massacres that took place at four main locations – in Zanzibar Town, and at Wete, Micheweni, and Chake Chake on Pemba Island. Human Rights Watch concludes that upper-level government and security officials planned the crackdown in advance.

Human Rights Watch
said the Tanzanian army and police opened fire without due cause on January 27, 2001, attacking thousands of supporters of the opposition Civic United Front (CUF) who were protesting against alleged fraud in national elections held three months earlier. In the following days, the security forces, aided by ruling party officials and militias, went on a house-to-house rampage, indiscriminately arresting, beating, and sexually abusing island residents. Some two thousand Zanzibaris fled to nearby Kenya, though most have now returned following an agreement between the government and the CUF.

“These events were among the worst in a long history of differences between the mainland government and political opposition in the semi-autonomous Zanzibar islands,” said Takirambudde. “The Tanzanian security forces were willing to shoot, beat, torture, and commit sexual abuse to silence the political opposition.”

No one was reprimanded for a role in the killings, torture, or destruction of property. Instead, Tanzanian President Benjamin Mkapa publicly congratulated the security forces for restoring order on the islands, and several security forces officers were subsequently promoted. The government-appointed commission of inquiry was set up in January 2002 following an agreement last October between Tanzania’s ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party and the CUF, and is due to announce its findings by July. The October agreement also commits the government to introduce various constitutional reforms.

"THE BULLETS WERE RAINING"
Shooting Worshippers at Mwembe Tanga Mosque on January 26, 2001

Following Friday prayers at the Mwembe Tanga Mosque in Zanzibar Town on January 26, worshippers did gather outside the mosque in conversation, as was their custom following a service on their holy day. In responding, police who were on duty at the time told Human Rights Watch that a group of police officers were dispatched from Madema police station armed with rifles (contrary to routine practice) directly to Mwembe Tanga.27 Some twenty police arrived at the mosque and ordered those gathered there to freeze. They then shot dead the mosque's imam, Juma Mohamed Khamis, as he was in the process of unlocking his moped to leave. The police shot him directly in the face, killing him instantly. Two worshippers were shot by the police: Hamad Said was killed with a shot to the stomach, and Seif Juma was injured by two bullets in the leg and ankle as he attempted to flee.28A witness who was present at the mosque testified (to Human Rights Watch interviewer) that the shootings were unprovoked …….

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

MKAPA IS ACCOUNTABLE FOR:
1. The killing of the Imam of Mwembe Tanga Mosque on 26 January 2001 in Zanzibar (see HRW report).

2. The massacres of 35 CUF demonstrators on 27 January 2001 - again in Zanzibar (see HRW report).

3. The exodus of over 2,000 Zanzibaris from Pemba and their settlement in REFUGEE CAMPS IN MOMBASA, KENYA. This was the first time in Tanzania’s history to produce Refugees to any country!!

4. The killing of four Worshippers at Mwembechai Mosque on Friday 13 February 1998 and the stripping naked of the Muslim women “arrested” after the Friday Prayers at the same Mosque.

5. The incarceration of Chuki Athumani, a 17-year old student who was wounded by a police gunshot at Mwembechai but who for several weeks could not be treated at the Muhimbili Hospital because the police had permanently enchained his legs and hands at the posts of his hospital bed, and that the young boy has since paralysed. This was the highest degree of cruelty!

6. The banning of the book, “Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania” by Dr. Hamza Mustafa Njozi simply because most of the incriminations therein either touched him or the (Roman) Catholic Church.

7. IT IS DURING MKAPA’S 10-YEAR RULE WHICH CREATED MOST OF THE “MAFISADI” AND, ALTHOUGH HE WAS GIVEN THE WARIOBA REPORT, HE DID NOT TAKE ANYBODY TO COURT. IT IS JK WHO IS NOW CLEARING HIS MESS. WORST OF ALL, 'BEN-JAMIN' MKAPA HIMSELF WAS RUNNING BUSINESSES IN THE STATE HOUSE PREMISES WHILE HE WAS STILL IN POWER CONTRARY TO HIS OATH OF OFFICE!

Surprisingly, Mkapa was one of the Nominees of the Bo Ibrahim Award again this year, and also this month he was awarded an Honorary degree by the University of Ghana for the so-called good governance, disciplinarian, diplomat, upholding human rights (?), among other things. Really? With the exposure of several shoddy dealings and wrongdoings, MKAPA DID NOT DESERVE THESE ACCOLADES. IT IS HIGH TIME HIS IMMUNITY WAS REPEALED AND IMMEDIATELY BE CHARGED IN A COURT OF LAW OF CORRUPTION, HUMAN RIGHTS VIOLATIONS AND ABUSE OF POWER!!

_______________________________________________________________

KIATU CHANGU KIPANA LAKINI KINANIBANA
 
Hii yote ni sehemu ya "Human Rights Watch Report!" au kuna mchanganyiko?

Source?
 
Hii yote ni sehemu ya "Human Rights Watch Report!" au kuna mchanganyiko?

Source?

It is a combination of two websites but both atrocities caused by MKAPA:

1. Go to Home | Human Rights Watch, search "Tanzania or Zanzibar" and you will see the Report: Tanzania: Zanzibar Election Massacres Documented | Human Rights Watch

2. Visit this link: Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania and
http://www.igs.net/~kassim/mwembechai/index-ch1.html

Nyambala

Quote:
Dini tena??????????


Yes, it can be "udini" depending on which side you support. Mkapa knew about the killings when he was abroad akitumbua na Wazungu. But because those slaughtered were ALL MUSLIMS:
a) He did not cut short his European visit
b) He did not punish the murderers until now
c) He failed to reveal the outcome of the Commission he promised Human Rights Watch (if you know it, please post it here!)
d) He never compensated the families who were forced to become Refugees in Mombasa nor paid sympathy to them
e) There in no Inquest on the Mwembechai killings to date.

If Nyambala is capable of telling HUMAN RIGHTS WATCH the "udini" details just reply them in their website
 
Someni between lines sasa acheni ubishi. Sehemu yeyote ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania semeni nitawapatieni mchambue na sii kuongea kama kijiweni. We are elites atiii!!!

Wewe na nani ?

Na u-elite wenu ni kwenye kitu gani ?

Kama unatuongelea jamvi zima naomba include me out!

"We are elites"! Ha haa aaaaaa!
 
Wewe na nani ?

Na u-elite wenu ni kwenye kitu gani ?

Kama unatuongelea jamvi zima naomba include me out!

"We are elites"! Ha haa aaaaaa!

Wote ni elites but at least educated/learned guys if you are outing yourself that is fine and need not permission from me! Kuvutana is not good can you contribute to the forum or stay silent forever?
 
Meza asprin utanielewa kisha kabla ya kulala tumia sheladol

Nilianza kufikiri labda sielewi lugha unayotumia, lakini maadam umetumia hiki cha kwetu sasa nimeona tatizo liko wapi: humo kichwani. Nitakwambia kwa nini.

Kama unasema nikimeza aspirin nitakuelewa basi sitahitaji sheladol tena!

Ulichokisema hapo juu kinafunua, kina reveal, mengi sana kuhusu mantiki zinavyoshughulikiwa (au zisivyoshughulikiwa kabisa) kichwani mwako: kwa mkorogo!

Ndio maana hatuelewani.

Sasa, on top of matatizo hayo ya asili, ukichanganya tena na hoja zako za aspirin na sheladol, hapo sidhani kuna tumaini.
 
Kama nimeelewa vizuri sehemu hiyo ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 kuhusiana na rais, naona aliye na kinga tena kiduchu ni rais aliye madarakani na bado sioni ikiwa aliye madarakani ana kinga isiyo mia kwa mia then how about the mstaafu. Should I betray myself kuwa hana kinga? Kwa kuwa hamna pahala panaposema BOLD kuwa na kinga! Narudia na kurudia sipaoni kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania panapotetea uozo namna hiyo. Remember katiba hii ni biblia takatifu ya nchi na serikali yetu na kamwe isingeweza kutoa mwanya huo. Niseme tu sijaona kinga dhidi ya rais mstaafu eg. mkapa katika katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 na kwa kuwa katiba ni sheria mama na nyingine zote zatokana na misingi ya katiba sidhani ipo yeyote derived from katiba ambayo itapingana na katiba otherwise .......convinced otherwise I do not see the immunity

Kinga dhidi ya
mashataka ya
na madai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.20 ib…

46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mshiiri, hizo post hapo juu zote ni zako; kinga ya BWM umeionesha mwenyewe kwenye kifungu 46(3), soma vizuri usije kuji'betray yourself'!!
 
Back
Top Bottom