Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,822
- 24,481
Tumechoka na maneno yenu.Mambo mangapi mazuri Mkapa ameifanyia Tanzania?Ila kwa vile mmeumbwa kuona mabaya tu hamtaki kuyakumbuka mazuri.Waulizeni awamu ya nne ile jeuri ya kuunda baraza la utitiri wa mawaziri waliipata wapi?
Halafu kwa nini mumuone Mkapa tu?Mbona hamzungumzii ufisadi alioufanya Mwinyi na mama siti awamu ya pili?Mbona hampigi kelele na wao wafikishwe kwenye mkono wa sheria?
Au bado mna wivu wa kike kwavile aliwaambia ni wavivu wa kufikiri?
Tuchukulie kuwa unayosema ni kweli, kuna mambo mazuri aliyofanya Mkapa ambayo hatuyaongelei.
Je, umewahi kuona mwanamke aliyelea mimba ya mtoto pamoja na usumbufu wake mpaka akamzaa mtoto na akamlea mtoto yule vizuri hadi alipofikia umri wa kuanza shule ndipo mama yule akamvunja mtoto mikono yote na kumtupa porini? Je unadhani mama huyu atakushukuriwa kwa kumlea mtoto hadi umri ule au atakumbukuwa kwa madhara aliyomwachia mtoto yule maisha yake yote.