FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 731
Safi sana. Ndio ukomavu na uelewa.
Bado wengine unatutukana, eti Nkapa ni msafi??? uuuffffss@!&#xxxszi tuombe msamaha na hilo
Mimi najua sasa hivi tatizo la ufisadi, ambalo kwa kweli ni kubwa, limekuwa na multiplied effects ikiwemo kuwafanya watu wasiwe objective sana kwenye analysis zao. Kwa hiyo inahitaji roho ya chuma kuweza kusema anything positive about such people as Mkapa, Rostam, etc., maana kwa kufanya hivi huchelewi kuwa labelled mtetezi wa mafisadi!!! Binafsi I am prepared to take this risk by saying something positive about Mkapa's administration. Yes, overall, Mkapa failed us badly but not as badly as Mwinyi did and as Kikwete has done and will do.
Inabidi kwanza tuwe na vigezo fulani au niseme angalau ka-theoretical framework fulani katika kujenga hoja zetu. Binafsi ninatathmini mafanikio au mapungufu ya kiongozi kwa kuangalia mambo mawili, ambayo ni uwezo wake kiutendaji (effectiveness) na maadili yake kama kiongozi (ethical conduct).
Nitaanza effectiveness. Unapopima effectiveness ya kiongozi huanzi kwa kuangalia yale ambayo wewe uliyataka, bali unaangalia yale ambayo kiongozi huyo alisema atafanya na ambayo yalimfanya achaguliwe. Hapa ndipo tatizo linapoanzia, watu wengi wanamtathmini Mkapa kwa kuangalia yale wao waliyoyataka ayafanye badala ya kuangalia yale ambayo yeye aliahidi kuyafanya akiwa madarakani.
Hatua inayofuata inabidi tujikumbushe Mkapa alisema anataka kufanya nini alipoomba urais? Alikuwa na ajenda kubwa nne:
Agenda ya 1 ilikuwa uchumi, bila kujiingiza kwenye academic jargons, katika hili unaweza ku-summarise dira na malengo ya Mkapa in one sentense: kujenga na kuimarisha sekta binafsi, ikiwemo ubinafsishaji wa mashirika ya umma yaliyokuwa vichaka vya majambazi wa fedha za umma. Sasa kama kuna mtu anasema Mkapa hakuuimarisha sector binafsi hiyo ni shauri yake. Matokeo ya zoezi hili la kuimarisha sekta binafsi yanajulikana, ikiwemo kushuka kwa inflation, ukuaji wa uchumi, n.k. Sasa je matokeo ya yote haya yalimsaidia mwananchi wa kawaida ku-improve maisha yake? Highly doutable, lakini hakuna shaka kwamba yaliweka misingi imara ya kuelekea huko in future, ambayo bahati sana utawala wa JK, ama kwa ujinga wa kutokujua cha kufanya au kwa makusudi, wapo busy kuibomoa! Kwa kipengele hiki ninampa Mkapa two resounding pluses with a star ( ++*).
Agenda ya 2 ya Mkapa ilikuwa ni kuweka nidhamu ya matumizi ya mali na fedha ya umma (Discipline in the management of public finances). Waliofanya kazi serikalini na hasa kwenye idara za fedha wanajua alichokifanya Mkapa katika hili. Ni hatua yake hii ya kuweka nidhamu ya matumizi ya fedha ya umma iliyosababisha hao wakubwa anaowaongelea MKJJ warudishe imani na kukubali kutufutia madeni pamoja na kuanza kutukopesha tena baada ya kuacha kwa miaka kadhaa wakati wa utawala wa Mwinyi. Kwa hiyo, Mwanakijiji, yes Nyerere's and Oxfam's rhetorics on this issue helped, but them alone would never convince the international monetary institutions to restore faith in the Tanzanian Government. Kwa hapa ningempa Mkapa two big pluses (++).
Agenda ya 3 ya Mkapa ilikuwa kurudisha heshima ya wafanyakazi wa serikali kiutendaji, kinidhamu na kimapato. Mtakumbuka kwamba wakati wa Mwinyi ilifika mahala ilikuwa aibu kujitambulisha kwamba wewe unafanya kazi serikalini! Yaani ilikuwa ni bora useme mimi ni machinga nina kibanda changu pale stand ya bus kuliko kusema mimi ni mwalimu, karani au afisa wa kitengo fulani serikali. Wakati wa mwinyi ulikuwa ukiingia ofisi za serikali, hata mawizarani, hutamani kurudi tena, sakafu na furniture zimechoka, wafanyakazi walikuwa hoi ile mbaya, wanapiga miayo, wanasinzia na wengine wanauza chai na vitumbua. Mkapa alifanya kazi ya ajabu katika hili hadi ikafika mahala wafanyakazi wa serikali wakawa proud na kazi zao, mishahara ikaongezeka, maofisi ya serikali yakaboreshwa sana-matokea yaka kila mfanyakazi wa serikali atakwambia kwamba tija imeongezeka, na sio siri hata wananchi walianza tena kufurahia huduma za serikali. Matatizo yaliendelea kubaki, lakini kusema kweli yalishughulikiwa kwa asilimia kubwa. On this basis, I would give Mkapa on this one a big plus (+).
Agenda ya 4 ya Mkapa ilikuwa swala zima la kujenga utawala bora na kuimarisha utawala wa sheria-hapa mimi ni mojawapo anayeaamini kwamba likuwa total disaster. Yote hii ni kwa sababu Mkapa aliweka mapenzi makubwa zaidi kwa maendeleo ya CCM kuliko demokrasia ya nchi. Matokeo yake alijikuta akileta ubaguzi wa kutisha kwenye swala la utekelezaji wa sheria-wana CCM walikuwa na impunity ya kutisha wakati wa Mkapa. Vilevile, ni kipindi cha Mkapa ambapo uhuru, kujitegemea na utaalamu (professionalism) ya vyombo vyetu vikubwa vya kulinda na kutekeleza sheria, ikiwemo tume ya uchaguzi na TAKURU vilimomonyolewa, kwa sababu viliamua kufanya kazi kwa minajili ya kuisaidia CCM ibaki madarakani kwa gharama zote. kwa kifupi, Mkapa ni kiongozi conservative aliyeamini kwamba wenye uwezo na haki ya kutawala Tanzania ni CCM tu kwa gharama yeyote ile hata kama wananchi waliwakataa. So, on this one, I would give Mkapa two resounding minuses (- -).
Sasa twende kwenye kipengele cha pili, cha maadili. Hapa tunaangalia mwenendo wa kimaadili wa kiongozi kabla na baada ya kuingia ofisini. Maadili haya ni yale mambo binafsi ambayo kiongozi anapoyafanya analeta madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo, kwa mfano, wizi, matumizi mabaya ya ofisi yake. Technically, hatuwezi kujumuisha yale mambo ambayo kiongozi aliyafanya binafsi ambayo, japokuwa yanaweza yakawa hayapendezi au hayakubalika mbele ya macho ya wengi ya wanajamii, lakini hata madhara kwa mtu mwingine yeyote moja moja au kwa jamii kwa ujumla. Sasa hapa ndio wengi tunakubaliana kwamba Mkapa alitutenda-na ushahidi wenyewe ni ukwali kwamba Mkapa ameibuka na utajiri wa kutisha baada ya kumaliza madaraka yake, utajiri ambao kwa vyovyote vile, hata kama angeshinda tuzo ya Mo Ibrahim, haulingani na mapato yake. Hapo ndio sasa wengi tunakubaliana kwamba Mkapa alituvuruga, ana because of that on this one, I have to give him three disastrous minuses (- - - *)
My verdict: Yes, though hard evidence is yet to be unequivocally unveiled regarding his misconduct in office, there are clear indications which would appear to suggest that Mkapa did behave in a manner that leaves a lot to be desired and that has gravely compromised his ethical standing as a politician and a former statesman. In any case, Mkapa's unethical conduct in office, bad and disgusting as it is, does not undo his performance in other areas of his leadership, especially with regard to being firm and clear in his vision and for taking bold decisions that, more often than not, clearly cost him popularity and public image standing. That is what I call leadership, as opposed to drifting, dithering and manipulation as we constantly see in our chaguo la Mungu!
Kitila Mkumbo,
Mkuu hakika umenisikitisha sana niliposoma hoja zako ambazo hazina kipimo hata kidogo kwa jinsi unayapima mazuri ya Mkapa...Yaani duh mkuu kama kweli upimaji wenyewe ndio huu basi Tanzania tumekwisha!...
Nitaanza na sekta Binafsi..
Umesema seara zake zilijenga na kuimarisha sekta binafsi, ikiwemo ubinafsishaji wa mashirika ya umma yaliyokuwa vichaka vya majambazi wa fedha za umma!...
Mkuu ni kwa kutumia matokeo yapi umelkitazama swala hili ikiwa:-
1. Ni wakati wa Mkapa tumeona mifano ya kuundwa kwa mashirika yaliyochukua fedha za EPA..Mkapa mwenyewe kufanya biashara akiwa Ikulu, Mkewe mwenyewe kuchukua majumba ya serikali, Mawaziri wake kina Yona na Mrema kujitajrisha (hakuna viongozi matajiri kama mawaziri wa Mkapa hadi leo hii), Kina Karamagi kuchukua tender za bandari ambako leo container unasubiri miezi sita kulitoa tena kwa rushwa, Kina Mzee Kingunge kuchukua vituo vya mabasi kama kwamba ardhi ile ni urithi wa babu zao... Hivi ni kipi anachokifanya Kikngunge astahili kulipwa yeye uendeshaji wa kituo cha mabasi!... yaani hata kurasa hazitoshi kujaza Ufisadi chini ya Mkapa..
Kuibuka nguvu ya mafia kina Chande na Patel, huku Rostam akiwa mhasibu wa chama. Mafisadi na sio Mabepari kupewa nafasi kubwa ya kuendesha mashirika hayo ambayo kila mwaka yamekuwa yakiweka tobo na mirija yao ktk mfuko wa Taifa...Haya majambazi unayozungumziwa yalijengwa hadi kufikia vyombo vyetu vya Usalama na ushahidi tumekuja kuuona hivi majuzi tu kina Mahita hatufahamu alianza lini!...Jamani leo hii imefikia watu mnasahau jinsi Majambazi walivyopata uhuru kuwatesa wananchi.. Kumsifia Mkapa ani sawa kabisa na kumsifia Mugabe tofauti zao ni kwamba Mugabe alichukua ardhi ya wazungu kuwapa vigogo wake..
Hivi ni shirika gani ambalo wewe kweli unaweza kusimama hapa na kusema kwamba limeboreshwa zaidi na sio kichaka cha Majambazi wezi wa mali ya Umma. Maanake kama kweli hiyo ndio ilikuwa sababu ya wewe kusema ubora huo itakuwa vizuri sana kama unaweza kutuonyesha kuwa majambazi hao hawapo tena!..
Mkapa ni kiongozi aliyekataa kabisa kuwasaidia wajasiriamali akisema hawana uwezo (elimu na fedha) jambo ambalo hata Kikwete amekuja dhihirisha kwamba liliwezekana na kweli amebadilisha sura ya wajasiriamalia mabao Mkapa aliwapoinda! tunaona Ubora wa maisha ya watu wachache ktk kundi hilo. Bottom line mkuu binafsi leo hii ktk sekta ya biashara ndogo ndogo nadhani Kikwete ameweza kusaidia zaidi wananchi wa chini kuliko Mkapa, tatizo ni Ukiritimba na rushwa ambalo limekithiri kutokana na mfumo mbaya wa serikali..Maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu ni mfano mzuri sana ambao umeonyeshwa na wajasiriamali...
Makosa yote ambayo unayaona kwa Kikwete yalikuwepo kwa Mkapa na ktk hatua mbaya zaidi, hawa wote nguvu za Ubabe wao zimeanza toka wakati ule labda mwenzetu hukufuatilia vijiwe vilivyopita. ni kwamba wananchi hatukuruhusiwa kabisa kuyazungumzia hadharani. Leo hii hawa viongozi wote wanatisha kwa sababu ujenzi wa himaya zao umeanza wakati wa Mkapa, hata huyu Kikwete nguvu yote ya Mtandao imetokana na Uongozi wa Mkapa ambaye ndiye chimbuko la kukigawa chama CCM ktk mafungu mawili makubwa!
2. Unapozungumzia Matumizi mazuri ya fedha, hapa mkuu bado kabisa sijakuelewa kwa sababu kama kifungu cha kwanza kinatisha kiasi hicho inakuwaje unasema kuna matumizi mazuri ya fedha... Unapima kitu gani hasa hizo safari za Kikwete against safari za Mkapa?... what about billions ambazop zimechukuliwa kwa kuwekwa mikataba feki? - Rada na ndege ya rais ni mifano midogo tu ya kuanzia!.. Kama kweli kulikuwepo na matumizi mazuri ya fedha za Umma imekuwaje Balali kaonbdolewa!.. Ujenzi wa Benki kuu pekee kufikia zaidi ya dollar millioni 500, fedha ambazo zingeweza kabisa kujenga Twin tower za New York zilizoangushwa ktk hesabu za gharama za leo hii!..Hivi kweli ni matumizi yapi unayojaribu kuyazungumzia hapa!...
Hivi kweli mheshimiwa unafikia kumpa sifa za UOngozi wa NCHI -TAIFA rais wa nchi kwa sababu ya Furniture?...Hivi kweli rais wa nchi badala ya kushughulika na mambo muhimu ya Taifa unakuja kumpa sifa kwa sababu kulikuwepo namabadiliko ya furniture maofisini?...
Well, kama kweli ndio nyie viongozi tunaowategemea kesho mkuu utanisamehe sana!... Sintawaunga mkono kabisa!... Unapobadilisha maisha ya wananchi wako kama Mkapa alivyoweza kubadilsiha hizo furniture ndipo mimi naweza kusema nampa point.. Kwa hili mkuu nasema ni afadhali ya KIkwete kwa sababu leo hii Ukienda Tanzania unaweza kuiona tofauti kubwa!... Vijana na kina mama wajasiriamali sasa hivi wamewezeshwa ku design nguo, viatu, na kadhalika na wananchi wanaweza kuzinunua. Hizi ndio furniture za maendeleo ya mwananchi. Ukiweza kuutunza mwili wako bila shaka kuyatunza makazi yako.. Usafi huanzia mwilini..
Mkuu Mkapa ni sawa na Mzazi aliyemzaa mtoto wa kike kisha akatembea naye kimwili... hizo sifa za Uzazi mkuu mpe wewe mwenyewe!
I suppose baadhi yenu (Mwanakijii especially) mmekasirishwa sana kwa mimi kutumia neno 'foolish." You don't have to. "Foolish person" kwa definition yangu ni " someone who is easily tricked". Nasema "easily ticked," coz Kikwete's inner circle wame-manufacture nyingi ya hizi kashfa kuhusu mzee Ben, kisha wakazi-leak kwenye press, bloggers nao wakazidakia, huo moto hauzimiki. The daunting quesion is: kwanini watu hawataki ku-pose na kujiuliza, "wait a minute, kwanini Kikwete anaacha hizi kashfa ziende unaswered kama Mkapa ni fisadi kweli?"
Fisadi Mkapa pia aliamua kuziuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa pamoja na Watanzania wengi kupinga uamuzi huo, mpaka leo bado serikali inaingia gharama kubwa kuwaweka mahotelini maofisa wao na familia zao kutokana na kutokuwa na nyumba za kutosha, haya ni matokeo ya sera za fisadi Mkapa.
Kuna mengi yamesemwa/andikwa kuhusu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa: "Oh, mkapa ni fisadi," "Mkapa alitumia madaraka ya Urais vibaya," "Mkapa ajitete mbele ya umma," "Blah... blah... blah..."
Lakini ukweli ni kwamba: ni Mzee Ben, na sio Mzee ruksa, wala this Kikwete guy, ambaye ameifanyia nchi hii mema na mazuri. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, Mkapa alipokea nchi iliyokuwa katika hali mbaya kupindukia.
Rushwa ilikuwa imekithiri. Pato la taifa lilikuwa chini. Ukwepaji kodi ulikuwa katika kiwango cha kuogofya. Na miundo mbinu ilikuwa imechoka kupindukia.
Ni chini ya utawala wa mzee Ben ndipo watanzania kwa mara ya kwanza tulipoanza kuona sera ya taifa kuhusu uchumi ikipewa kipaumbele. Miundo mbinu ikiboreshwa. Pato la taifa likikua. Na kamba dhidi ya vita ya rushwa ikikazwa.
Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.
Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (1) mikataba mibaya hususani madini (ambayo hata hivyo ni mwanasheria mkuu ndiye anapaswa kulaumiwa);(2) kumuachia mke wake a-dictate badhi ya shughuli za kiserikali ( one of his weakness). (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...
Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.
Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).