Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

wahenga walishasema " Ushirika wa wachawi haudumu"! waache wakifikiri ushirika wao ni wa milele, leo ni siku ya kuandika historia ya Mh. Ngeleja ambaye kwa siku zote wamejaribu kutuonyesha ni mtu makini.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Umenena Ya liyo ya kweli ,ila nachokwambia na walichoamua baada ya kikao kilichopita cha Baraza la Mawaziri,wameweka msimamo wa Serikali.Ni Pinda alishatoa Muungozo wa nini Kitakachojiri leo.na Mambo ambayo wameamua kufanya kwa kifupi

Wameshindwa kutuzuga na wameamua kutulazimisha tukubali
Rejea kauli ya Pinda kuhusu suala la Meremeta,walishatuzuga sana kipindi kile kuhusu Kampuni hii,alijaribu karamagi akashindwa na njia ambayo wametumia sasa ni kutumia Ubabe wa kutulazimisha tukabalia hata kaam hatutaki.Ndiyo maana Pinda akapindisha kwa kusema Merermeta ilikuwa ni mali ya Jeshi na Usalama.Sian uhakika ni lini Nchii hii ilishaanzisha Vyombo vya Usalama kwa Ajili ya Biashara.

Na hili la leo watatulazimisha tukubali kile ambacho hatukitaki na tunakijua kwamba walihujumu na kuchukua mali zetu.Kama Jana Ulimsikia Ngeleja akitoa Muhtasari utajua ni nini leo atazungumza

Kuhusu DOWANS na Richmond
Leo tutegeme mambo ambayo hatukuwahi kabisa kujua ila tutalazimishwa kuyameza,Jana Ngeleja akihojiwa na TBC! alisema seriklali haiikuwahi kuwa na Mkataba na Dowans na wameuvunja,cha kujiuliza hapa ni hiki

1.Je serikali ambayo tunaiamini iliwezaje kulipa pesa nyingi kiasi hicho bila ya kuwa na mkataba na kampuni hii.Kama ni hivyo ina maana hata malipo yaliyofanyika haijulikani yalilipwa kwa nani.Huku ni kutulazimisha kwa nguvu baada ya uzugaji kushindikana

2.Mkataba ulivunjwa na TANESCO,ila ukiangalia mwanzoni serikali ilikuwa ya kwanza kufanya nao mazungumzo,ilikuwaje TANESCO haikufanya hivyo ila baadaye waje wavunje mkataba.

3.Dr. Idrisa Rashid Alisema kwamba Wamevunja Mkataba,Serilai inasema kulikuwa hakuna Mkataba,sasa tumuelewe nani?Leo tutapata Majibu


Tumuachie Ngeleja azungumze Msimamo wa Serikali,ila siyo mawazo yake na hii ndiyo mbinu mpya ya serikali iliyobuniwa ili kujibu mapigo.Ndiyo maana hata Rais kwa sasa hatoi Hotuba za mwisho wa Mwezi na kamuachia Rweyemamu ambaye atakuwa akipewa maelekezo kutoka kikao cha Baraza la mawziri na makatibu wakuu.

Naomba nijibiwe leo,Msimamo wa serikali ni kitu Gani,Je Serikali imechaguliwa na Nani,Bila sisi kuna Serikali??Ikiwa Kama ni sisi tunasababisha inakuwapo serikali Je Msimamo wetu ni upi?
NINGEKUWA MIMI NDIYO NGELEJA,NIGESEMA UWAZIRI WENU CHUKUWENI,nikabaki na ubunge wangu
 
Zitto anaumwa na ndio maana ameshindwa kuhudhuria Bunge leo (Ni ugonjwa wa kawaida tu, si wa kutia shaka, at least kwa sasa.)
Hotuba imeshasomwa na ufafanuzi kuhusu Kiwara na uhusiano wake na Mkapa haukutolewa. Ningeshangaa sana iwapo Ngeloeja angehusisha ufafanuzi wake huo katika bajeti yake kwa sababu kwa mujibu wa malekezo ya Pinda, anatakiwa kuandaa taarifa mahusis kuhusiana na suala hilo. taarifa hiyo anaweza kuitoa kama kauli za Mawaziri. kama angeiweka kwenye hotuba ya bajeti angekwua ameinyima haki.
Lakini hoja za M.M.M bado ni valid na tusubiri lini Ngeleja atandaa taarifa hiyo na kuitoa Bungeni
 
Naamini kuwa Serikali itakiri kuwa uuzwaji wa Kiwira kwa timu ya Yona na Mkapa ulikiuka taratibu (hawatasema ulivunja sheria) na baada ya majadiliano na wamiliki mgodi huo unarudishwa serikalini baada ya serikali kuwalipa wawekezaji hao mabilioni kwa kuvunjwa mkataba. Mkapa na Yona watanyang'anywa kiwira.
 
Naamini kuwa Serikali itakiri kuwa uuzwaji wa Kiwira kwa timu ya Yona na Mkapa ulikiuka taratibu (hawatasema ulivunja sheria) na baada ya majadiliano na wamiliki mgodi huo unarudishwa serikalini baada ya serikali kuwalipa wawekezaji hao mabilioni kwa kuvunjwa mkataba. Mkapa na Yona watanyang'anywa kiwira.
Mzee Mwanakijiji,

Hivi kwanini wanatulazimisha tukubali siye ni wajinga??Nchi ya mandondocha?ni sheria zipi ambazo wenyewe wanaamini zikivunjwa basi mambo yanaharibika
 
Kuna mengi yamesemwa/andikwa kuhusu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa: "Oh, mkapa ni fisadi," "Mkapa alitumia madaraka ya Urais vibaya," "Mkapa ajitete mbele ya umma," "Blah... blah... blah..."

Lakini ukweli ni kwamba: ni Mzee Ben, na sio Mzee ruksa, wala this Kikwete guy, ambaye ameifanyia nchi hii mema na mazuri. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, Mkapa alipokea nchi iliyokuwa katika hali mbaya kupindukia.

Rushwa ilikuwa imekithiri. Pato la taifa lilikuwa chini. Ukwepaji kodi ulikuwa katika kiwango cha kuogofya. Na miundo mbinu ilikuwa imechoka kupindukia.

Ni chini ya utawala wa mzee Ben ndipo watanzania kwa mara ya kwanza tulipoanza kuona sera ya taifa kuhusu uchumi ikipewa kipaumbele. Miundo mbinu ikiboreshwa. Pato la taifa likikua. Na kamba dhidi ya vita ya rushwa ikikazwa.

Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.

Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (1) mikataba mibaya hususani madini (ambayo hata hivyo ni mwanasheria mkuu ndiye anapaswa kulaumiwa);(2) kumuachia mke wake a—dictate badhi ya shughuli za kiserikali ( one of his weakness). (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...

Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.

Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).
 
Well, uwanja wa fisi ni part ya Tanzania pia. Point niliyokuwa nina-make ni kwamba: Linganisha utendaji wa serikali za awamu ya pili, tatu, na nne kisha eleza ni nani ambaye ana-deserve credit.
 
- na ni chini ya utawala wa Mkapa ndipo wizi mkubwa kabisa katika Benki Kuu umetokea!
- Ni chini ya Mkapa Usalama wa Taifa was compromised kwa kubadilisha sheria ya usalama na kuunda picha ya kitu kinachoitwa Usalama wa Taifa na hivyo kuruhusu wezi kuingia hadi jikoni kuiba huku picha hiyo ikiwa imesimama mlangoni!
- Ni chini ya Mkapa Sheria mbovu ya Madini ya 1998 imeandikwa ambayo ilifungua mlango kwa upotevu wa mabilioni ya shilingi katika sekta hii muhimu kwa uchumi.
- Ni chini ya Mkapa sheria mbili za fedha zenye mambo ya ajabu ziliandikwa 2001, 2004 ambazo pamoja na sheria nyingine ziligeuza tanzania kuwa kisima cha uchotaji wa fedha na kuzirusha nje.
- Ni chini ya Mkapa makampuni feki yaliyoundwa na kuchota fedha za umma ikiwemo Meremeta yalipoundwa na yeye mwenyewe akiwa ni mmoja wa watu waliojua nini kinaendelea!
- Ni chini ya Mkapa kwa mara ya kwanza Rais wetu alitumia nafasi yake kuingia kwenye ubia na taasisi iliyo chini na hivyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi - na hili si dogo, ni kubwa mno! Nchi nyingine rais anaondolewa na Bunge!
- Ni yeye aliyemteua Mwanasheria Mkuu mbovu kabisa katika historia ya Tanzania huru


Hitimisho:

Mkapa alifanya aliyoyafanya na katika aliyoyafanya aliyoyafanya kwa kuyafanya vibaya kabisa ni yale aliyoyafanya ambayo hataki kuyazungumzia kuwa aliyafanya!
 
Nashangaa watu wanavyomsifia Mkapa,Don’t praise Mkapa that much, When you look at the Tanzanian economy timeline you will realise Mwinyi had a country at hard time .it was a time when Tanzania was going under structural adjustment programme, which helped the country on prevailing economic, social and political structures from socialism . all of the structural adjustment programmes experienced in the 1980-1990s e.g multy party democracy .In general, adjustment measures included exchange rate devaluation, fiscal policy restructuring, monetary discipline and interest rate rationalization, as well as an array of institutional reforms that involved redefining the role of the state and public enterprises engaged in a range of activities that why during mwinyi time the exchange rate was very good. Let’s say TSH 400 was equal to 1 USD.

When Mkapa came in power the world Bank, Initiated new polices at time and that was Market Economy, that was the time when all the public company was sold. and it did open up the economy by more FDI inflows , which stabilised the economy but at same time people used that chance to benefit themselves mafisadi hao.

In conclution it doesn’t matter who is a president, what worries me is all the polices from world bank, because they are ones can determine the state of the county therefore Mkapa has nothing to credit himself because hata Mr Nice angekuwa raisi it would happened.
 
Mzee Mwanakijiji, you're a man of fine intelligence, but I must respectively disagree with you on this matter.

You know it's relatively easy for critcs who don't like Mkapa to say anything negative about him, but impossible to say his positive contribution to our nation.

It seems obvious to me that all these trash talks about Mkapa is a well-orchestrated campain by Kikwete's team ( which you guys have also bought in) to just kick dirty to Mkapa's eyes.

It's a wishful thinking to think that Mkapa alone (in 10 yrs) could have undone the wrongs and errors of colonial institutions, ujamaa policies, and Mwinyi's economy, stupid.

Now, it doesn't matter, though, how much you guys will continue to trash mzee Ben; but the truth of matter is, he is one of the finest presidents that our country have ever produced.
 
Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...


Hiyo statement hapo juu ime-summarize kila kitu kuhusu who you are and what you are standing for , to make a long story short it will be wastage of time to debate with you. I am completely flabergasted ... Kweli kuishi ni kuona mengi . Kufanya biashara Ikulu ni nini ?
 
Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ... kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...

Kikwete and his inner circle ...wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina...

Unajua unachokiongea wewe au unatumia uhuru wako wa kuongea?

Biashara Ikulu ni minor thing? Kikwete ndio anamchafua Mkapa au ndio anamlinda?

You are almost ridiculous!
 
Well, uwanja wa fisi ni part ya Tanzania pia. Point niliyokuwa nina-make ni kwamba: Linganisha utendaji wa serikali za awamu ya pili, tatu, na nne kisha eleza ni nani ambaye ana-deserve credit.

Fisadi Mwizi hadiserve credit yoyote. Yeye alikuwa busy kuiba na kufanya biashara wakati Watanzania wakipoteza kazi zao kila kukicha kwa mashirika yaliyouzwa bei ya bure kabisa. Matokeo ya sera za fisadi Mkapa ndiyo hayo yanasababisha mashirika yetu kama TANESCO na TTCL yana hali taabani na si ajabu yanaweza kufa.

Fisadi Mkapa aliwaleta Makaburu wa Net Problems kwa mtutu wa bunduki pamoja walikuwa hawajui chochote kuhusiana na umeme na Watanzania wengi kupinga makaburu hao kuiendesha TANESCO . Aliwalipa mapesa chungu nzima kama mishahara, marupurupu na management fees. Pia aliingia mikataba ya ajabu ajabu ambayo haina maslahi yoyote na Watanzania kama IPTL na uchimbaji wa madini. Mikataba ya madini aligoma kabisa kuitoa hadharani kama vile rasilimali za madini zilikuwa ni za kwake Mkapa na siyo Watanzania wote.

Fisadi Mkapa aliamua kununua rada kwa $40 millioni pamoja na kuwa Watanzania wengi tulipinga uamuzi huo na kusema pesa hizo zingeweza kutumika vizuri sehemu nyingine ambapo zingekuwa na umuhimu mkubwa sana, lakini hakutusikia yeye na mshirika wake fisadi Mramba wakatamka 'hata majani tutakula' lakini lazima rada inunuliwe, kumbe walikuwa wana commision ya $12 millioni waliyokuwa wanaizengea na fisadi mwenzao aka wakala Vithalani.

Fisadi Mkapa akishirikiana na fisadi Vithalani tena kama wakala wakaingia mkataba wa kununua ndege ya Rais, magari na helikopters za jeshi ambapo pia kulikuwa na utata mkubwa na ufisadi ambao bado unafichwa lakini ipo siku Watanzania tutakuja kujua ukweli kuhusu ufisadi wa haya.

Fisadi Mkapa pia aliamua kuziuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa pamoja na Watanzania wengi kupinga uamuzi huo, mpaka leo bado serikali inaingia gharama kubwa kuwaweka mahotelini maofisa wao na familia zao kutokana na kutokuwa na nyumba za kutosha, haya ni matokeo ya sera za fisadi Mkapa.

Fisadi Mkapa akishirikiana na fisadi Yona waliiba Kiwira na kujimilikisha mgodi huo kwa bei poa kabisa ya shilingi milioni 700 wakati thamani ya mgodi huo ni shilingi bilioni 4. Hakukuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa kuhusiana na kuuzwa kwa mgodi huo. Hakukuwa na kamati yoyote iliyoamua kwamba mgodi huo uuzwe kwa bei ya shilingi milioni 700 hakukuwa na kamati yoyote iliyoamua ni nani kati ya watu mbali mbali waliotuma maombi ya kununua mgodi huo alichaguliwa na kamati labda kwa kuwa na bei kubwa au plan yake ya kuundeleza mgodi huo ilikuwa ni nzuri kuliko mwingine yeyote.

Akiwatumia makaburu aliowaweka katika management positions pale TANESCO akawashinikiza wasaini mkataba kati ya 'kampuni yake' na TANESCO wa shilingi bilioni 326 mkataba ambao unazidi kuongeza bei ya umeme kwa Watanzania wote na pia kuifanya TANESCO ishindwe kujiendesha kwa faida. Wizi wote huu aliufanya wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Tafuta lingine la kutuzuga lakini la hili la fisadi Mkapa eti kuwa ni safi labda ukawadanganye wengine lakini siyo hapa JF kamwe hatutakupa ukumbi wa kusambaza uwongo na propaganda zako za kumsafisha fisadi Mkapa, ni fisadi wa hali ya juu na mlafi wa utajiri kwa kupitia njia za haramu.
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people.
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people.

Wewe mbona umekasirishwa na 'foolish people'? Nani foolish zaidi?

Una test na ku prove upeo wa Watanzania kutumia thread iliyojibiwa na watu wanne watano? Nani foolish zaidi?

Unasema wanaomkosoa Ben Mkapa ni inner circle ya Kikwete? Nani foolish kati yetu na wewe?
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people.

Kama kuwa smart ni kuamini kwa Fisadi Mkapa ni safi na siyo fisadi kama ambavyo ushahidi mbali mbali unavyoonyesha bora tubaki na upumbavu wetu.
 
nilidhani kuwa unataka mjadala lakini naona umetuona sisi sote ni foolish people.. so no need to engage you katika mjadala huo. I'm so foolish that I can't even think about talking to you. Na utapoteza muda kuzungumza na foolish people.. I mean foolish Tanzanians.. I remember somebody also said something like this "Watanzania ni wavivu wa kufikiri" isipokuwa Mtanzania yeye!
 
Back
Top Bottom