MamaParoko
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 463
- 61
Bachi bachi nyamala ntoto, yamekwicha utu uzima dawa siye wenzio tushakuelewa haina haja ya kuendeleza mjadala, usirudie tena enhee umechikia toto zuri?
hoja imetulia cha msingi tuijadili objectively. tatizo wabongo tunapenda simple mind kujustify hata mambo ya msingi. Mzee Ben ni kiongozi pekee katika taifa hili aliyejenga uchumi unaoweza kusimama duniani kwa mazingira ya kishindani. Kafanya mengi mnoo ambayo nina hofu kwa sasa yanapotea kiholela kutokana na USANIIIIII. Ni kosa kubwa na garama yake tutailipa wenyewe kwa kuendekeza usaniii. He is a visionary leader of his TIME. Mabadiliko ya sera za kiuchumi alizosimamia ni alama ya picha ya tz ya sasa. misingi imara ya ukusanyaji wa kodi, miundo mbinu(ushahidi upo tembea nchini uone), mabadiliko ya utumishi wa umma nk. Amefanya mengi mpaka kwa muda aliokaa magogoni ameleta heshima kimataifa. Uwezo wake binafsi KIAKILI ni ushahidi tosha(fuatilia maendeleo yake shuleni), kujenga na kutetea hoja kitaalamu baada ya mwalimu hakuna kama yeye, cheap popularity HATAKI, umbea na mtandao hapendi.
Nchi yenye uchumi dhaifu kama yetu inahitaji watu makini kuusimamia na sio porojo. tuko kundi la nchi maskini si kwa sababu hatuna rasilimali, tatizo WATU.
kwa sasa tuamke tujue hawa viongozi hatuwapi nafasi kupiga picha na watu wa magharibi na kupongezwa kifalaaa bali kufikiri jinsi ya kuongoza kwa mafanikio.
Mzee Ben historia itamhukumu. tunachojifunza kutokana na historia ni kutokujifunza chochote kutokana nayo...
Aliimarisha uchumi na sio blah blah. gafla wasanii mjini wakapotea, watumishi wakaheshimika. TUKAZE ALIPOACHIAAAAA.
UWANJA HUO KWA MANENO YAKE....NITAWAACHIA UWANJA WA KISASA. PITA CHANGOMBE UJIONEE. BONGO BIASHARA GANI NDANI YA DK 90...MAPATO MILION 600..
TFF WANANGAAAA, SOKA ITABIDI LIKUE HAKUNA UJANJA WALA SIO USANIII WA WACHACHE KICHOCHEO KIPOOOOOO.
Muungwana ni vitendo sio maneno, umeonyesha uungwana kuomba radhi.
Mwanakijiji huu ni uongo "Ni yeye aliyemteua Mwanasheria Mkuu mbovu kabisa katika historia ya Tanzania huru"
Chenge aliteuliwa na Mwinyi akichukua nafasi ya Jaji Damian Lubuva ambaye aliwekwa pale baada ya Julius K.Nyerere na Mwinyi kumvika Sinde Warioba Uwaziri wa mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais.
Udhaifu wa Mkapa ni matunda ya CCM na Mafanikio ya CCM 1995-05 ni matunda ya kuthubutu kwa Mkapa kuleta mageuzi ya kweli ktk uchumi na vita dhidi ya umaskini.
Hakuna sheria inayomkataza rais kuwa mjasiliamali na vivyo hivyo kutafuta mianya ya kujiendeleza kiuchumi.
Tutamuhukumu Benjamin Mkapa kama tu alijitwalia amali za umma kwa kwa udanganyifu.
Kama Kiwira iliuzwa kwa udanganyifu sheria ichukue mkondo lakini hatuko tayari kuona watu wazima wakihuburi haki na sheria huku wakihimiza wananchi kuwatukana wenzi wao kwa tuhuma ambazo hazina hadhi ktk sheria.
Mimi nasisitiza, kumtuhumu mtu na kumdharirisha mtu pasipo kufuata taratibu za sheria kwa miaka 3 mfululizo huu ni uhuni.
Please sign my autograph. Maana wewe ni FDR.junir kweliweli. Point nzuri kabisa maana inaonyesha wazi kuwa Mkapa ameisha hukumiwa hapa JF long time ago.
Ok...Tukiamuwa kuifuta HUKUMU YA MKAPA HAPA JF...JE MTAKUBALI MAHAKAMA NAYO IMSAFISHE?
AMA NYIE MNTOSHA?
Ningeshukuru sana kama ungenijibu swali hilo...Je mahakamani ni haki yake?
PM.. sidhani kama sisi tunafikiri mbali sana. Upande mmoja tunatafuta mafuta kwa kiasi kikubwa na dalili kuwa yapo ni kubwa tu, lakini hatujaanza kutengeneza miundo mbinu ya kitu kama hicho at least kwa kulingana na data ambazo zunazo hadi hivi sasa. Tunaishi in the now sana kiasi kwamba mambo ya mwakani yatasumbukiwa mwakani.
Mkuu MMJJ,
Naona argument yako ni nzuri sana lakini sijui kwa nini hukupinga ule ujenzi wa barabara ya Rombo kuwa ni kosa. Ndio maana wengine tuliona kuwa uboreshwaji wa barabara ya Marangu-Tarakea ulikuwa ni upendeleo wa wazi kwani kuna maeneo muhimu mengi zaidi ambayo yangepaswa kupatiwa mawasiliano.
Mkapa hawezi kushtakiwa kwa makosa ya jinai aliyoyafanya akiwa Rais, kwa maana akitekeleza majukumu yake kama Rais. Siyo kwamba kama anambaka mtu ati hawezi kushtakiwa!
angekuwa Kaweka Uchumi Ulisimama, Leo Hii Tusingekuwa Tunapeleka Mchanga Wa Dhahabu Kusafishwa Nje, Tusingekuwa Tuna Zungumzia Minining Sector/contract Review, Tungekuwa Na Wakulima Wakubwa Angalau Hata Wa Wili Tu, Kama Alivyo Kuwa Steyne? Kule Arusha. Tungekuwa Na Processing Industry Ya Chakula Na Mifigo Inayo Fanya Kazi.
...mkapa kafanya mengi ya maendeleo...ni bahati mbaya kuwa kwa mtu aliyeondoka hapa tanzaia miaka ile ya 90"s na kutokomea ughaibuni......hata umshawishi vipi ....hataweza kuona maendeleo yaliyofanyika ndani ya miaka kumi ya mkapa.....watu wengi walio ughaibuni bado wana mentality fulani.....tunaoingia na kutoka anytime ...kuna katofauti kakubwa ...
pamoja na makosa ya utawala wake .....mafanikio ya mkapa hayatafutika.....
Nimejaribu kufuatilia, nimeona kweli watu wanauchungu na nchi. Kama Pundit anavyosema hapo juu ni kweli kabisa Mafanikio yanaweza kupitwa na matatizo aliyotuletea. Naungana na wengine katika kumlaumu Mkapa kwa mikataba mibovu ya madini na grand corruption kuanzia ladar, EPA, IPTL n.k. Nafikiri yeye kama mkuru wa nchi anapaswa kuwajibika kwa hayo. Nasema hivyo kwa kuwa sisi wote tunajua uwezo wa huyu bwana kiakiri. Kwa uwezo alionao haiwezekani kabisa kwamba hakuyaona haya ila tu aliamua kuyafumbia macho for whatever reasons. May be uchukuwe muda atueleze yeye mwenyewe.
Lakini sometimes nikijaribu kuangalia kwa undani hii mada naona ni kwa kiasi gani mtoa mada anaweza kuwa na point. Hii ni kwa sababu serikali ya JK kweli kazi wameishindwa sasa wanajaribu kudivert attention. Swala la mikataba mibovu ya madini na uuzwaji wa makampuni yetu tuliyajua siku nyingi wakati bado akiwa rais lakini leo ndiyo tunaona uchungu. Hii ni daliri kwamba meli MV Danganyika imepoteza mwelekeo na sasa tunaanza kuangalia makosa badala ya kutafuta solutions.
Jamaa wa sasa kama angekuwa kiongozi makini, nafikiri Wadanganyika wala tusingekuwa tunapiga kelele hapa JF. Tatizo Nahodha wetu sasa hajui anaelekea wapi ingawa alituahidi atayaendeleza ya Mkapa (at least kulikuwa na mweleko). Anyway, kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa by 2015 nafikiri hii amani na utulivu itakuwa ni history TANZANIA.
Mungu ibariki Tanzania,.......
Tanzania, Tanznia, Nakupenda kwa moyo wote.............