Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa Killed the Tanzanian economy. why ? Any country if it want to ruin its economy import Oil.

Mkapa did as the same what is happening in the world economy now speculators are shutting down the oil refineries ili waweze kupunguza supply while the demand is going up, and that is the main resorn pushing up the oil price.

Mkapa na uchu wake wa fedha, on the expense ya wananchi he killed TIPA, why did he allow the TIPA to die, this was because he wanted to open doors to his allies company like OIL COM where he has financial intrest.

This action pushed the fuel bill to go up 50% by importing refined oil while tulipokuwa tuna refine wenyewe price was less than 50% sasa kama wewe nimchumi na unakili timamu hebu niambie , Taifalipoteza kiazi gani.

We ended paying more than 10 Billion usd, on top of the nomal oil bill we had , Sasa niambie, what could 10 billion a year could have done to improve the economy and life of Tanzanian people,thats means kwa miaka kumi aliyokaa mkapa taifa limepoteza 100 Billion USD, Which could had took the country to the next level.

You come and ask yourself was Mkapa insane, or he didnt think that we had a good thinking capacity..........

i am wrting this kwa uchungu na machozi because I know what Mkapa has Costed us....na watu wengine bila kuangalia kwa makini mnamsifia.....

Mfano Uchumi wa kenya uko juu kuliko wa Tanzania kwasbabu hawakufunga refinery yao ya mombasa, Hivyo Fuel bill ya kenya is lower than ours and thats why the can afford to pay 96 % of their budget from their economy, Ila mkapa na ulimbuken wake akauza TIPA na kuendelea kuchukua hela za wahiasni ku lipia budget how stuip is that

..guys muwe mnasoma historia .....hata magazeti basi!...mkapa hakuuwa TIPPER...hichi kiwanda kiliuliwa na market forces...hichi kiwanda kilikuwa kinasafisha crude oil...na kutoa petrtoleum products..initially ilikuwa ni faida kwa sababu crude ni bei nafuu kuliko product ....what happened ni kuwa kutokana na kuendelea kwa teknelojia ..nchi zinazozalisha petrol ilifikia mahali zikawa zinasafisha crude kwa bei nafuu[cost cut due to improved automation]..hii ilifanya kununua crude oil na kuja kuosha wenyewe iwe GHALI MARADUFU KULIKO KUNUNUA READY PRODUCTS...THAT MADE TOTALLY UN ECONOMICAL TO REFINE MAFUTA HAPA...WIMBI LA KUFA KWA VIWANDA VYA REFINERY VILIKUMBA NCHI NYINGI AMBAZO HAZIZALISHI MAFUTA ..ie MOMBASA REFINERY...

SECOND REASON ...ni trade liberalization policy za 1985 - 1995..kila mmoja anajua kwa hali tuliyokuwa nayo ..maduka ..hayana vitu..viwanda havina malighafi..hakuna pesa za kigeni ..hata za kununua mafuta...ilibidi jukumu kuu la kuagiza mafuta liwe huria kwa kila mwenye mtaji alete....ingekuwa vigumu kuwalazimisha wafanyabiashara waagize mafuta ghafi ..waje tena waawalipe tiper Wfanye refinery ....wafanyabiashara wanataka profit...hili likawa pigo la pili tiper...

baada ya kampuni kuonesha dhahiri ni hasara ...hata wabia wake SERIKALI YA ITALIA ikaamua kujitoa..third problem....kiwanda kikafa ..hata kabla ya 1995....

kosa walilofanya serikali pale ni kukimbilia kufunga ...wangeweza wakabadili matumizi yaendane na soko.....tiper ingeweza kuwa kama PETROL RESERVE ....na serikali kukodisha yale matanki kwa waagizaji..badala ya kuacha mali ziharibike...kwa namna yeyote UMUHIMU WA TIPER UTAKUJA PALE TUTAKAPOANZA KUCHIMBA MAFUTA YETU....LAZIMA TUTAHITAJI REFINERY!!!
 
Mimi sikubali kubali vitu kirahisi ndio maana kura yangu hata siku moja hairubuniwi na fisadi. Mashaka alikuja hapa anaomba msamaha kwa kutetea sera za mafisadi baada ya kuona video ya dakika 20 ya travesty za Uwanja wa Fisi. Nikamuuliza, kabla hatujakusamehe tueleze vizuri, hayo mambo ya dakika 20 kwenye ki video ulikuwa hujawahi kuyaona maishani kweli? Nini kweli kimekufanya ugeuke, hakuwa na jibu. Hatujakaa sawa, siku chache baadae, anarudi na sera zile zile za kukejeli upinzani. Kumuonyesha maneno yake ya kuomba msamaha akawa hana la kusema. Kwa hiyo watu kama hao mimi hawanirubuni

Swali langu kwako wewe: Kwa nini hata baada ya kuona watu hawajapenda lugha yako ya 'nyinyi wapumbavu' uliendelea kuwaaambia waliokusihi usisene hivyo kwamba ni "vijana tumedata"? Sasa ni nini kimekufanya ugeuke ghafla? Unaona aibu kwamba watu wamekusamehe na ku engage mjadala wako? Can't hoodwink me!
 
Mimi najua sasa hivi tatizo la ufisadi, ambalo kwa kweli ni kubwa, limekuwa na multiplied effects ikiwemo kuwafanya watu wasiwe objective sana kwenye analysis zao. Kwa hiyo inahitaji roho ya chuma kuweza kusema anything positive about such people as Mkapa, Rostam, etc., maana kwa kufanya hivi huchelewi kuwa labelled mtetezi wa mafisadi!!! Binafsi I am prepared to take this risk by saying something positive about Mkapa's administration. Yes, overall, Mkapa failed us badly but not as badly as Mwinyi did and as Kikwete has done and will do.

Inabidi kwanza tuwe na vigezo fulani au niseme angalau ka-theoretical framework fulani katika kujenga hoja zetu. Binafsi ninatathmini mafanikio au mapungufu ya kiongozi kwa kuangalia mambo mawili, ambayo ni uwezo wake kiutendaji (effectiveness) na maadili yake kama kiongozi (ethical conduct).

Nitaanza effectiveness. Unapopima effectiveness ya kiongozi huanzi kwa kuangalia yale ambayo wewe uliyataka, bali unaangalia yale ambayo kiongozi huyo alisema atafanya na ambayo yalimfanya achaguliwe. Hapa ndipo tatizo linapoanzia, watu wengi wanamtathmini Mkapa kwa kuangalia yale wao waliyoyataka ayafanye badala ya kuangalia yale ambayo yeye aliahidi kuyafanya akiwa madarakani.

Hatua inayofuata inabidi tujikumbushe Mkapa alisema anataka kufanya nini alipoomba urais? Alikuwa na ajenda kubwa nne:

Agenda ya 1 ilikuwa uchumi, bila kujiingiza kwenye academic jargons, katika hili unaweza ku-summarise dira na malengo ya Mkapa in one sentense: kujenga na kuimarisha sekta binafsi, ikiwemo ubinafsishaji wa mashirika ya umma yaliyokuwa vichaka vya majambazi wa fedha za umma. Sasa kama kuna mtu anasema Mkapa hakuuimarisha sector binafsi hiyo ni shauri yake. Matokeo ya zoezi hili la kuimarisha sekta binafsi yanajulikana, ikiwemo kushuka kwa inflation, ukuaji wa uchumi, n.k. Sasa je matokeo ya yote haya yalimsaidia mwananchi wa kawaida ku-improve maisha yake? Highly doutable, lakini hakuna shaka kwamba yaliweka misingi imara ya kuelekea huko in future, ambayo bahati sana utawala wa JK, ama kwa ujinga wa kutokujua cha kufanya au kwa makusudi, wapo busy kuibomoa! Kwa kipengele hiki ninampa Mkapa two resounding pluses with a star ( ++*).

Agenda ya 2 ya Mkapa ilikuwa ni kuweka nidhamu ya matumizi ya mali na fedha ya umma (Discipline in the management of public finances). Waliofanya kazi serikalini na hasa kwenye idara za fedha wanajua alichokifanya Mkapa katika hili. Ni hatua yake hii ya kuweka nidhamu ya matumizi ya fedha ya umma iliyosababisha hao wakubwa anaowaongelea MKJJ warudishe imani na kukubali kutufutia madeni pamoja na kuanza kutukopesha tena baada ya kuacha kwa miaka kadhaa wakati wa utawala wa Mwinyi. Kwa hiyo, Mwanakijiji, yes Nyerere's and Oxfam's rhetorics on this issue helped, but them alone would never convince the international monetary institutions to restore faith in the Tanzanian Government. Kwa hapa ningempa Mkapa two big pluses (++).

Agenda ya 3 ya Mkapa ilikuwa kurudisha heshima ya wafanyakazi wa serikali kiutendaji, kinidhamu na kimapato. Mtakumbuka kwamba wakati wa Mwinyi ilifika mahala ilikuwa aibu kujitambulisha kwamba wewe unafanya kazi serikalini! Yaani ilikuwa ni bora useme mimi ni machinga nina kibanda changu pale stand ya bus kuliko kusema mimi ni mwalimu, karani au afisa wa kitengo fulani serikali. Wakati wa mwinyi ulikuwa ukiingia ofisi za serikali, hata mawizarani, hutamani kurudi tena, sakafu na furniture zimechoka, wafanyakazi walikuwa hoi ile mbaya, wanapiga miayo, wanasinzia na wengine wanauza chai na vitumbua. Mkapa alifanya kazi ya ajabu katika hili hadi ikafika mahala wafanyakazi wa serikali wakawa proud na kazi zao, mishahara ikaongezeka, maofisi ya serikali yakaboreshwa sana-matokea yaka kila mfanyakazi wa serikali atakwambia kwamba tija imeongezeka, na sio siri hata wananchi walianza tena kufurahia huduma za serikali. Matatizo yaliendelea kubaki, lakini kusema kweli yalishughulikiwa kwa asilimia kubwa. On this basis, I would give Mkapa on this one a big plus (+).

Agenda ya 4 ya Mkapa ilikuwa swala zima la kujenga utawala bora na kuimarisha utawala wa sheria-hapa mimi ni mojawapo anayeaamini kwamba likuwa total disaster. Yote hii ni kwa sababu Mkapa aliweka mapenzi makubwa zaidi kwa maendeleo ya CCM kuliko demokrasia ya nchi. Matokeo yake alijikuta akileta ubaguzi wa kutisha kwenye swala la utekelezaji wa sheria-wana CCM walikuwa na impunity ya kutisha wakati wa Mkapa. Vilevile, ni kipindi cha Mkapa ambapo uhuru, kujitegemea na utaalamu (professionalism) ya vyombo vyetu vikubwa vya kulinda na kutekeleza sheria, ikiwemo tume ya uchaguzi na TAKURU vilimomonyolewa, kwa sababu viliamua kufanya kazi kwa minajili ya kuisaidia CCM ibaki madarakani kwa gharama zote. kwa kifupi, Mkapa ni kiongozi conservative aliyeamini kwamba wenye uwezo na haki ya kutawala Tanzania ni CCM tu kwa gharama yeyote ile hata kama wananchi waliwakataa. So, on this one, I would give Mkapa two resounding minuses (- -).

Sasa twende kwenye kipengele cha pili, cha maadili. Hapa tunaangalia mwenendo wa kimaadili wa kiongozi kabla na baada ya kuingia ofisini. Maadili haya ni yale mambo binafsi ambayo kiongozi anapoyafanya analeta madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo, kwa mfano, wizi, matumizi mabaya ya ofisi yake. Technically, hatuwezi kujumuisha yale mambo ambayo kiongozi aliyafanya binafsi ambayo, japokuwa yanaweza yakawa hayapendezi au hayakubalika mbele ya macho ya wengi ya wanajamii, lakini hata madhara kwa mtu mwingine yeyote moja moja au kwa jamii kwa ujumla. Sasa hapa ndio wengi tunakubaliana kwamba Mkapa alitutenda-na ushahidi wenyewe ni ukwali kwamba Mkapa ameibuka na utajiri wa kutisha baada ya kumaliza madaraka yake, utajiri ambao kwa vyovyote vile, hata kama angeshinda tuzo ya Mo Ibrahim, haulingani na mapato yake. Hapo ndio sasa wengi tunakubaliana kwamba Mkapa alituvuruga, ana because of that on this one, I have to give him three disastrous minuses (- - - *)

My verdict: Yes, though hard evidence is yet to be unequivocally unveiled regarding his misconduct in office, there are clear indications which would appear to suggest that Mkapa did behave in a manner that leaves a lot to be desired and that has gravely compromised his ethical standing as a politician and a former statesman. In any case, Mkapa's unethical conduct in office, bad and disgusting as it is, does not undo his performance in other areas of his leadership, especially with regard to being firm and clear in his vision and for taking bold decisions that, more often than not, clearly cost him popularity and public image standing. That is what I call leadership, as opposed to drifting, dithering and manipulation as we constantly see in our chaguo la Mungu!

Kikitila,

Nimejaribu kutafuta manifesto ya CCM iliyotumika katika uchaguzi wa mwaka 1995 na ile ya mwaka 2000 sikuweza kuzipata, ila nina imani kuwa inawezekana wewe ulizisoma na kuainisha hizo ajenda tano zilizoahidiwa na Mkapa kutekelezwa kwa miaka kumi ya utawala wake. Ninataka kuongelea hizo agenda tatu uliyotolea daraja la A na zaidi.

Ajenda 1: Katika kujenga Uchumi, umesema kuwa kazi ya Mkapa ilikuwa ni kuimarisha sekta binafsi kwa kuuza mashirika ya umma, na hapo umempa A-plus kubwa sana. Ingawa ninakubaliana nawe kuwa kweli Mkapa alifanikiwa kwa kuuza mashirika ya umma, nataka kukumbusha kuwa ukimpa mtu yeyote yule duka lenye bidhaa na kumwambia kuwa aziuze, hatashindwa kufanya hivyo. Utampima ufanisi wake kama atauza kwa hasara au atauza kwa faida. Kama atauza kwa hasara akamaliza bidhaa zote dukani, huwezi kusema kuwa amefanikiwa; Mkapa aliuza kwa hasara. Kuhusu uimarishaji wa sekta binafsi, sijui Mkapa aliweka sera gani iliyopromote sekta binafsi. Ninachofahamu ni kuwa aliuza kila kitu kwa watu wa nje, wakati watu binafsi wa ndani walikuwa na ugumu sana wa kununua mashirika hayo, hata yale ambayo yalikuwa yanajiendesha kwa faida. Kuna kumbukumbuku kuwa Bwana Mengi alinyimwa kununua Kilimanjaro Hotel kwa sababu ambayo baadaye ilikuwa pindishwa pindishwa ili kufica uchi wa Mzee. Watanzania waliofanikiwa kununua mashirika hayo ama ni akina Mzindakaya au akina Mkapa, wengine wote walikuwa ni wa-South Africa na jamii ya aina hiyo. Mkapa hakuweka utaratibu wowote wa kuwahamasisha raia binafsi kujiunga na sekta hiyo, badala yake alivutia watu wa afrika ya kusini tu. Sidhani kama kweli hatua ya namna hiyo ni ya kujivunia na kumpa mtu A-plus plus.

Ajenda ya 2: Umesema kuwa Mkapa aliweka nidhamu ya matumizi ya mali na fedha ya umma, bila kutambua kuwa hiyo haikuwa initiative yake bali aliikuta kutokana na shinikizo lililosababishwa na misamaha ya kodi ya Prof. Malima, na ilikuwa imeanza kutekelezwa na serikali ya Mwinyi wakati Kikwete akiwa waziri wa fedha. Utakumbuka katikati ya mwaka 1995, nadhani wakati wa sikukuu ya wafanyakazi, raisi Mwinyi katika hotuba yake alisema "ndugu zanguni, ombi lenu ni jema lakini wakati huu siyo mwafaka kwa vile Jakaya mkali." Pamoja na hayo vile vile hutendi haki unopatenganisha matumizi ya hela za kodi na matumizi ya raslimali nyingine za umma, kwani ingawa kweli Mkapa alikuwa na usimamizi mzuri sana wa fedha za kodi zilizokusanywa na TRA, hakusimamia raslimali nyingine za nchi kama sote tunavyofahamu.

Ajenda ya 3: Kuhusiana na kurudisha heshima ya mfanya kazi ni kitendwaili kweli kweli kwani inategema unazungumzia mfanya kazi wa aina gani na Mkapa alirudisha heshima hiyo kwa namna gani. Ninachofahamu ni kwamba, wakati wa utawala wa Mwinyi, kulikuwa na loopholes nyingi sana za kupata hela kwa njia za mkatomkato hasa kutokana na taxation system iliyokuwa legelege. Kwa viyo kijana wa mtaani alikuwa akiweza kutumia masaa mawili tu pale long room na kujipatia mamilioni ya shilingi wakati mfanyakazi wa serikali akiosta mwezi mzima kwa shilingi alfu hamsini tu. Hela zilizokuwa zinapatika kiharamu namna hiyo zilikuwa zinasambaa kiharamu vivyo hivyo nchi nzima na kusababisha wafanyazki waonekane wanapoteza muda wao. Baada ya kuzibwa kwa loopholes hizo za fedha za haramu (jambo lilioanza mwishoini mwa utawala wa Mwinyi), vijana wa kijiweni wakawa hawana njia za mkato na ndipo kazi ikaanza kuthaminiwa tena. Pamoja na kuwa hilo lilikuwa jambo jema, ni byproduct ya jambo jingine kabisa ambalo siwezi kusema kuwa eti ilikuwa ni juhudi ya Mkapa kuboresha maisha ya wafanyakazi na kurudisha heshima yao. Chini ya utawala wa Mkapa, HDI ya Tanzania iliendelea kudorola ambapo hadi wakati anaondoka madarakani nchi ilikuwa ya nane kwa umaskini duniani.

Mambo yote mema yanayohusishwa na Mkapa yalikuwa by default, si kwa initiatives zake mwenyewe. Mambo yaliyotokana na initiatives zake yote yalikuwa ugolo tu kwa nchi. Ingawa ni kweli kuwa Mkapa alikuwa ni bora kuliko Mwinyi na Kikwete, siwezi kusema kuwa Mkapa alifanya mambo mengi mazuri kwa nchi hii. Hakuna signature issue yoyote ambayo ninaiona kama ilikuwa ni matokeo ya kuwa na rais Mkapa, labda BOT Twin Tower (kwi!!! kwi!!! kwi!!!)
 
apologies accepted!
suala la Mkapa msafi, hiyo ni wazo lako na since una uhuru wa kusema unachotaka kusema, then okay! yawezekana u-Mkapa mwenyewe au ndugu wa karibu wa Mkapa huwezi sema ni mchafu hata kama ananuka.
Ila utambue kuwa uko kwenye wrong direction! na ninapokea pia apology ya pili kuhusu mkapa, maana vey soon utakiri kuwa mkapa ni Mchafu, (kama ni mtu wa haki, anyway)
 
nakushukuru ndugu yangu mlima sio kichuguu tena.
mahali alipoweza kufanya vizuri nkapa ni pale alipo simamiwa na waangalizi wa kimataifa au mwl.
mfano mambo ya kodi na ubinafsishaji ni sera za donors etc, walio mwambia usipofanya dash and dash no msamaha wa mkopo au msaada. alipoachiwa yeye kutekeleza kwa akili yake or his personal intiative alikuwa bure kabsa kabsa, kama hiyo twin tower, kiwira radar, ndege ya raisi , uteuzi usio na mikono wala miguu, bali kutimiza kiu yake ya pesa. sasa kwa asio ona hilo sijui tuseme nini.
nakumbuka kuna hadithi ya mkuu moja wa majeshi aliye weza kujenge sababu vijana walikuwa wakimpelekea pololo au kumjenge, while at the same time fedha nyingi alikuwa na tumia kwa vimwana, sasa vbasing on that scenerio huwezi kusema kwamba huyu mtu alikuwa anaakili kwa kuwa kajenga, bali amejenga by default. na vivyo vivyo kwa nkapa alipo fanikiwa si kwa juhudi zake au akili yake, bali circumstance au nguvu za ziada au za nje ndio zilizo mwezesha kufanya hivyo.
 
Phillemon mikael,
Mkuu umesema mengi sana kuhusiana na TIPPER na kuegemeza kufa kwake na soko!...
Nimejaribu kutafuta Oil refinery ambazoi zimekufa kwa sababu kama uilizotoa sikupata.. naomba nakala hata moja inayofanana na hiyo ya TIPPER. Kisha naomba unipe hizo dataz ambazo zinasema Mombasa refinery ilikufa pia kwa sababu naelewa kwa miaka mingi imekuwa Oil refenery pekee East Africa baada ya kifo cha TIPPER..
 
BongoTZ,

U kinda smart bob, yaani baada ya kutuweka kidole cha nyuma kisha unasema samahani hukukusudia!...Of all the places... kwii kwii kwii! duh kazi kweli mchezo wa Pwani..
Halafu basi watu wamekusamehe vile vile... duh! sisi wapole kweli..Ama kweli ndio maana sii kiongozi mbaya!
 
BongoTZ,

Let me start by reminding you of exactly what you said. I quote:

You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.
Foolish people.
Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!
Be smart people
.

And then you added something like this, I quote:

I suppose baadhi yenu (Mwanakijii especially) mmekasirishwa sana kwa mimi kutumia neno 'foolish." You don't have to. "Foolish person" kwa definition yangu ni " someone who is easily tricked". Nasema "easily ticked," coz Kikwete's inner circle wame-manufacture nyingi ya hizi kashfa kuhusu mzee Ben, kisha wakazi-leak kwenye press, bloggers nao wakazidakia, huo moto hauzimiki. The daunting quesion is: kwanini watu hawataki ku-pose na kujiuliza, "wait a minute, kwanini Kikwete anaacha hizi kashfa ziende unaswered kama Mkapa ni fisadi kweli?"

You never stopped there but went on:

I suppose humu vijana wengi wamedata kwelikweli. Nevertheless, "If you judge, investigate." Acheni tabia ya kurukia mambo msiyoyajua.

And then finally to drive the last nail in a coffin you agreed with Mkamap thus:

"Mkapa is the best president.Ila kosa lake tu nikuongoza Taifa bovu kama Tanzania." I couldn't agree more with you (Mkamap).

Come on be serious for a moment BongoTZ, you cant eat your cake and have it. By continuing to defend Mkapa you are just rubbing more salt into our injuries. I will accept your apology half heartedly until you come up with the real reason why you think kutoka kapa is a good thing. Kwa Mkapa tumetoka kapa. Period.
 
Phillemon mikael,
Mkuu umesema mengi sana kuhusiana na TIPPER na kuegemeza kufa kwake na soko!...
Nimejaribu kutafuta Oil refinery ambazoi zimekufa kwa sababu kama uilizotoa sikupata.. naomba nakala hata moja inayofanana na hiyo ya TIPPER. Kisha naomba unipe hizo dataz ambazo zinasema Mombasa refinery ilikufa pia kwa sababu naelewa kwa miaka mingi imekuwa Oil refenery pekee East Africa baada ya kifo cha TIPPER..

mkuu mkandara,

...ni wazi kuwa nchi nyingi za ukanda huu hazifanyi tena refinery siku hizi...tofauti ya MOMBASA REFINERY na TIPER ni kuwa pamoja na kuwa zote biashara yake ilidorora kwa wakati mmoja...wenzetu wa kenya hawajafunga ya kwao pamoja na kuwa haifanyi faida ..wamebaki nayo...wakiamini kuwa in future mambo yatabadilika[ie mafuta bado yanatafutwa ukanda huu..ie siku uganda wakiaza kuchimba mafuta inaweza kuwa rahisi kusafirisha mafuta kwa bomba hadi mombasa yakasafishwa na kuuzwa nje-na hilo bomba la mafuta kwenda kisumu linajengwa....].............like wise pia mimi nilikuwa na maoni kama haya kwa tiper yetu ....we could subsdise it au kuitumia in other commercial feasible option wakati tunangojea hali ya mafuta iboreke....na as you know prospects for oil are very positives here...i have reliable informations of these findings......kitendo cha tiper kufungwa kimesababisha mitambo iharibike na tunakosa wataalamu ambao wameshastaafishwa.....hata kuja kukifufufa itakuwa kuanza moja...na ni wazi kuwa bado we need refinery.....ili tutakaposhimba mafuta ..tuyauze kwa bei nzuri....
 
PM.. sidhani kama sisi tunafikiri mbali sana. Upande mmoja tunatafuta mafuta kwa kiasi kikubwa na dalili kuwa yapo ni kubwa tu, lakini hatujaanza kutengeneza miundo mbinu ya kitu kama hicho at least kwa kulingana na data ambazo zunazo hadi hivi sasa. Tunaishi in the now sana kiasi kwamba mambo ya mwakani yatasumbukiwa mwakani.
 
Mwanakijiji huu ni uongo "Ni yeye aliyemteua Mwanasheria Mkuu mbovu kabisa katika historia ya Tanzania huru"

Chenge aliteuliwa na Mwinyi akichukua nafasi ya Jaji Damian Lubuva ambaye aliwekwa pale baada ya Julius K.Nyerere na Mwinyi kumvika Sinde Warioba Uwaziri wa mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais.

Udhaifu wa Mkapa ni matunda ya CCM na Mafanikio ya CCM 1995-05 ni matunda ya kuthubutu kwa Mkapa kuleta mageuzi ya kweli ktk uchumi na vita dhidi ya umaskini.

Hakuna sheria inayomkataza rais kuwa mjasiliamali na vivyo hivyo kutafuta mianya ya kujiendeleza kiuchumi.

Tutamuhukumu Benjamin Mkapa kama tu alijitwalia amali za umma kwa kwa udanganyifu.

Kama Kiwira iliuzwa kwa udanganyifu sheria ichukue mkondo lakini hatuko tayari kuona watu wazima wakihuburi haki na sheria huku wakihimiza wananchi kuwatukana wenzi wao kwa tuhuma ambazo hazina hadhi ktk sheria.

Mimi nasisitiza, kumtuhumu mtu na kumdharirisha mtu pasipo kufuata taratibu za sheria kwa miaka 3 mfululizo huu ni uhuni.
 
BWM ni mzuri sana katika kujenga hoja, kwa nini asizungumzie hizi tuhuma zinazomhusu kwa uwazi na ukweli?. otherwise anajiharibia yeye mwenyewe kwa kukaa kimya, maana akikaa kimya kizazi cha sasa na vijavyo havitamuelewa vyema.au ameamua kuja kuandika kitabu?.
 
Mzee Mwanakijiji, you're a man of fine intelligence, but I must respectively disagree with you on this matter.

You know it's relatively easy for critcs who don't like Mkapa to say anything negative about him, but impossible to say his positive contribution to our nation.

It seems obvious to me that all these trash talks about Mkapa is a well-orchestrated campain by Kikwete's team ( which you guys have also bought in) to just kick dirty to Mkapa's eyes.

It's a wishful thinking to think that Mkapa alone (in 10 yrs) could have undone the wrongs and errors of colonial institutions, ujamaa policies, and Mwinyi's economy, stupid.

Now, it doesn't matter, though, how much you guys will continue to trash mzee Ben; but the truth of matter is, he is one of the finest presidents that our country have ever produced.

Tunakubali yote mazuri aliyoyafanya, na huo ulikuwa wajibu wake, lakini mabaya aliyoyafanya yalijawa na kiburi, ubinafsi na makusudi ambayo ni matusi kwa watanzania. Ben hakuwa Raisi safi
 
Mkapa Killed the Tanzanian economy. why ? Any country if it want to ruin its economy import Oil.

How can you kill something that is/was already dead? Tanzania was a "container" economy long before the days of the fat one and in retrospect our figures in days before Mkapa took over didn't make the most pleasant of readings (a feature prevalent since the early 1907s if you want to be pedantic about it).

Tanzania has always been an oil importing economy and the increases in oil imports were inevitable as the economy expanded. a fairly weak argument to make if you ask me.

Mkapa did as the same what is happening in the world economy now speculators are shutting down the oil refineries ili waweze kupunguza supply while the demand is going up, and that is the main resorn pushing up the oil price.

In economics there is something called "on one hand", and "On the other hand". Two viewpoints used to explain the same thing. Whilst I am not dismissing your argument about the "shutting down of oil refineries", but it a fairly weak position in which to make your point.I suggest you revisit your argument of supply and demand again!

Mkapa na uchu wake wa fedha, on the expense ya wananchi he killed TIPA, why did he allow the TIPA to die, this was because he wanted to open doors to his allies company like OIL COM where he has financial intrest.

This action pushed the fuel bill to go up 50% by importing refined oil while tulipokuwa tuna refine wenyewe price was less than 50% sasa kama wewe nimchumi na unakili timamu hebu niambie , Taifalipoteza kiazi gani.

Unafahamu capacity ya TIPPER at the time ilikuwa ni kiasi gani? Je TIPPER on its own would it have been able to satisfy the nation's energy demands?
Bei ya vitu ilikuwa ndogo kwa sababu tulikuwa hatuna mfumo unaoeleweka wa ukusanyaji wa mapato ya serikali and a result serikali ilikuwa haina mapato ya kutosha ya kuendesha shughuli zake. Just a little anecdote for you, real public sector wages in Tanzania fell throughout the 1980s and 1990s when compared to those in 1969. In the 90s, a typical Dar based average public sector employee's take-home wage could only service 40% of his/her monthly consumption needs.

Another reason why the price of fuel went up was that with dwindling govt's revenues and a disorientated economy, one of the ways of beefing up the public coffers is through taxation. The level of sophistication ya uchumi wetu
at the time and even until now created led to problems of moral hazard and adverse selection when constructing a tax base, leading to a very narrow one and hence the high tax rates.

Mfano Uchumi wa kenya uko juu kuliko wa Tanzania kwasbabu hawakufunga refinery yao ya mombasa, Hivyo Fuel bill ya kenya is lower than ours and thats why the can afford to pay 96 % of their budget from their economy, Ila mkapa na ulimbuken wake akauza TIPA na kuendelea kuchukua hela za wahiasni ku lipia budget how stuip is that[/SIZE]

Don't even go there. Different countries and slightly different economic structures. Uchumi wa Kenya uko juu sana kwa sababu ya kilimo cha kisasa (not your Western 21st century one but something close to a typical South Asian 1980s-1990s one) pamoja na medium scale industries. Refinery ya Mombasa whilst inasaidia lakini mchango wake si mkubwa kama unavyofikiria.Bei ya mafuta Kenya is very very high.

All in all, whilst I detest and hold Mkapa accountable for some of the ills still engulfing our motherland, it is unfair to summarily dismiss his 10 years as a complete waste of time.He did get somethings rights.

Word to the wise, don't let anger cloud your judgement.
 
hoja imetulia cha msingi tuijadili objectively. tatizo wabongo tunapenda simple mind kujustify hata mambo ya msingi. Mzee Ben ni kiongozi pekee katika taifa hili aliyejenga uchumi unaoweza kusimama duniani kwa mazingira ya kishindani. Kafanya mengi mnoo ambayo nina hofu kwa sasa yanapotea kiholela kutokana na USANIIIIII. Ni kosa kubwa na garama yake tutailipa wenyewe kwa kuendekeza usaniii. He is a visionary leader of his TIME. Mabadiliko ya sera za kiuchumi alizosimamia ni alama ya picha ya tz ya sasa. misingi imara ya ukusanyaji wa kodi, miundo mbinu(ushahidi upo tembea nchini uone), mabadiliko ya utumishi wa umma nk. Amefanya mengi mpaka kwa muda aliokaa magogoni ameleta heshima kimataifa. Uwezo wake binafsi KIAKILI ni ushahidi tosha(fuatilia maendeleo yake shuleni), kujenga na kutetea hoja kitaalamu baada ya mwalimu hakuna kama yeye, cheap popularity HATAKI, umbea na mtandao hapendi.

Nchi yenye uchumi dhaifu kama yetu inahitaji watu makini kuusimamia na sio porojo. tuko kundi la nchi maskini si kwa sababu hatuna rasilimali, tatizo WATU.
kwa sasa tuamke tujue hawa viongozi hatuwapi nafasi kupiga picha na watu wa magharibi na kupongezwa kifalaaa bali kufikiri jinsi ya kuongoza kwa mafanikio.

Mzee Ben historia itamhukumu. tunachojifunza kutokana na historia ni kutokujifunza chochote kutokana nayo...
Aliimarisha uchumi na sio blah blah. gafla wasanii mjini wakapotea, watumishi wakaheshimika. TUKAZE ALIPOACHIAAAAA.
UWANJA HUO KWA MANENO YAKE....NITAWAACHIA UWANJA WA KISASA. PITA CHANGOMBE UJIONEE. BONGO BIASHARA GANI NDANI YA DK 90...MAPATO MILION 600..
TFF WANANGAAAA, SOKA ITABIDI LIKUE HAKUNA UJANJA WALA SIO USANIII WA WACHACHE KICHOCHEO KIPOOOOOO.
 
Come on be serious for a moment BongoTZ, you cant eat your cake and have it. By continuing to defend Mkapa you are just rubbing more salt into our injuries. I will accept your apology half heartedly until you come up with the real reason why you think kutoka kapa is a good thing. Kwa Mkapa tumetoka kapa. Period.[/QUOTE]

And your point is...?
 
BongoTZ,

U kinda smart bob, yaani baada ya kutuweka kidole cha nyuma kisha unasema samahani hukukusudia!...Of all the places... kwii kwii kwii! duh kazi kweli mchezo wa Pwani..
Halafu basi watu wamekusamehe vile vile... duh! sisi wapole kweli..Ama kweli ndio maana sii kiongozi mbaya!

Nadhani huyu BongoTz yuko mbele yetu hatua kumi na zaidi. Kwasababu inaonyesha wazi kwamba kuna game anaicheza hapa ulingoni ambayo sidhani kama kuna mtu ameishtukia so far.
 
Tunashukuru ka kutambua kosa na kuomba radhi. mi nimekusamehe.

Nami pia nakusamehe sina jinsi. Ila kwa "Mkapa ni msafi aliyejaa uchafu!!!!!"

kwa mkapa uchafu umezidi usafi kwahiyo ni MCHAFU....aje nae atutake radhi na arudishe mali za wananchi.
 
Ni kitu gani ambacho Mkapa alikifanya na kinahitaji kusifika ambacho kilikuwa nje ya majadiliano ya IMF, WB au Paris Club na wafadhili wengine? Ni hatua gani alizichukua kuliinua Taifa na kulihamasisha kujitegemea nje ya Wafadhili?

Ni mambo gani ambayo alikuwa na uwezo wa kuyazuia lakini hakuyazuia?
 
Yamekwisha lakini jitahidi kumleta mzee Nkapa nae aombe msamaha kwa jamii akikataa mlete hata hapa JF sio mbaya sana.
 
Back
Top Bottom