Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa alifanya biashara kama mjasiriamali yoyote yule, hakuna tatizo na hilo jamani.

Sometimes demokrasia ina matatizo yake, Masaka haya unayoyaongea hapa ni matunda ya demokrasia haya JF. Naamini unaitumia mikono yako na vidole vyako vyema kama demokrasia hapa JF inavyokuruhusu. Inabidi uanzishe blog nyingine itakayokuwa na link na gazeti la Mzalendo au Uhuru. Naamini utawawezesha kupata traffic kibao kwenye sites zao especially watu ambao walishindwa ku-vomit yale MAJI ya KIJANI
 
kpleo.jpg

Huu Ni Ushari Wakuuuu
 
Tatizo letu wabongo nikushindwa kuelewa ukweli, hivi waweza mfananisha Ben na Julius? kwa maisha ya kiongozi Mwadilifu! kama hapana kwa nini tusiseme Ben Fisadi no matter ur CCM or Not?
 
Last edited:
Huyu naye ni another looser kama Kada .Yaani guys you waste your time kumkjibu huyu kula kulala ? NIlisha waambia mada za Kada , Masaka na the likes ziacheni zinakufa zenyewe hawa ni vichaa ambao mishipa ya aibu hawana kama vile Mkapa na wengine wasivyo kuwa nayo .
 
Huyu naye ni another looser kama Kada .Yaani guys you waste your time kumkjibu huyu kula kulala ? NIlisha waambia mada za Kada , Masaka na the likes ziacheni zinakufa zenyewe hawa ni vichaa ambao mishipa ya aibu hawana kama vile Mkapa na wengine wasivyo kuwa nayo .

ni kweli kada mimi sina mshipa wa aibu na nilishasema hivyo before na ndio maana huwa nawatolea uvivu hata pale mnaposhabikia upuuzi !

sasa lunyungu now its official ! nimesikia upuuzi wako humu frequently na nilikuwa nakuchunia nilidhani utatulia, sasa itabidi uchezee tu filimbi maana naona umeipuliza vya kutosha !

Ignoring kada wont solve your problems, wont make me go quite, wont starve me, yaani hivyo ni failed prescritption ! Nitasema what i think is right at any given time, AND THEREFORE MY MESSAGE WILL BE SENT, mjibu msijibu, ujumbe mtakuwa mmeshaupata ! huo ni ushauri tu ambao nimeona nikupe wewe maskini wa mawazo !

watu walishaanza kukuignore na sasa unatafuta comeback kwa kumciticise kada, ovyo sana wewe !
 
Nyiye waandishi, mwacheni babangu
2008-06-13 09:28:35
Na Godfrey Monyo


Mtoto wa Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, Steven Mkapa, amevishutumu vyombo vya habari kwa kumwandika vibaya baba yake kuwa ni fisadi.

Alisema kuwa kinachofanywa sasa na vyombo hivyo ni kumshushia baba yake heshima na utu alionao katika jamii.

Mtoto huyo ambaye alijigamba kuwa kinachotafutwa na waandishi wa habari katu hakiwezi kupatikana kwa kuwa uelewa wao ni mdogo.

Aidha, Bw. Steven, aliwashangaa waandishi hao pamoja na watu wengine wanavyopoteza muda wao kukaa na kumjadili baba yake badala ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Nipashe wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni inayojishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya maji ya ERV East Africa.

Bw. Mkapa, anadaiwa kufanya biashara akiwa Ikulu ambapo mwaka 1999 ilianzisha kampuni iliyoitwa ANBEM.

Aidha, anadaiwa kuchukua mkopo wa dola za Marekani 500,000 katika Benki ya Biashara (NBC) bila ya kuweka dhamana yoyote.

Pia Bw. Mkapa maarufu kama ``Mr.Clean`` anadaiwa kununua mgodi wa Kiwira Coal and Power Limited kwa bei ya ``kutupa`` ya Sh. milioni 70 wakati mgodi huo unathamani ya Shilingi bilioni nne.

Aidha, anadaiwa kumiliki baadhi ya majumba ya kifahari sehemu mbalimbali hapa nchini sambamba na kumiliki ekari 600 ya miwa huko Mtibwa mkoani Morogoro.

Aidha, kiongozi huyo hajawahi kukanusha taarifa za kuwa yeye ni mshiriki wa Benk M.

Bw. Steven alionekana wazi kuwa na ghadabu na waandishi wa habari kutokana na kile alichodai kuwa wanatumiwa na watu wachache kumchafua baba yake.

Alisema kuwa waandishi hao wamekuwa wakipewa fedha kidogo na kutumia muda mwigi kuhangaika na baba yake, jambo ambalo alisema katu hawataweza kupata kitu.

``Najua na wewe ni miongoni mwao kati ya wale wanaotumiwa kumchafua baba lakini hamtaweza kitu hizi ni namba zingine,`` alisema Bw. Steve.

Mtoto huyo wa Mkapa ambaye anajulikana zaidi kwa jina la ``Merinyo`` alisisitiza kuwa maneno yake yanatoka moyoni na anazungumza kwa kujiamini bila ya kuogopa kitu na hivyo wahusika wapatiwe taarifa ili watafute kazi zingine za kufanya.

``Wewe unakuja kunichora hapa maswali mengi ... Nikikuuliza mimi unanijibu kwa kuniuliza swali maana yake nini? kama umekuja kunijulia hali mzee anaingia vipi kwenye mazungumzo yetu?`` Alihoji Merinyo.

Merinyo ambaye pia alionekana kukerwa sana na madai kwamba baba yake ni mimiliki wa mgodi wa Kiwira alihoji kwa nini habari za Kiwira haziishi katika vyombo vya habari.

Hata hivyo, alipolulizwa kwa sasa anajishulisha na kazi gani ambayo inampatia kipato alisema kwa hasira kuwa anafanya kazi katika mgodi wa Kiwira.

``Najua unataka niseme nini... Nenda kaseme, nafanya kazi Kiwira... Kwa sababu nadhani nyiye bila Kiwira na Mkapa hamna cha kuandika,`` alisema Merinyo huku akinyanyua glasi yake tayari kwa kunywa.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Mark Bomani, ambaye alikuwa mgeni rasmi aliishauri serikali kuwa wepesi kukubali ushauri unaotolewa na watalamu.

Jaji huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kiwanda cha bia cha Serengeti ambayo ndio ilikuwa moja ya wadhamini wa hafla hiyo, alisema yapo mambo mengi ambayo kama serikali ikikubali ushauri yataweza kuiletea faida kubwa nchi na hivyo kuongeza pato la taifa.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kutumia vifaa vinavyopendekezwa katika kutoa huduma za maji kama vile vipuri vya kusambazia maji.

``Yapo maji mengi yanapotea njiani lakini kama kungekuwa na vifaa imara vinavyotumika yasingepotea kiholela,`` alisema Jaji Bomani.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ERV East Africa Bw. Phillemon Ntahilaja, alisema kuwa wanakusudia kuwapatia mafunzo zaidi wataalamu wao.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuweza kuboresha zaidi huduma zao na kwa watanzania kwa ujumla.

SOURCE: Nipashe
 
Ccm wilaya ya moshi mjini hususani jimbo la vunjo lina mpasuko mkubwa sana wa kisiasa kwamakundi makubwa mawili ambapo kundi moja dogo na lisilo na ushawishi likijaribu kumtetea Mh Aloyce Kimaro dhidi ya kauli yake tata kuwa Ben Mkapa ashtakiwe,na kundi jingine kubwa na linaloungwa mkono na madiwani na wananchi likisema ni ukosefu wa adabu kwa chama na kwa shemeji yao Mkapa,hivyo wanadai mipango ya kumuondoa Kimaro ianze mapema.
Wafanyabiashara wakubwa wameungana na madiwani wote kwa ajili ya kumuondoa huyu bwana ambaye ni mlopokaji mkubwa,kuonyesha hali ilivyo mbaya ilifika mahali wiki aliopita kuliitishwa mkutano wa chama ambapo bwana Kimaro aliomba amani iwepo kwa muda ili aweze kutekeleza ilani japo kwa muda na kuomba msamaha wale aliowakwaza kwa namna moja au nyangine.
Baada yaujio wa katibu mpya wa mkoa mama mauldine Castico imebidi kuchukua hatua za haraka kwa kuwahamisha kituo cha kazi Katibu wa Chama wa wilaya Mama Mpambalyoto na msaidizi wake Ndg Chale,jambo ambalo kwa uchunguzi wa harakaharaka haliwezi kumsaidia Kimaro kupata adhabu ya wapiga kura wake.
 
Last edited:
Sio Jambo La Ajabu Kwani Kama Ambavyo Sita Atapopolewa Ndivyo Yeye Atapopolewa,amedandia Mambo Hasiyoyaweza....lazima Atolewe Tena Kwa Aibu.
 
Mtoto huyo wa Mkapa ambaye anajulikana zaidi kwa jina la ``Merinyo``


Wakuu wa Nipashe, kwenye hili mmmekosea sana hili MERINYO ni jina la mdogo wake Steve, anayeitwa Nico, ambalo alipewa na Bibi yake mzaa baba, akiwa mdogo sana, ni marekebisho kidogo, ngoja nimalizie article kwanza.
 
unapoema mama butiku anakusudia mama yake butiku au mkewe maana sisi kiswahili chetu kina mambo !!!
 
Kwanini asiwe na kiburi wakati tumewaruhusu kutuibia bila kuwafikisha mahakamani?

Huku kwa wenzetu huwezi kukuta mtoto au ndugu ya jambazi anamtetea jambazi waziwazi, lakini kwa TZ naona kamtindo kanaanza kujengeka kwa ndugu za mafisadi
kutetea ndugu zao hadharani wanapoandamwa.

Kwasababu utetezi huo hauwezi kuwa na madhara kwao siku za mbeleni basi kila mtu ni kutetea tu hata pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha matendo mabaya.

Huyu Steve ni mropokaji siku nyingi na hata kule Tanzanet alikuwa anaropoka sana mpaka wajuaji walivyomkabili kwa hoja.

Haya tunayoyandika hapa kuhusu mafisadi yanawauma, tuendelee tu kuwaandika, hata kama tutashindwa kuwapeleka jela lakini hawatakula hizo pesa kwa raha zote.
 
Anachukia nini hapo?kwani si kweli baba yake si fisadi?mbona yeye mwenyewe hajakanusha?asituzingue mbona hata yeye ana vielement vya kifisadi tutamlipua tu mpaka aone aibu hata kutembea barabarani na tutaendelea kumzomea tu.
 
Nadhani dogo anaingia katika maeneo yasiyomuhusu.Watanzania wana haki ya kuhoji once wanaona mambo ya hovyo yanafanyika babake alipewa uraisi na watanzania na si kuwa alizaliwa nao so kama kujitetea aache babake ajitetee mwenyewe ye dogo aendelee na issue zake...

Nadhani anataka tujue kuwa naye yupo??? atulie asilete za kuleta katika maisha ya watu...
 
huyo dogo aache kelele amlete baba yake ajibu tuhuma moja baada ya nyingine mbele ya waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla ndio tutamwelewa la sivyo tutamwandama mpaka kaburini. na si yeye tu hata maswahiba wake wakina mramba na wengineo tutawasakama mpaka kieleweke.
 
kumbe castico yuko huko ? huyu si ndo yule alikuwepo kiswandui zanzibar au mwengine ?


na kama ndie ile kesi yake ya uraia imefikia wapi ?
 
Back
Top Bottom