Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Does Tanzania have conflict of interest laws? maana kama zipo basi viongozi wetu ni very daring, au kama hazipo, basi hatuna la kuongea mpaka sheria na kanuni ziwekwe.

Nashindwa kuelewa ni vipi viongozi watakosa woga na kujifanyia mambo kiholela huku wanajua "kuna" sheria za kuwawajibisha na hata kiuwafunga?

Can we demand that the conflict of interest laws, leadership, ethics and moral conduct laws to be written and clearly state what a persono in position of power could and could not do?
 
Pili sijaona mahala kua hilo shamba kalinunua kutoka kwa mtu binafsi ama lilibinafisishwa kutoka serikalini .Na hata hivyo kama alinunua kwa kufuata sheria huo mimi nafikiri ni moja ya njia ktk uwazi ,kinachoshawishika hapa ni kua kwanini alipolinunua shamba hilo hakuenda ktk vyombo vya habari na kuwatanganzia watanzania sasa anamiliki shamba Fair point

Is there a reason or a law that obligates a President to declare to the Radio, nimenunua Baiskeli ya Mchina?

I woud have thought that this was done on annual assets and debts declaration form but not through Matangazo ya Gazeti au hotuba.
 
``Hata kama wanasema amekosea amevunja miiko, ni vugumu kumuondoa kwenye familia, kwa vile hata akiondoka, hata waliosalia wengine huenda wana madhambi kibao,``alisema. QUOTE]

Nimesema tena na kurudia.

Mkapa hakuvunja sheria yeyote ya maadili ya uongozi. Anashindwa kujitetea tu. Na siju Mawakili wake wanamshauri nini.

Alitekeleza mambo mawili muhimu wakati wake:

1. Falsafa ya RUKSA aliyoanzisha Raisi mstaafu Mwinyi. falasa iliyokuwa imeshika hatamu na kasi.

2. Alitekeleza kwa vitendo Azimio la Zanzibar lilofuta Azimio la Arusha.


Mwenye azimio la zanzibar aliweke hapa uone..kuwa Mkapa was was just loyal to it. Ajitokeze ajitetee. Someni azimio la zanzibar Kwa makini Mkapa hakuwa na Tatizo.

Mkapa achukue ushauri huu wa bure if he want.

Ajitokeze na akorome kikamilifu kuwa hakuvunja sheria yeyote ila ALIKWENDA NA WAKATI NA MAAZIMIO YAKE...alitekeleza sera na maazimio muhimu ya wakati wake. Leo watu wanazomea kwa kutumia azimo la arusha wakati waliweka azimio la zanzabar. Mkapa(Clearn Man) dont you see what confused you. Come foward and say it all!

Mkapa njoo onyesha past history zako na UADILIFU wako uliopelekea mpaka Baba wa taifa akakubali, na onyesha kuwa usingeweza kubadilika over night kama sio kwa misingi hiyo miwili hapo juu. Ulishawishiwa na kushawishika kwa maazimio na falsafa hizo nilizotoa hapo juu. Cha kuongelewa ni azimio la zanzibar na clear definition ya RUKSA. RUKSA ilikuwa ina maana gani hasa.

Aonyeshe kuwa ilitokea akakubalina na azimio la zanzibar na mwenendo wa nchi wa wakati ule ambao ilikuwa unawahimiza viongozi wastaafu KUCHANGAMKA na kuwa wajasiriamali ..azimio la zanzibar lilielekeza hivyo na halikukatza mtu kufanya biashra ikulu. Mambo ya miiko ya uongozi na kufanya bishara ikulu ..ilikuw ani azmio la arusha...ambalo hatunalo. AU lipo?

Mkapa jitokeze jipange kwa misingi, mwelekeo wa nchi ulikuwa umebadilika kabisa wakati ule na mtu yeyote angeweza kufanya kama ulivyofanya. Na wengi walifanya.

Cha kuongelewa ni Misingi ya Maazimio yote mawaili

Azimio la arusha na Azimio la zanzibar na sio Mkapa.

MKapa umenisikia?

Nataka majibu.
 
sheria au taratibu mbovu haziwezi kuwa kinga dhidi ya wizi wa mkapa.
 
Kwa kutumia vigezo alivyovisema bwana Makongoro, kwa hiyo anataka kutueleza kwamba ukoo wao unaweza kumkaribisha kwa mikono yote miwili "Mzee wa Vijisenti" ukooni pamoja na makashfa yote aliyonayo? Nasikitika kusema kwamba nafikiri huyu mheshimiwa ana uzembe wa kufikiri. It is quite immoral to spin words to this extent!!!. Anataka evidence ipi ili a-prove kwamba huyu jamaa hana maskandali yote haya?

I hope kuna wenye busara ukooni ambao wata-come up na kumfukuza huyu mjasirimali wa Ikulu.
 
sheria au taratibu mbovu haziwezi kuwa kinga dhidi ya wizi wa mkapa.

Nina maana mpka sasa zipo. Kama Mkapa anafungwa nazo..Zenyewe zinaachwa tu?

Waliozintunga hizo mbovu waachwe wachekelee?

Nina maana ni wakati muafaka sasa kuongelewa Uharibifu uliofanywa na azimio la zanzar kwa hii nchi.

Azimo la zanzibar lilichafua viogozi wengi..Mkapa ni mmmoj TU HALIWEZI KUCHWA BILA KUJADILI KWA KINA NA MAPANA.
 
Nina maana mpka sasa zipo. Kama Mkapa anafungwa nazo..Zenyewe zinaachwa tu?

Waliozintunga hizo mbovu waachwe wachekelee?

Nina maana ni wakati muafaka sasa kuongelewa Uharibifu uliofanywa na azimio la zanzar kwa hii nchi.

Azimo la zanzibar lilichafua viogozi wengi..Mkapa ni mmmoj TU HALIWEZI KUCHWA BILA KUJADILI KWA KINA NA MAPANA.

Kama Fisadi Mkapa alikuwa anajua kwamba Azimio la Zanzibar linamlinda katika maamuzi yake ya kufanya biashara akiwa Ikulu mbona hakuamua kuwaambia wale waliomchagua kwamba ameamua kufanya biashara akiwa Ikulu? 😕😕😕😕
Unafikiri angeamua kuwafahamisha Watanzania kwamba ameamua kufanya biashara akiwa Ikulu Watanzania wangemuonaje? Na je, reaction ya Watanzania ingekuwa ni positive au negative?
 
Makongoro anataka kutuambia nini? anyway baba hata akizaa kibaka ni mwanae tu; ohhhh hata aki adapt kibaka pia kisheria bado ni mwanaye tu. Hivyo si hoja BWM kubaki katika familia ya Nyerere. Maana wali adapt kibaka.
 
dawa ya hawa mafisadi ni kuwatenga tu kama akija kubainika ni mtu safi ndio akaribishwe ushahidi uliopo mpaka sasa unaonyesha kwamba ni mafisadi sasa tukianza kuwakaribisha na kuwapokea kwa mikono miwili tujue kabisa kuwa tutakuwa tunajichafua wenyewe mi narudia tena kusema kama wakina Prof.Mahalu tumewapeleka mahakamani basi na hawa tuwapeleke pumba na mchele vikajulikane huko la sivyo watuambie kuwa siku hizi mtu akituhumiwa asikamatwe wala kufikishwa mahakamani mpaka ushaidi upatikane.
 
MkamaP ni kweli si rahisi ku establish ufisadi wa mkapa katika hili. Lakini wana JF naomba kuuliza hivi hawa viongozi wetu tunaowalipa pesa nyingi sana hivi kama pension! wana haki gani ya kujiingiza katika biashara? maana kwa kweli wanapata malipo kibao ya kuwawezesha kuishi kwa raha maisha yao yote. Na wakati huo huo wakina sisi tunalipwa pesa ambayo hata kukupeleka huko mjini kuliko na ofisi za TRA nauli yenyewe haitoshi pesa unazokwenda kulipwa. Je hapa kweli ni fair kiongozi kupitia cheo chake ajilimbikizie mali? Huyu Mkapa hakuwa mjasiriamali alipoingia Ikulu. Yeye na mwalimu walituthibitishia kuwa BWM ni safi ajajilimbikizia mali. Hii ndiyo inayosababisha kelele leo. Si unajua hata Nyerere alianza ukulima alipostaafu na hakuna kelele zilizopigwa kutoka nje? Bali badala yake alipostaafu watu tulimchangia ngombe na vifaa vya kilimo zikiwamo pembejeo ili akaanze ujasiramali? Mkapa sivyo. Kajichomeka kwenye vijibiashara vingi tu hata kabla ya kumaliza kipindi chake cha uraisi unadhani alikuwa fair kwa competitors wake wengine kwenye hivi vibiashara?
 
tunaongea sana yani... vitendo hafifu ndo mana hawa jamaa wanajibu na kufanya watakavyo mana wanajua wananchi maneno mengi yasiyovunja mifupa
 
Kama Fisadi Mkapa alikuwa anajua kwamba Azimio la Zanzibar linamlinda katika maamuzi yake ya kufanya biashara akiwa Ikulu mbona hakuamua kuwaambia wale waliomchagua kwamba ameamua kufanya biashara akiwa Ikulu? 😕😕😕😕
Unafikiri angeamua kuwafahamisha Watanzania kwamba ameamua kufanya biashara akiwa Ikulu Watanzania wangemuonaje? Na je, reaction ya Watanzania ingekuwa ni positive au negative?

Bado na nikweli kabisa kuwa Msingi na chimbuko la UFISADI unaoshamiri nchini sasahivi ni Azimio la zanzibar na Falsafa ya RUKSA.

Mkapa hahitaji kujieleza kwa wananchi. Ila wanachi wanahitaji kuuliza UHALALI wa AZIMO LA ZANZIBAR.

Soma azimio la zanzibar...(sio kulipitia) soma beteen the line! + SERA YA RUKSA Hata wewe ungekuwa Mkapa Ungelifanya alivyofanya.

Waziri yeyote KIOGOZI YEYOTE.. aliyekuwa madarakani wakati ule angefanya alivyofanya...Vijisenti...kupitisha mikataba feki..etc.

Mkapa ni Mwoga tu! Au He is not smart enogh...

Hahitaji kujificha ....anatakiwa aweka wazi hadharani Jeuri yake ilipotoka. Kubomolewa kwa Azimio la arusha lililokuwa limejikita vichwani na kwenye fikra za viongozi wengi...na hivyo..kujiona huru ..tena huru kabisa...RUKSA kijiingiza hovy hovyo kwnye biashara ..na pengine biashara haramu ..au biashara kwa njia haramu.

AZIMIO LA ZANZABAR/ALZ lili halalisha kwa KIOGOZI YEYOTE Kufanya biashara kujiongezea kipato etc....HALIKUTOA MWOGOZO WOWOTE Kwa wale waliokuwa IKULU KUWA WASINFAYE HIVYO au wakitaka kufanya wafanyeje...SO why Mkapa asifanye?

ALZ liliruhusu viongozi wote kuwa na hisa na ubia..na kuwekeza kwenye makampuni na hata makampuni ya Kibebari na kusisitiza hasa kwa wale waliokaribu kuustaafu....Ili wasipate matatizo baada ya kustaafu...haikutoa maelekezo yeyote kwa walikuwa ikulu..Kwanini mkapa asichukue advantage? Please leave Mkapa alone ..deal with the real cause!!

Mkapa sio Fisadi...Aliwezeshwa...Na AZL + SERA YA RUKSA baada ya kuzimika kwa AZIMIO LA ARUSHA.

AZIMIO LA ZANZIBAR + SERA YA RUKSA NDIO KIINI CHA UFISADI unaoshamiri na kuota mizizi.
 
Kwa upande wangu mtu kuwa mkulima sioni tatizo kama tulivyokwisha jadili sana huko nyuma katika threads nyingine tatizo ni jinsi alivyoweza kupata eneo la kulima. Na kwanini aliamua kutafuta eneo hilo wakati akiwa Rais, angetafuta eneo hilo wakati ule Mwalimu alipoamua kung'atuka na kuanza kilimo pale Butiama mimi ningempa apoti. Tatizo ni matumizi haya ya NEMBO ya IKULU. Maana ni suala la kuwaambia wananchi
RAIS ANATAKA HAPA ALIME, UNATIMKA KWA FURAHA KWAMBA RAIS KAPENDA SHAMBA LANGU. RAIS TUELEZE TU UMEWEZAJE KUPATA VYOTE HIVYO UKIWA IKULU? AU HATA HILO UNASINGIZIWA????
 
Ndugu MWENYEKITI
"Kuna hadithi ya kiongozi fulani wa dini, kiongozi wa kanisa masikini, ambaye alikuwa na mazoea ya kupata matatizo ya kifedha na mara kwa mara mwomba Askofu wake msaada. Hatimaye, Askofu alipoteza subira. Akamkemea yule kiongozi wa dini kwa kuomba mara nyingi mno. Haukupita muda mrefu Askofu akapokea simu kutoka kwa yule kiongozi wa dini, ikisema, “Hili si ombi. Ni taarifa. Sina nguo ya ndani!”

Nataka kuwahakikishia kwamba serikali yangu haitayachukia maombi yenu kiasi kwamba mwisho wa yote ikawaacha bila ya nguo zenu za ndani za kiuchumi! (B.W.Mkapa,April 2001 ,Sheraton hotel,dsm)

Hii ni kali!!!
Alikuwa anajustify something I guess!
 
MKAPA ana hisa kubwa Kagera Sugar, kiasi cha kumfukuza mr.Foy aliyekuwa akifanya kazi TRA alipojaribu kuhoji kwanini Kagera sugar hawalipi ushuru. Masikini bwana Foy hakujua kama kiwanda cha Mkapa. ikatoka oda ikulu atimuliwe kazi.

nadhani tungejadili kuhusu KAGERA SUGAR kiwanda kilichokuwa mali ya Taifa kaamua kujibinafsisha.
 
Nimeona mjadala juu ya shamba la Mkapa huko Mtibwa. issue kubwa Mkapa anamiliki Kagera sugar nadhani tunapaswa kuumiza vichwa vyetu kwa kiwanda hiki mali yetu.anayetaka kujua aulize FOY wa TRA alivyofukuzwa kazi kwa kuhoji kwanini KAGERA SUGAR isilipe ushuru stahiki? MKAPA akatoa oda akiwa Ikulu kuwa mzigo upitishwe na FOY atimuliwe kazi.
 
Nimeona mjadala juu ya shamba la Mkapa huko Mtibwa. issue kubwa Mkapa anamiliki Kagera sugar nadhani tunapaswa kuumiza vichwa vyetu kwa kiwanda hiki mali yetu.anayetaka kujua aulize FOY wa TRA alivyofukuzwa kazi kwa kuhoji kwanini KAGERA SUGAR isilipe ushuru stahiki? MKAPA akatoa oda akiwa Ikulu kuwa mzigo upitishwe na FOY atimuliwe kazi.

Lete ushahidi hapa. Usilete roumars tu!
 
mhu makubwa!je hii ni kweli!au ssa mkapa ndo anatupiwa kila kitu tu?
 
Back
Top Bottom