Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Aende tu huko mahakamani.. ile sheria ya maadili ya 1995 itatumika hata kama ina mapungufu..
 
yaani alikuwa anamtetea wakati anamtosa au Sumaye alikuwa ni ndumilakuwili?
 
Mkuu Halisi,
Hao kina Mbuna walishindana na nani kwenye zabuni ya kuununua huo mgodi ?
 
hii nchi ni mwendo wa sinema kwa kwenda mbele

Iweje akae kimya siku zote hizo then now ndo anakuja na haya??

alikuwa anapika vitu huyu sasa vimeiva ndo anataka kutenga

But magazeti nayo yakae tayari
 
JAMANI kumbukeni kuwa JOSEPH MBUNA ni mkwewe Mkapa!!! inakuwaje wanasema huo mgodi hauna uhisiano na familia ya Mkapa? zaidi tunajua mbuna hapo kabebwa tu kufunika jina la mzee
 
Hivi, mshitaki aweza shindwa kesi na kuadhibiwa hapo hapo? ama akishindwa kesi huishia hapo.. mpaka atokee mwingine wa kumshitaki ndo aadhibiwe?

There is no way Kiwira itaweza tenganishwa na ANBEM, utumiaji madaraka kukwapua mali za umma, ukosefu wa uwazi na 'fast tracking' ya umilikishwaji wake hata ubadilishwaji wa umiliki bila uwazi/tendering baada ya kutumia influence ya madaraka!! kuukwapua mgodi!
 
JAMANI kumbukeni kuwa JOSEPH MBUNA ni mkwewe Mkapa!!! inakuwaje wanasema huo mgodi hauna uhisiano na familia ya Mkapa? zaidi tunajua mbuna hapo kabebwa tu kufunika jina la mzee

Duu Pole sana Mbuna,
Yaani binti yako kuolewa kwa kijana wa fisadi nawe unajikuta unalazimika kuwa fisadi??? Heshima yako yote mzee ndo inazama hivi hivi?? Naweye binti Mbuna ulokole wote unaishia kuwa fisadi? pole mwanangu!
 
hii nchi ni mwendo wa sinema kwa kwenda mbele

Iweje akae kimya siku zote hizo then now ndo anakuja na haya??

alikuwa anapika vitu huyu sasa vimeiva ndo anataka kutenga

But magazeti nayo yakae tayari

Alikuwa anasubiri magazeti mengi yamuandike ili apate mabilioon zaidi. Si umesikia kuwa atadai 2 billion kwa kila gazeti!!!!!!

Mahesabu yeke: kwa Magazeti 10 (10 x 2,000,000,000 = 20,000, 000,000 Tshs)
 
Huyu babu ana wajukuu kweli? na kama ana wajukuu hao hawatakuwa na watoto...matendo na sura sawa sawa.Kuna watu hata wakifa leo wengi wetu tutashangilia.kwanini watu hawana huruma???
 
Sawa sawa, unajua hii nchi ingeihamia kure mara(musoma) basi kusingekuwa na shida, wale wakurya hawana utani ndugu zangu
 
Rais (mstaafu) wa Tanzania Benjamin William Mkapa yuko katika mchakato wa mwisho kuyashtaki magazeti ambayo yamekuwa yakimwandama kwamba ni fisadi.

Habari kutoka ndani ya familia yake zinaeleza kuwa taratibu za kuyashitaki magazeti hayo zimekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kutolewa kwa taarifa za awali kwamba yeye na mkewe, mjasiriamali Anna Mkapa hawana hisa katika mgodi wa Kiwira.

Zaidi ya hapo inaelezwa kuwa magazeti yatakayoshikiwa bango ni Kulikoni, Thisday, Mwanahalisi, Mwananchi, Tanzania Daima, Majira na Mtanzania.

Mtoa habari huyo aliyeona makabrasha ya mashtaka hayo ameeleza kuwa kila gazeti litadaiwa bilioni mbili; akieleza kuwa anadai kiasi hicho kwa kuwa angalau kinalinganalingana na hadhi yake ndani na nje ya nchi.

Hivi majuzi kampuni ambayo ilinunua mgodi wa Kiwira wa kuzalisha makaa ya mawe iliibuka na kueleza kuwa Mkapa na mkewe hawana hisa eti kwamba walijitoa muda mfupi baada ya kugundua kuwa ilikuwa ikijiandaa kununua mgodi huo kwa bei ya kutupwa ya sh. milioni 700 (zililipwa 70 kwanza za kukopa kutoka Benki) wakati mgodi wenyewe ukiwa na gharama kubwa ya bilioni 4.

Mawakili sita wamejipanga kwa kazi hiyo, huku mmoja akiwa kutoka Afrika Kusini ambaye anaeleza kuwa mzoefu katika kesi zinazohusu kashfa kwenye vyombo vya habari.
Mkuu habari hii imetoka ndani kwa BWM?
 
baada ya balai kufa sio? je, JOSEPH MBUNA si mkwe wake mkapa? na hapa atakataa nini?
na MBUNA hapo alibebwa tu'. hiyo ni dili ya mzee mkapa mwenyewe asitake kututisha hapa

Hii point nili i raise katika discussion ya bill ya ethics aliyoileta Zitto hapa.Familia ni vizuri kui define vizuri ama sivyo kama tuna define vitu ki west kwa nucleus family tunapigwa bao hivi hivi.
 
----Tanpower Resources ilisajiliwa 29/12/2004 na kupewa namba 51080 ikiwa na dhumuni kuu la kwanza kuchimba mkaa wa mawe nakuzalisha umeme, wakati huo Mkapa bado ana hisa na alijua sababu za kuanzishwa kwake. Wakati inasajiliwa wanahisa walikua ANBEM hisa 200,000 na aliyesaini ni Anna Mkapa, Devconsult ya Yona na Mwanae (hisa 200,000), Universal Tech (hisa 200,000), Choice Industries ya Mbuna (200,000) na Fosnik Enterprises ya Nicholus Mkapa na mkewe Foster wakiwa wameiga jina la kampuni ya baba na mama zao ya ANBEM (wao wakiwa na hisa 200,000) na aliyesaini ni Nico

-----Lakini jambo la hatari ni kwamba, kabla hata ya TANPOWER kusajiliwa ilikwishaanza kufanya kazi na Evans Mapundi akiwa Mkurugenzi wake, alifanya mawasiliano Desemba 15 na wakatembelea Kiwira Desemba 18 na 20, kwa baraka za Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona. Yona akiwa pia mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo.

----Mkapa na Mkewe kupitia ANBEM walijitoa TANPOWER Februari 21, 2005 ikiwa tayari hata mkataba wa ubia kati ya TANPOWER na Kiwira umekwishaandaliwa na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.... Hata baada ya Kujitoa, Mwanae Nico na mkewe Foster na baba mkwe wao Mbuna walikua ndani ya Kiwira.

----Ni mwaka huo ambao Yona na bosi wake waliitosa STAMICO na kuchukua eneo jingine lenye hazina kubwa ya mkaa wa mawe liitwalo Kabulo rig ambalo serikali ilikopeshwa USD milioni 50 kufanya utafiti. STAMICO hadi sasa wanalilia eneo hilo ambalo limechukuliwa na TANPOWER/Kiwira bureeeeeeeeeeeee

-----
 
Back
Top Bottom