Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Umekataa hiyo wewe kama nani Tanzania!!? You are nobody in Tanzania usitake kujikwezakweza na kujipa umaarufu usiokuwa nao. Walikamatwa waanzilishi wa JF kwa kisingizio kwamba ni wachochezi na wanatukana viongozi, lakini baada ya hao waliokamata hao vijana kuangalia JF kwa undani wakakosa ushahidi na wakaamua kuwaachia.

Vipofu na wale wasiowatakia mema Watanzania kama wewe ambao labda mlifaidika na ufisadi wa fisadi Mkapa kwa namna moja au nyingine siku zote hamtakubali ushahidi chungu nzima uliokusanywa dhidi ya fisadi Mkapa, lakini kwa Watanzania walio wengi sasa wanaelewa kwanini wanaambiwa uchumi umekuwa ukikua kwa silimia 5 au zaidi na wakati huo huo hawaoni improvement yeyote katika hali ya maisha yao. Kumbe mafisadi walikuwa wanachota mabilioni ya shilingi na kuinvest ndani na nje ya Tanzania. Mwalimu Nyerere alimwamini na kumuona mtu wa maana na hatimaye kumpigia debe ili awe Rais wa Tanzania, lakini hata kabla ya kufariki alishaanza kujutia uamuzi wake huo. Angekuwa hai leo hii asingeona aibu kuwaambia Watanzania kwamba wamsamehe kwa makosa makubwa aliyoyafanya wakati wa uhai wake wa kumpendekeza fisadi Mkapa ili awe Rais wa Tanzania. Angewaambia huyu mimi nilimuona huyu ni mnyenyekevu wa hali ya juu muadilifu na mchapa kazi mzuri sana, kumbe alikuwa kajivisha ngozi ya kondoo ni mwizi wa hali ya juu na asiye na mapenzi hata kidogo na Tanzania na Watanzania.

Za mwizi ni arobaini na fisadi Mkapa maji yameanza kumfika shingoni na sasa anatapatapa huku na kule. Anajua kibano chake hakiko mbali na siku hiyo Watanzania wa kila kona ya Tanzania na wale walio nje ya Tanzania watashangilia kwa nderemo, makofi na vifijo vya hali ya juu fisadi Mkapa atakapoonekana ana hatia ya wizi wa mabilioni na hivyo kupelekwa lupango na mali yake yote ndani na nje ya nchi kufilisiwa. Nchi nyingi za Afrika hili liliwezekana na Tanzania pia litawezekana.

Itakuwa ni aibu iliyoje kwa njemba iliyojiita 'mr clean' na 'awamu yake ya uwazi na ukweli' kumbe ilikuwa ni changa la macho ni mwizi wa hali juu na hana uwazi na ukweli wowote. Pamoja na Watanzania kumlipa mshahara na marupurupu manono ili awatumike vizuri lakini kwa tamaa ya fisi aliyokuwa nayo akaona hazimtoshi ikabidi afanye wizi ili akidhi matakwa yake ya kuwa tajiri wa kupindukia. Hili litakuwa ni fundisho kubwa kwa wanasiasa wote ndani ya Tanzania na nchi za Afrika kuacha kutumia nyadhifa zao ili kujitajirisha

this wont work !

Oh yes it will. It's called public outrage or political pressure.

That's why you're starting to see Mkapa running around the country like a chicken with his head cut off, defending himself or being defended at people's funerals thru the Minister of Propaganda. And we won't relent!

Oh yeah, it's getting to him!
 
Mimi nashauri topic zote zinazomhusu Mkapa ziunganishwe halafu zipelekwe kwenye udaku au closed topic. Kama tunataka kujadili hii issue tena basi iwe at the next level siyo ya udaku na uropokaji kukuza heshima ya forum.


What is udaku to you, maybe a very good news article to others.
 
Oh yes it will. It's called public outrage or political pressure.

That's why you're starting to see Mkapa running around the country like a chicken with his head cut off, defending himself or being defended at people's funerals thru the Minister of Propaganda. And we won't relent!

Oh yeah, it's getting to him!

its working the other way round sir !

kinyume na vile mnavyotaka nyinyi !
 
Tusubiri mtetezi wetu mama Kilago atasema nini kesho.
 
Sasa inabidi waeneza propaganda wawe makini kwa kuwa hakuna marefu yasiyo na incha ndiko tunakuenda tutajua yote tu ,masuke yakiwa machanga ni vigumu kutofautisha na nyasi.Sasa na nadhani ni muda muafaka wa kutambua fitna za watu mbalimbali na ni wenye macho na masikio ndio watako ona na kisikia no imagination no rumor no more.We are going to get in black and white now.
 
Sasa inabidi waeneza propaganda wawe makini kwa kuwa hakuna marefu yasiyo na incha ndiko tunakuenda tutajua yote tu ,masuke yakiwa machanga ni vigumu kutofautisha na nyasi.Sasa na nadhani ni muda muafaka wa kutambua fitna za watu mbalimbali na ni wenye macho na masikio ndio watako ona na kisikia no imagination no rumor no more.We are going to get in black and white now.

Wiki mbili zilizopita Ballali alifariki. Huyu ndiye ambaye angeweza kutoa ushahidi kuhusiana na shilingi bilioni 288 ambazo ziliingia kwenye mifuko ya mafisadi na vikampuni vyao uchwara vya kifisadi ikiwemo CCM ili kugharamia uchaguzi mkuu wa 2005. Leo KCM 'wanamsafisha' fisadi kwamba si mmiliki wa KCM pamoja na kuwa kamati ya Bomani labda ilionyeshwa documents mbali mbali kuhusiana na ownership ya KCM inayoonyesha kwamba kampuni ya mafisadi Mkapa na Yona ndiyo mmiliki wa KCM. Mikakati mikali sana, lakini Watanzania tuko macho hatutalala usingizi mpaka kieleweke.
 
Oh yes it will. It's called public outrage or political pressure.

That's why you're starting to see Mkapa running around the country like a chicken with his head cut off, defending himself or being defended at people's funerals thru the Minister of Propaganda. And we won't relent!

Oh yeah, it's getting to him!

Kuhani mkuu hapa tuko ukurasa mmoja, and I love it!
 
Ni sahihisho tu la kichwa cha habari... jadili

Kiwira yamsafisha Mkapa
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,June 01, 2008 @19:01

........................................
Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro, alisema ingawa katika hati za umiliki (Articles of Association) inaonyesha kuwa Mkapa ni sehemu ya Tanpower, lakini baadaye alijitoa.

"............

Kwa hiyo Tabaro anasema 'don't believe the documents, believe me, I am not lying but I cannot prove what I am saying'

Who is paying this piper's salary anyway, is it the Gov't (which owns only 15%) or Tanpower (which stole 85%)?

Sitapenda kodi yangu iende kulipa watu kama hawa.
 
Huyu Tabora amejibu kwa porojo kama vile majibu ya Mkapa kule kijijini kwake. Maswali ya msingi aliyopaswa kujibu ni WALIPATA VIPI KUNUNUA MGODI HUYU? TENDA ILITANGAZWA NA ILIKUWA WAZI?

Hoja ya pili: Huyu Bwana katoa jibu lisilo na shaka kwamba Mkapa alinunua Kiwara Coal Mine. Ila alijitoa baada ya kuona mambo yanawaka moto. Lakini bado kuna swali la msingi hapa JE MKAPA ALIJITOA LINI KCM?

Kutoa maelezo bila kueleza majibu ya maswali haya kunazidisha hasira za wazalendo, ebo! kwanini kuwapuuza Watanzania na kuwaona kama hawaezi kufikiri vile. Utetezi gani huo? eti mbona Serikali haiwatetei, wanataka kuzidi kumchafua Rais Kikwete hawa, walitaka Kikwete awatetee eti! ebo! Mhe. Kikwete, tafadhali Mkulu, tunaomba ripoti ya Jaji Bomani itolewe, na mapendekezo yatekelezwe mara moja.

Wahe. Wabunge, wembe ni uleule, tuchange pesa mil. 70,000/= tumrudishie Bw. Tabora na Mzee Mbuna, ili tuchukue mgodi wetu.
 
Nziku, hawa ni wezi na kwa maoni yangu hawastahili kurudishiwa hata senti tano.
 
Kiwira coal power project: Mkapa-Yona: The link gets stronger




-Tanpower Resources was their joint brainchild

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam (August 14, 2007)

FORMER president Benjamin Mkapa and senior cabinet minister Daniel Yona together oversaw the formation of Tanpower Resources Company Limited, the private local company holding at least 85 per cent shares in the pending, $271.8m (approx. 340bn/-) Kiwira coal-fired power project in Mbeya Region, it has now been established.

Our investigations have revealed that Tanpower Resources was officially registered on December 29, 2004, when Mr Mkapa was still the sitting president of the United Republic and Yona was the minister in his government directly in charge of both energy sector and mining sector affairs.

At the time of the company's establishment, its first listed directors were the then first lady Mrs Anna Mkapa; the then minister for energy and minerals Daniel Yona; Nicholas Mkapa (the president and Mrs Mkapa's son); Joseph Mbuna (Nicholas Mkapa's father-in-law); and Evans Mapundi.

According to our findings, it was the same company that in mid-2005 secured up to 85 per cent of the shares in Kiwira Coal and Power Limited, a once fully state-owned enterprise that has now entered into a controversial contract with the Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) for the supply of 200MW of power to the national grid.

When this shares exchange deal took place, both Mr Mkapa and Yona were still holding their all-powerful positions in the third phase government. The remaining 15 per cent shares in Kiwira Coal and Power Limited were formally retained by the government.

And in what could loosely be construed as 'perfect timing', the takeover bid by Tanpower Resources occurred right in the middle of advanced negotiations between TANESCO and Kiwira Coal and Power Limited for the coal mine to start substantial generation of power for supply to the national grid.

These negotiations culminated in the signing of the increasingly-questionable, 20-year power purchase agreement (PPA) between TANESCO, Kiwira Coal and Power Limited, and the government of the day in March 2006.

Amongst many other things, some stated objectives of Tanpower Resources are to ''carry on the business of miners of coal and iron, to process such coal and iron and generally treat, prepare, render marketable, sell and dispose of such coal and iron or by-products resulting therein in their raw or manufactured state.''

The company was also licensed to ''deal with coal mining in order to generate electricity for consumption and sale; to generate power generators, transmitters and general distributors; and to provide power and general projects management, project appraisers and consultants.''
Mrs Mkapa served on Tanpower Resources' first board of directors through ANBEM Limited, a private company she co-owns with Mr Mkapa in which they are listed as sole shareholders, directors and 'entrepreneurs,' which was formed in 1999 when the couple were still at State House.

Yona is represented in Tanpower Resources through a private company called DEVCONSULT Limited, in which he owns 90 per cent of the shares while his own son, Danny Yona, holds the remaining 10 per cent.

Before being appointed minister for energy and minerals - a position he served until the end of the Mkapa administration in December 2005 - Yona held a number of other key portfolios under the ex-president, including minister of state in the president's office (planning), and minister of finance.

It has also been established that Mr and Mrs Mkapa's son, Nicholas, has his own shares in the same Kiwira and Coal Power Limited company, via Tanpower Resources, through another company going by the name of Fosnik Enterprises Limited.

Records show that Mkapa junior owns Fosnik Enterprises on a 50-50 basis with his wife Ms Foster (Mbuna) Mkapa, while his father-in-law Joseph Mbuna is also one of the shareholders and major figures in Kiwira Coal and Power Limited through yet another company, Choice Industries Limited, which also falls under the umbrella of Tanpower Resources.

Other shareholders of Kiwira Coal and Power Limited company have been identified as Evans Mapundi and Wilfred Malekia through the Universal Technologies Limited company, also under Tanpower Resources.

Interestingly, the companies owned by Nicholas Mkapa and wife (Fosnik Enterprises), father-in-law Joseph Mbuna (Choice Industries), Mapundi and Malekia (Universal Technologies) all share the same postal address - P.O Box 8764, Dar es Salaam.

The government continues to formally hold 15 per cent of the shares in Kiwira Coal and Power Limited.

According to THISDAY's government sources, signs of potentially disastrous discrepancies in the multi-billion shilling contract between TANESCO and Kiwira Coal and Power Limited are now beginning to emerge as delays continue to hamper the still-pending launch of the project – more than 16 months since the signing.

The sources, who are privy to the details of the contract, say there are now growing fears that the deal could eventually turn out to be another expensive trap for the national economy, along the same lines as the infamous 1995 IPTL affair.


They say TANESCO could end up being liable to pay Kiwira Coal and Power Limited a staggering $6m (approx. 8bn/-) each month once the firm starts delivering on the agreed 200MW of electricity, which would bring TANESCO's monthly obligations to three independent power producers (IPTL, Songas and Kiwira) to a figure exceeding $20m (approx. 26bn/-).

According to the sources, this is well beyond the estimated $19.35m (around 25bn/-) per month that TANESCO currently earns from its revenues, and will therefore inevitably necessitate yet another power tariff hike of up to 30 per cent by TANESCO.
 
WAJIUZIA MGODI WA BILIONI 4/- KWA MILIONI 700/- TU

NYARAKA mpya zilizopatikana hivi karibuni zinaonyesha kwamba rais mstaafu Benjamin Mkapa na waziri wake wa nishati na umeme Daniel Yona, waliuza kampuni ya umma ya Kiwira Coal Mines Limited kwa kampuni yao binafsi kwa milioni 700/- tu mwaka 2005 wakati thamani halisi yam god huo ilikuw abilioni 4/-

Kwa mujibu wa rekodi sahihi za serikali ambazo gazeti hili limefanikiwa kuziona, mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira uliojengwa na serikali katika miaka ya 1980 kwa fedha kutoka serikali za China na Tanzania uligharimu kiasi cha bilioni 4.29/-, Upembuzi uliofanywa na mwnajiolojia wa Kichina mwishoni mwa miaka ya 1970 ulionyesha kwamba mgodi huo ulikuwa na hazina ya makaa ya tani milioni 35.14, na hazina iliyothibitishwa ya tani milioni 22.14.

Katika ubinafsishaji wenye utata wa mgodi huo wa makaa ya mawe, ambao ulifanikiwa kwa usiri mkubwa, serikali iliuza hisa kwa kampuni ya Tanpower Resources Company Limited, kampuni binafsi iliyoanzishwa na Mkapa, Yona na ndugu zao w karibu.

Wakitumia nyadhifa zao ndani ya serikali wakati huo, Mkapa na Yona waliharakisha ubinafsishaji wa mgodi huo na kuhakikisha kwamba ulitakiwa kuuzwa kwa bei ya kutupa kwenye kampuni yao binafsi, vyanzo mbalimbali vimeeleza.

Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) Ilisaini makubaliano na kampuni ya Tanpower Resources mnamo juni 8, 2005, ya kuuza asilimia 70 ya hisa za mgodi huo wa makaa ya mawe kwa kampuni hiyo ya Mkapa na Yona.

Lakini, Tanpower Resources haraka iliongeza umiliki wake hadi kufikia asilimia 85 na mnamo Machi 2006 ikaingia katika mkataba wenye utata wa dola za Marekani milioni $271.8 (takriban bilioni 340/-) na shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kuzalisha megawati 200 za umeme ambazo ungeingizwa kwenye gridi ya taifa.

Asilimia 15 zilizobaki za umiliki wa mgodi wa Kiwira ndizo pekee mpaka sasa zinazomilikiwa na serikali Nyaraka za serikali zinaonyesha kwamba serikali iliuza mgodi huo kwa bei ya kutupa kwa tanpower Resources kwa kiasi cha milioni 700/-, huku kampuni hiyo ikipewa muda mrefu wa malipo.

Imebainika kwamba kampuni hiyo ilitakiwa kulipa milioni 70/- siku ya kusaini makubaliabo hayo, huku kiasi kilichosalia ambacho ni milioni 630/- kikitakiwa kulipwa ndani ya miezi sita tangu kusainiwa kwa makubaliabo hayo.

Mkataba wa ubinafsishaji wa mgodi huo wa makaa ya mawe ulisainiwa kwa niaba ya serikali na Mwenyekiti wa PSRC, John Rubambe, na mwanasheria wake mkuu, M. Mahanyu.

Kwa upande mwingine, meneja mkuu wa zamani wa mgodi huo, Adam Salim Abdu, na meneja wa fedha na utumishi, Ramadhan Idabu, walisaini makubaliano hayo kwa niaba ya Kiwira Coal Mines Ltd.

Walioiwakilisha Tanpower Resources kwenye utiaji saini huo wa mkataba wenye utata walikuwa Evans Mapundi na Wilfred Malekia.

Mapundi na Malekia wanamiliki hisa ndani y a Kiwira kupitia kampuni yao ya Universal Technologies Limited, ambayo pia ipo chini ya mwamvuli wa Tanpower Resources. Mapundi na Malekia pia wako kwenye bodi ya wakurugenzi ya Kiwira yenye wajumbe sita.

Uchunguzi uliofanywa kwa kuongozwa na nyaraka mbalimbali kutoka wakala wa usajili wa kampuni na liseni (Brela) umeonyesha kwamba Tanpower Resources ulikuwa ni mkakati na mpango wa pamoja baina ya mkapa na Yona, ulioanzishwa mwishoni mwa kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya tatu wakati Mkapa alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania na Yona akiwa waziri wa nishati na madini.

Wakati kampuni hiyo ikisajiliwa mwaka 2004. wakurugenzi wake wa kwanza walikuwa ni mke wa rais wa wakati ule, Anna Mkapa; waziri wa nishati na madini wa wakati huo Daniel Yona; Nicholas Mkapa (mtoto wa Mkapa); Joseph Mbuana (baba mkwe wa Nichola Mkapa); na Evans Mapundi.

Kama ilivyowahi kuripotiwa na KULIKONI na gazeti dada la THISDAY, Yona, ambaye aliongoza wizara ya nishati na madini katika serikali ya awamu ya tatu chini ya Mkapa, na mwanawe, Danny Yona, walikuwa wanahisa wakubwa wa baada ya kampuni ya Kiwira kubadili jina na kuitwa Kiwira Coal and power Limited chini ya mwavuli wa Tanpower Resources Company Limited.

Wao wanawakilishwa na kampuni ambayo haifahamiki sana, lakini yanye nguvu ya Tanpower Resources kupitia kampuni yao binafsi ya DEVCONSULT LIMITED, mbayo Yona (waziri wa zamani) mkubwa anamiliki hisa asilimia 90 na Yona mdogo anamiliki asilimia 10 zilizosalia.

Uchunguzi wa gazeti hili tayari ilishaeleza kwamba mkapa na mkewe, Anna Mkapa, wana hisa kwenye kampuni ya Kiwira kupitia kampuni yao binafsi ya Anbem Limited, ambayo ilisajiliwa mwaka 1999 huku wanahisa hao wakiwa wanaisa wakuu wakati wakingali Ikulu.

Mbali ya hisa zinazomilikiwa na Anbem Limited, imeelezwa pia kwamba mtoto wa Mkapa, Nicholas Mkapa pia ana hisa zake kwenye kampuni ya Kiwira kupitia kampuni ya Fosnik Enterprises Limited ambayo anamiliki yeye na mkewe, Foster Mbuna kwa asilimia 50-50.

Wakati huo huo, baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Joseph Mbuna, pia ni mwanahisa wa Kiwira Coal and Power Limited mgodi ambao uko mkoani Mbeya

Mbuna, ambaye hisa zake katika kapuni hiyo zinapitia kampuni yake ya Choice Industries Limited ambayo yeye ndiye mmiliki mkuu, kwa sasa ndiye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kiwira
Coal and Power Limited, ambapo Nicholas Mkapa ni mmoja wa wakurugenzi.

Kama ilivyo kwa kampuni za Anbem Limited, DEVCONSULT Limited na Fosnik Enterprises Limited, Choice Industries Limited pia ipo chini ya mwanamvuli wa Tanpower Resources.

Ilifahamika baadaye kwamba Kiwira Coal and Power Limited ilipewa kwa mizengwe nyongeza ya eneo lenye hazina kubwa ya makaa ya mawe ambalo awali lilikuwa likimilikiwa na serikali.

Vyanzo vya ndani zinaeleza kwamba eneo la Kabulo linalodhaniwa kuwa na makaa ya mawe ambalo pia lipo mkoani Mbeya ulipo mgodi wa kiwira lilitwaliwa kutoka shirika la Madini la Taifa (Stamico), linalomilikiwa na serikali, na kukabidhiwa kwa wamiliki wa Kiwira.

Tafiti zilizowahi kufanywa kwa mwongozo wa serikali yenyewe zinaonyesha kwamba eneo la Kabulo, ambalo lipo katika mkondo wa bonde la Ufa la Afrika Mashariki, kusini magharibi mwa Tanzania, limethibitika kuwa na hazina ya tani milioni 14 za makaa ya mawe.


(Imetolewa na Kulikoni, issue no 294, Jumatano April, 2, 2008)
 
Alafu inasemekana katika hiyo million 700 wametoa million 70 tuu.
 
Kwa manasiasa kuwatukana waandishi wa habari ni kitendo cha ushujaa kwani waandishi wa habari wanaweza kukumaliza in a second.
Mimi namshauri Mkapa aitishi mkutano na waandishi wa habari nione mate yatakavyokuwa yanawatoka mdomoni. Wanamshindwa JK watamuweza Mkapa.

Tatizo sio uwezo wa mtu kuongea bali ni fact zilizokuwepo . Nashindwa kuelewa unaposema udaku unamaanisha ni nini ? Ni kweli kwamba hiyo kampuni ilianzishwa na Mkapa na mke wake wakati wakiwa ikulu na mbaya zaidi kutumia inside information kwa manufaa binafsi. Mimi sidhani kama unatakiwa kuwa rocket scientist kuona uozo uliofanywa na huyu bwana . Simply kwa sababu sipendi policy za Kikwete ainizuii kuona uozo wa Mkapa !

Swali la kujiuliza kama kweli huyu bwana ni smart kama unavyodai jee kwa nini akuirefute hizi allegation mara tuu zilipotoka ? Na hata ile article ya mwenyekiti wa Kiwira uliyoileta hapa ni utumbo mtupu kwani hakuna substance yoyote . Pia imeweza kuonyesha ya kuwa ni kweli Mkapa alinunua huo mgodi . Sama nashindwa kuelewa Mkapa anakulipa nini mpaka unakuwa mstari wa mbele kutetea utumbo alioufanya?
 
Hivi kwa nini sasa Mkapa na wenzake wanaanza kuongea baada ya kuona kuna tume itaundwa kuchunguza huo uozo wa kiwira ? Nadhani ili ni swali muhimu kujiuliza!
 
Back
Top Bottom