Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Hukumu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ya mjane wa bilionea wa madini, Bilionea Msuya, Miriam Steven kusomwa leo.

Miriam pamoja na mshtakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, wanakabiriwa na shtaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria, mdogo wa marehemu bilione Msuya.

Hukumu hiyo inatarajiwa kusomwa na Jaji Edwin Kakolako, ambayo ndiyo itaamua hatima yao kama wana hatia au lah. Kama watakutwa na hatia hukumu ni kunyongwa hadi kufa.

Watuhumiwa wamekuwa mahabusu kwa nane na leo ndio hatima yake, je, nini kitatokea leo Mambo yatakuwaje? Nini itakuwa hukumu ya kesi hii? Mke wa Msuya na mwenzake watakutwa na hatia au lah?

Pia soma:

Mjane wa Bilionea Msuya alikuwa anatetewa na Wakili Peter Kibatala.

UPDATE: AACHIWA HURU

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemkuta hana hatia Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, bilionea Erasto Msuya hivyo ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.

Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wakidaiwa kumuua kwa kumchinja Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.

Miriam na mwenzake Muyella walidaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, imetolewa leo Februari 23, 2024 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Soma hukumu hapo chini.
 

Attachments

  • Republic_versus_Miriam_DO_Steven_Mrita_another_Criminal_session.pdf
    1.1 MB · Views: 9
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, bilionea Erasto Msuya.

Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, Miriam na mwenzake Muyella wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth, Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Aneth alikuwa mdogo wa bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SMG eneo la Mijohoroni, Barabara Kuu ya Moshi-Arusha wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Agosti 7, 2013.

Hukumu hiyo inayotarajiwa kusomwa na Jaji Edwin Kakolaki aliyeisikiliza kesi hiyo, ndio itakayoamua hatima yao iwapo wana hatia au la.
Na kama wana hatia, adhabu ni kunyongwa hadi kufa na kama hawana, wanaweza kuachiwa huru.

Mpaka leo hukumu hiyo inapotolewa, washitakiwa wameishi mahabusu kwa takribani miaka minane wakisubiri kukamilika kwa usikilizwaji wa kesi, kwa kuwa shtaka la mauaji linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria nchini.
 
Back
Top Bottom