Kesi ya mjane wa Bilionea Msuya ngoma nzito

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
Mjane wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (45) ameieleza Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, jinsi alivyoshiriki katika mgao wa mali za mume wake kwenda kwa ndugu wa Erasto Msuya.

Amedai mgawanyo wa mali za marehemu mume wake, Erasto Msuya ulifanyika Februari 2014, ambapo baba na mama wa marehemu, walipewa Sh225 milioni kila mmoja huku wifi zake, walipewa Sh73 milioni kila mmoja.

Pia, alidai kuwa hakukuwahi kuwa na ugomvi wala mgogoro wa mali baina yake na wifi yake Aneth Msuya anayedaiwa kumuua.

Mrita ametoa maelezo hayo, leo Oktoba 25, 2023 mbele ya Jaji, Edwin Kakolaki wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kujitetea.

Mrita na Miriam na mwenzake, Revocatus Muyella ambaye ni mfanyabiashara, wanakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kumuua dada wa marehemu Erasto Msuya, Aneth Msuya kwa kumchinja nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, tukio wanalodaiwa kulitenda Mei 25, 2016.

Bilionea Msuya, aliuawa kwa kupigwa risasi aiba ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7, 2013 eneo la Mijohoroni.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, Mrita alidai fedha hizo zilikuwa katika akaunti mbalimbali za benki alizokuwa anamiliki mume wake ambaye pia alikuwa mfanyabaiashra tajiri wa Mirerani, Erasto Msuya.

Alidai baada ya kifo cha mume wake Erasto kilichotokea Agosti 7, 2013 aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi na hakukuwahi kuwa na ugomvi wa mali wala mirathi baina yake na ndugu yeyote wa marehemu.

"Hivyo, Februari 2014 nilifanya mgawanyo wa mali baina ya ndugu wote waliostahili ambao ni baba wa Erasto Msuya, Elisaria Elia Msuya alipewa mgao wa Sh225 milioni na mama wa Eresto Msuya, Ndeshukurwa Msuya yeye alipewa Sh225milioni," alidai Shahidi na kuongeza,

Pia mgao huo wa mali uliwahusisha dada zake Erasto Msuya (wifi zangu) ambao ni Happy Msuya, Nantuja Msuya, Esther Msuya, Bahati Msuya, Joyce Msuya na Aneth Msuya, ambao kila mmoja alipewa Sh73 milioni na pointi kadhaa," alidai Mjane huyo.

Alifafanua kuwa fedha hizo zililipwa kupitia mfumo wa benki, kutoka benki ya Exim kwenda kwenye akaunti za wanandiugu hao na kisha kusaini nyaraka zinazoonyesha kuwa fedha hizo zimeingia katika akaunti zao kupitia mwanasheria kutoka kampunit ya Royal Attorney, mkoani Arusha.

"Mheshimiwa jaji, fedha hizo zilizokuwa zinatoka katika benki ya Exim kwenda kwa ndugu wa Erasto Msuya, zilikuwa ni dola, hivyo tulizibadilisha ndio tukawatumia," alidai Mrita.

"Mheshimiwa jaji, fedha hizo zilizokuwa zinatoka katika benki ya Exim kwenda kwa ndugu wa Erasto Msuya, zilikuwa ni dola, hivyo tulizibadilisha ndio tukawatumia," alidai Mrita.

Alidai baada ya mgawanyo huo hakuna mahali popote ambapo Aneth aliwahi kulalamika au kufungua mashtaka ya kuupinga wala kulalamika kutoridhishwa nao wala kudai chochote.

"Hata ushahidi wa upande wa mashtaka waliotoa mahakamani hapa mpaka wanafunga ushahidi wao, hakuna shahidi yoyote aliyeleta uthibitisho wowote kwamba kulikuwa na mgogoro wa mali au mirathi baina yangu na Aneth," alidai.

Alidai kuwa katika mali zilizomilikiwa na mume wake ambazo ni Kampuni ya Utalii ya SG Northen Adventure, Erasto Msuya alikuwa na hisa 600 huku yeye akiwa na hisa 200, huku Kampuni ya Madini ya Tanzanite one, alikuwa na hisa 400, wakati yeye alikuwa na hisa 100.

Yeye sio msimamizi wa mirathi:
Katika hatua nyingine, Mrita alidai kwa sasa yeye sio msimamizi tena wa mali za marehemu Erasto kwa kutokea uamuzi ambao ulitolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kuwateua watoto wake kuwa wasimamizi wa mirathi.

Alidai Oktoba 27, 2021 alisikiliza kwa njia ya video akiwa gerezani uamuzi uliosomwa na Jaji Devotha Kamuzora kuhusu kuhamisha usimamizi wa mali za Erasto kutoka kwake kwenda kwa watoto wao, ambao ni Kelvin Msuya na Glory Msuya hivyo sasa yeye si msimamizi tena wa mali hizo.

Uamuzi wa Jaji Kamuzora ulitokana na shauri lililofunguliwa na mama mkwe wake, Ndeshukurwa, aliyetaka Miriam anyang'anywe usimamizi apewe yeye jambo ambalo ambalo Jaji alilikataa na kulitupilia mbali shauri hilo kisha kuhamisha usimamizi kwa watoto kwa kile alichosema kuwa umri wa Ndeshukurwa ni mkubwa sana kuweza kupewa jukumu hilo, lakini pia Miriam yuko gerezani.

"Mimi na Marehemu Erasto Msuya, tulijaliwa kuwa na watoto watatu ambao ni Kelvin, Calvin na Mourine Msuya" alidai.

Kuhusu kauli iliyotolewa na David Mhanaya (shahidi wa upande wa mashtaka) kwamba alielezwa na Getruda (dada wa kazi wa Aneth) kwamba Miriam alisema mali atafute yeye na mume wake wengine wafaidi, alidai si kweli.

Alijibu kuwa kama angekuwa na nia mbaya katika mali hizo asingezigawa kama alivyofanya baada ya kupewa usimamizi na pia alikana kuhamisha umiliki wa mali yeyote kutoka kwenye jina la Erasto kwenda kwenye jina lake na hata hakuna shahidi wa upande wa mashtaka aliyetoa uthibitisho wa jambo hilo.

Alifafanua kuwa hata baada ya mgawanyo wa mali hizo hakuna mahali palitokea migongano wala malalamiko yoyote kuhusu mgawanyo wa mali hizo.

Kuhusu kukabidhiwa Aneth na kuishi nae:
Katika ushahidi wake wa masaa saba, Mrita alidai kuwa hakukuwahi kuwa na ugomvi wala mgogoro wa mali baina yake na wifi yake Marehemu Aneth Msuya anayedaiwa kumuua.

Aliyasema hayo leo baada ya Wakili Peter Kibatala kumuuliza kuhusu hoja iliyotolewa na shahidi wa upande mashtaka, David Mhanaya kwamba alimuua Aneth kwa sababu ya mgogoro wa mali.

Alijibu swali hilo, Mrita alidai hakuwa na sababu ya kumuua Aneth kwa kuwa ni mtoto wake wa kumlea aliyekabidhiwa na wakwe zake tangu akisoma shule ya msingi mpaka anaolewa na wakati wote waliishi kwa amani.

"Aneth alikuwa ni mtoto wetu wa kumlea mimi na mume wangu Erasto Msuya, namaanisha alikuwa ni mtoto wa mwisho wa familia ya Elisaria Msuya, baada ya kuolewa na Erasto, wazazi wake Erasto walitukabidhiwa Aneth kama mtoto wetu wa kumlea akiwa anasoma shule ya msingi," alidai.

Aliendelea kudai kuwa walimlea Aneth mpaka alipofikia umri wa kuolewa na mahari ilipokelewa nyumbani kwake akimaanisha kuwa alimlea vizuri bila tofauti yeyote.

"Baada ya Aneth kumaliza masomo yake alikuja Dar es Salaam kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakati huo wote alikuwa chini ya uangalizi wetu, baadaye alipata mchumba anayeitwa Wilbard Kimario, akaja kujitambulisha kwetu na mimi nikaenda kutoa taarifa kwa wazee (baba na mama yake Aneth) ambapo walituambia shughuli ya kutoa mahari na kuvishwa pete ya uchumba tuifanye sisi, na tulifanya hivyo mimi na marehemu mume wangu," alidai.

"Mtu wa kwanza kuniambia amepata mchumba, alikuwa ni mimi kama mama yake mlezi, nilichukua jukumu la kwenda kuwaeleza wazazi Mererani, wakaniambia mtoto tuliwakabidhi ninyi mumlee, mtaamua wapi mnataka kufanyia shughuli yake," aliongeza.

Alidai alirejea nyumbani kwake na kumweleza mume wake, kwa pamoja walikubaliana ifanyike nyumbani kwao Arusha na yeye alikabidhiwa mahari ya mama baada ya mama mkwe wake Ndeshukurwa Msuya kuridhia kwamba anastahili kupokea mahari hiyo kwani ndiye aliyemlea Aneth.
 
Nisiwachoshe msinichoshe
kula chuma hiko


Credit: Mwananchi
 
Kazi ipo...
Miaka inaenda kasi now is 10yrs toka bilionea auwawe...
 
Jamani Leo ndo hukumu. Mlioko kwenye viunga vya mahakama mtujuze mahakama imeamua nini
 
Back
Top Bottom