Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Historia fupi juu ya Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya, Kuuawa kwa Dada yake, Kukamatwa kwa Mke wake hadi Kuachiwa kwake

Agosti 7, 2013 Saa 7 Mchana ya Jumatano, taarifa mbaya za mauaji zinaanza kusambaa Jijini Arusha zikieleza kuwa Mfanyabiashara Maarufu na Mmiliki wa Migodi ya Madini ya Tanzanite, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa Risasi 21 na Watu wasiojulikana akiwa karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Mwili wa Bilionea Msuya ulikutwa pembeni ya Gari lake aina Range Rover na ndani ya Gari kulikutwa kiasi cha Fedha zinazokadiriwa kufikia Tsh. Milioni 100, Bastola, Simu za Mkononi na iPad.

Swali gumu linaanzia hapo, hawa wauaji walikuwa wanataka nini kama hawajachukua hata Tsh. 100?

Tukio hilo ndilo linatajwa kuzalisha Mgogoro uliokuja kusababisha Kifo kingine cha Aneth Msuya, mtumishi wa Wizara ya Fedha ambaye ni Dada wa Marehemu Bilionea Msuya.

Mei 25, 2016 Jijini Dar es Salaam katika eneo la Kibada Block 16, Kigamboni, zinaanza kusambaa tena taarifa mbaya za kuchinjwa kwa Aneth Msuya, mama wa mtoto wa mmoja.

Kifo cha Aneth kilikuja kuhusishwa na Mgogoro uliodaiwa kuwepo kati ya Mke wa Bilionea Msuya na Wifi mtu huku sababu ikitajwa kuwa ni Ugomvi wa Mali za Marehemu.

Agosti 7, 2016, Vikosi vya Upelelezi vya Makosa ya Jinai kupitia Jeshi la Polisi vilimkamata Miriam Mrita maarufu kama Mke wa Bilionea Msuya pamoja na Revocatus Muyella kwa tuhuma za mauji ya Aneth Msuya ambapo anaishia kusota Gerezani kwa miaka takriban 7​

Ikumbukwe, katika moja ya vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani na Wakili wa Serikali Patrick Mwita, ilidaiwa kuwa Mjane huyo alikiri kuhusika na mauaji ya Wifi yake kutokana na kumsumbua katika masuala ya Mirathi ya Erasto Msuya na alimlipa Revocatus Tsh. Milioni 20 kwaajili ya kusimamia mipango ya uhalifu huo

Februari 23, 2024, Mke wa Bilionea Msuya akiwa anatetewa na Wakili Peter Kibatala katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, anaachiwa huru, pamoja na Revocatus Muyella ambaye alitajwa kushiriki kupanga njama za mauaji ya Aneth Msuya, na yote ni baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
 
Back
Top Bottom