Rajatullahi
New Member
- Sep 12, 2013
- 2
- 0
Una Elimu gani??!
Millioni 1.35 ni mshahara wa kufuru? Kweli tunatofautiana.watu wanalipwa dola 25000 ambayo ni kama millioni 40 kwa mwezi endelea kulalamika na vyeti vyako
wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
Millioni 1.35 ni mshahara wa kufuru? Kweli tunatofautiana.watu wanalipwa dola 25000 ambayo ni kama millioni 40 kwa mwezi endelea kulalamika na vyeti vyako
Unashangaa nini sasa hapo? Huo si mshahara bali masikhara tu. Uliza watu huko kwingine wanaanzia kiasi gani? Sasa unataka ashushiwe mshahara wake? Badala ya kuomba na kumshinikiza mwajiri wako nawe uongezewe unaanza kuwangalia wenzio kwa kijicho na husda. Kwanza ujue katika nchi hii miongoni mwa watu ambao wanalipwa maskhara ni pamoja na hao wanaoitwa wahasibu.
mamabo ya kishamba sana haya kwanza kwa huyo kukuonyesha salary slip yake ili iweje,,,,???? kwa akili yake kaona kajipatia ujiko na ulivyotolea mimacho kwa ushamba wako ndugu we ulisikia wapi mshahara kama huo ukawa wa kufuru kwa taarifa yako hata walimu wanapata mshahara huo na ni kawaida tu na kwa ushamba wako huenda umeona gross salary wewe ukakurupuka mshahara mkubwa na kwa ushamba wako zaidi ukaleta huu uzi humu. wajanja huwa hawashangai na hawaonyeshi mishahara wewe na mwenzio woooteee na wenye tabia kama hizi ni USHAMBA.
hapo bold sasa umeanza matusi,
una uhakika gani kwamba mtoa mada ni mwanamke??
je wewe mama yako alikuwa baba?? na dada yako ni kaka??
mwanao wa kike ni mvulana na mkeo ni mume??
Bongo watu wengi hatuna discipline katika mambo kama kauli.
NIshamsikia Pius Msekwa, noted legislature scholar, erudite lawmaker, ruling party cadre, speaker of parliament, akaenda kusema neno hilo, publicly.
Sasa nilipoona kina baba viongozi wenyewe ndo hawa kina Msekwa, nikajua huku kwingine itakuwa balaa tu na wala sishangai sana.
Ndio haya tunayoyaona sasa.
Millioni 1.35 ni mshahara wa kufuru? Kweli tunatofautiana.watu wanalipwa dola 25000 ambayo ni kama millioni 40 kwa mwezi endelea kulalamika na vyeti vyako
Kweli kuna watu na viatu, unamuonea wivu rafiki yako?
Mleta mada atakua ni mfanyakazi wa halmashauri.over
Mie nachukua 700.000 after tax na maisha yangu Alhamdulilah! Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
Mdau Gsana na wengine! Umeeleza vema sana na kwa hoja zenye mashiko. Lipo tatizo kwa baadhi yetu wengi, hatusoma na kuielewa hoja na tunabaki kujivimbisha mabega na vifua kuwa tunajua watu wanaolipwa zaidi ya alichoshangaa mtoa mada.
Mtu anakuja na rejea ya serikalini na kioja rejea kinakuja na mishahara ya mashirika binafsi, huku ni kutoupa kazi ubongo na kusukumwa na mihemuko ya ndoto-jua.
Tunatambua misharaha ya serikali na hasa kwa wanaoanza kazi bila kujali kada imesimama kuanzia laki tano+. Zipo taasisi na mamlaka za serikali Sumatra ikihusika inalipa kutokana na kanuni walizojiwekea kama mamlaka huru.
Ndiyo, lazima nishangae na ni kweli kulinganisha 1.5m kwa 0.5m.
Tujifunze kutafuta maarifa na si kujifanya kuyajua yote