Waraka wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa Serikali

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
5,183
3,278
Wadau, nimejaribu ku'attach' doc hii nimeshindwa. Nimeamua niipaste hapa:

WARAKA WA WANAFUNZI WA ELIMU JUU KWA SERIKALI KUHUSU MIGOMO NA MAANDAMANOYA MARA KWA MARA VYUO VIKUU HAPA NCHINI Tunapenda kuchukua fulsa hii kwanza kuomba msamaha na kuwataka radhi wazazi wetu mliotutuma kwenda kutafuta Elimu vyuo vikuu hapa nchini kutokana na vurugu, migomo na maandamano ya mara kwa mara ambayo mmekuwa mkiyasikia au mkiyaona kupitia vyombo vya habari katika vyuo mbalimbali hapa nchini, pia tunaomba radhi toka moyoni mwetu kwa walimu wetu (lecturers) kwa adha inayowakuta pale inapotokea migomo na maandamano. Pia tunawaomba msamaha viongozi wetu wa dini ambao kwa namna moja ama nyingine wamekua wakitulea kiroho na kimaadili. Lakini tutakuwa hatujawatendea haki watanzania ambao kodi zao ndizo zinazogharamia Elimu yetu hapa chini, bila shaka walitegemea kutuona tukisoma kwa bidii na kufaulu vuzuri ili tutakaporudi katika jamii zetu tutumie elimu tuliyoipata kuwakomboa watanzania wenzetu ambao mpaka sasa wanalia na kuangamia na vita kubwa ya UJINGA, UMASKINI, MARADHI NA UFISADI. Lakini wameendelea kushuhudia migomo na Maandamano ya Mara kwa Mara yasiyo na kikomo. Baada ya kutafakari kwa kina kama wasomi tukaona kama hatutakaa chini na kufanya utafiti wa kina (research) ya vyanzo na sababu zinazotufanya tuwe na migomo, tuandamane na kufanya vurugu za mara kwa mara vyuoni. hatutaeleweka na tutaonekana kweli sisi ni wahuni, au tunatumiwa na watu ama wanasiasa wakati hizi ni tuhuma ambazo hazina ukweli hata chembe ndani yake, Lakini tunapenda kuwataarifu viongozi wetu, wazazi na watanzania kwa ujumla kwamba matatizo haya yanatokana na vitendo vichafu vya baadhi ya watumishi pamoja na sera mbovu za kiukandamizaji, kibaguzi, manyanyaso na uonevu uliovuka mipaka kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (vyuo vikuu). Na hatutaeleweka kwa walimu wetu waliojitolea kwa uzalendo wao wa hali ya juu kutufundisha japo maslahi yao ni madogo ukilinganisha na kazi kubwa wanayoifanya, Pia kama tungekaa kimya viongozi wetu wa dini ambao ni walezi wetu wa roho na maadili wasingeuelewa. vilevile hatutaeleweka zaidi kwa watanzani ambao wanatozwa kodi kwa ajira ya kugharamia elimu yetu ya juu ili tusome kwa bidii ili turudi kulitumikia taifa. Tumefanya utafiti huu wa migomo, vurugu na maandamano ya mara kwa mara ili tutoe taarifa ya upande wa pili wa wanafunzi kwani kumekuwa na desturi au utamaduni wa vyuo kutoa taarifa zisizokuwa na ukweli kwa wananchi(umma) kwa kuwasingizia wanafunzi kwamba wanatumiwa na viongozi wa siasa kufanya fujo, vurugu na migomo pindi matatizo haya yanapojitokeza, Taarifa hizi zisizokuwa na ukweli zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watawala wa vyuo ili kukwepa kutekereza madai yetu ya msingi kwa kisingizio hiki kisicho na ukweli ndani yake hata chembe kama ilivyonekana katika gazeti la mtanzania ISSN 0856 - 5678 toleo namba na 5842 Jumapili Januari 15 2012 makala ya 13 yenye kichwa cha habari kilichoandikwa kwa herufi kubwa na kusomeka hivi VURUGU UDSM. Uongozi wa chuo wadai waliofukuzwa ni wanasiasa pia habari kama hiyo ilichapishwa katika gazeti la uhuru ilisomeka hivi katika ya kwanza ya gazeti hilo VURUGU ZA UDSM: CHAMA CHA (……..) CHA SHUKIWA KUWA NYUMA YA MGOMO. ukweli wabainika nalo gazeti la mzalendo jumapili 15 January 2012 makala ya 7 ilikua na habari kama hizo. Kwa bahati Mbaya kwa upande wa wanafunzi hatukupata nafasi ya kukanusha madai hayo kwa ushaidi wa wazi kwa wazazi wetu, walimu wetu, viongozi wetu wa dini, na watanzania waliolipa kodi zinazotusomesha wakaamini madai yaliotolewa na serikali na utawala chuo kuwa ni sahihi. Wakatuhukumu na kuwafukuzwa chuo wenzetu kwa kutuhusisha kutumiwa na vyama vya siasa kitendo ambacho si kweli. Ili kukwepa na kupinga hoja na madai yetu ya msingi kwa majibu mepesi eti tumetumwa ni ajabu kweli! Namna hii siasa zinaingizwa katika chuo matokeo yake chuo kinakuwa sehemu ya kisiasa jambo ambalo si sahihi chuo ni taasisi inayojitegemea inapaswa kuendesha mambo yake bila kuingiliwa na taasisi nyingine. Hali hii ikiachwa iendelee kama serikali haitatekeleza mapendekezo yetu ambayo ni njia sahihi ya kupunguza vurugu migomo na maandamano vyuo vikuu nchini kama sio kumaliza kabisa tutaomba wazazi wetu, walimu wetu, na watanzania walipa kodi mtuelewe kwa maamuzi magumu tutakayo yachukua kama itakavyoonekana inafaa. Lakini vyuo vikuu vitapoteza sifa yake ya ndani na nje ya nchi. Vitabaki ni vyuo vya migogoro ya migomo, vurugu na Na kufukuza wanafunzi sio mwarobaini wa tatizo kwani maandamano, vulugu, migomo itaendelea kuwepo. Iwapo madai na mahitaji ya wanafunzi hayatatekezwa pia. Yapo madhara makubwa ambayo yanatokana na migomo vyuoni ikiwemo kuharibika rasilimali za chuo, kuharibu ratiba za masomo, Serikali inaingia hasara na gharama za ziada chuo kinapofungwa kwa mgomo. Kwani bajeti ya chuo inakua Ishapitishwa pia na gharama za kupeleka polisi na magari ya maji ya kuwasha na mabomu ya machozi n.k. Mbaya zaidi ni kwa wanafunzi kufukuzwa na kusimamishwa masomo ambao wamegharimiwa na kodi za watanzania wakitarajiwa kuhitimu na kurejesha mkopo na kulitumikia taifa letu. Tunaomba wazazi wetu, walimu wetu, viongozi wetu wa dini na watanzania walipa kodi. Kwa pamoja mtumie fursa hii kuishauli serikali kutekeleza mapendekezo yetu ili kuinusuru sekta mama ya elimu nchini isiyumbe na kuporomoka kwa kasi ya ajabu. Ni matumaini yetu kila kundi litatumia nafasi yake kuishauli serikali kupeleka mapendekezo yetu Inshallah. Ili binaadamu aweze kuzikabili changamoto za maisha na kujikomboa katika lindi la umaskini, lazima awe na elimu. Elimu ndio msingi wa kujitambua, kuyatawala na kuyatumia mazingira anayoishi binadamu ili kuboresha maisha yake na kujiletea maendeleo ya haraka, ni wazi kuwa elimu ndiyo ukombozi wa binadamu kuiona kesho iliyo bora zaidi na kuogelea katika bahari ya utandawazi ambayo inamtaka kila mmoja, aogelee kwa namna awezavyo. Kwa kutambua ukweli huo Serikali ya Tanzania imetoa fursa kwa wadau wa elimu kuwekeza katika sekta hiyo ili kujenga taifa la watu wenye Maarifa, ujuzi na uwezo wa kuzalisha. Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) pamoja na sera ya Elimu na mafunzo, zote zinaeleza umuhimu wa elimu ili kuiwezesha nchi kusonga mbele. watanzania na wazazi kwa ujumla wanatarajia kuona watoto wao wanapata Maarifa uwezo ili wachangie juhudi za watanzania na wazazi wao kutatua changamoto zilizopo katika jamii. Wanafunzi wenye Maarifa na ujuzi huwa na uwezo wa kufanya mambo mengi mapya kwa usahihi na kuwaongoza wenzao. Katika maendeleo ya ukweli katika jamii tunayoishi, Matendo ya wasomi, kazi zao, majukumu yao na shughuli mbalimbali wanazofanya zinapaswa kudhihirisha matunda ya elimu waliyonayo. Zao muhimu la elimu kwa mtoto ni kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri kwa makini . Uwezo huu ndio unahitajika sana katika jamii ya leo. Mtu mwenye uwezo wa kufikiri ndiye Mwenye nguvu ya kuibua dhana mpya na kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo. watu walioibua teknolojia tulizonazo, waliongozwa na upeo wa kufikiri ndipo wakaibuka na dhana mpya. Tendo la kufikiri lipo ndani ya akili na utashi wa mtu bila kufikiri matokeo ya juhudi za mtu mara nyingi huwa anguka au hasara. Serikali pamoja na wadau wa elimu nchini. Wanamchango mkubwa wa kuibua taifa la wasomi na kutekeleza Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025, mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) pamoja na sera ya Elimu na mafunzo ambazo zote zinaeleza umuhimu wa elimu ili kuiwezesha nchi kusonga mbele. “Kukua kwa uchumi pamoja na mambo mengine hutegemea uwekezaji hasa wenye manufaa kama elimu ili kupata wataalamu ambao ndiyo watainua uchumi wetu, kimsingi uchumi hauwezi kukua bila wasomi’, Nchi lazima iandae rasilimali watu ambao wanaitajika ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Na kusaidia familia zao. Maskini. Rais wa kwanza wa Tanganyika kwa sasa Tanzania aliwahi kusema maneno yafuatayo katika hotuba zake kwa wananchi kwamba. Hakuna serikali yoyote duniani inayowawekea wananchi wake hela mfukoni bali “the only best way to enrich a poor people is to educate their children”. Yaani njia pekee ya kuwasaidia wananchi maskini ni serikali kuwasomeshea watoto wao. Hii alikusudia kwamba ukimsomesha mtoto wa maskini atakapopata hiyo elimu ataitumia kuinua familia yake kiuchumi na Taifa kwa ujumla. Na ndiyo maana baada ya kupata uhuru Tanganyika, hayati Mwalimu Julius Nyerere alitambua maadui watatu MARADHI, UMASKINI na UJINGA. Lakini ili ukabiliane na maadui hawa lazima uanze na Adui ujinga kwa kutoa elimu bora kwa wananchi ili waondoe umaskini na maradhi. Lakini tume Shuhudia Serikali kwa sasa inavyo suasua katika sekta hii muhimu ya Elimu nchini. Na katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 9 kifungu kidogo cha (i) inasema hivi 9 (i) “Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi; Baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, na baadae Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – Tanzania Mwaka 1964, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alitangaza vita kwa maadui watatu, Ujinga, Maradhi na Umasikini. Mwalimu alihakikisha anafanikiwa katika Mapambano hayo. Alianza kuweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukazia elimu ili kufuta ujinga, kupatikana madaktari wa kupambana na adui maradhi na wataalamu wa uchumi wa kupambana na adui umasikini. Fikra hii ya Mwalimu ilidumu hadi kufikia maziko ya AZIMIO LA ARUSHA na kuanzishwa AZIMIO La Zanzibar – Februari 1991. ambalo liliamua kufuata Mfumo wa kibepari ambayo ilikusudia kumilikisha rasilimali ya Tanzania kwa wachache “Matajiri”. Baada ya hapo, Maadui hawa kukaa mbali waliwavamia Watanzania. Ujinga ulianza kuongezeka (idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika iliongezeka), maradhi yakaongezeka vifo kwa mama na mtoto, Uchumi ukadorora, umaskini ukaongezeka, shillingi ya Tanzania ikashuka thamani siku hadi siku huku mfumuko wa bei ya bidhaa ikiwaumiza wananchi wa kipato cha chini. Hilo ndilo Azimio la Zanzibar. Elimu ya Tanzania haijulikani iko wapi, mpasuko mkubwa baina ya watoto wa maskini na matajiri katika nyanja ya elimu imeongezeka. Shule za kimataifa (International Schools) zinafundisha masomo yote kwa kingereza wakati shule za akina kayumba zinafundisha masomo yote kwa lugha ya Kiswahili. Matajiri wanafanya kufuru kwa kuwalipia watoto wao ada katika shule za msingi inayolipwa na mtoto wa maskini katika vyuo vikuu, la ajabu kama si kushangaza akimaliza anaungana naye kutafuta mkopo, na cha ajabu anapewa kwa sababu ni mtoto wa kiongozi Fulani au tajiri Fulani, mtoto wa Maskini anarejeshwa nyumbani eti hajatimiza masharti na vigezo. Kama wameamua kujitenga kwa sababu ya fedha walizonazo, kwa nini wasiundiwe vyuo vyao na balaza lao la mitihani? Kwa nini wanafanya mtihani wa taifa ule ule kwa siku moja katika lugha mbili fofauti? Hii si mikakati ya mafisadi kuhakikisha kuwa madaraka ya nchi hii yanabaki kuwa ya kuridhishana kwa sababu ya watoto wao kuwa na elimu nzuri? Kwa nini elimu ya msingi katika nchi moja huru ifundishwe kwa lugha mbili tofauti tena chini ya wizara moja? Wakulima wanadanganywa kwa kuwekewa Shule za Sekondari za kata ambazo hata mtoto wa Diwani au Mratibu elimu wa kata, hasomi kule shule haina walimu wa kutosha, Vitabu, nyumba vya madarasa havitoshi, uwiano mbaya wa vitabu kwa kila mwanafunzi, mrundikano wa wanafunzi darasa moja, uhaba wa nyumba za walimu. wakati wengine wanabebwa kwa magari na kusoma katika vyumba vyenye viyoyozi, walimu wenye uwezo mzuri wa kufundisha na vitabu hali hii si kujenga chuki kwa jamii? Kama kweli dhamira ya kujenga utitiri wa Shule za Sekondari za kata ni kuinua elimu ya Tanzania ni kwa nini hakuna hata watoto wa viongozi yeyote wanaosoma katika shule hizi? Hii si sababu tosha ya shule hizi kukosa usimamizi mzuri, Enzi ya Baba wa Taifa, watoto wa watanzania ambao ni viongozi sasa. Walikuwa wanasoma pamoja, wanafanya mtihani mmoja, wanafundishwa kwa lugha moja, wanachaguliwa na kuwa katika sekondari moja, wanaishi kwa pamoja wakishirikiana katika kila jambo, sasa ni ubaguzi mtindo mmoja. Ukipita karibu na shule hizi za serikali utakutana na vibao vya wakina Pwagu na Pwaguzi, vibao vyenye kauli mbiu tata, za uongo mtupu, “Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi” Ingia ndani ya shule hizo au madarasani uone madudu yaliyomo kule. Ni kweli katika shule zile zinafundisha Ufundi au kunafundishwa Ufundi ? Kuna haja gani ya kutangaza biashara usioifanya ? Ni ufundi gani unafundishwa katika shule hizi za msingi? Wanamfurahisha nani katika Matangazo hayo? Watanzania wanapumbazwa kwa sababu ya maradhi, ujinga na umaskini uliopaliliwa na Azimio la Zanzibar. La kujiuliza na kushangaza katika shule hizi zote za msingi za serikali ambazo vibao hivi vimekuwa ni sehemu ya urembo, barabarani, hakuna hata Mwalimu aliyepewa hata kozi ya elimu ya ufundi ili aweze kuwafundisha wanafunzi japo kwa kubabaisha ni ajabu sana! Sera ya elimu ya kimataifa inaeleza kuwa ni wanafunzi 45 katika kila chumba cha darasa, watanzania kwa kuchakachua ni jadi yao mpaka wanapigana na wataalamu wa kimataifa. Ilimradi tu ruzuku imeongewa katika wilaya ufisadi ufanyike. Inafahamika kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi hutoa ruzuku kufuatana na wingi wa wanafunzi katika wilaya husika. Hivyo kinachosababisha wanafunzi kujazwa darasani katika chumba ambacho kinapaswa kuchukua Watoto 45 ni uongozi wa elimu wa wilaya zao maafisa elimu wa wilaya wanashinikiza wanafunzi waandikishwe wengi ili kupata ruzuku iliyo kubwa wapate cha kugawana. Sera ya Tanzania ya elimu ni watoto wote wapate elimu, lakini Je? Ni katika mateso kama haya ya kurundikwa katika chumba kimoja watoto zaidi ya 100? Walimu na hasa wanaofundisha shule za vijijini wanalalamika kuwa wanapewa mzigo mkubwa katika kufundisha, kwa sababu ya wanafunzi kuwa wengi na miundombinu finyu, uhaba wa walimu hadi wanashindwa hata kupumua, lakini pamoja na walimu hawa kulalamika kwa nini wanashindwa kutii sheria hii ya kimataifa ya wanafunzi 45 kwa chumba kimoja? Ukalimu wa walimu na uwoga wa walimu unatufikisha pabaya sasa wanazalisha taifa la wasiojua kusoma na kuandika kwa sababu ya uzembe wa Serikali. Tuangalie Elimu ya juu. Vyuo vikuu serikali ina mkakati gani wa kumaliza migogoro na vurugu zilizopo katika Elimu ya juu ya mara kwa mara yakiwepo maandamano. Yasiyo isha. Japo hata kipindi cha nyuma migomo hasa chuo kikuu cha Dar es Salaam ilikuwa inatokea lakini sio kama ilivyo kwa sasa. Na migomo ya wakati wa kipindi cha awamu ya kwanza na pili ilikuwa ya kupinga sera tofauti na migomo na maandamano ya sasa ya kupinga matokeo ya sera mbovu. Ni kweli wanafunzi wa vyuo vikuu leo hii wamekuwa na madai ya msingi kwa serikali hivyo kutokana na viongozi kutokuwa na utamaduni wa kukutana nao mapema kujua matatizo yao wanafunzi hulazimika kutumia njia ya kuandamana na kugoma kufikisha ujumbe wao kwa njia ya mgomo au maandamano kwa viongozi serikalini. ebu tuone baadhi ya migomo, vyuo vikuu nchini HALI YA ELIMU KATIKA MIAKA 50 UHURU WA TANZANIA (1961 - 2012) I. VUGUVUGU LA UJENZI WA SHULE NA VYUO VIKUU NA MATATIZO YAKE. 1. Nikiangalia matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini, machozi humilengalenga hasa kutokana na kutambua ukweli kuwa ubora wa Taifa lolote lile hutegemea na ubora wa elimu itolewayo kwa watu wake. Maana yake ni kwamba, Watanzania tukitaka kuharibu ubora wa Taifa, letu njia nyepesi ni kuua au kuharibu misingi ya kupatia na kutolea elimu bora. Kwa hiyo Watanzania tukikiuka misingi ya kutolea na kupatia elimu bora misingi hiyo itatukiuka. Leo hii Elimu Tanzania imekuwa ya kufanyiwa majaribio kila mara na viongozi wetu awamu ya Rais wa kwanza ilijitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika sekta ya Elimu kwani aliamini ndiyo sekta pekee ambayo ingeweza kutatua adui wengine wawili ujinga, maradhi na umaskini kama alivyobainisha. Baada ya nchi yetu kupata uhuru 1961 watanzania asilimia kubwa walikuwa hawajasoma. Serikali yake ikaleta Mfano wa Elimu ya watu wazima. Mwalimu Julius Nyerere Alisema: “ Elimu siyo miujiza fulani unaotokea darasani tu. ni kujifunza kutoka kwa wengine na kujifunza kutokana na mafanikio na makosa yetu wenyewe ya siku zilizopita” Mwalimu alisema Mwaka huu wa 1970 ni muhimu nguvuzikaelekezwakuwaelimisha wananchi na hasa watu wazima ili kutimiza ahadi za TANU. Alisema hiyo inasema “Nitajielimisha kadri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Katika salamu za mwaka mpya zilizo tangazwa kwa njia ya redio, Mwalimu alisema kuwa ingawa waanzania wengi wanazungumza sana habari ya Elimu ya watu wazima. “kamati kuu ya TANU sasa imeamua kwamba lazima tufanye kazi hiyo katika mwaka 1970 Miezi 12 ijayo lazima iwe na lengo la kuwaelimisha watu wazima” alisema. Mwalimu aliendelea “sisi ni maskini na tuko nyuma na watu wengi mno miongoni mwetu wanaikanili hali tuliyonayo kama kwambwa ni amri ya Mungu na wanadamu kuwa hatuna la kufanya kuondoa hali hiyo. Shahada ya kwanza ya Elimu ya watu wazima alisisitiza Mwalimu., lazima iwe Elimu ya kujiondoa katika kuikubali hali ya maisha ambayo watu wa Tanzania wameishi karne nyingi zilizopita. Alisema watanzania hawana budi kufahamu kwamba si lazima waishi katika vibanda vibovu, au walime kwa vijembe vibovu na katika hali ya udhaifu wa Afya, bali hawana budi kutambua wanaweza kuyakabili mambo hayo. Kazi ya kwanza ya Elimu ya watu wazima itakuwa kuwafanya wakatae vitu hivyo na kwamba wana uwezo wa kupata nyumba nzuri zaidi, vyombo vizuri ya zaidi vya kufanyia kazi na afya nzuri zaidi. Shahada ya pili ya Elimu ya watu wazima ni jinsi ya kujifunza jinsi ya kuyabadili maisha na hivyo hawana budi kujifunza jinsi ya kuongeza mazao katika mashamba katika viwanda na kwenye ofisi zao. Mwalimu aliongeza, watanzania hawana budi kujifunza habari za mipango ya maendeleo ya uchumi ili waweze kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa muda mrefu serikali na wadau wa masuala ya elimu wamekuwa wanatafuta sababu ya wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne kutokana na ukubwa wa tatizo hilo serikali iliamua kufanya uchunguzi na kubaini mojawapo ya sababu za ufaulu duni kwa wanafunzi hasa kidato cha nne ni kushushwa hadhi kwa mitihani ya kidato cha pili. Mtihani huo wa taifa wa kidato cha pili ulianzishwa mwaka 1984 kwa lengo la kutathimini maendeleo ya wanafunzi, baada ya miaka miwili ya masomo shuleni ambapo aliyeshindwa kufikisha alama zilizowekwa alirudia darasa. Hata hivyo 2008, serikali ilitamka wanafunzi ambao hawatapata asilimia 30 ya alama katika mtihani huo. Hawatarudia darasa ila wataendelea na masomo ya kidato cha tatu na kupatiwa mafunzo rekebisho. Ni kweli uamuzi wa kurudisha makali ya mtihani wa kidato cha pili ni wa msingi kwa kuwa unawapa wanafunzi sababu ya kusoma. Hata hivyo tatizo lililopo katika mfumo wa elimu Tanzania ni mchanganyiko wa uamuzi. Wakati ule ambapo mungai Joseph Mungai, akiwa waziri wa Elimu, alifuta masomo ya biashara shuleni, athari zake zinaonekana sasa hivi kwa wanafunzi wanaokuja vyuo vikuu. Yale masomo yalikuwa yanamwandaa mwanafunzi kwa masomo ya chuo kikuu sasa mtu anakuja akiwa hana maandaizi ya awali, hili ni tatizo. Mgongano wa uamuzi kama huo. Ndiyo pia uliofanya kufutwa kwa mtihani kwa kidato cha pili na matokeo yake wanafunzi wakawa wanaona hakuna sababu ya kusoma. Lakini kuhusu suala la kuwatoa kwenye mfumo rasmi wa elimu wale watakao kariri darasa mara moja na kushindwa kufaulu. Hili sio haki na tunaiomba serikali ibadili sera hii ya kuwaondoa wale wanafunzi watakao kariri darasa na kushindwa kufikisha asilimia 30 waruhusiwe kuendelea kukariri darasa mala mbili. Kwa sababu zifuatozo: i.Wale watoto ni wadogo sio vizuri kuwafukuza shule lakini wakiwa wanarudia darasa itawasaidia kujitahidi na kuhakikisha wanafanya vizuri. ii. Athari hii itawaathiri sana wanafunzi wa shule za kata ambao hawana walimu wa kutosha, vitabu maabara na ukosefu wa maktaba. Wapimwe sawa katika mtihani moja na wanafunzi wenye walimu bora,vitabu,maktaba, maabara na madarasa ya kutosha watakuwa hawajatendewa haki kwa sera ya serikali ya kutaka waondolewe kwenye mfumo rasmi na kubaki tu mtaani, itakuwa hawajawasaidia kw alolote lile, badala yake itakuwa ni mzigo kwa serikali na jamii kwa ujumla. Na ikizingatiwa uhaba wa shule za ufundi nchini. 2. SERIKALI HAIWATHAMINI WALIMU KAMA WAFANYA KAZI WENYE TAALUMA. Leo hii serikali imewatekeleza walimu na haiwadhamini kama wafanya kazi wengine. Mwalimu ambaye ndiye Mwaaandaji wa wataalamu wa fani zote. Kitu ambacho kimepelekea wanafunzi na jamii kwa ujumla kuiona siyo kazi ya maana. Huku serikali ikiwapumbaza walimu kwa maneno ya ualimu ni wito ili iwanyime haki zao za msingi na wawe wepesi” kuvumilia shida kama ualimu ni wito na siyo Taaluma mbona kuna vyeti vinatolewa vya ualimu mbona kuna madaraja na ngazi za ualimu, hizi zote ni njia za Serikali za kuwapumbaza walimu ili isiwalipe mishahara mizuri, nyumba nzuri za kuishi mafao yao mengine ya msingi. Leo hii ualimu umeonekana ni kazi anayoichagua Mwanafunzi baada ya kukosa kazi zote au kufeli, kabisa na kukosa sifa ya kusomea fani nyingine. Walimu wanaonekana kama wafanyakazi waliokata tama na kazi yao, wanaonekana wanyonge hawako huru katika kazi yao (peace in mind) kutokana na sababu zifuatazo. i. Kucheleweshwa na kutopandishwa madaraja na wanapopandhishwa madaraja mishahara yao haipandishwi. ii. Mazingira magumu ya kazi kama nyumba hazina umeme, maji na nyumba kuwa na hadhi ya chini/mbaya. iii. Umbali/mwendo wa muda mrefu kwend akazini/shuleni hawana vyombo vya usafiri. iv. Kunyimwa na kuzungushwa kupewa ruhusa ya kwenda kusoma/kujiendeleza kielimu. v. Idadi kubwa ya wanafunzi inayowaelemea kuhimili kuwafundisha. vi. Kutoshirikishwa katika ubadilishwaji wa mitaala mara kwa mara. vii. Kupewa mishahara midogo na serikali ambao hauendani na hali halisi ya maisha ya sasa. viii. Kupangiwa vipindi vingi vya kufundisha shule ni kutokana na uchache wa walimu shuleni. ix. Kudhalilishwa. Kwa kuadhibiwa na viongozi serikalini kama tulivyoshuhudia baadhi ya maeneo. x. Serikali kukataa kuwalipa malimbikizo yao ya mishahara kwa kisingizio cha kuhakiki majina uongo mtupu. Ni uhakiki gani huo usioisha muda wote. Leo hii walimu wameamua kujishughurisha na ujasiliamali wa biashara ndogo ndogo na kuamua kutangaza mgomo baridi ambao bado serikali haijaushtukia yaani wanafika kazini kama kawaida lakini wanafanya kazi nchini ya viwango wanaingia darasani lakini hawafundishi kama inavyopaswa kujitolea. Mfano mwalimu Juma anayefundisha shule ya Mtoto wa mkulima somo la Hisabati darasa la Tano lenye wanafunzi 120 atapata wapi muda wa kuelekeza kila Mwanafunzi aelewe (Individual) atapata wapi muda wa kupitia madaftari ilihali anakipindi kingine darasa la NNe, pia anakipindi kingine darasa la sita cha kiingeleza kwa siku na yote madarasa yana zaidi ya wanafunzi 100 kila darasa. Matokeo yake leo hii tunashuhudia Maelfu ya wanafunzi shule za msingi wakimaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika huku kidato cha NNe na sita wakiambulia daraja la mwisho (division iv na zero) Na serikali ikishindilia kabisa kudidimiza Elimu nchini kwa kuchukua wale wanafunzi waliofeli au waliofanya vibaya katika mitihani yao ya Taifa eti ndiyo wasomee ualimu ili wawe waalimu. Labda ndiyo Maana haiwadhamini na kuwatekeleza kiasi hiki ukilinganisha na wafanyakazi wengine. Ni kichekesho Mwanafunzi aliyepata daraja la NNe (Division iv) awe mwalimu amwandae mwanafunzi ambaye hana vitabu, maabara na uchache wa walimu apate daraja la kwanza (Division i) kati ya wanafunzi 100 utapata wanafunzi 5 na wanafunzi 95 watafeli wengi wao watapata (Division iv) kama yeye wengine zero. 3. Kuna wakati Tanzania ikisherehekea uhuru wake, hayati Mwalimu Julius k. Nyerere Rais wa kwanza wa habaari kutoka nje ya nchi. Jamhuri ya Tanzania aliauzwa swali lifuatalo na waandishi wa habari kutoka nje ya nchi. Kitu gani. hasa kinawafanya Watanzania msherehekee siku hii ya Uhuru weni? Hayati J.K Nyerere aliwajibu kuwa Watanzania walikuwa wakisherekea siku ile kwa sababu ya kuwa hai hadi siku ile. Huenda jibu lile lilikuwa sahihi. Hata sisi tungeulizwa swali kama lile leo bila shaka tungejibu kama alivyojibu hayati J.K Nyerere. 4. Je hali ya elimu nchini ikoje? Kuna wakati nchi yetu ilisifika sana kwa kufanikisha Elimu ya Msingi kwa kutumia njia za kimapinduzi chini ya ushauri wa mzee Nicholas Kuhanga. Wakati huo Tanzania ilitoa Elimu ya Msingi na Elimu ya kisomo bura kwa watoto na watu wazima wote. Vilivile serikali ilitoa elimu ya sekondari nayo vyuo vikuu kwa malipo kidogo. Kumbuka elimu hiyo itlithaminiwa kote duniani. Dosari kubwa katika utoaji wa elimu ya sekondari nayo vyuo vikii ni kwamba kwa muda mrefu hata baada ya Tanzania kupata uhuru iliendelea kutolewa kwa watu wachache sana. Leo elimu ilele inatolewa kwa watu wengine zaidi na kwa gharama nafuu zaidi. II. VUGUVUGU LA UJENZI WA SHULE NA VYUO VIKUU NA MATATIZO YAKE. 5. Ni katika miaka ya hivi karibuni tu ndipo vuguvugu la ujenzi wa shule za sekondari za serikali, za binafsi na vyuo vikuu lilianza kujitokeza na kusababisha leo Tanzania kuwa na vyuo vikuu na vyuo vishiriki kufikia 40. leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaota kama uyoga. Pongezi ziwaendee wananchi na wote waliohusika na ujenzi wa shule hizo. Kwa upande wa sekondari watu binafsi wanajenga shule hizi kwa kutegemea fedha zitokanazo kwa wazazi wa watoto wakati kwa upande wa Vyuo vikuu watu binafsi wanajenga kwa kutegemea mikopo toka BODI YA MIKOPO. Kwa hiyo bila mikopo hiyo (Loan Board). Baadhi ya vyuo vikuu haviwezi kudumu. 6. Hata hivyo mwamko wa wazazi kupenda elimu umesababisha elimu kupatikana kwa njia za ulanguzi. Shule za binafsi ni za watu wenye uwezo, kama zilivyo hospitali binafsi. Leo shule za serikali ndizo shule za watu wa kawaida. Tatizo jingine linatokana na wamiliki wa shule za binafsi ni kuwarubuni walimu wa shule za serikali ili wajiunge na shule zao na ili kuwapata huongeza mishahara na malupulupu mengine mengi. Matokeo ya kufanya hivyo ni shule za binafsi kufaulisha watoto vizuri kuliko shule za serikali. Leo baadhi ya wazazi wako tayari kupelekea watoto wao katika shule za binafsi hata kama wamechaguliwa kwenda katika shule za serikali. Wazazi hawaelewi kwa namna gani shule yenye 7. wanafunzi zaidi ya 400 inaweza kuendelea kielimu wakati ikiwa na walimu watatu au wane tu. Shule tunazo lakini zinakabiliwa na uhaba wa kila kitu (walimu, vitabu, maabara, vyumba vya madarasa, mabweni, matundu ya vyuo, nyumba za walimu, maktaba nk.) maneno ya kuzingatia hapa ni UHABA na UKOSEFU walimu wa masomo, huduma ya maji, umeme, zahanati, mabweni, viwanja vya michezo, vifaa vya michezo na kadhalika. Msamiati huu pia unatawala vyuo vikuu, vya ualimu, shule za Elimu ya Msingi, vyuo vya ufundi na kadhalika. NI UHABA NA UKOSEFU wa mahitaji katika kila ngazi ya elimu. Shule za sekondari za kata au shule za madiwani zote zinakabiliwa na uhaba na ukosefu waq mahitaji ya shule. 8. Kutokana na UHABA NA UKOSEFU huo elimu inaporomoka KATIKA NGAZI ZOTE. Hii ndiyo hali ya elimu nchini Watanzania wanaopenda ukweli wanajua ukweli huu. Kazi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vitapoteza umuhimu wa kuwepo kwake. Tume ya elimu ya 1982 inasisitiza sual hili. Naomba wale ambao hawajasoma ripoti ya TUME YA ELIMU ya mwaka 1982 na mapendekezo ya tume yake waisome. Sehemu kubwa ya mapendekezo yale ni muhimu zaidi leo kulilo mwaka 1982. inasikitisha kuona kuwa Watanzania wengi hatuna muda wa kusoma vitabu au maandishi! Tuna muda wa kufanya mambo mengine! Binafsi naamini kuwa TUME ya 1982 ilifanya kazi nzuri. Wajumbe wa tume ile wengi wao wangalia hai. Kwa namna gani wanashirikishwa katika kuboresha elimu nchini ni swala zuri la kujiuliza. Kwa tabia ya watanzania si rahisi kuwashirikisha watu wengine katika mambo yetu. Kwa mfano, Mwalimu Nicholas Kuhanga aliyefanikisha UPE katika nchi yetu kwa nini tusimshirikishe katika uboreshaji wa elimu nchini? 9. Leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaongezeka wakati ubora wa elimu unazidi kupungua. Kwa mfano, katika matokeo ya mwaka 2010 nusu ya vijana wa kadato cha nne waliofanya mtihani wa Taifa hawakufaulu. Hata katika miaka mingine, vijana wengi wanafaulu kwa viwango vya chini yaani, divisheni 3 na 4 idadi ya wale wanaoshindwa mitihani ya mwisho minazidi kuongezeka. (Tanzania kiambatanisho) kuonyesha kuwa ubora wa elimu nchini unaporomoka. 10. Labda wengine hawapendi kusikia maneno, kushuka kwa ubora au kuporomoka kwa elimu. Naomba watushauri tutumie maneno gani? 11. Sisemi kuwa elimu imekufa bali nasema ubora wa elimu umepungua (vijana wengi kushindwa mtihani wa kidato cha nne). Mfano Baraza la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana 2011 yanaoneasha kuwa asilimia 53.59% ya wanafunzi 426,314 waliofanya mtihani huo wamefaulu huku ikitangaza viwango vya ufaulu kama ifuatavyo. Wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni 33,577 sawa na 9.98% wamefaulu huku wasichana waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 10,313 sawana 7.13% na wavulana ni 23,267 sawa na 12.13% Na waliopata Daraja la NNe ni 146,639 sawa na 43.60% ambao wavulana ni 87,039 sawa na 45.40% na wasichana 59,600 sawa na 41.22% Na waliofeli (zero) ni 156,089 sawa na 46.41% kati yao wavulana ni 81,418 sawa na 42.47% na wasichana wakiwa na 74,667 sawa na 51.64%. kwa maana hawa hawatapata vyeti vya kuhitimu kidato cha NNE. Na huku wanafunzi 3,303 wakifutiwa matokeo kutokana na udanganyifu Mwaka juzi 2010 wanafunzi 450,324 walisajiliwa kufanya mtihani ambao wasichana walikuwa 201,799 sawa na 44.81% na wavulana 248,525 sawa na 55.19% ufaulu wao ulikuwa kama ifuatavyo 2010. wasichana waliofaulu ni 69,913 na wavulana 110,303 kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 44,910 wasichana wakiwa 20,972 na wavulana 23,938; Hivyo kwa mahesabu ya kawaida wanafunzi 180,216 ndiyo waliofaulu kati ya 450,324 mwaka 2010 na wanafunzi 270,108 wako barabarani wanaungua na jua sababu walifeli kabla wazazi hawajaishiwa na uchungu wa wanao kufeli kidato cha NNe 2010 konteina la NECTA limeshusha mzigo mwingine wa wanafunzi 156,089 mwaka 2011 nao wamefeli poleni sana wazazi wetu, poleni sana wadogo zetu kwa matokeo hayo mabaya ambayo hata cheti cha kidato cha NNE hamtapata. Hivyo ndani ya miaka miwili 2010 na 2011 Ndugu zetu wanafunzi wa kidato cha NNE 426,192 wamefeli kati ya 876,638 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 na 2011. Hili tunaomba Serikali ilitangaze kama (JANGA LA KITAIFA) kama vijana 426,192 wako mtaani wanateseka na ugumu wa maisha na ni upi mustakbali wa maisha yao watapataje ajira hawa hata vyeti vya kidato cha nne hawatapata Na hii ni miaka miwili je itakuwaje miaka 50 ijayo. Pia tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu hali ya elimu katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania imeonyesha kuwa Tanzania inatoa elimu hafifu kuliko katika zoezi hii unaweza kuendelea ila naomba tutenganishe utaalamu na siasa. Kwa mfano, kuna baadhi ya wana siasa wanapendekeza kuwa mitihani ifutwe katika ngazi zote Fulani za elimu. Lakini hawapendekezi njia gani zitumike katika kupima elimu itolewayo nchini. Hata hivyo sielewi lengo lao nini hasa. Watanzania tukikiuka msingi ya kutolea na kupatia elimu bora, misingi hiyo itakiuka. 12. Lazima tujiulize maswali yafuatayo kuhusu Elimu itolewayo katika nchi yetu: Tunataka nini katika elimu yetu. Tuataka elimu yetu itatue matatizo gani? Je elimu hii inatatua au inaongeza matatizo? Je tunataka elimu ya bure nay a lazima kwa watanzania wote na ifikie ngazi tunataka elimu ya bure nay a lazima kwa watanzania wote na ifikie ngazi gani? (MSINGI AU YA SEKONDARI AU VYUO VIKUU) je kuna uhusiano gani kati ya maendeleo katika katika elimu na maendeleo yetu kiuchumi? Je, kwa namna gani BODI YA MIKOPO itaweza kukidhi mahitaji ya vyuo bila kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sera ya Elimu? Kwa nini watoto wa matajiri ambao tangu elimu ya awali, msingi na sekondari wamekuwa wakisoma katika shule za binafsi kwa gharama kubwa leo wanaomba mikopo na serikali inawapa mikopo hiyo. Tatizo hili halijatatuliwa. III. TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA ELIMU LAKINI Elimu ni ufunguo wa maisha, ndivyo ambavyo watanzania wengi tunaamini hivyo, kwani elimu husaidia kutupa maarifa ya kuweza kuishi vyema kutokana na mazingira tuliyopo na kupanua upeo wetu wa mawazo. Pia elimu hutusaidia kupata ajira au kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali, kujitambua kuwa na upeo wa kunga’mua mambo mbalimbali ili kuweza kuishi sambamba na mazingira. Katika nchi yetu miaka ya hivi karibuni kiwango cha elimu kimeonekana kushuka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Tumejaribu kumtafuta mchawi, lakini mpaka sasa hajapatikana, ukweli ni kwamba tatizo kubwa lililopo ni mfumo mbovu wa elimu uliopo, walimu wengi wamepoteza ari ya kutimiza majukumu yao ya ufundishaji. Kubadilika badilika kwa mitaala, uchache wa zana za kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi, uongozi mbovu, walimu kutolipwa stahiki (madeni) kwa wakati na matatizo mengine lukuki yaliopo katika wizara ya Elimu ni tatizo kubwa linalorudisha maendeleo ya elimu nyuma hapa nchini. Mfumo mzima wa elimu katika nchi yetu umekuwa haueleweki hivyo kusababisha kuwachanganya walimu na wanafunzi katika masomo. Kila kiongozi anayeingia katika wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi anakuwa na msimamo wake, wakati wa uongozi wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Bw. Benjamin Mkapa, kuna waziri alipewa dhamana kuiongoza wizara hiyo na matokeo yake akakulupuka na kuamua kuyavunja masomo ya Jiografia, Uraia na Historia katika shule za msingi na kubakiza somo moja ambalo aliliita Maarifa ya jamii. Tanadiliki kusema kuwa alikurupuka kwani hakuweza kufanya uchunguzi na kujua uwezo wa walimu wake wa kufundisha masomo hayo matatu kwa mara moja tena kwa mwalimu mmoja. Na baadae ilikuja kugundulika kuwa kuna baadhi ya walimu hawawezi kumudu masomo yote hayo na badala yake anauwezo wa kufundisha Uraia, lakini hana uwezo wa kufundisha Historia hivyo Mwanafunzi ndiye anayeumia kwa kutopata taaluma iliyokamilika. Kwenye shule za sekondari Waziri huyo aliamua kuunganisha masomo ya chemistry na physics na kunganishwa kama somo moja na kuitwa (chemistry with physics) la kujiuliza hivi huyo waziri alijiuliza kama kama Mwalimu aliyesoma fani (combination) CBG hawezi kuimudu au kufundisha PHYSICS akipangiwa kufundisha somo la chem./phy. Ninashukuru kwa kuwa serikari iliyopo madarakani imeliona hilo na kuamua kurudisha mfumo wa zamani wa kila somo kujitegemea ingawa kodi za wananchi ziliteketea kwa kutunga tena vitabu badala ya hizo pesa kufanya kazi nyingine kwa jamii. Kuna tatizo la walimu kupoteza ari ya kufundisha, hali hiyo imesababisha wanafunzi kutopata taaluma iliyokamilikan matokeo yake kufeli na kufutiwa mitihani mfano kidato cha nne mwaka huu wanafunzi 3303 na darasa la saba wanafunzi 9700 wamefutiwa mitihani kwa madai ya kuibia mtihani ni muhimu Serikali ikajiuliza kwa nini Wanafunzi hawa wanaibia mitihani?. Hii inasababishwa sana na walimu kutolipwa madeni yao ambayo wanaidai serikali na kutoboleshewa mishahala, mazingira ya kazi na wakati mwingine kupoteza kabisa matumaini ya kutolipwa stahiki zao na wao kuamua kulipiza kisasi kwa kutofanya kazi kwa bidii na maarifa. . Walimu wapo kwenye mgomo baridi serikali ifanye utafiti itagundua bado haijashutuka. Lakini Wanaoumia zaidi ni wanafunzi na walimu wengine wameamua kuacha kazi na kuamua kurudi mitaani na kuendelea na maisha mengine. Katika hatua yoyote ya ufundishaji na ujifunzaji zana ni muhimu, lakini cha ajabu na kushangaza shule nyingi hazina zana za kufundishia wala kujifunzia na pale ambapo zipo ni chache, haziko imara au zimepitwa na wakati. Hapo ndugu zangu Watanzania mnategemea Elimu ipande labda kwa nguvu za miujiza ya Mungu au nguvu za giza. Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu na kidato cha NNE mwaka huu tumeshuhudia wanafunzi wengi wakifutiwa matokeo yao kwa kile kilichoitwa Eti ni udanganyifu. Tunazitupia lawama zote kwa serikali, mfano huyu mwalimu ambaye halipwi vizuri, hana nyumba nzuri ya kuishi (haina umeme,maji,choo), mshahara hautoshi (ugumu wa maisha) hana zana za kufundishia na hata motisha pia hapati mwaka mzima, ATAWEZAJE KUFUNDISHA?. Na je? Wanafunzi watapataje maarifa ya kutosha na kuweza kujibu maswali kwa usahihi katika mitihani yao kama si kuwatafutia majibu ili wafaulu hata wasiojua kusoma wala kuandika kama sio kuwatupia mzigo? Pamoja na hayo yote, lakini pia tunaipongeza Serikali kwa kujenga shule za kata, ambazo hazina zana za kufundishia. Mwalimu mmoja shule nzima yeye ndiye mwalimu mkuu na pia ndiye mwalimu wa somo, yeye ndiye mwalimu wa zamu, nidhamu, taaruma na uchache wa madawati HIVI HAPA TUNATEGEMEA KUPATA TAIFA LENYE WASOMI KWELI WATANZANIA? Na kurudishwa kwa mitihani ya kidato cha pili hatudhani kama ni hatua ya kuokoa Elimu ya Tanzania. Ni sababu gani zilipelekea mitihani hiyo ya kidato cha pili kufutwa na sasa kurudishwa? Jamani ELIMU SIYO SIASA YA MAJARIBIO. Suala la msingi kwanza ni kubadili mfumo mzima wa ELIMU TANZANIA na kuboresha shule za kata zinazochukua maelfu ya watoto maskini kwa kuwaajiri walimu wa kutosha wenye uwezo mzuri wa kufundisha, kuwalipa walimu stahiki zao, kubolesha mishahala yao (kima cha chini) na pia Serikali iwasikilize wadau mbalimbali wanapotoa maoni yao juu ya uboreshaji wa Elimu yetu ili tulikomboe Taifa letu. Zaidi rejea mapendekezo yetu. katika makala haya tunazungumzia mafanikio na matatizo ya elimu katika miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Takwimu kuhusu idadi ya shule, vyuo, walimu na wanafunzi zinapatikana kwa urahisi kutoka wizara husika. Takwimu hizo zinaonyesha kuongezeka kwa kila kigezo cha kutolea na kupatia elimu nchini. Tunashauri tuzitumie vizuri taarifa hizo. Kwa mfano, idadi ya dhule za sekondari za serikali imeongezeka sana. Kwa mfano, idadi ya walimu wa shule hizo, lakini vipi uwiano kati ya walimu na wanafunzi katika shule hizi? Ukweli ni kwamba walimu ni wachache kwa uwezo wa kufundisha na kwa idadi yao. Kutokana na uchache na uwezo wao mdogo wanafunzi katika ngazi zote za elimu nchini hawapati “dozi” kamili ya elimu wanayotakiwa kupata hali inayosababisha wanafunzi kumaliza elimu wakiwa hawajapata “dozi” kamili ya elimu wanayotarajia kuipata. Kwa hiyo watanzania tusishangae kwa nini nchi yetu ni ya mwisho katika utoaji wa elimu bora katika Afrika ya Mashariki. Kamwe vijana wetu hawataweza kupata elimu bora ya Msingi au ya sekondari,na Vyuo vikuu kwa kukaa tu katika majengo yaliuoandikw “shule” au Chuo kikuu. Kamwe vijana hawatawez kupata elimu ya ngazi yoyote ile kwa njia ya OSMOSIS. Upatikanaji wa elimu bor un kanuni na misingi yake. Tukikiuka misingi ya utoaji elimu bora misingi itatukiuka. Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya. IV. TUNAPATA WAKATI MGUMU KATIKA MASUALA YA ELIMU Watanzania tunapita wakati mgumu kiasi kwamba hata kubaki hapa tulipo ni kazi ngumu, kurudi nyuma ni kazi rahisi, kwenda mbele ni kazi ngumu zaidi. Breki za gari tulilopanda hazishikiki. Kuna hata ya gari kuruki nyuma. Gari hili ni nchi yetu ya Tanzania. Nchi ikirudi nyuma tutapoteza hata mafanikio kidogo tuliyoyapata katika miaka 50 ya uhuru. Hali inazidi kuwa mbaya. Vyanzo vya maji vinakauka, nchi inakosa umeme gharama za huduma muhimu zinazidi kupanda mfumuko wa bidhaa unapanda kwa kasi vijana wanakosa ajira na nguvu kazi yao haitumiki. Maana yake ni kwamba mapendekezo yoyote ya kuboresha elimu lazima pia yaonyeshe nchi itapata wapi fedha kufanyia kazi hiyo? Kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa ushuru kuondoa na kufuta aina zote za posho za semina, (sitting allawance) katika ofisi za umma Taasisi za umma kwani ni pesa nyingi zinapotelea huko bila sababu za msingi, fedha za kutosha za kuboreshea sekta ya elimu. Fedha ya misululu ya magari makubwa yaendayo Zambia, Malawi na Congo kila siku inatumikaje? Watu wamepata wapi fedha ya kununua utitiri wa malori, magari madogo na mapikipiki yanayosababisha barabara zisipitike katika miji yetu? Pamoja na umaskini wetu lazima watanzania tujue kuwa maendeleo yetu yataletwa na sisi wenywewe kwa bidii, maarifa, nidhamu, na kwa kuitegemea. Serikali inauwezo mkubwa wa kutunga sheria na kuweka taratibu za kusimamia uchumi lakini haina uwezo wa kusimamia taratibu zake. Ni nchi zenye serikali imara kama Marekani ndizo zinaweza kusimamiea uchumi wake. Kwa mfano serikali bila kupanga imekabidhi uchumi wa Tanzania kwa watu wachache ambo inashinswa kuwatoza kodi. Kwa nini tusichukue hatua zifuatazo:- a. Tusimamie vizuri shughuli zote za maendeleo ili kuzuia ufujaji wa fedha. b. Serikali isimamie elimu italewayo nchini ili kuondoa Ulanguzi Utapeli nauchakachuaji na iboreshe zana za kusomea hasa shule za kata (vitabu maabara walimu maktaba) c. TCU iongezewe madaraka zaidi kuhusiana na vyuo vikuu d. Tuongoze ufanisi katika kazi zetu na kupenda kufanya kazi e. Tubane matumizi na kutumia vizuri kila senti tunayopewa. f. Tuache rushwa, ufujaji mali ya umma na uvivu. g. Tupunguze sherehe, tafrija, mikutano, semina na kpngamano yanagharimu pesa nyingi. h. Tutumie vizuri wakati i. Tupunguze michango ya starehe (Inner partu, Send-off, Bag Party, Kitchen Party na Wedding part) na tuwekeze elimu . j. Tusipinge migomo badala yake tujue kwa undani sababu ili kama ni uzembe hatua kali ziwe zinachukuliwa kwa wahusika mapema. k. Kama idadi ya wanafunzi wa kwenda vyuo vikuu huwa haijulikani hadi mwezi mmoja kabla ya vyuo kufunguliwa tunategemea nini. Tujisahihishe. Nani alaumiwe? Kama migomo huzaa matunda kwa nini ifutwe. l. Tuanzishe michango ya maendeleo ya elimu badala ya michango Harusi. m. Tubadili mwelekeo wetu au mtazamo wetu kuhusu umuhimu wa mambo (mindset). Kwa mfano kuongeza ubora wa elimu bila kuwashirikisha wananchi katika gharama. 12. Kama kuna wakati mzuri wa kubadili mambo au kufanya mapinduzi katika elimu basi wakati huo ni sasa. Mwamko wa watu wa kuelewa na umuhimu wa kutoa elimu kwa watoto wao umeongezaeka. Matatizo ni mengi, na hakuna nchi isiyo na matatizo ni muhimu suala la Elimu liwekwe wazi katika katiba mpya ijayo. 13. Elimu kwanza. Kwanza Inaelekea treni la elimu liko nje ya reli. Watanzania tunawezaje kulirudisha treni katika njia yake. Tanzama baadhi ya shule za Elimu ya Msingi bado baadhi ya wanafunzi wanamaliza karasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika ½ ya wanafunzi wanaomaliza kadato cha nne wanafeli mtihani wa mwisho. Kama watoto wanamaliza elimu ya msingi bila elimu ya msingi wataendeleaje mbele? Ni Elimu gani hii ambayo haimwezeshi mwanafunzi kuwaelezea watu kile anachokijua au kubuni na kuibua mabo, kufikiri kisayansi, au kupeleleza na kuchambua mambo, kuumba vitu, kutafuta njia sahihi za kutumia katika kutatua matatizo yake. Tukubali kuwa elimu yetu ni butu. Tofauti na wenzaao walioachwa nyuma baada ya kumaliza elimu ya Msingi hawawezi kulima, kuzurura mitaani na kucheza disco. Lakini ajabu ni kwamba vijana hawa wanataka makuu, wanataka wakipanda mahindi asubuhi wavume jioni. Mara wakianza kazi wanataka kuwa na simu pana, gari la kuendea kazini na nyumba nzuri ya kuishi. Pale wanapokosa vitu hivi hupauka akili na huwafanya wafanye yasiyotegemewa. Vijana hawa ni wengi na wanaongezeka kila mwaka. Serikali isipowatumia vijana hawa watu waovu watawatumia. V. HOJA YA KUTUMIA UZOEFU ULIOKO NCHINI. 14. Duniani hakuna kidumcho isiopkuwa mabadiliko. Watanzania wana haki ya kupata kilicho bora katika nchi yao ikiwa ni pamoja na kuwatumia watumishi bora waliostafu na vijana wenye akili kwa faida ya nchi yao. Tabia ya kuwatenga au kutowatumia watu hawa ni tabia mbaya inayodidimiza nchi yetu. Kuwatenga watu kwa sababu za kisiasa au kwa sababu ya kuwaogopa au kwa sababu ya roho mbaya ni ufisadi wa aina yake. Wenzetu huko Ulaya ambako tunainga mambo mengi wanafanya hivyo. Si vema kwa baadhi ya watanzania kuonekana hawatakiwi au wanaishi kwa hisani ya watu Fulani. Wale wenye uwezo au madaraka wanaweza kumuua raia yoyote au kumtesa au kumtenga kwa sababu zozote zile ila sssshawawezi kunyang’anya utaifa na uraia wake, hawawezi kumfukuza katika nchi yake. 15. Tume ya elimu ya chini ya uenyekiti wa MAKWETTA (1982) ilichambua hali ya elimu iliyokuwa ikitolewa wakati ule hapa nchini. Pia ilitembelea nchi nyingi zilizoendelea na zisizoendelea ili kujifunza taratibu zao za utoaji elimu. Tume ilijifunza mengi na kutoa mapendekezo kwa serikali. Ni muda mrefu umepita tangu (1982). Kama serikali inatekeleza au haitekelezi mapendekezo ya Tume mimi sina la kufanya. Ajabu tangu tume ripoti ili hawajawahi kuitwa au kuulizwa lolote na wizara husika kuhusu elimu nchini. Kwa maoni yangu hii ni kasoro kubwa katika nchi yetu.nchi haifaidiki na utajiri wa uzoefu wa watu walio nje ya mkondo wa serikali kwa sababu ya sababu zilizoeleweka (wataalamu majaji, wanajeshi,walimu, mawaziri hawatumiki). Watu hawa ni hazina ya nchi na si tishio kwa yeyote. Nchi hii ni yetu sote. Tusiwaenzi watu wliostaafu baada ya kufa kwa kuhudhuria mazishi yao. Tusisubiri watu wafe ndiyo tuseme mazuri yao. VI. BAADHI YA VIKWAZO VILIVYO MBELE YETU. Huenda mapendekezo ya Tume ya MAKWETTA yamepitwa na wakati. Hofu yangu ni kwamba tangu Tume ili itoe mapendekezo yake kwa serikali hawajawahi kuitwa kutoa ushauri au ufafanuzi wowote kuhusu mapendekezo ya Tume. Napendakeza iundwe Tume nyingine kwa madhumuni yaleuale ili kukidhi mazingira ya karne ya 21. tusichezee elimu madhara ya uharibifu yatakuja jitokeza miaka michache ijayo. 16. Hapa chini tunatoa mapendekezo lakini mapendekezo haya yatafanikiwa tu kama baadhi ya mambo yaliyoko yatabaki kama yalivyo. Mabadiliko katika baadhi ya mambo yalioko leo yataathiri nguzo muhimu za kutolea na kupatia elimu. Kwa hiyo mapendekezo yoyote kuhusu mabadiliko katika mfumo wa elimu nchi nzima yazingatie mambo yafuatayo:- 1) Kuongeza kwa idadi ya watu ambao hawana elimu ambako kuasababisha kukua kwa umaskini. 2) Kuweko kwa watu wenye uzoefu na kutotumia uzoefu wao kujenga Taifa letu kwa sasabu ya tofauti za kisiasa. 3) Kushuka kwa uchumi kutokana na kupungua kwa mafuta, gesi, maji, umeme, madini nakadhalika. 4) Uhaba au kukosekana kwa chakula (njaa). 5) Kukua kwa umaskini na kukosekana kwa amani. 6) Kukosekana kwa ajira na kutotumika kwa nguvu kazi. 7) Ubaguzi wa kipatao (maskini na matajiri) kuongezeka kwa mpasuko kati wenye nacho na maskini. 8) Kurudi kwa ukoloni mambo leo na utumwa 9) Wenyenavyo watashika mali na utawala wa nchi 10) Kustawi kwa ukoloni mamboleo. Nchi itageuka nchi ya ombaomba. Kesho ni leo na leo ni kesho. Kwa hivyo kila jambo tufanyalo au tusilofanya leo linajenga au kubomoa missingi ya maendeleo yatu ya kesho. [The future is now.] VII. HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUZUIA KASI YA KUPOROMOKA KWA ELIMU NCHINI. 17. Kobe kufanya maendeleo pale tu anapothubutu kutoa shingo yake nje ya gamba lake. Kwa hiyo pamoja na yote yanayosemwa kuhusu elimu, ni vigumu sana kutabiri kuhusu mambo yatakavyokuwa kesho. Labda tutumie ujenzi na uzoefu wetu katika kuelezea baadhi ya viini vya matatizo katika shule na vyuo vyetu:- 1. Wizara ya Elimu iunde haraka Tume ya Elimu ili kutizama matatizo ya elimu na mwelekeo wake kwa lengo la kuzuia Tanzania kuachwa nyuma kielimu au kuzuia kuporomoka kwa elimu. 2. Serikali isimamie na kuratibu elimu katika ngazi zote ili kuzuia biashara na ulanguzi katika elimu chini. 3. kutokana na uwezo mdogo wa walimu hasa walimu wa shule za sekondari, yaanzishwe mafunzo ya kuboresha elimu yao wawapo kazini 4. Serikali itizame upya sera ya kugharamia elimu nchini ili kuhakikisha kuwa fedha ya umma inatumika vizuri na inatolewa mapema kwa wahusika. 5. Hatua za kuboresha elimu zianzie katika vyuo vya ualimu, vyuo vikuu na shule za msingi na mafunzo kazini. 6. sekta ya ukaguzi imarishwe kwa kuongeza wakaguzi na vyombo vya usafiri. 7. migomo shuleni na vyuoni inaathiri sana maendeleo ya elimu nchini licha ya kuharibu mali ya umma. (Sera ya Mikopo bado hafifu) 8. wanafunzi washirikishwe katika masuala ya maamuzi yanoyo wahusu na sio watawala wanawaamulia kila kitu bila wao kushilikishwa 9. wanafunzi wajihusishe na ubora na usalama wa mazingira ya shule na vyoo badala ya kubaki na 3ks tu yaani KUSOMA,KULA NA KULALA. 10. ubadilishwaji wa mitaala ushilikishe pande zote kama walimu, wadau wa elimu, wanafunzi wenyewe na wizara ya elimu na sio kiiongozi mwenye dhamana anaamua atakavyo sio sahihi athari yake tunaiona inavyotuathiri kwa sasa. 11. Walimu wawezeshwe kwa kupewa vyombo vya usafiri (kupitia mikopo) 12. Baadhi ya wazazi watatakiwa kulipa ada yote katika vyuo vikuu ili kupunguza kuelemewa kwa serikali katika suala hili. 13. Udhaifu wa serikali usielezwe kwenye vyombo au taasisi zisizohusika (BODI YA MIKOPO) na utoaji wa huduma Fulani muhimu. 14. taarifa kuhusu uwezo wa wazazi wa watoto kiuchumi zijulikane mapema. 15. Ziundwe BODI ZA ELIMU katika ngazi za wilaya ili kusaidia Wizara ya Elimu kusimamia kwa kuwahusisha wadau wote wa Elimu Wilayani. 16. Serikali itizame upya sera kuhusu lugha ya kufundishia shuleni na vyuoni. Lugha ya “Kiswakinge” inayotumika leo shuleni inaaathiri elimu. Leo Kiingereza ni Kiswashili cha dunia! 17. Serikali iwe na utaratibu wa kuendelea kuwatumia walimu waliostaafu (Sera au Mwongozo) 18. Liingizwe somo la Maadili katika ngazi zote za kutolea elimu nchini. 19. Itolewe tafsiri sahihi kuhusu maana ya shule na kuhusu maana ya shule na mahitaji ya shule, chuo. Shule au chuo ni majengo, walimu bora na wakutosha, vifaa bora vya kutosha nk. 20. walimu walipwe madeni yao yote kama malimbikizo ya likizo na posho ya kufundishia ili waweze kuendelea kufundisha kwa bidii. 21. walimu wenye sifa ya kupandishwa madaraja wapandishwe madaraja na mishahara yao iendane na madaraja waliuopandishwa mara moja. 22. Yaboreshwe mazinga ya kazi kwa walimu shuleni kama nyumbani za kuishi, umeme, maji. 23. serikali iboreshe mishahara ya walimu. Kutokana na ugumu wa maisha kuongezeka (mfumuko wa bei za bidhaa) ili waweze kuyamudu maisha. 24. Sera ya elimu iwe wazi katika ngazi zote. Je ni elimu ya bure kwa watoto wote kuanzia Elimu ya Awali, Msingi (UPG) elimu ya Sekondari (UDE) na ya vyuo vikuu (UUE) na kadhalika. Hakuna kidumucho isipokuwa mabadiliko Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya. Elimu itolewayo katika Tanzania ni ufunguo wa maisha bora au ni ufunguo wa matatizo? Je vijana wetu wanasoma kwa malengo? Je Elimu itolewayo nchini inakidhi malengo yao? Kama haikidhi kwa nini umma wa nchi hii uendelee kugharamia elimu isiyo na manufaa? Kama shule na vyuo vyetu havifundishi kufikiri, kudadisi haviumbi kazi bali vinaibua tamaa ya kupenda starehe na kazi nyepesi. Tatizo kubwa la nchi hii ni serikali kutofuatilia, wala si tatizo la kukosekana kwa sera. Hili ni taifa la wasemaji maneno na siyo taifa la watekelezaji. Mapendekezo ya tume ya MAKWETTA ya mwaka 1982 licha ya kukubalika na serikali yamewekwa kabatini. Hayatekelizwi kwa sababu wahusika hawataki kupata “taabu”. Baada ya kuichambua tena ripoti ya TUME mimi naona bado yana manufaa hadi leo. Sasa naelewa kwa nini V.I Lenin alisema matumizi ya nguvu ni lazima kwa mama aliyefikia siku za kujifungua. Kwa maneno yake Lenin alisema “force is a midwifery of any society pregnant of a new one”. Kwa maoni yangu Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefika lakini hajifungui.bila kumpasua mama, wote wawili mama na mtoto watakufa. Kwa hiyo. a) Mama akipasuliwa wote wawili wanaweza kuokolewa (au mmoja wao). Tanzania inahitaji kupasuliwa ama la sivyo itaendelea kudidimia kiuchumi milele. b) Nchi ya Tanzania inahitaji kiongozi shupavu mwenye msukumo mwenye akili na siyo mkusanyaji au malafi, mwaminifu, awe mchapakazi mpenda haki na anayeona mbali. c) Rushwa na utawala usiothubutu ni kama mjamzito: Inahitaji kupasuliwa ili kuwaendeleza watanzania kiuchumi. 18. Tufafuteni kwanza maendeleo katika elimu na mengine yote yatafuata.  Twende pamoja  Tushirikiane  Tuboreshe elimu  Tujinge nchi yetu, Tanzania. NI LIPI SULUHISHO LA VURUGU, MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU NCHINI. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa aliahidi bungeni kwenye mkutano wa nne kwamba serikali imepata mkakati wa kumaliza migogoro na matatizo katika vyuo vikuu nchini na kwamba hatua za haraka zingechukuliwa kama sehemu ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2011/2012 . Hata hivyo badala ya migomo na migogoro kumalizika Tunashuhudia tena kurejea kwa wimbi la uvuguvugu,migomo, maandamano na sitofahamu katika vyuo vyetu vikuu. Katika siku za karibuni pamekuwepo na Maandamano na migomo ya mara kwa mara katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDOM) chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi (Muhas) chuo kikuu cha mtakatifu John Tanzania (SJUT) Aidha hali ya mambo chuo kikuu cha Dodoma haijatulia mpaka sasa huku vurugu, migomo na maandamano hayo yakipelekea wanafunzi wenzetu 934 kufukuzwa vyuo vikuu na wengine kusimamishwa masomo kutokana na vurugu hizo ambazo zimetajwa na uongozi wa taasisi na utawala wa vyuo hivyo kwamba vurugu hizo zimehatarisha maisha na kusababisha uharibifu wa mali . Tunaomba Serikali itambue kwamba chanzo cha migomo ya hivi karibuni (UDSM)iliyopelekea wanafunzi 56 kufukuzwa chuo na 99 kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana, na kupelekea kuvunjwa serikali ya wanafunzi (DARUSO) ni matokeo ya kugeuzwa kwa utaratibu za utoaji mikopo kutoka bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwenda vyuoni na hatimaye kuchelewa kwa malipo ya wanafunzi na wengine kupata pungufu au kukosa kabisa. Huku chanzo cha mgomo tarehe 11-`1-2011 kikiwa ni kucheleweshwa kwa pesa zao za kujikimu (boom)na wanafunzi kuamua kusitisha masomo kwenda Ofisi za utawala kuzuia shughuri zozote kufanyika hadi pesa zao za za kujikimu zitakapotolewa (boom) zitakapoingizwa na chuo. Huu ndiyo utaratibu mpya unaonyesha kutofanikiwa kumaliza vurugu migomo na maandamano vyuo vikuu nchini. Kwa upande wa Muhaso ambapo wanafunzi 85 walisimamishwa masomo chanzo cha vurugu hizo pamoja na mambo mengine ni madai ya wanafunzi hao kutaka kurejeshewa serikali yao ya (Muhaso) iliyovunjwa na Baraza la chuo Juni 2011. baada ya kukaidi waraka wa serikali wa Mwaka 2009 uliozitaka serikali za Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kubadili katiba zao. WITO wetu tunaomba uongozi wa chuo uwafejeshe chuoni wanafunzi wote 85 waliosimamishwa masomo badala ya kuwahukumu kwa kutumia matokeo ya tatizo (Sera) kama chazo cha mgogo wa (muhaso) ambao ni tofauti katika utekelezaji wa agizo la serikali la tarehe 12 Juni,2009 (GN.178) ambayo imefanya mabadiliko makubwa kwenye uendeshaji wa serikali za wanafunzi katika vyuo vikuu na hivyo kuanzisha mivutano baina ya wanafunzi na utawala katika chuo hicho na vyuo vingine nchini Wanafunzi wa chuo kikuu Muhimbili wakiwa katika sehemu ya mgomo wao wa kishinikiza utawala wa chuo hicho, kurudishwa serikali yao.(Muhaso) Serikali irejee kwamba chanzo cha migomo (UDOM) ni Madai ya msingi ya wanafunzi kuhusu mafunzo kwa vitendo na malalamiko mengine kutoka kwa wahadhiri. Toka wanafunzi 670 wasimamishwe masomo mwezi Juni 2011 mpaka sasa Ikiwa imepita karibu miezi sita (6) wanafunzi 670 bado hawajalejeshwa chuoni hivyo bado wamesimamishwa masomo huku zoezi la kumhoji mmoja mmoja likisuasua na kutarajiwa kwamba limepangwa kumalizika Mwishoni Mwa Mwezi Marchi 2011. WITO wetu kwa serikali kuhusu wanafunzi wenzetu waliosimamishwa masomo 670 tunaomba uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma kuwasamehe na kuwarudisha chuoni kwani chanzo cha vurugu na mgomo ni kudai mafunzo kwa vitendo ambayo ni madai ya msingi. Pia Serikali inaweza kabisa kwa kushirikiana na chuo kuharakisha taratibu za kinidhamu. Wakati huo huo kushughulikia Madai ya Msingi ya wanafunzi ili kuepusha Mazingira ya mivutano ya kudumu kwa muda Mrefu. Tunaomba Serikali itambue kwamba chanzo cha mgomo wa hivi kariburi tarehe 19-12-2011. hadi 21 Disemba mwaka 2011 ni kugeuzwa kwa taratibu za utoaji mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi kwenda vyuoni na hatimaye kuchelewa kwa malipo ya wanafunzi na wengine kupata pungufu au kukosa kabisa. Ambapo mgomo huo chuoni umesababisha wanafunzi 15 wa chuo hicho kikuu cha mtakatifu John Tanzania (SJUT), kusimamishwa kuendelea na Masomo chuoni hapo kwa kipindi kisichofahamika kwa kile kilichoelezwa kuwa ni vinara wa mgomo na fujo chuoni hapo. Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni siku kadhaa tangu chuo hicho kilipofungwa ghafla tarehe 21-12-2011 ambapo wanafunzi wake wa shahada ya mwaka wa kwanza waliondoshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi sababu kwamba, ikiwa ni kuepusha madhara ya vurugu ambazo zingesababishwa na mgomo uliokuwa umepangwa. Taarifa ya chuo hicho kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa chuo hicho kitafunguliwa 02-01-2012. lakini wanafunzi 15 waliosimamishwa hawatatakiwa kurejea chuoni hapo hadi chuo kitakapofikia Uamuzi wa kuwarejesha au la kuwaonya kutoonekana kabisa katika mazingira ya chuo hicho. Chuo hicho kilikumbwa na jinamizi la mgomo na vurugu kuanzia tarehe 19-12-2011 ambapo utawala wa chuo hicho uliamua kukifunga ghafla na kuwataka wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kutoweka katika maeneo ya chuo ndani ya kipindi cha masaa matatu (3). Hata hivyo kauli ya utawala wa chuo pamoja na ya mwakilishi wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambaye alifika chuoni hapo na kutoa uthibitisho kuwa fedha bado hazijaingizwa chuoni hapo lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwa jazba za wanafunzi hao. Hali katika vyuo vikuu hivi na vingine haiendani na ahadi ambayo waziri Kawambwa alizitoa bugeni na kwa umma miezi kadhaa iliyopita katika kukabiliana na migomo na migogoro katika Elimu ya juu. Serikali na uongozi wa vyuo vikuu umekuwa ukichukua hatua dhidi ya matokeo badala ya kushughulikia vyanzo vya matatizo kitu ambacho kimepelekea wanafunzi wenzetu kufukuzwa na kufunguliwa kesi mahakamani ni suala la ajabu kweli. Nitakumbusha kisa ambacho wazee watakuwa wanakumbuka. Ili tulinganishe Maandamano ya wakati wa Serikali ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na serikali zilizofuata katika kutoa uhuru kwa wanafunzi haki yao ya msingi kuandamana kufikisha ujumbe wa hisia zao kwa viongozi serikali baada ya njia ya mazungumzo hushindikana. Na kwa hili naomba vyombo vya dora na jeshi la polisi lijifunze namna linavyotumia nguvu nyingi kukabaili maandamano ya amani ya wanafunzi kwa maagizo ya viongozi wao kwa kutumia Risasi za moto, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, virungu dhidi ya Maandamano ya amani ya wanafunzi ambao huandamana wakiwa na mabango yenye ujumbe wa madai yao bila kuwa na aina yoyote ya silaha au dalili za kufanya fujo au kuathiri shughuri zozote za kitaifa. haya yalikuwa maandamano ya amani ya wanafunzi kuelekea Ikulu wakati wa serikali ya kwanza. Itakumbukwa Baada kuingizwa kwa jeshi la kujenga Taifa kikundi cha Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kiliandamana hadi Ikulu kupinga kupelekwa kwenye “kulitumikia taifa” kama sehemu ya mchango wao baada ya Taifa kuwalipia gharama yao ya elimu ya juu. Serikal ilikuwa imesema kwamba, wasomi wetu wote watalipwa kiasi cha fedha ambacho kilikuwa chini ya kipato cha mshahara wa mtumishi wa umma na sehemu ya Mshahara wao ambao wangelipwa ilikuwa ni zile gharama ambazo taifa limeingia juu yao.(walikuwa wanasoma bure). Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam waliamua kuandamana kupinga mtindo (sera) wakidai kuwa ulikuwa unanyonya nguvu kazi zao hivyo walitaka walipwe kama watumishi wengine. Walipofika Ikulu (hapo hapo anapoishi kikwete leo) walipokewa na Rais Mwenyewe Julius Nyerere pamoja na Mzee kawawa. Hawa wanafunzi Hawakuitiwa mbwa wala polisi au Mabomu ya Machozi na vilungu kama ilivyo kwa wanafunzi wa sasa wanapoitisha maandamano ya amani kuelekea kwa viongozi kufikisha madai yao huambulia vilungu mikong’oto, mabomu ya machozi, Risasi za moto, maji ya kuwasha na utumiaji wa nguvu kubwa kupita kiasi kuthibiti maandamano ya wanafunzi. Bali msafara wa maandamano huo kipindi cha Julius Nyerere kuelekea Ikulu waliruhusiwa kuja na hoja zao na kuzungumza kwa uhuru wote kueleza Manun’g’uniko yao. Rais Nyerere hakuwatisha wala kufanya lolote baya zaidi ya kuwasikiliza kwa kina. Kiongozi wa Msafara huo alihitimisha hoja yake kwa kumwambia Rais Nyerere kuwa wao hawa kuwa tayari kwenda JKT na kama Serikali itawalazimisha basi “miili yetu itaweza kwenda, lakini roho zetu hazita kwenda na mapambano kati ya wanyonge na walionacho yatadumu”. KIINI CHA MIGOMO VYUO VIKUU NCHINI NI HIVI:  Bodi ya mikopo Elimu ya juu [HESLB]  Mfumo mpya wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi 2011/2012. vikiwemo vipaumbele vya serikali  Serikali kuingilia Jumuiya na Serikali za wanafunzi.  Uhaba na uchache wa hostel vyuo vikuu nchini  Tatizo la ada kupandishwa mara kwa mara vyuo binafsi nchini  Ubovu wa miundombinu vyuoni nchini Kuifuta au kuitafutia ufumbuzi wa kudumu sera ya cost sharing, bodi ya mikopo na mchujo ni wakati muafaka kuelekea uundwaji wa katiba mpya ili kutafuta suluhu sahihi, ila kwa sasa nashauri serikari ibadilishe utaratibu wake wa mchujo (means testing). Utaratibu huu ndio unoleta mgogoro sasa kwani wanafunzi wahitaji hawapewi mkopo ipasavyo na wale wasiopaswa kupata ndio wanapewa mkopo. Makosa ya wanafunzi wengine kupewa mkopo mara mbili au zaidi yanajitokeza mara kwa mara. Wajiulize juu ya hiyo means testing isiwe ya kienyeji (kilocal local) kwani kuna ripoti za waliotumwa kufanya utafiti juu ya nchi jirani zinavyofanya means testing, kwa nini ripoti hizo zisitolewe wazi ili zijadiliwe kama kuna uwezekano tuanze kuzitumia hata kama ni gharama sana, ni heri kuliko kuendelea kusahaulisha uzalendo kwa vijana…Si busara kwa chuo kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na kufunga chuo tena kwa muda usiojulikana kwani hii ni aibu na ninachelea kusema sijui itakuwaje. Hivi serikali inajua shida/adha/kero n.k. Vinavyowapata wanafunzi wa vyuo hasa baada ya chuo kufungwa, hasa wale wa nje ya nchi na wasio na ndugu hapa mjini….. Yanipasa kutoa kisa cha binti aliyeutunza ubinti wake sanaa ila chuo kikuu cha UDSM kilipofungwa mwaka 2008 kwa kuwa hakuwa na ndugu DSM aliangulia mikononi mwa jibaba lililokuwa likimfuata fuata kwa muda mrefu hadi aliponaswa wakati huo {boom} limeisha, kwao ni mkoani mbali, hayo na mengine mengi yakamfanya ajipatie hifadhi kwa hili jibaba lililomgeuza mkewe na kumwambukiza VVU!  Ni mabinti wangapi wanageuka machangudoa……  Laiti jamii inayothubutu kuwalaumu wanafunzi ingeelewa matatizo yawapatayo wanafunzi hawa hivi vyombo vya habari viko wapi kuelezea na kuchambua kidedea na kiini cha matatizo. Wakowapi hao development partner kufuatilia chanzo cha matatizo [grass root] badala ya kiridhika na ripoti za viongozi wetu,wako wapi kutoa technical assistance na capacity building badala ya kutoa fedha tu.  Pia Serikali inapata hasara kubwa chuo kinapofungwa kwa sababu ya mgomo au vurugu za madai ya wanafunzi kwani tayari bajeti ya chuo inakuwa ishapangwa ya mwaka mzima wa masomo. Kumbuka hizo pesa ni za walipa kodi wa nchi hii ambazo zingepelekwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo. Hivyo ni muhimu kwa Serikali kubadili sera zinazopelekea migomo na vurugu vyuoni. Hawa ni wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani wakiwa nje na mizigo hawajui waelekee wap i baada ya chuo hicho kufungwa gafla mwaka 2008 MIGOMO VYUO VIKUU NCHINI. Serikali isikilize hoja badala ya kupinga na kutumia nguvu za polisi Polisi ikitumianguvu kuwatawanya wanafunzi Chuo kikuu cha Muhimbili baada ya kuitisha mgomo wa kushinikiza utawala kurudisha serikali yao.(MUHASO) Hapa ni polisi wakiwa wamemshikilia mwanafunzi huyu wa chuo cha Muhimbili kwa madai ya kuhusika katika mgomo huo wa kuredeshwa serikali yao (Muhaso). Migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini vilivyolazimishwa kufuguliwa baada ya Uchaguzi wa Octoba 2010. Ilifikia kilele. Ni kilele kwa sababu ilianzia kwingineko kwa madai yanayofanana. Kote walikogoma awali walikuwa wakilalamikia ucheleweshwaji wa fedha za kujikimu kutoka bodi za mikopo (HESLB). Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya mlimani,ambao walianza kuhamasishana kugoma siku ya Alhamis na siku iliyofuata kuanza maandamano kuelekea Ikulu. Walikua na madai tofauti. Hawa walikuwa na matatizo tofauti. Ingawa ni matatizo tofauti kimsingi, liliwagusa wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini. Walitaka serikali iengeze fedha za kujikimu wonayokopeshwa kwa siku kutoka sh elfu tano hadi elfu kumi. Wanafunzi wa UDSM walipaza sauti. Serikali kama kawaida yake ikaagiza wapigwe mabomu. Mabomu ndio msemaji wa serikali kwa kila tatizo linalopelekewa. Wakati wa uchaguzi watu walichoka kusubiri utangazwaji wa matokeo, waliandamana, Polisi wakapiga mabomu. Hayo yalitokea Mbeya mjini,Mbozi.Arusha mjini, Mwanza na kwingineko. Chuo kikuu cha Dodoma- UDOM walipogoma kushinikiza hoja zilizo wazi kabisa za kuweko kwa mafunzo kwa vitendo walipikwa mabomu. Mtoto wa mkulima waziri mkuu Mizengo Pinda alikwena huko na kukiri kuwa wanafunzi walikuwa na hoja za msingi, akaagiza ishughulikiwe. Wanafunzi wa UDSM tuliandamana kudai nyongeza za kujikimu,kwa siku,tukapikwa mabomu. Mawaziri Mh shukuru kawambwa wa elimu na Mh. Shamsi Vuai Nahodha,jumaosi wakakutana na menejimenti ya chuo na wawakilishi wa wanafunzi na kukiri kuwa madai ya wanafunzi ni ya msingi. Hata tukajiuliza je? serikali ni lazima ipige watu wake mabomu ndipo itambue uzito wa madai yao ya msingi? Hawa ni wanafunzi wa Elimu ya juu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani wakiandamana kuelekea Ikulu tarehe 4/02/2011.kushinikiza Serikali kuongeza pesa ya kujikimu, kutoka 5000 hadi 10,000 kwa siku. Hili la upigaji mabomu tuliache kwanza maana inaitaji makala nzima kuijadili. Yafaa pia polisi na wanajeshi wa Tunisia na misri, walioapa kutotumia nguvu zidi ya waandamanaji, waliomng’oa madarakani Ben Ali wa Tunisia na waliomtaka Hosni Mubaraka wa misri aondoke pia. Wapongezwe. Akitoa taarifa inayoonekana kuchelewa mmno,mshauri wa wanafunzi UDSM, Dr. Martha Qorro, aliwataka wanafunzi kuacha mgomo na maandamano kwa kuwa wizara inayohusika na mikopo katika serikali ya wanafunzi – DARUSO tayari ipo katika majadiliano na serikali, ili kuweza kutambua gharama halisi ya maisha kwa siku, sasa mabadiliko yaingizwe katika mchakato wa bajeti wa 2011/2012. katika taarifa yake hiyo kwa wanafunzi aliyoitoa siku ya ijumaa wakati maandamano yakiendelea Dr.Qourro alisema viwango vya fedha za kujikimu kwa siku,vimekuwa vikibadilishwa kama ifuatavyo:- • Hadi kufikia mwaka 2005/2006 wanafunzi walikuwa wakikopeshwa Sh. 2500/= kw siku. • Mwaka 2006/2007 kiwango hichi kolipandishwa hadi Sh. 3500/= kwa siku na • Mwaka 2007/2008, kiwango hicho kilipandishwa hadi sh 5000/= wanayoendelea kukopeshwa hadi sasa. Hii inamaana kuwa fedha wanazopewa kwa siku imebaki 5000/= kwa miaka mine iliyopita. Ni aibu kubwa kwa Taifa linalotaka kujenga jamii yenye amani,na haki na usawa kusubiri maandamano ndipo serikali ilewe kuwa sh.5000/=. Zilizomwezesha mwanafunzi kujikimu kwa siku miaka mnne iliyopita leo haitoshi.ipo aibu nyingine, ikiwa Dr. Qorro ambaye ni mshauri wa wanafunzi UDSM alijua kuwepo kwa mchakato wa kubadili kiwango hiki, kwa nini hakuwapa taarifa wanafunzi mapema? Tujiulize swali lingine. Ni mara gapi Serikali imeboresha mishahara ya wafanyakazi wake wabunge kuanzia mwaka 2007/2008,hadi leo kwa madai ya kupanda kwa ghalama za maisha? Hawa wanafunzi kulikoni?, ni vigenzo gani vilivyoitajika au kubainishwa ili kuwezesha fedha yao ya kujikimu inaongezwa? Je walikuwanayo maduka yao yenye bei tofauti? Hoteli, mabasi yao je/ Yaani wapo kwenye Tanzania nyingine tofauti yenye kuhitaji utafiti tofauti na ule unaowahusu Watanzania wasiokuwa wanafunzi? Kuna hoja nyingine mwaka 2007/2008,wakati kiwango cha sh. 5000/= kiliidhinishwa kwa siku kila mwanafunzi alikuwa na hakika na maradhi katika hostel za vyuo. Serikali imeongeza idadi ya wanafunzi vyuoni, kwa kasi ya ajabu bila kuongeza hostel za kuwawezesha wanafunzi hao, kupatoa marazi kwa ghalama nafuu hili limefanyika hivyo katika vyuo vyote nchini vya umma na visivyokuwa vya umma. Fedha za marazi hujilipia kutoka katika hicho hicho cha shilingi 5000/=,alizokuwa anapewa kwa siku sambamba na nauli yake,Chakula,Maji,Sabuni na Mahitaji mengine yote.kwa sasa Mwenye uhakika wa maradhi katika hostel za vyuo. mfano UDSM ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Wenye uhakika wa kupata hostel tu. Wengine wote hupaswa kupanga nyumba mtaani,ambako bei ya chumba kwa mwezi inafika sh. 50,000/= Kulikuwa na hoja nyengine ndani ya maandamano haya: Wanafunzi wa elimu ya juu wanafikiri,wanatafiti na kufanya uchambuzi wa mambo ya kijamii, kisiasa,Kiuchumi na Kiutamadumi. Wanaangalia namna serikali inavyowatendea wao na kuwapendelea wengine. Wanashanga serikali inavyowafanya waishi kwa shida huku ikiendekeza utaratibu wa ajabu wa kulipana posho katika ofisi za umma. Kama wabunge, mashirika na taasisi za Serikali pia Wanaona usimamizi wa rasilimali za taifa ambavyo haufanywi kwa usahihi. Ni bahati mbaya kuwa jeshi letu la polisi lilifundishwa intelijensia ya unabii na utabiri wa kutokea vurugu katika maandamano pekee. Ikiwa lingejifunza interejensia ya kubaini hoja za wanaotaka kuandamana ningeitaka serikali kutoa majibu kabla ya kuwepo kusudio la maandamano ni kwa ajili ya udhaifu wa interejensia ya polisi na serikali kwa ujumla hoja hizo na njengine zifuatazo hazina majibu ila waandamanaji watapigwa mapomu. Ukosefu wa ajira: serikali imeasisi mpango wa shule ya sekondari kwa kila kata. Ikahimiza wanafunzi wasome uwalimu. Watu wakaitika wito. Katika hali ya ajabu imeajiri baadhi tu ya walimu hawa huku shule zikikosa walimu. Waliokosa ajira sasa hivi wataungana na wanaomaliza vyuo tena mwaka huu. Wote wataandamana kudai ajira serikalini. Natarajia watapigwa mabomu. Miaka inakwenda haraka 2013 itafika, wengine watahitimu tena, serikali itasema uchumi haujakuwa kwa kasi iliyotarajiwahuku ikiingia mikataba feki na hivyo itashindwa kuajiri. Wataandamana kudai ajira nao watapigwa mabomu. Mfano. Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2010 katika shule ya Benjamini Mkapa katikati ya jiji kati yao 282 wamepata sufuri. Hawa watawakusanya wenzao waliofeli hapa DSM, wataungana na wahitimu wa vyuo walionyimwa ajira ili wawafundishe kuwaponya wasifeli, wataungana na machinga waliozuiwa kuuza bidhaa wanapopata mtaji ili mradi hawavunji sheria ; wataungana na wafanyakazi wasiopandishwa madaraja kazini; wataungana na waliochagua mgombe “A” akashinda lakini mshindi akatangazwa kuwa ni ngombea “B” ndiye ameshinda, wote hawa kwa pamoja wataunda jeshi la waandamanaji wasiokuwa na silaha. Wote wataunganishwa na wimbo unowakilisha mahitaji yao. Kwamba wamechoka kuongozwa na viongozi wasiojali maslahi ya wanyonge. Intelijensia ya jeshi na serikali yake haizioni hoja hizi ila wakati wa maandamano watatabiri vurugu. Na hivyo watawapiga mabomu waandamanaji. Serikali makini haisubiri maandamano ya jinsi hii yatokee. Hujitahidi kutenda vitendo visivyozalisha majeruhi wa tabaka tawala kwenye tabaka tawaliwa. Waandamanaji wa UDSM walisikika wakisema nguvu ya umma haijawahi hushidwa na jeshi lolote duniani. Tuangalie mifano ya Afrika kusini na India enzi za Mahatma Ghandhi, Tunisia,Ufaransa, Urusi, China, Irani ya Ayatolla Khomenei na kwengineko. Watu wenye njaa hujua kuwa wanakaribiwa na kifo. Huona heri kuwaambia watawala tuna njaa wakawaua kama hawataki kuwasikiliza kuliko kukaa kimya na kufa kwa njaa. UDSM walisema wanakufa na njaa kwa sababu sh. 5000/= ya mwaka 2007 leo mwaka 2011 haitoshi. Je mabomu ndilo jawabu lao? Tume ya vyuo vikuu Nchini (TCU) ilitangaza majina ya wanafunzi 27,924 ambao ni sawa na asilimia 69.3 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka 2011/2012 wa masomo kati ya wanafunzi 48,477. hivyo wanafunzi 10,553 hawa kubahatika kuchaguliwa na (TCU) zikiwemo sababu kadha kama sifa, kutotimiza masharti na udanganyifu. Katika ujazaji fomu kwa njia ya mtandao. Wakati TCU ikitoa Idadi hiyo ya wanafunzi waliochaguliwa, Bodi ya mikopo ya vyuo vya Elimu ya juu (HELSB), nayo ikatangaza bajeti ya Sh. 317.8 billioni zitakazotumika kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu ambazo ni ongezeko la SH.80 billioni ikilinganishwa na Sh.237.8 billioni zilizotengwa mwaka 2010/2011. Wakati huo huo Bodi ya mikopo ya vyuo vya Elimu ya juu (HELSB) ikatangaza na kutoa majina 24,628 ya wanafunzi watakao pewa mkopo mwaka wa masomo 2011/2012. kati ya wanafunzi 37,924. hivyo wanafunzi 13,296. wakaachwa wajisomeshe wenyewe na kujigharamia kwa masomo yao. Hawa ni watoto wa wakulima, walimu wanaotabika huko vujijini kwa mishahara ambayo wao wenyewe haiwatoshelezi mahitraji yao ya msingi lakini serikali kupitia bodi yake ya mikopo (HESLB) Ikaamulu waubebe msalaba wa kuwasomesha watoto wao licha ya ugumu wa maisha unaowakabili na familia zao. Athari zake ni kwamba wanafunzi wengi wamekosa au wameona hawawezi kumudu gharama za elimu hiyo ya juu na kuamua kutafuta kazi za kufanya (manual work), wengine wamelazimika kwenda kusoma elimu ya stashahada wakati walikuwa na sifa za kusoma elimu ya shahada, wengine wameenda vyuo kwa msaada wa ndugu na jamaa au wahisani. Hivyo kumaliza kwao vyuoni kukiwa kwa mashaka kwani wahisani, wazazi, ndugu na jamaa wakisitisha kufariki kwa wazazi wake au ndugu ni vitu ambavyo vinaweza kumfanya asitishe masomo. Hii ni hali inayoonyesha serikali kushindwa majukumu yake ya kutoa elimu kwa watu wake. Kwa kuwepo mzigo wake kama serikali wa kuwasomesha bure wanafunzi wote wenye sifa za kusoma elimu ya juu. Kwa Mfana: chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na vyuo vishiriki vya chuo kikuu cha Dar es salaam.yaani chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) Pamoja na chuo kiuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE) kwa pamoja vilisajili wanafunzi 6580 kwa mwaka wa masomo 2011/2012 kati ya wanafunzi 6580 waliosajiliwa ni wanafunzi 4547 ndiyo waliopata mkopo kati ya 6580 hivyo wanafunzi 2033 hawakupata mkopo ndiyo maana ngomo na maandamano ya tarehe 11/11/2011. chuo kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya mlimani ilikuwa kuishinikiza serikali kuwapa wanafunzi wote 13,296 nchi nzima ambao hawakupewa mkopo kwa hoja njepesi za kwamba serikali haina uwezo, vipaumbele vya serikali na masharti ya ujazaji fomu kutozingatiwa. Hoja ya serikali haina uwezo wa kusomesha bure wanafunzi wote wa elimu ya juu haina mashiko bali serikali inao uwezo wa kusomesha ikiamua sekta mama ya Elimu kuwa kipaumbele cha msingi nchini. Ambayo naweza kusema kuwa kwa kushindwa kuijali impasavyo imeendelea kuwa sekta duni nchini. Walimu bado wanafanya kazi katika mazingira magumu. Serikali hajalipa madeni yao ya malimbikizo ya mishahara na madai mengine. Hali hii ndiyo ilipelekea matokeo ya kidato cha nne 2010 yawe ya kisikitisha kwani zaidi ya asilimia 80 ya watahiniwa walipata madaraja ya nne na sifuri hali iliyochchea mjadala wa kitaifa kuhusu mustakabali wa elimu wa elimu nchi kadhalika Desemba 14-2011. wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ilitangaza matokeo ya darasa la saba ikielekeza kuwa wanafunzi 9,736 wamefutiwa matokeo kutokana na kugundulika kufanya udanganyifu. Hili ni janga la kitaifa 2011. serikali ijiulize kwa nini wanafunzi wamafanya udanganyifu? Kwenye mtihani? Majibu unayo mengi kwa hilo nisaidie kufikiria. SERIKALI IVUNJE UONGOZI WA BODI YA MIKOPO (HELSB) Serikali imechelewa sana kuvunja uongozi wa bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini. Imechelewa aidha kwa kutokuwa makini kujua matatizo na kufanya kile ambacho imekuwa ikifanya vizuri zaidi kusubiri hadi mambo yaharabike kabisa ndio ianze kunchangamka. ambayo yameharibika katika bodi ya mikopo, wizara na hazina linapokuja suala la kuhakikisha watanzania wanapata fedha kwa ajili ya kugharimia elimu ya juu, Serikali kutokana na kutokujua ifanye nini na kwa kukosa uongozi unaostahili imeachilia mfumo wa mikopo ya elimu ya juu ambao hauweki kipaumbele kwenye weledi, ufanisi na matokeo. Upande mwingine ni kuwa uongozi ambao umekaa kwenye bodi hii ya mikopo muda huu wote wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega hawezi kabisa kukwepa lawama za mfumo na utaratibu wa bodi ya mikopo. Kinyume na madai ya Nyatega kuwa tatizo lipo kwenye kupata fedha kutoka hazina kubwa bado tatizo kubwa lipo katika mfumo wake wa kutoa mikopo kwa wanafunzi. Tunaambiwa tanesco wanataka fedha zaidi ili waweze kutoa umeme zaidi, ATCL wanataka fedha zaidi ili wawe na ndege zinazosafiri zaidi, TRA wanataka fedha zaidi ili waweze kuboresha huduma, na sasa bodi ya mikopo nao wanataka fedha zaidi ili wanafunzi wengi wapate fedha zaidi. Na watu wanaamini kwamba fedha zaidi ni sawasawa na huduma “ bora zaidi”. Hakuna anayetaka kuangalia mifumo, hakuna anayetaka kuangalia watendaji na hakuna anayeangalia utaratibu na sharia. Wote wanaangalia “fedha, fedha, fedha”. Bodi ya mikopo ina matatizo makubwa ya aina tatu. La kwanza ni tatizo la kisheria na la pili ni tatizo la kiutendaji. Matatizo ya kisheria ni yale yanayotokana na sharia ya 2004 iliyounda bodi ya mikopo. Bodi ya sasa ya mikopo inaongozwa na sharia hiyo ambayo bado haijafanyiwa mabadiliko. Sheria hii ilivyo sasa inaweka mfumo wa mahusiano kati ya bodi, waziri na wanafunzi, Bahati mbaya sana tatizo la kwanza ambalo linaonekana ni kuwa bodi ya mikopo siyo chombo huru cha kusimamia mikopo ya wanafunzi nchini. Ni chombo ambacho kinategemea kiongozi wa kisiasa (waziri) katika kufanya mambo yake. Ibara ya 33 ya sheria hiyo inatoa nguvu kubwa kwa waziri kuweka utaratibu wa namna na jinsi mikopo itatolewa baada ya kushauriana na bodi ya mikopo. Hii ina maana nini? Ibara hiyo haimlazimishi waziri kukubaliana na bodi matokeo yake Waziri anaweza kushauriana na bodi, mke/mume wake au na watu wa chama chake halafu akafanya maamuzi yake. Lakini hilo kama halitoshi, sharia haiweki utaratibu wa kumwajibisha waziri au kumsimamia waziri; sharia inamdhania (presume) waziri kuwa atakuwa na hekima na uwezo wa kuamau mfumo ulio bora. Sheria hiyo hiyo inasema katika ibara ya 30 kuwa wajumbe wa bodi watalipwa fedha kama waziri atakavyoamua baada ya kushauriana na bodi. Yaani wajumbe wa bodi wanaweza wakaamua walipwe kiasi gani na wakatoa mapendekezo yao kwa waziri na waziri akikubali basi ndio watalipwa hivyo. Lakini tatizo kubwa la msingi na la kisheria liko kwenye ibara ya kifungu cha b na c ambavyo vinahusiana na uwezo wa bodi kutengeneza mfumo na utaratibu wa utoaji wa mikopo na pia kuweka vigezo vya nani anataka kupatia mikopo hiyo. Hii ni mojawapo ya makosa makubwa sana kwa sababu juu ya nani anastahili kupewa mikopo maana yake bodi inakuja na kigezo chake ambacho binafsi ninaamini ni cha kibaguzi, kakina haki, na hakiwatendei haki Wataznania wanaolipa kodi ambayo inatumika kugharimia elimu ya juu. Katika utaratibu wao wa mikopo bodi imejaribu kijiingiza kwenye matatizo kwa kutafsiri vibaya ibara ya 16.1 inayosema kuwa “subject to the provisions of the Act, the Board may provide, on a loan basis, financial assistance to any eligible student who is in need of the loans and who has applied for such assistance as a required to meet all or any number of the students welfare costs of Higher Education”. Tafsiri nzuri kuwa bodi yaweza kuwa msaada wa fedha kwa njia ya mikopo kwa mwanafunzi yeyote anayestahili ambaye anahitaji mkopo na ambaye ameomba mkopo huo akiwa wametimiza vigezo mbalimbali. Wanapoandika utaratibu wao bodi ya mikopo inasema kuwa “For purpose of these Guidelines, Needy applicant means:” Sasa hapa ndipo mahali penye tatizo. Inanishangaza kuona hata walio wasomi wanashindwa kutofautisha maana ya “in need of” kama sharia inavyosema na “Needy”. Kosa lililofanywa na bodi ni kufikiria na kulazimisha kuwa sharia iliposema “in need of” ilimaanisha “needy”. Kwa kutumia kamusi ya Random House ya 2011 neno needy maana yake ni “in a condition of need or want; poverty-stricken; impoverished; extremely poor destitute”. Tafsiri hii inakubaliana pia na ile ya kamusi ya Kiingereza ya Oxford ambayo inasema maana ya needy “lacking the necessities of life very poor”. Ni wazi kuwa bodi ya mikopo ilichukua tafsiri hii kuwa wenye kustahili mikopo siyo wenye mahitaji ya mikopo bali walio maskini na fukara! Ndio maana katika vigezo vyao vya needy wanasema mwenye kustahili mikopo. Kifungu cha 2.2 cha taratibu zao za mikopo chote kinategemea tafsiri hiyo ya kuwa mwanafunzi mwenye kustahili mikopo ni Yule mwenye matatizo na maskini. Sheria ya Bodi ya mikopo haisemi hivyo. Sheria inasema mwenye mahitaji ya mikopo – haisemi hali yake ya maisha iko vipi!. Haisemi Mtanzania ambaye familia yake ina uwezo hastahili mikopo. Sharia haisemi aliyefaulu sana ndio anastahili mkopo na ambaye hakufaulu hastahili au anastahili zaidi mikopo. Naweza kuendelea kulichambua hilo kwa kina lakini wakati huu itoshe kusema tu kuwa bodi ya mikopo imeweka utaratibu kinyume na sharia na kuwa sheria nyenyewe ilivyo (na haihakikishi uhuru, weledi wala utendaji mzuri wa bodi. Hilo lilikuwa tatizo la kwanza- la kisheria. Tatizo la pili ambalo naamini ni kubwa zaidi vile vile (kwani la kisheria ni rahisi kulishughulikia) ni suala la watendaji. Kwa ushahidi wa jinsi gani wametengeneza taratibu za mikopo ambazo zinatakiwa kufuatwa na vyuo na wanafunzi ni wazi kuwa bodi ya mikopo inahitaji mabadiliko ya haraka ya kifikra kwani watu wale wale wenye fikra zile zile wataendelea kufanya madudu yale yale. Nyatega ameshindwa kuongoza bodi hiyo na amesimamia mojawapo bodi hiyo na amesimamia mojawapo ya vyombo vingeweza kuleta mabadiliko ya haraka kwa wananchi wetu wanaotaka elimu ya juu. Kwa kuweka vigezo ambavyo ni kinyume na katiba – kwa sababu vinabagua wanachi ya fedha za mikopo na kuwapendelea maskini. Kwa mfano mtoto anayetoka familia yenye ahueni na matajiri na kwa sababu Fulani wazazi wake hawataki kumlipia elimu ya juu je afanye nini ilia pate elimu ya juu? Inakuwaje kwa Mtanzania ambaye kutokana na majukumu mbalimbali lakini anashindwa kupata fedha kwa elimu ya juu na si maskini kwa kipimo chochote kile? Haiwezekani bodi inalazimisha watu kudai umaskini ili wapate mikopo? Yote ni kwa sababu Nyatega na kundi lake wameshindwa kutafuta mfumo mzuri, wenye haki, ambao unazingatia mahitaji siyo ufukara au umaskini wa mtu ili kumpatia mikopo. Na ni tatizo kubwa kwa sababu pia bodi hii hii ndio inatakiwa ikusanye fedha zilizotolewa kama mikopo, tena kuanzia ile ya mwaka mikopo, tena kuanzia ile ya mwaka 1994: na yote inategemea huruma na moyo wa waliopewa. Matokeo yake ni kuwa bodi haijaweza kukusanya vizuri mikopo na matokeo yake imebakia kuhimiza watu “warudishe mikopo”. Yote ni chini ya Nyatega na bodi yake. Sasa wanapotokea viongozi na serikali kudai kuwa tatizo siyo bodi nashindwa kuelewa kama bado wana uwezo wa kufikiria au ndio imekuwa nao wanaimbishwa kuwa tatizo ni fedha. Wanafikiri kwamba wakipata fedha zaidi ndio tatizo la bodi ya mikopo litaisha. Kuna tatizo la utendaji ambalo bodi ya sasa haiwezi kushughulikia na binafsi nina uhakika mara baada ya bodi kuvunjwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali aende na kupitia vitabu vya bodi hiyo na kuangalia kama matumizi ya fedha yameeendana na vile vilivyopatikana. Tatizo la tatu ambalo naamini ni la kinadharia ni kuiita hii ni bodi ya “mikopo. Hatuwezi kuendesha elimu ya juu kwa kutumia mikopo tu. Mfumo wa kutegemea mikopo unaanza kutengeneza watu wenye madeni mapema mno na katika nchi ambayo ina mfumo wa utawala wa kifisadi tunaanza kutengeneza watu wapya ambao wataingia kwenye ajira wakiwa na mzigo wa madeni ya shule na wakati huo huo hali ngumu ya maisha na matokeo yake tunaanza kutengeneza mafisadi watarajiwa. Tunachosema ni kuwa ni lazima tuwe na mfumo mzuri wa kufadhili elimu ya juu ambao mikopo itakuwa ni sehemu yake tu. Kwa sasa hivi bodi washabolonga katika vigezo na wafungwa mikono katika mikopo. Pia tumebahatika kupata mapendekezo yaliyowasilishwa bungeni kama mswaada ili upitishwe na uwe sheria ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, sura ya 178 ya sharia a Tanzania, kama kilivyowasilishwa Bungeni. Mswaada unapendekeza kufanya marekebisho katika vifungu kadhaa vya sharia ya bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu, sura ya 178 ya sheria za Tanzania. Kwanza, inapendekezwa kurekebisha kifungu cha 5 cha sharia hiyo kwa kuongeza idadi ya wajumbe wa bodi ya mikopo wa elimu ya juu kutoka wajumbe kumi na tatu waliopo chini ya sheria ya sasa hadi wajumbe kumi na nne. Hii inafanywa kwa kuongezwa mwakilishi wa tume ya vyuo Vikuu Tanzania na mwakilishi wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu za umma; na kupunguza uwakilishi wa watu mashuhuri wenye utalaam na uzoefu katika uendeshaji wa taasisi za elimu ya juu. Kwa mujibu wa sheria ya sasa, Tume ya vyuo vikuu na wanafunzi wa taasisi ya elimu ya juu za umma hawana uwakilishi katika bodi ya mikopo. Pamoja na inavyoonekana kuwa nia njema ya kutoa fursa ya uwakilishi wa taasisi hizi katika bodi ya mikopo, hakuna ushahidi wa kuthibitisha kwamba kutokuwapo kwao kumeathiri utendaji wa bodi ya mikopo. Aidha, hakuna uhakika kwamba uwepo wao katika bodi ya mikopo utaongezea bodi hiyo tija yoyote. Hii ni kwa sababu ya mujibu wa kipengele cha 9 cha nyongeza ya sheria ya Bodi ya Mikopo, maamuzi ya Bodi hayawezi kubatilishwa kwa sababu tu yakutokuwepo kwa mjumbe, au kutokana na mapungufu ya uteuzi wa mjumbe yeyote. Vile vile kamati imepata taarifa kwamba licha ya kuwa wajumbe wa Bodi ya Mikopo kwa mujibu wa sheria ya sasa, mwakilishi wa wanafunzi wa taasisi ya elimu ya juu za binafsi amekuwa hawalikwi kwenye vikao vya Bodi kwa viongozi mbalimbali. Hii ina maana kwamba kuongeza uwakilishi wa wanafunzi wa taasisi za umma wakati wawakilishi wenzao wa taasisi ya binafsi hawashirikishwi kwenye vikao vya Bodi, hakutatatua matatizo mbalimbali ya Bodi ya Mikopo, Sehemu ya pili inayopendekezwa kulekebisha ni kifungu cha 7 cha sheria ya Bodi ya Mikopo.Kifungu hiki kinaainisha mamlaka mbalimbali ya Bodi ya Mikopo. Hapa inapendekeza kurekebisha kifungu cha 7 (i) kwa kuipa bodi mamlaka ya kuamua idadi ya juu ya wanafunzi wanaostahili kupatiwa mikopo kila mwaka “kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya Serikali”. Kwa mujibu wa Madhumuni na sababu za Muswada huu, kwa sasa Sheria”..inaelekeza mikopo itolewe kutokana na vigezo vya ukopeshaji… ambavyo vinaruhusu wanafunzi kukopeshwa bila kuzingatia ukomo wa bajeti…”. Pendekezo hili linaleta dhana potofu kwamba bodi inatoa mikopo kwa wanafunzi wengi bila kuzingatia ukomo wa bajeti inavyotolewa kwa Bodi ya mikopo kutoka serikalini, kuwapo kwa sheria hii, Bodi ya Mikopo inalazimika kuendelea kuzingatia ukomo wa bajeti ya Serikali katika kutoa mikopo kwa wanafunzi. Pia kamati ya wanafunzi inaona kwamba sababu halisi ya pendekezo hili ni kuipa Bodi ya Mikopo na Serikali kinga ya kisiasa dhidi ya tuhuma kwamba imeshindwa kutatua matatizo makubwa ya mikopo ya wanafunzi, ambayo yamepelekea mogogoro isiyoisha kati ya Serikali na wanafunzi wa karibu taasisi zote za elimu ya juu nchini. Sehemu ya tatu inayopendekezwa kurekebishwa ni kuiongezea Bodi ya Mikopo mamlaka ya kutoa ruzuku (grants) msaada wa masomo (bursary) na fedha za kusoma (scholarships). Hata hivyo, utekelezaji wa lengo hili zuri inaelekea kukanushwa na kufifishwa na sharti la, uwepo wa fedha ambalo limewekwa kayika pendekezo la kifungu kipya cha 7(j) cha Sheria ya Bodi ya Mikopo. Kama imeshindikana kuwapa wanafunzi mikopo wanayoihitaji kwa madai ya uhaba wa fedha, Bodi ya Mikopo itatumia muujiza gani kupata fedha za kutoa ruzuku, fedha za msarifu na misaada ya masomo ambayo kwa kawaida hotolewa bure kwa wanafunzi wanaostahili? Pendekezo la kifungu kipya cha 7 (k) nalo linatia mashaka makubwa juu ya utekelezaji wake. Kifungu hicho kinapendekeza kuipa Bodi ya Mikopo mamlaka ya kuomba na kupatiwa taarifa za wanufaika wadaiwa wa mikopo kutoka kwenye mifuko ya hifadhi za jamii kama vile LAPF, NSSF, POPF na PSPF. Masharti haya yatazihusu pia malaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Kwa vile hakuna masharti kwa taasisi zote hizi kuisaidia Bodi ya Mikopo kukusanya madeni ya manufaika wadaiwa, kama ilivyo kwa waajili kwa mujibu wa vifungu vya 20 na 21 vya Sheria ya Bodi ya Mikopo, haieleweki ni kwa namna gani taarifa za wanufaika wadaiwa zilizoko kwenye mifuko ya hifadhi za jamii au BRELA au TRA “(zi) tarahisishwa urejeshwaji wa mikopo inayodaiwa”. Kama inavyodaiwa kwenye Madhumuni na sababu za Muswaada huo. Eneo la tano lenye utata linahusu mapendekezo ya marekebisho ya vifungu vya 16 na 17 vya sheria ya Bodi ya Mikopo. Kifungu cha 16 kinaipa Bodi wajibu kisheria wa kutoa mikopo kwa wanafunzi; mamlaka ya kupanga asilimia ya gharama za elimu ya juu ambayo mwanafunzi atatakiwa kuchangia; na kinachomtaka mwanafunzi kuchangia kiwango cha fedha sawa na asilimia ambayo imepangwa na Bodi. Kwa mujibu wa mapendekezo ya marekebisho, mikopo sasa itatolewa kwa wanafunzi waliadahiliwa moja kwa moja kwenye taasisi ya elimu ya juu baada ya kumaliza elimu ya sekondari. Aidha, inapendekezwa kwamba wanafunzi waotokea makazini hawatastahili kupewa mikopo, ijapokuwa makatazo haya hayatahusu wanafunzi waliodahiliwa kusomea, taaluma za kipaumbele cha kitaifa. Kwa upande mwingine, kifungu cha 17 kinaanisha sifa mbalimbali anazotakiwa kuwa nazo mwombaji wa mkopo. Sasa inapendekeza kwamba licha ya sifa hizo, Bodi ya Mikopo inatakiwa iangalie pia uwezo wa kitaaluma wa mwombaji, mahitaji yake na udahili katika taaluma za kipaumbele kitaifa. Vile vile Bodi inatakiwa kuangalia mwenendo wa zamani wa mwombaji katika kulipa ada katika shule za sekondari; uwezo wa kifedha wa mzazi au mlezi; na hali ya kifamilia kwa maana ya uyatima au ulemavu wa mwombaji. Hata hivyo, na licha ya masharti haya mapya, Bodi inatakiwa kuwapa kipaumbele wanafunzi waliodahiliwa katika kozi za kipaumbele kitaifa zilizoainishwa katika Nyongeza ya Pili inayopendekezwa kuingizwa katika Sheria. Kozi zinazotajwa katika Nyongeza hiyo ni pamoja na ualimu wa sayansi na hisabati, sayansi, sayansi na hisabati, sayansi, sayansi na udaktari na uhandisi. Nyingine ni sayansi za kilimo, mifugo, udaktari wa mifugo na hisabati. Mapandekezo haya yanazua maswali mengi. Kwanza, mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 16 yanakinzana moja kwa moja na masharti ya kifungu cha 17 cha sheria ya sasa. Hii ni kwa sababu wakati marekebisho yanapendekeza wanafunzi waliotokea makazini wasipewe mikopo isipokuwa tu kama wamedahiliwa kusomea taaluma za kipaumbele kitaifa. Kifungu cha 17 (1) (e) cha Sheria ya sasa kinampa haki ya kufikiriwa kupatiwa mkopo kila mwanafunzi anayeendelea na masomo na ambaye amefaulu mitihani ya kumwezesha kuendelea na masomo kwa mwaka au hatua ya masomo inayofuata. Kifungu hiki hakijaguswa kabisa na mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 17. Kwa sababu ya ukimya huu, kama athari za kupitishwa kwa mapendekezo ya ibara ya 6 ya Muswada huu ni pamoja na kurekebisha, by implication, masharti ya kifungu cha 17 (1) € ya Sheria ya sasa kwa kadri inavyowahusu wanafunzi waliotokea makazini. Vile vile, kama wanafunzi wanaotokea makazini, na ambao kwa mujibu wa kifungu cha 17 (1) € cha Sheria ya sasa wanastahili kupatiwa mikopo, watanyimwa mikopo hiyo endapo mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 16 yatapitishwa na kuwa sheria. Athari ya pili kupitishwa kwa mapendekezo ya marekebisho ya vifungu vya 16 na 17 vya Sheria ya Bodi ya Mikopo itakuwa ni kuingiza ubaguzi mkubwa katika mfumo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika nchi yetu. Kwa mfano, wanafunzi wanaotokea makazini sasa wataweza kinyimwa mikopo, wakati wanafunzi wanaotokea shule za sekondari moja Kwa moja watakuwa na haki ya kupata mikopo hata kama wote wanasomea taaluma zile zile! Aidha, wanafunzi waliodahiliwa katika kile kinachoitwa, kozi za kipaumbele kitaifa” watakuwa na haki yakupatiwa mikopo, wakati wanafunzi wenzao waliodahiliwa katika kozi nyingine zilizoruhusiwa na Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu hawatakuwa na haki hiyo. Na kama ni hivyo, kwa nini Serikali isitangaze wazi kwamba ni marufuku kwa wanafunzi wa Kitanzania kusoma taaluma ambazo Serikali inaziona si za kipaumbele kitaifa! Mapendekezo haya yateleta ubaguzi mkubwa pia kati ya masikini na matajiri hapa nchini, na kati ya wanafunzi wanaotokea vijijini na wale wanaotokea mijini. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kubisha ukweli kwamba shule za sekondari za kata amabazo zimejengwa kwa maelfu latika maeneo ya vijijini ni shule za watoto wa masikini amabao kwa kiasi kikubwa wanaishi vijijini. Vile vile hakuna anayeweza kubishia ukweli kwamba shule hizi zina upungufu mkubwa wa karibu kila kitu kinachotakiwa katika elimu ya sekondari, kuanzia walimu wa masomo yote, vyumba vya madarasa, maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi, maktaba, vitabu, madawati, mabweni, chakula, maji, umeme, N.K. Hakuna anayeweza kubishia ukweli kwamba shule nyingi za binafsi na za Serikali zinazoongoza kwa ubora wa mahitaji ya kitaaluma, ndizo zinazoongoza kwa viwango vya ufaulu na ndizo zinazosomesha wanafunzi wanaotoka kwenye familia tajiri na/au za wenye kipato kikubwa. Nyingi ya shule hizi pia ziko maeneo ya mjini au pembezoni mwa miji, na kwa hiyo zimeunganishwa na miundombinu bora ililinganishwa na shule za vijijini. Kwa sababu za upungufu wa mahitaji haya muhimu kielimu, ufaulu wa wanafunzi wa shule za sekondari za kata ni wa chini sana, kulinganisha na ufualu wa wanafunzi wa shule za sekondari za binafsi au za Serikali zilizoko kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya mjini. Kwa mapendekezo ya marekebisho ya kifungu kipya cha 17 (3)(a)(i) cha Sheria ya Bodi ya Mikopo, itakuwa ndoto kwa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini na vijijini na mijini na ambao wamesomea katika shule za sekondari za kata, kupatiwa mikopo kwa sababu ya ufaulu wa chini kwa ujumla wa shule hizo, na kwa sababu ya ufaulu wa chini katika masomo ya sayansi ambao utawazuia wanafunzi hao kusomea taaluma za kipaumbele kitaifa”. Kwa upande mwingine, kwa mapendekezo haya, ni wanafunzi wanaotoka familia zenye vipato vikubwa ana wanaoishi maeneo ya mijini na kusomea katika shule bora za binafsi na za Serikali ndiyo pekee watakaokuwa na haki ya kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo, kwa sababu ya viwangovyao vikubwa vya ufaulu katika msomo yote kwa ujumla na hasa hasa katika masomo ya sayansi, Itakuwa imetimiza kile kilichoandikwa katika maandiko matakatifu kwamba aliyenacho atanyang`anywa hata kile kidogo alicho nacho”! Ibara ya 13(2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inatamka wazi kwamba “ ni marufuku kwa sheria yeyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”. Ibara ya 13(5) inatafsiri neno, bagua” kumaanisha”… kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia…pahala walipotokea…au hali yao ya maisha kwa namna ambayo wati wa aina Fulani wanafanywa…dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima….”vile vile, ibara ya 11 (2) inatamka wazi kwamba “kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na staili na uwezo wake.” Zaidi ya hayo, ibara ya 11(3) inaitaka Serikali kufanya”… jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.” Ni suala la aja kupitisha sheria ambayo itaongeza ubaguzi kati ya vijana masikini na matajiri na kati ya vijana wanaosomea shule za kata zilizoko vijijini na wale wanaosomea shule za binafsi na/au za serikali zilizoko mjini. Kamati ya wanafunzi vyuo vikuu kwa niaba ya wanafunzi wote wa elimu ya juu tunapendekeze kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya vifungu vya 16 na 17 ambayo ni ya kibaguzi kwa dhahiri na kwa taathira yake; na kwa hiyo yanakiuka katiba yetu. Kamati ya wanafunzi inaitaka Serikali kudhibitisha kwa wanafunzi kwamba ubaguzi huu katika mfumo wa utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini, unalenga kulekebisha matatizo gani mahususi katika jamii yetu ili uweze kuhesabika kuwa sio ubaguzi” kwa minajili ya ibara ya 13(5) ya katiba yetu. Mfumo wa utoaji Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini umekuwa na migogoro mingi na inayoelekea kwa sugu. Kiashiria kikuu cha migogoro hii ni migomo ya mara kwa mara ya wanafunzi wa taasisi karibu zote za elimu ya juu hapa nchini, ambayo imepelekea masomo kukatishwa, vyuo vikuu vingi kufungwa na wanafunzi wengi kufukuzwa vyuoni na wengine wengi kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya jinai mahakamani. Aidha, vyuo vingi vimekuwa kama uwanja wa mapambano vyenye kukaliwa kwa nguvu za kijeshi na vikosi vya kutuliza ghasia vya jeshi la Polisi. Militarization hii ya vyuo vikuu vya nchi yetu imeenda sambamba na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa wanafunzi. Katika mazingira haya, mwezi Machi mwaka jana Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete aliunda tume chini yaya uenyekiti wa Profesa Makenya Maboko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuchunguza kiini na sababu za migogoro isiyoisha katika vyuo vyetu vikuu pamoja na mfumo mzima wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini. Kamati ya wanafunzi ina taarifa kwamba tume ya Profesa Maboko ilikamilisha kazi yake, baada ya kufanya uchunguzi ndani ya nje ya nchi yetu na kuwasilisha ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais Mnamo mwezi Oktoba, 2011 Kamati ya wanafunzi ilitegemea kwa kuzingatia kwa unyeti wa udharura wa hali ya sasa katika vyuo vyetu vikuu kwamba serikali ingewasilisha ripoti ya tume ya Profesa Maboko kwa wadau wa elimu nchini na wawakilishi wa wananchi (wabunge) ili iwasaidie waheshimiwa wabunge, wadau wa elimu nchini, wanaharakati nchini, na wanafunzi wenyewe kuelewa kiini na sababu za matatizo ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kuweza kuchangia katika uboreshaji na kutafuta suluhisho la kudumu. Sasa tumebakiwa na uamuzi huu ambao wengine ndio wanazinduka leo kuona mantiki yake; vunjeni uongozi wa bodi ya mikopo, ingizeni bodi ya muda itakayobadilisha vigezo vya kupata mikopo na itakayoweka utaratibu wa mpito kuelekea chombo kipya cha kusimamia gharama ya elimu ya juu nchini. Chombo ambacho kitakuwa nje ya Wizara au Ikulu, na kitakuwa na watendaji ambao wana weledi na ambao kweli wanataka kuwasaidia Wanzania wamudu gharama ya elimu ya juu. Watendaji wote wa ngazi za juu wa bodi kuanzia na Nyatega wajiuzulu mara moja au watimuliwe. Hatuwezi kuendelea kulea uzembe na kufumbia macho kuwajibika. Vijana Tuungane pamoja kutaka hili litekelezwe haraka. MFUMO MPYA WA UTOAJI MIKOPO 2011/2012. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Makumila wakiwa katika maandamano wakilalamikia suala la ucheleweshwaji wa mikopo yao, jeshi la polisi lililazimika kutumia mabomu kuwatawanya, baada ya kuzuia barabara ya Arusha na Moshi Suala la wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu kukosa mikopo Limekuwa ni kero ya Muda Mrefu huku Serikali Ikishindwa kuweka jitihada za dhati katika kukabiliana nalo huku hali ikiendelea kuwa ngumu kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi kila kukicha ambapo baadhi yao wanashindwa kuhitimu masomo yao. Katika hali ya kusikitisha tangu Serikali ilipoamua kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo (HESLB) kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara huku wanafunzi wengi wakilalamika vigezo vyote vinavyohitajika Kwa kiasi kikubwa migogoro hiyo imekuwa ni kero kwa wanafunzi na taifa zima kwa ujumla ambapo imesababisha kuwaondolea umakini wanapokuwa Chuoni na kusababisha kutofanya vizuri katika masomo yao. Aidha migogoro hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya wanafunzi kuachishwa masomo licha ya wengine kitohusika katika migomo na maandamano hayo. Pia wengine wamekuwa wakipata hofu hivyo kubaki nyumbani pindi zinapotekea fujo vyuoni ambapo pia nao hukumbwa na adhabu ya kutohudhuria masomo na kuunganishwa kwenye kundi la wale wanaoandamana. Hali hii imesababishwa na mfumo mbovu uliowekwa na serikali katika kuhakikisha inawapa wanafunzi mkopo. Mathalani baadhi ya vigezo vilivyowekwa na bodi ya mikopo (HESLB) bado vinaweka ubaguzi mkubwa hasa kwa kupendelea baadhi ya matabaka Kwa mfano, Wanafunzi wanaochukua taaluma ya udaktari wao hupewa mkopo moja kwa moja bila masharti ya aina yoyote hata kama Mzazi wake ana kipato kikubwa huku mtoto wa mlalahoi anayechukua taaluma ya uhasibu, sheria au uchumi akikosa mkopo licha ya kwamba wote wana haki ya kunufaika na mkopo huo ili kuweza kufikia ndoto zao kielimu. Ukiondoa kundi hili la wanafunzi wanaosomea udaktari ambalo mara nyingi serikali hupata hasara kwa kuwafukuza vyuoni wanapodai haki zao za msingi kwa kuandamana, serikali imekuwa ikifadhili walimu huku ikitoa sababu ya kuwa ni kipaumbele cha Taifa, Swali la kujiuliza mbona kuna walimu wengi tu wamemaliza vyuo na hawajaajiriwa mpaka sasa? Huu ni ubabaishaji unaopaswa kukomeshwa. Serikali imekuwa haikaukiwi na sababu za kushindwa kufadhili wanafunzi kwa kiwango kikubwa Mara oh! Hawana vigezo, mara oh! Mwaka huu bajeti haitoshelezi, naweza sema huu ni uvivu wa kufikiri katika kutafuta suluhisho la Matatizo yanayowakabili Wanafunzi Maana Sidhani kama ipo siku Serikali yetu itatamka wazi kwa wananchi kwamba ina bajeti ya kutosha. Kwa kuwa inaonyesha kuanzia Wizara ya Elimu, Bodi ya Mikopo na Tume iliyoundwa na Rais kuhusu migogoro elimu ya juu pamoja wameshindwa kutatua tatizo hili. Tumependekeza njia za kumaliza migogoro hii kama serikali itatusikiliza. Hebu tufikirie na tuangalie mikakati ipi itakayoweza kuwasaidia na kupunguza adha ya migogoro ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu ambayo italeta tija na kumnufaisha kila Mmoja kwa wakati wake. Hali hii imekuwa ni kikwazo kwa wanafunzi wengi kwa kuzingatia umuhimu wa elimu na kuliendeleza taifa, serikali ina wajibu kushirikiana na sekta binafsi kwa kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini. Serikali haina budi kuzungumza na sekta za kibenki katika kutoa mikopo ambayo itawasaidia baadhi ya wanafunzi ambao hawana sifa za kupata mkopo kutoka serikalini kama wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza kiielimu na wenye sifa ikiwa ni kupambana na migogoro hiyo inayoendelea kila kukicha. Kwa kipindi hiki Serikali inayo fursa ya kuchagua benki ambapo kwa kujadiliana na wanafunzi waliomo kwenye ajira (inservice) kukubaliana na kuweka taratibu na sheria ambazo zitakuwa rahisi kwa wanafunzi hao mfano. polisi, walimu, na wafanyakazi wengine wa serikali. katika kupata Mkopo nafuu na haraka ambao utawasaidia kujiunga na masomo kwa wakati husika ili kupunguza mzigo kwa serikali wa idadi kubwa ya wanafunzi inayoongezeka kwa kasi kubwa tukiangalia kipindi hiki wanafunzi wengi hufanya kazi huku wakijisomesha hivyo kukiwa na mikopo ya elimu ya juu ambayo itatolewa na benki kwa udhamini wa serikali kwa ulipaji nafuu itasaidia hata wanaojisomesha na kuendelea kutumikia taifa lao. Asilimia kubwa ya wazazi nchini ni wakulima na wafanyakazi wenye kipato kidogo kama walimu,polisi n.k. hawa wana kipato ambacho hakijitoshelezi kwa wakati mmoja kufanikisha au kukidhi karo ya elimu ya juu itakuwa na manufaa kwa watu wa hali ya chini. Bado ya mikopo pia inawajibu wa kuimarisha usawa wa kuwapatia Mikopo hiyo na kutoa ufafanuzi mzuri wa jinsi ya kuchukua fomu zao na jinsi ya kuzijaza katika hali ya Umakini zaidi na kuondokana na Mvuto kati ya Bodi ya mikopo na Wanafunzi. Katika hili baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakiilalamikia bodi ya mikopo kwa kuwa na upendeleo na kutowathamini au kuwapa mikopo wale ambao wanatoka katika shule za binafsi kwa kuwapa mkopo kwa asilimia kidogo au kutowapa kabisa mkopo ikilinganishwa na waliotoka katika shule za serikali. Huu ni uonevu kwani kusoma shule za binafsi haimaanishi kwamba Mzazi anafedha nyingi kwa kuwa hali ya maisha kubadilika anaweza kuwa na kipato kikubwa leo, kesho akawa maskini, leo mzima kesho akafariki dunia au wazazi kuachana na kutengana. Pia ni lazima tuangalie thamani ya hao wanafunzi ambao ndio viongozi wetu wa kesho pamoja na kuangalia tulipotoka na tunapokwenda katika kuimarisha elimu iliyo bora zaidi na sio kuwatimu au kuwafukuza wanafunzi kwani serikali inajiongezea hasara kila kukicha kutokana na wengi wao kushindwa kumaliza masomo yao ambapo hata ajira itakayowafanya kulipa deni lao ni ndoto. WITO WETU KWA SERIKALI: Umefika wakati wa serikali kuingia mkataba na benki ili zisaidie kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaotoka makazini (in- service) njia ya mkopo kama nchi za wenzetu zinavyofanya ambapo imewasaidia kuwa na elimu ya uhakika kwa vijana wao. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka 2011 tarehe 14/02/2011. Mh.Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, DK.J.M Kikwete aliunda tume ya kuangalia na kutoa taarifa ya mapendekezo ya kuboresha utaratibu wa sasa wa ugharamiaji utoaji na urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu. Baada ya tume kukamilisha kazi hiyo na kuiwasilisha tarehe 29/04/2011. Ndipo serikali kupitia kwa Mh.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa ilitoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu ugharamiaji, utoaji na utejeshaji wa mikipo ya Elimu ya juu mnamo tarehe 19 Agosti 2011. Taarifa ya Serikali ilitoa ufafanuzi kuhusu ugharamiaji wa elimu ya juu, utoaji wa mikopo, urejeshaji wa mikopo na masuala ya kiutawala na ruzuku kwa wanafunzi wa sayansi ya tiba. Baada ya kuisoma na kuipitia vizuri taarifa ya serikali ambayo kimsingi ni utekelezaji wa mapendekezo na mawazo ya Tume iliyoundwa na Mh. Rais kupitia kamati teule ya wanafunzi wa Elimu ya juu ikishirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo viongozi mbali mbali kutoka katika serikali za wanafunzi vyuo vikuu nchini viongozi toka sehemu mbali mbali ndani na nje ya kamati yetu, wanaharakati pamoja na wadau wa Elimu nchini kwa pamoja tulijadili taarifa ya serikali kwa nyakati tofauti ni kwa jinsi gani tutakuja na msimamo wa pamoja kwa lengo la kutatua ama kupunguza matatizo yanayojitokeza baada ya tume kutoa mapendekezo na serikali kutangaza utekelezaji wake. Baada ya kujadili kwa kina tulibaini mapungufu makubwa ya Mfumo Mpya ya utoaji wa mikopo kwa Mwaka 2011/2012. kama ifuatavyo. I. Bodi ya mikopo iliwaacha watu wenye sifa linganifu na mature entry kuomba mikopo huku wakijua dhaliri hawata wapatia mikopo hiyo. Hii ni kinyume na utaratibu uliowekwa awali ukizingatia kwamba mabadiliko ya sera yalikuwa ya kushtukiza na taarifa hazikutolewa kwa wadau na kuwacha wanafunzi 13,296 bila mkopo. II. Mabadiliko haya ya vigezo/sera hayakuwashirikisha wadau zikiwemo serikali za wanafunzi vyuoni wala TAHLSO na kifanya Mfumo huu kukosa uhalali wa kukubalika. Kwani wahusika hawa kupewa nafasi ya kutoa maoni yao na matatizo yanayowasibu kuhusu Mfumo wa utoaji wa mikopo ya Elimu ya juu. III. Vigenzo vilivyowekwa na bodi ya mikopo katika kuwatambua wahitaji sahihi wa mikopo vimeshindwa kuweka wazi au kumtambua mhitaji halisia wa kupewa mkopo TOFAUTI ZA GREDI. [MEANS TESTING] Hili limekuwa tatizo la muda Mrefu tangu kuanzishwa kwa utaratibu mpya Mwaka 2005 wa kuwakopesha wanafunzi mikopo kwa ajiri ya masomo yao ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo Tanzania (HESLB) katika Mfumo wa (tes Means). Tunaomba ifahamike kwamba mfumo huu umekuwa hauna uhalisia katika kugawa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hasa katika kigezo cha uwezo wa kiuchumi wa familia Mwanafunzi hivyo kutoa mkopo kwa kuangalia uwezo wa kiuchumi kwa kuangalia mambo yafuatayo. I. Shule nilizosoma za sekondali kwa kuangalia kiasi cha ada (fees) ya shule ilikuwa kiasi gani Madhaifu ya Kigezo hiki. II. Naomba ifahamike kwamba kutokana na uchache wa shule za sekondari za serikali wazazi hulazimika kuwapeleka watoto wao shule binafsi baada ya serikali kuchagua idadi chache ya wanafunzi hasa wa kujiunga na kidato cha tano. Kutokana na uchache wa high school hivyo wazazi hulazimika kuwapeleka shule binafsi hata kama hawana uwezo. III. Tunaomba ifahamike kwa serikali kwamba baada ya matokeo ya kadato cha nne kutoka kila Mwaka. Huwa wanafunzi wanafaulu kwa viwango Tofauti kuanzia daraja la kwanza, daraja la pili, daraja la tatu na daraja la nne. Mara nyingi serikali huwa inachagua wale waliofaulu kwa daraja la kwanza, na la pili na IV. daraja la tatu. Hivyo huwa kuna wale daraja la tatu na la nne na ambao halazimika kurudia mtihani kutafuta (credit) kama hazikufika hawa wote hulazimika kwenda shule za binafsi sio kwa sababu wana uwezo wa kifedha bali hawakupata nafasi serikali hivyo familia nzima, ndugu na jamaa hulazimika kutoa mchango ili hawa wanao au watoto wao waweze kupata elimu. Hivyo Serikali hapa ikichukuwa kigezo cha ada ya shule aliyosomea mwanafunzi huyu itakuwa haijamtendea haki kwani alilazimika kwenda pale baada ya kutokuwepo uwezekano wa kupata nafasi kutokana na sababu hizo. V. Kigezo au utaratibu wa kusainisha fomu za bodi ya mikopo kwa wanafunzi wanaenda kuanza mwaka wa kwanza elimu ya juu. Naomba serikali ifahamu kuwa taarifa zinazoandikwa kwenye fomu hizo hazina uharisia na ukweli wa hali halisi ya maisha,ya mwanafuzi hili naomba niwe Mzalendo wa nchi yangu Tanzania na kuhurumia kodi za walala hoi. Kwa wanaohusu kuhakiki taarifa zilizoandikwa kwenye fomu ya kuomba mkopo ni katibu kata, na Afisa mtendaji wa kijiji na kata pamoja na wajumbe watatu (3). Lakini nimeshuhudia wanapopelekewa fomu hizo huomba kuonyeshwa eneo lao la kusaini bila kusoma taarifa zilizoandikwa. Na baadae taarifa hizo hutumwa bodi ya mikopo elimu ya juu.na hizo ndizo taarifa zinazotumiwa kupanga magurupu ya mikopo wakati taarifa hizo hazina uharisia wa maisha ya manafunzi fumilia yake. VI. VIPAUMBELE VYA SERIKALI KWA BAADHI YA KOZI. Mfano Elimu na Sayansi vinaacha Matabaka na Athari kwa jamii ya watanzania maskini hivyo tunapinga mfumo wa vipaumbele vya Serikali kwa hoja kuntu zifuatozo:- a) Nchi yetu bado inahitaji wataalamu wa fani mbali mbali ili kukuza uchumi wa nchi yetu na mendeleo ya familia zao kwa jumla. b) Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zipo kwenye mchakato wa uanachama wa shirikisho la Afrika Mashariki. Ambapo nchi yetu haiwezi kunufaika katika shirikisho hili kama haina Rasilimali watu hususani katika soko la Ajira. Hivyo tunaitaji wataalamu wa fani mbali mbali ili tuweze kunufaika na shirikisho hili kama wanauchumi, wanasheria, wataalamu wa mambo ya kijamii (Sociology, Psychology,HumanResources,politician,naBiashara,Wahasibu,(ACCOUNTANT). Lakini kama serikali itaendelea na msimamo wa vipaumbele vyake vya Elimu na Sayansi tu. Wataalamu hawa wa fani hizi ngingine tutawakosa kwa asilimia kubwa. c) Serikali kuweka vipaumbele vya Elimu na sayansi tu na kwenda kozi nyingine kuna athari kubwa ya kuathiri vipaji vya wanafunzi wanaotoka familia maskini. Kutokana na hali ngumu ya maisha wanafunzi wanotoka katika familia Maskini watalazimika kuchukua kozi ambazo serikali Imezipa kipaumbele Elimu na Sayansi na sio kuchagua kozi kulingana na vipaji vyao (Talent and Ambition) na kuharibu (future) zao. Hivyo Taifa linaweza kujikuta linazalisha wataalam ambao wamesomea kozi au fani ambazo sio vipaji vyao kutokana na umaskini wao. Kitu ambacho kinaweza kuwa hasara kwa Taifa kwani watashindwa kufanya kazi kwa ufanisi. d) Wanafunzi watakao chaguliwa kozi tafauti na vipaumbele vya serikali Elimu na Sayansi na wanaotoka katika familia Maskini watashidwa kuimudu gharama ya Elimu ya juu ili hali wana sifa zote za kusoma Elimu ya juu (chuo kikuu) na hili ni hatari kwa Taifa ambalo wananchi wake bado ni Maskini e) Serikali kuweka vipaumbele kwa baadhi ya fani na kuacha nyingine katika Elimu ni kukiuka katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 11 sehemu ndogo ya 2 na 3 kama inavyosema kwenye katiba. 11. (2) “kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.” Ibara ya 11. (3) inasema “Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fulsa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.” Vi. Pesa za kujikimu (BOOM) kutolewa vyuoni badala ya bodi ya mikopo (HELSB) Sisi kama kamati ya wanafunzi pamoja na wadau mbali mbali Wanaona mapendekezo hayo na utekelezaji wake ni mgumu sana na unaitaji kufanyiwa marekebisho mara moja kwa sababu zifuatazo:- i. Utaratibu huu utasumbua Mwanafunzi na kumpotezea muda wa kuondoa hali ya utulivu wa masomo kwa mwanafunzi asiyekopeshwa na bodi. Kwani uwezekano wa chuoni kugeuka sehemu ya kudai pesa na sio kusoma ni mkubwa kama tulivyoona baadhi ya vyuo kwa sasa (UDSM, MT. JOHN). Hawa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Tumainin Tawi la Dar es Salaam, wakiwa katika mgomo tarehe 3/01/2012.baada ya pesa yao ya kujikimu kucheleweshwa, kufuatia utaratibu mpya wa pesa hiyo kutolewa vyuoni badala ya Bodi ya mikopo (HELSB). ii. Baadhi ya vyuo watatumia fursa hii kutumia fedha za wanafunzi bila ridhaa yao kwa Malipo ya ada na makato mengine kitu ambacho kinaweza kuleta migogoro na mivutano kati ya wanafunzi na utawala. iii. Wanafunzi wameshindwa kujua mkataba wao ni aidha kati ya bodi ya mikopo (HELSB) au ni kati ya chuo husika. Hivyo utaratibu huu mpya unavunja nguvu ya kisheria katika makubaliano ya mkataba wa awali kati ya mwanafunzi na bodi ya mikopo na namna ya urejeshaji wa mikopo hiyo kwa muafaka. iv. Utaratibu huu mpya utapelekea na umepelekea migogoro na migomo vyuoni. Mfano Mgomo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam tarehe 12 na 13 mwezi wa 12/2011,(12,13/12-2011) ambapo wanafunzi 43 walifukuzwa chuo. Na chuo kikuu cha Mtakatifu John Tanzania (SJUT) hadi chuo kufungwa 21/12/2011 na wanafunzi 15 kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana. Nao wanafunzi wa kitovu cha Elimu ya Sanaa chuo kukii jcha Dodoma (udom) tarehe 3/01/2012 waliandamana kwa ajiri ya kushinikiza uongozi wa chuo hicho uwape fedha za kujikimu zinazotolewa na Bodi ya mikopo. Wanafunzi zaidi 2000 waliandamana hadi utawala ambapo walikutana na makamu mkuu wa chuo hicho. Profesa. Idris kikula. Kiongozi wa muda wa maandamano hayo alisema wameamua kuandamana ili kushirikiza uongozi uwape fedha zao za kujikimu. Alisema kuokana na hali hiyo wamekubaiana kutoingia madarasani hadi fedha zao zitakapopatikana. Alisema hali ya maisha imekuwa ngumu sana kwao kwa sababu hawana fedha za kujikimu kama kununua chakula, vitabu na masuala mengine ya kijamii alisema kuwa hawataacha kuandamana kwa ajiri ya kidai fedha zao kwa sababu wanaamini kuwa maandamano ndiyo suluhisho la matatizo yao. Mgomo chuo kikuu Tumaini. Tarehe 3/01/2012 wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es Salaam. Juma nne tarehe 2/01/2012 wanachuo hao walisitisha masomo kufuatia kwa baadhi ya wanafunzi kucheleweshewa fedha za mikopo kutoka Bodi ya Mikopo. Wanafunzi hao walisitisha masomo yao na kwenda kuonana na mlezi mshauri wao kwa ajiri ya kupata ufafanuzi kuhusu lini watapata pesa zao. Wanafunzi hao wamedai kuwa katika wakati ngumu wa kifedha kufuatia kucheleweshwa kwa mikopo yao na wengine kudai kucheleweshwa kulipa ada. Hata hivyo, walipokwenda Bodi ya mikopo, waliambiwa kuwa tatizo sio Bodi, bali ni chuo ambacho kilichelewa kupeleka majina ya wanaostahili kupata mikopo. Hiyo yote ikiwa ni matokeo ya mfumo mpya wa utoaji pesa ya wanafunzi vyuoni. Hivyo inapotoa zikacheleweshwa kutoka vurugu na migomo vyuoni haitaepukika kama tulivyoona baadhi ya migomo na vulugu baadhi ya vyuo hapa nchini. Ikiwa ni matokeo ya mfumo mpya wa Ripoti na mapendekezo ya tume ya Mh. Rais Jakaya Kikwete ya kuangalia na kutoa taarifa ya mapendekezo ya kuboresha utaratibu uliokuwepo. Elimu ya juu. Hawa ni wanafunzi wa Chuo kikuu Kampasi ya Mlimani wakiwa katika mgomo tarehe 11/12/2011. baada ya kucheleweshewa pesa yao ya kujikim(Boom), na kuamua kustisha masomo na kuzuia shughuli zote kufanyika Utawala, hadi pesa zao zitakapoingizwa na chuo. Ndugu Watanzania, Serikali yetu ya Tanzania, wadau wa Elimu na wapenda maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania. Ikumbukwe kwamba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete aliahidi Mwaka 2007 kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya wanafunzi wa Elimu ya juu nchini ili kupunguza migomo na migogoro vyuoni kote. Katika mkutanao wake na wanafunzi wa vyuo vikuu Mwezi Februari 2007 alikwenda mbali zaidi kwa kuwaeleza kwamba hakuna mtoto wa maskini atayeshindwa kuendelea na masomo kutokana na masharti ya mikopo au kushindwa kuendelea na masomo kutokana na umaskini au kutopata mkopo Sasa ni Miaka Mitano imepita toka ahadi hizo zitolewe. Migomo na Maandamano katika vyuo vikuu inaendelea kama tulivyoonesha hapo juu na pia wapo watoto wa walalahoi ambao wamefaulu kidato cha sita (6). Lakini wameshindwa kuendelea na masomo ya Elimu ya juu kutokana na kukosa mikopo. Hivyo serikali kupitia waziri isipochukua hatua za haraka na kutekeleza mapendekezo yetu haya itadhihirika kwamba ahadi za serikali kupitia Rais Jakaya kikwete zimekuwa kiini macho, na vyuoni hapatakuwa mahali pakusomea tena ila migomo na maandamano yasiyo na kikoma. SUALA LA UHABA NA UCHACHE WA HOSTELI VYUO VIKUU NCHINI Mwaka 2007/2008 wakati kiwango cha Sh.5000/= kikiidhinishwa kwa siku kila Mwanafunzi alikuwa na hakika ya malazi katika hostel za vyuo. Kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi. Serikali imeongeza idadi ya wanafunzi vyuoni kwa kiasi ya ajabu bila kuongeza hosteli za kuwawezesha wanafunzi kupata malazi vyuoni kwa gharama nafuu. Hili limefanyika hivyo vyote nchini vya umma na visivyo kuwa vya umma (private) tumeshuhudia na tunashuhudia hivi vyuo vya private kama st. August(SAUT) na Tumaini university. Jinsi wanavyofungua matawi sehemu mbali mbali hapa nchini huku wanafunzi wake wakipata taabu na sehemu za kulala, nenda mwanza ukaone nyumba zilizopo pembeni ya chuo hicho (SAUT) Chumba kwa mwaka ni Sh. 700,000 hadi 800,000. hivi serikali iko wapi kuvishinikiza navyo kuboresha miundombinu ya awali kabla ya kufungua matawi mapya sehemu nyengine. Njoo chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM, uone taabu tunayopata, nenda IFM, DUCE, MKWAWA, MUHIMBILI University uone wanafunzi wanavyotaabika mtaani kutafuta vyumba vya kupanga kwa gharama kubwa. Serikali imeongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu mwaka wa masomo 2011/2012 kutoka Sh.5000, hadi 75000. cha kushangaza ongezeko Sh.2500, halitaweza kumsaidia mwanafunzi kwani kiasi kilichoongezwa kwenye pesa ya kujikimu, anakitumia kulipa kodi ya chumba mtaani huku ugumu wa maisha ukiwa palepale. Huku mahitaji ya msingi yakiwa palepale kama nauli ya kwenda na kurudi chuo, chakula,maji,sabuni,vitabu,na mahitaji mengine ya kidharura na ya msingi. Mfano: Chuo kikuu na chuo mama hapa nchini Tanzania. Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kwa sasa kuna wanafunzi wanaokaribia 20,000. lakini cha ajabu na kusikitisha katika chuo chetu hiki cha Taifa. Kina nafasi 6950 tu za vitanda vya kulala wanafunzi katika hostel zake. Ni kwa jinsi gani utaona idadi kubwa inavyobaki nje ya hosteli kwa sababu ya kukosa vyumba chuoni kwa idadi ya vitanda 6950 na wanafunzi karibia 18,000 utaona nijinsi gani wanavyopata taabu ya kutafuta au kupangisha vyumba mtaani. Kwa sasa wenye uhakika wa malazi katika hosteli za chuo UDSM ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Wengine wote hupaswa kupanga vyumba mtaani ambako bei ya chumba kwa Mwezi inafika Tsh. 50,000 kwa mwaka ni sawa na laki sita 600,000 bado kununua godoro kama Tsh.40,000, umeme na maji kwa mwaka Tsh.100,000, kima cha chini na vitu vingine vya ndani vya ndani vya msingi hivyo wanafunzi analazimika kutumia zaidi ya Tsh. 740,000 kwa matumizi ya chumba tu. Bila kuingiza gharama za lazima kama nauli, chakula , vitabu vya kujisomea na mahitaji mengine ya msingi na ya kidharura. Watanzania wenzangu sio ajabu kumkuta Binti Msomi wa ngazi ya chuo kikuu akijiuza au kufanya biashara ya ukahaba kutokana na ugumu wa maisha unaotukabili. Tunaomba serikali, wazazi wetu watanzania kwa ujumla matatizo haya ndiyo yanayotupa ujasiri wa kuimili Risasi mabomu na virungu wakati wa maandamano ya kufikisha ujumbe huu kwa serikali. Tunaomba serikali itambue kuwa suala hili linasikitisha na linawaumiza wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wanavyoangaika mtaani kutokana na uhaba wa hosteli na kuwa chache vyuoni. Leo hii wanafunzi wanalazimika kutumia pesa zao wanazopewa na Bodi ya mikopo za kujikimu kwenda kulipa gharama ya vyumba mtaani. Tunaomba Serikali itambue kwa wanafunzi wa Elimu ya juu wanaathirika sana kutokana na uhaba na uchache wa hosteli vyuoni na kuamua kupangisha vyumba mtaani kama ifuaavyo. 1). Kuathirika kiuchumi: Tunaomba Serikali itambue kuwa. Iliongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kutoka Tsh.5,000 hadi 75,000/= kwa siku kutokana na hali ya maisha ilivyo nchini. Lakini kwa bahati mbaya wanafunzi wamejikuta hawanufaiki na ongezeko hilo kutokana na gharama kubwa kuitumia kwa ajiri ya kodi ya nyumbani zaidi ya Tsh.740,000/= kwa mwaka wa masomo kama tulivyoona kwenye mchanganuo hapo juu, hili ni tatizo kubwa linalohitaji mpango mkakati wa kidharura kulitatua. Ndiyo maana kabla ya muda wa pesa ya kujikimu kwa wanafunzi kutolewa tayari wanafunzi wanakuwa wameishiwa kabisa. Hivyo inapotokea pesa ya kujikimu kuchelewa kuingizwa kwa wanafunzi. Huwa na ujasiri wa ajabu na kuonyesha hisia zao kwa kuitisha maandamano na migomo Vyuoni. Pia serikali itambue kuwa na wanafunzi hawa wanaathirika moja kwa moja na ongezeko la bei za umeme, vyumba vya kupanga, na maji mtaani ilihali hawana kipato (Income) na hawajaanza kufanya kazi. 1) Kuathirika kielimu: Tunaomba Serikali ituelewe na itusikilize kuwatatizo la uhaba na uchache wa hosteli vyuo vikuu hali hii haituathiri kiuchumi tu bali kielimu pia. ieleweke kuwa wanafunzi wa nje ya hosteli za vyuo (out of universty) kunatuathiri sana kimasomo. Kwani wanafunzi wanaoishi mtaani au wanaopanga nje ya chuo hupata usumbufu asubuhi wakati wa kwenda vyuoni na jioni wakati wa kurudi makwao. Kutokana na foleni za magari baraarani: a) Hivyo ujikuta wakichelewa masomo ya asubuhi. b) Hukosa muda wa kukaa pamoja na kama wanafunzi ili kusoma kwa njia majadilianao (discussion/group dicussion). c) Kuchoka kutokana na adha ya usafiri barabarani hivyo kujikuta wamechoka wafikapo jioni au usiku huko wanakoishi kitu ambacho huwafanya kukosa uwezo wa kusoma kutokana na uchovu mwingi. d) Kukosa muda wa kujisomea katika maktaba za vyuo (Library) wakiwahi kurudi majumbani wanakoishi. Haya na mengine yanapelekea viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kushuka. 2) Suala la ulinzi na usalama wa wanafunzi wakiwa nje ya chuo ni mdogo. Tunaomba seriakali itambue kwamba kuna matukio mengi yameripotiwa kwa wanafunzi wenzetu wanaoishi nje ya vyuo vikuu kwa kupanga mtaani vyumba kuibiwa mali zao,kubakwa mabinti wa kike,na kukosa uangalizi wa karibu kutoka jumuiya na serikali zao za wanafunzi wa vyuo vikuu kutokana na kuwa mbali na serikali zao . Ni suala la huzuni na kusikitisha kuona Binti wa kike aliyetoka huko mkoani Kagera, Mwanza,Mbeya,Mtwara,Iringa,Mbeya n.k. akachaguliwa chuo Kikuu cha Dar es Salaam. UDSM, IFM, DUCE, Ardhi, Muhimbili university Anafika chuo alichochaguliwa anaambiwa atafute sehemu ya kuishi mwenyewe kutokana na uchache wa hosteli. Ebu watanzania tujiulize huyu ni Binti wa kike akapangishe mtaani katika mji au jiji ambalo kwake ni mgeni kama jiji la Dar es Salaam na kwingineko na uhuni uliomo mtaani ni mkubwa mno. Na cha kusikitisha zaidi wapo wanafunzi wengi wa kike vyuo vikuu wamejikuta wakijiingiza kwenye biashara ya Umalaya na kujiuza ama kwa kupangishiwa vyumba na mijibaba (mafataki) wenye lengo la kutimiza mahitaji yao ya kimwili(Ngono) kutokana na uhaba na uchache wa vyumba vya kulala vyuoni (hosteli). Wengi Ndugu zetu wanafunzi wa kike hasa wa mikoani wamejikuta wakiambukizwa magonjwa hatari ya kufanya biashara ya Ngono kama (Ukimwi) kutoka kwa mafataki huko mtaani ambao huwalipia kodi za vyumba, kodi za maji na Umeme. Hili ni suala la huzuni, kusikitisha,kusononesha na kukatisha tamaa kwa wanafunzi wa Elimu ya juu namna serikali inavyolifumbia macho suala hili linalogharimu na kuingiza maisha ya wanavyuo hatarini. WITO WETU KWA SERIKALI 1) Tunaiomba serikali ije na mpango mkakati katika bajeti yake ya 2012/2013. kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi na mkakati wa ujenzi wa hosteli vyuo vikuu vya umma. Kote nchini ili kuondoa adha na matatizo yote tuliyoyabainisha hapo juu na kwa mustakabali wa Elimu kwa kuingia mkataba na mifuko ya hifadhi ya kijamii kama NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, au kupitia wakala wa nyumba (TBA), Benki za hapa nchini au njia nyingine kama itakavyoonekana inafaa serikali iingie mkataba na mashirika haya kwa ujenzi wa haraka. 2) Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi isimamie na kushinikiza vyuo vyote visivyo vya umma (private University) kujenga hosteli zinazotosheleza wanafunzi waliopo vyuoni hapo na kutoruhusiwa kufungua matawi sehemu nyingine hadi miundombinu iliyopo inawatosheleza waliopo kama madarasa, walimu na hasa hosteli. SERIKALI KUINGILIA JUMUIYA NA SERIKALI ZA WANAFUNZI ELIMU YA JUU HASA WAKATI WA UCHAGUZI WA KUPATIKANA VIONGOZI WA SERIKALI ZETU. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha IFM wakimsikiliza kiongozi wao (Waziri Mkuu). Kufuatilia ngogoro wa wanafunzi na Utawala wa chuo. Mwaka jana 2011. Serikali imekuwa na kawaida ya kuingilia katika vyombo vyetu vya maamuzi hasa wakati wa uchaguzi ili kupata viongozi wao kwa maslahi yao ya kisiasa. Wote ni mashahidi kwa kilichotokea (TAHLISO) umoja wa wanafunzi wa Elimu ya juu Tanzania kwa muda mrefu tangu uchanguzi wa mwaka 2008. hali iliyopelekea wanafunzi kukosa imani na chombo hicho kwani tutakuwa mashahidi maandamano ya chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2008. ya kudai nyongeza ya pesa ya kujikimu na malazi bila kuishirikisha Tahliso pia na maandamanao ya 3/02/2011 kuelekea Ikulu kwa Rais kutaka kuongezwa pesa ya kujikimu kutoka Sh.5000 kwenda 10,000. ni baada ya chombo chenye mamlaka kuingiliwa na serikali (TAHLISO). Lakini pia tumeshuhudia chaguzi mbalimbali vyuoni namna zinavyoigiliwa na serikali kupitia usalama wa Taifa na utawala kuweka vibaraka wanaowataka kwa mwamvuli wa mchujo wa (screening) na sababu za kisiasa na uwezo wao wa kushughulikia matatizo ya wanafunzi wenzao. Ndio maana tumeona mara baada ya kupatikana viongozi kumekuwepo pande mbili la kwanza wanafunzi wakiongozwa na wanaharakati kudai haki zao. Mfano madai ya nyongeza ya pesa ya kujikimu mwaka 2008 kutoka 3500 hadi 5000 na mwaka 2011 kutoka 5000 hadi 7500. Na upande wa pili ni serikali ambayo yenyewe huwa upande wa utawala na kushirikiana nao kupinga harakati za kudai haki za wanafunzi na mara nyingi tumeshuhudia migomo ya wanafunzi ya kutaka kupindua viongozi wao. Mfano chuo kikuu cha Dar es salaam 20/02/2011, kampasi ya mlimani yalikuwepo mgomo wa kutaka kung’oa Rais Matias kipara kwa sababu alichaguliwa kuwa Rais wa TAHLISO, kwa nembo ya chuo kikuu cha Dar es salaam ilihali chuo kikuu cha Dar es salaam kilishajiondoa sio mjumbe tena baada ya mgomo na maadamano ya mwaka 2008. ya kushinikiza serikali kuongeza pesa ya ya kujikimu kutoka sh. 3500 hadi 5000 cha ajabu kama siyo kushang’aza Uongozi wa TAHLISO wakati huo ulipinga maandamano na mgomo huo. Japo pesa ziliongezwa. Lakini kuna suala la pili ambalo tunaiomba serikali iingilie kati kuhusu vyama vya siasa kuingilia serikali za wanafunzi kwa kupandikiza vibaraka wao wakati wa uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi hii ni hatari mfano mwepesi ni leo hii Rais wa TAHLISO ni mjumbe wa (uvccm) hii ni hatari ina maana ataongoza kwa matakwa ya chama chake kinavyotaka. Kuna haja sisi kama wanafunzi wa Elimu ya juu kuifanyia marekebisho ya katiba ya TAHLISO au tukivunje chombo hiki tuunde upya chombo kisicho na wadudu (virus) wa kisiasa ili kiwe mali ya wanafunzi kitakachotetea na kusimamia haki na maslahi ya wanafunzi wa Elimu ya juu. Naomba ifahamike kwamba serikali katika kuhakikisha kwamba inaingilia Jumuiya na serikali za wanafunzi, tarehe 12 Juni 2009 (GN.178) Serikali ilikuja na miongozo ya Sheria za wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi serikali ilitoa waraka uliotaka kubadili katiba za Jumiya na serikali za wanafunzi vyuo vikuu. Tanzania ambazo zimeonyesha kuingilia serikali za wanafunzi katika kupata viongozi wao ,na kubadili mfumo mzima wa uongozi wa wanafunzi vyuo vikuu. Mfano kufuta nafasi ya Rais, Mawaziri na manaibu waziri na kubaki na wenye viti na makatibu tu. Mfumo huu ukarudisha mamlaka ya serikali ya wanafunzi kwa Mshauri/Mlezi wa wanafunzi ambaye yeye ni sehemu ya utawala, wakati huo huo ni Rais wa wanafunzi hiyo haingii akilini hata kama unaudhaifu wa kufikiria haitoshi hayo mabadiliko ya mfumo wa uongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu ya kufanywa hata bila kushirikishwa wanafunzi wa Elimu ya juu ambao ndiyo wenye hizi serikali. Sisi tunaamini hizi ni mbinu za kisiasa za kutaka kuuwa sauti za wasomi nchi hii kwa uoga wa viongozi wachache wenye maslahi binafsi katika Taifa letu la Tanzania. Athari yake tayari ishaanza kujitokeza baada kutokea migomo mfululizo chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (Muhas) baada ya kuwasimamisha wanafunzi 85 masomo uongozi ukidai kwamba walikua vinara wa mgomo uliohatarisha maisha na kusababisha uharibifu wa mali wakati chanzo cha migomo au vurugu (Muhas) ni madai ya wanafunzi huo kutaka kurejeshewa serikali yao ya [MUHASO] iliyovunjwa na Baraza la chuo Juni Mwaka 2011. baada ya kukaidi waraka wa serikali wa Mwaka 2009 uliozitaka serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini ya juu kubadili katiba zao. Wanafunzi wa chuo kikuu Muhimbili wakiwa katika sehemu ya mgomo wao wa kishinikiza utawala wa chuo hicho, kurudishwa serikali yao.(Muhaso) WITO: Chonde chonde tunaiomba serikali isiingilie serikali za wanafunzi vyuoni na jumuiya zao iwaache wajiongeze wenyewe na matatizo yao au shida zao wazipeleke serikalini kupitia viongozi waliowachagua wao wenyewe ili kuepusha wanafunzi kuchukua uamuzi wa kuandamana na kugoma vyuo vikuu. Tunaiomba serikali kupitia usalama wa Taifa na utawala vyuoni kutoingilia mchakato wa upatikanaji viongozi wakati wa uchaguzi ili wanafunzi wachague chaguo lao kuondoa mpasuko mara tu ya uchaguzi kati ya wanafunzi na serikali za wanafunzi ili kuepusha migomo na maandamano ya mara kwa mara. Vyuo vikuu nchini. 3) SUALA LA ONGEZEKO KUBWA LA WANAFUNZI ZAIDI YA MIUNDOMBINU ILIOPO. : kama vile Kumbi za mihadhara (lectura rooms) Madarasa yaliyopo kwa sasa hayatoshi.Kuna mrundikano mkubwa wa wanafunzi wakati wa vipindi hadi kufikia baadhi ya wanafunzi kusimama wakati wa vipindi hadi wengine wanafunzi kumsikiliza Mwalimu wakiwa nje ya vyumba au kuchungulia madirisha ni suala hili ni tatizo tunaomba serikali ilichukulie kwa uzito kwani imefika mwalimu kutumia vyombo vya sauti kama anahutubia mkutano wa hadhara kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi na ufinyu wa madarasa ya kusomea (lecture rooms na seminar rooms) Athari ya suala hili ni wanafunzi kushindwa kumsikiliza Mwalimu vizuri kutokana na idadi ya wanafunzi kuwa kubwa na kushindwa kuomba msaada wa kimaelekezo kutoka kwa mwalimu wakati wa kipindi darasani kutokana na idadi ya wanafunzi kuwa kubwa hivyo kuathiri kiwango cha uelewa kwa wanafunzi na viwango vya ufaulu kushuka kwa ujuml WITO wetu kwa serikali tunaiomba au iandae mpango mkakati wa kidharura wa kukabiliana na hali hii kwa kuongeza madarasa yatakayoendana na idadi ya wanafunzi darasani ili kunu suru hali hii kwa haraka na kwa manufaa ya taifa kupata wasomi bora. TATIZO LA ADA KUPANDISHWA MARA KWA MARA VYUO VIKUU BINAFSI HAPA NCHINI. Kumekuwepo na utaratibu wa vyuo visivyo vya umma (Private university) kupandisha ada (fees) mara kwa mara hata shule binafsi za serikali nazo pia serikali imeziacha kujipangia Ada (fees) kadri wanavyotaka. Kibaya zaidi wakati mwingine Ada hizi hupandishwa katikati ya muda wa masomo, Tunaomba serikali ifikirie kama mwanafunzi anaingia Mwaka wa pili, mzazi wake amejifunga mkanda kumpeleka mwanae hapo chuo cha binafsi au ndio amechaguliwa na (TCU) ghafla linatokea ongezeko la asilimia 60% kwenye Ada (Fees) je? Amwachishe chuo. mfano ada ya chuo Kikuu Tumaini imepanda kutoka Tshs 1,500,000 hadi Tshs. 2,500,000 mwaka huu wa masomo hili ni pigo kwa walalahoi, Jamani serikali mko wapi vyuo binafsi wanapandisha ada (fees) wanavyotaka huku serikali kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi mko kimya. Walala hoi watasoma kweli vyuo hivi? Hawa ni wanafunzi wa Chuo cha (IMTU) ikiwa ni sehemu ya mgomo kushinikiza utawala wa chuo hicho. Kulipa ada kwa Tsh.badala ya dola ya Marekani na kupunguzwa kwa fees ya masomo yao. Tunaomba serikali itambue kuwa kumekuwepo usiri mkubwa kati ya vyuo binafsi (private) na wizara husika ya Elimu na mafunzo ya ufundi kuhusu upandishaji holela wa ada vyuo binafsi. Pamoja na shule binafsi za sekondari na msingi kupandisha ada (fees) kiholelaholela ni ajabu serkali kuwa kimya na kuviacha vyuo hivi kufanya watakavyo katika maamuzi ya kupandisha gharama za Ada (fees) vyuoni bila serikali kuvizibiti na kusimamia katika masuala ya upandishaji wa ada zao vyuoni. Na kama serikali haitaliingilia kati suala hili sugu la upandishaji holela wa ada (fees) vyuo binafsi (private) na shule binafsi (Private) za sekondari na msingi ipo hatari shule hizi na vyuo hivi kugeuka biashara kitu amabacho ni mzigo na maumivu kwa wananchi wa kipato cha chini. Lakini tunaomba serikali itambue kuwa suala la vyuo kupandisha ada (fees) holela tayari limezua vurugu na migomo baadhi ya vyuo vikuu vya binafsi hapa nchini kama tunavyoona hapo juu. Chuo cha CBE tawi la Dodoma tarehe 07/03/2011 siku ya Jumatatu wanafunzi waliitisha mgomo pamoja na madai mengine mojawapo ilikuwa ni upandishaji wa ada kiholela, mgomo ulianza tarehe 07/03/2011 Jumatatu na Jumanne walioshiriki mgomo ni wanafunzi wa shahada tu. Na siku ya Jumatano mgomo ukawa wa chuo kizima kwa kuhusisha wanafunzi wa ngazi zote (certificate hadi postgraduate) Chuo Kikuu (IMTU) International and medical Technology University) kwa muda mrefu tumeshuhudia wakiwa katika mgomo wa muda mrefu zaidi ya miezi mitatu. Hawa wanafunzi wa (ifm) wakiwa katika mgomo, wakipinga malipo ya ada kiholela. Kwa muda mrefu wanafunzi wa (IMTU) walikuwa wakilalamika na kuingia kwenye mgomo uliochukua muda mrefu wakipinga kutozwa ada (fees) kwa kutumia viwango vya dola badala ya Tanzania shilingi Tshs. Hadi hapo walipoandamana hadi wizara ya Elimu . baada ya kufika wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi. Katibu mkuu wa wizara ya Elimu profesa Hamisi Dihenga alisema kushuka kwa shilingi. Shs. Mwaka hadi mwaka kumesababisha ada kupanda mara kwa mara kwa mujibu wa profesa Dihenga ada ya mwaka 1996 ilikuwa dola (4,500) za kimarekani sawa na Tshs. Milioni 2,700,000 wakati kwa kiasi hicho mwaka huu ada ni T.shs milioni 7,299,000 hii ni hatari kwa maskini ni hatari kwa wazazi wenye vyuo hivi hasa walala hoi karibia vyuo vyote vya binafsi kama Bagamoyo University na vingine bado ada yao iko juu kiasi kwamba mkopo anaopewa mwanafunzi hautoshi kulipa ada tu. Inasikitisha kuona madaktari wetu wajao wanavyo teseka na swala la upandishaji ada kiholela. Tunaomba ifahamike kwamba bodi ya mikopo nayo ilitoa waraka wa wazi kwa mwaka wa masomo 2009/2010 ikinukuliwa kwamba bodi ya mikopo (loarn board) haitawajibika kwa chuo chochote kuongeza ada (fees) ya wanafunzi huku vyuo vingine vikitii amri vingine vikikaidi amri halali ya bodi ya mikopo. WITO WETU KWA SERIKALI Tunaiomba serikali kupitia wizara ya Elimu iunde chombo maalum au kupitia (TCU) cha kulatibu ada ya Elimu ya juu vyuo binafsi na shule binafsi ili kuondoa ukilitimba wa kibiashara katika elimu na kutoa fursa kwa jamii maskini nao wapate Elimu. Hivyo tunaiomba serikali iliangalie suala hili kwa jicho la huruma na umakini sana. Kama Serikali iliona umuhimu wa kuundwa vyombo kama Ewura, Sumatra kwenye mafuta,maji gesi, na usafiri ni wakati mwafaka kuundwa chombo kitakachosimamia Elimu na Ada (fees) shuleni hadi vyuo vikuu ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. MAPENDEKEZO YETU KWA SERIKALI 1) Tunakuomba sana mheshimiwa Rais pamoja na waziri wa Elimu kwa mamlaka uliyonayo mh. Rais ya kikatiba ibara ya 45 kipengele kidogo Cha 1, a,b,c na d utoe msamaha kwa wanafunzi wote zaidi ya 900 waliosimamishwa masomo, waliofukuzwa vyuo na wale waliofunguliwa Kesi mahakani ili kuepusha migogoro inayiweza kujitokeza kwa wanafunzi kushinikiza utawala vyuo na serikali kuwarudisha wenzetu Vyuoni kwani wao pia wanahaki ya kupata elimu kama watanzania Wengine. 2) utaratibu wa utoaji fedha (boom) za wanafunzi urejeshwe bodi ya mikopo [HESLB]ili kuondoa na kuepusha vurugu zilizoanza kujitokeza kati ya wanafunzi na utawala wa vyuo vikuu .pili itasaidia kuondoa wizi [ufisadi] ulipoanza kujitokeza kutokana na pesa kupelekwa vyuoni kwa kuingiza majina hewa ya wanafunzi .mfano .kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma[poac] imebaini wizi wa sh.miliomi 66 katika chuo kikuu cha mkwawa baada ya kubaini majina hewa ya wanafunzi 32. ambayo yalikuwa yanafanana mwanzo na kufautiana mwisho yakiwa na saini halali za wanafunzi yakionyesha kupewa mikopo 3) bodi ya mikopo ifanyiwe mabadiliko ya uongozi ikiwa ni pamoja na kufanywa marakebisho ya sheria zinazoipa nguvu bodi ya mikopo [HESLB] ya kubadili na kufanya mabadiliko ya sera mara ya kwa mara kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini 4) Uanzishwe utaratibu mpya na bodi ya mikopo kuajiri maofisa mikopo kila chuo kikuu ili wawe kiunganishi kati ya bodi mikopo na chuo husika na kupereka taarifa muhimu Bodi ya mikopo kwa wakati. 5) ofisa mikopo chuoni atakuwa na jukumu la kuakikisha majina ya wanafunzi halisi ambae amesajiriwa na chuo na anatakiwa kupewa mkopo na kubaini wale waliopoteza sifa za kuendelea kupewa mikopo katika muda muafaka mfano mwanafunzi akifukuwza chuo mwanafunzi akisimamishwa masomo kwa muda furani mwafunzi akifeli masomo [discotinuty] na mwanafunzi akifariki afisa mikopo atatakiwa kutuma taarifa bodi ya mikopo ili akaunti ya benki ifungwe mara moja. 6) Ofisa mikopo chuoni atatakiwa kusainisha majina ya wanafunzi na kuyatuma bodi ya mikopo kwa muda muafaka ili kuondoa tatizo la ucheieshwaji wa pesa wanafunzi kutoka bodi ya mikopo kwa kusingizia Eti chuo kichelewesha majina bodi ya mikopo saopo kwa kushirikiana n utawara wa chuo husika watamsaidia kumpatia taarifa muhimu kuhusu wanafunzi kwa muda muafaka 7) Ofisa Mikopo chuoni atawajibika iwapo mgomo au vurugu zitatokea chuoni kwake napofanyia kazi kwa sababu ya uzembe wake hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi mara moja. 8) Kwa kuwa imezoeleka kila inapotakiwa kuongezwa pesa ya kujikimu na malazi kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili ziendane na hali halisi ya maisha ni lazima wanafunzi wagome na kuandamana ndio pesa hiyo iongezwe kama turivyoonyesha mwaka 2008 kutoka sh3500 hadi5000 mwaka 2011 kutoka sh 5000 hadi 7500/= Tunashauri na kupendekeza serikalini kiundwe chombo Maalum ndani ya wizara ya elimu kitakacho kuwa na jukumu kutathimini na kufanya tafiti ya hali halisi ya gharama ya maisha na pesa wanayokopwa mwanafrunzi elimu juu ili kufanya maboresho kwa kushauriana na wizara fedha na hazina ya Taifa na sio kusubiri wanafunzi wagome na kuandmana ndio pesa iongeze wakati wanafunzi wanafukuzwa vyuo na kusimamishwa masomo kwa madai eti walikua vinara wa migomo hiyo na ni aibu kwa nchi yetu inayo hubiri sera ya utawala bora kusubili migomo na maandamano ndiyo inatekeleza madai hayo itakua haina maana. 9) Tunaomba utaratibu wa kujaza fomu ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu juu urejeshwe ngazi ya wilaya kila wilaya kupita mkurugenzi wake au afisa elimu wilaya utaratibu huu utakuwa na faida zifuatazo:- i. Utaratiku huu utasaidia selikali kutambua uwezo wa mwafunzi kiuchumi na kumpa asilimia na gredi zinazostairi kwa mwafunzi na kuondoa vigezo vinavyo tumiwa na bodi ya mikopo ambayo havina ukweli ndani yake kama kigezo cha shule aliyosoma mwanafunzi kwani wanafinzi wanaoludia mitihani na ambayo hawachaguliwi na selikali kidato cha kwanza na kidato cha tano hulazimika kwenda shule binafsi. ii. Utaratibu huu mpya utasaidia selikali kufuatilia urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wanapoanza kazi baada ya kuhitimu masomo yao. Zoezi ambalo litakuawa jepesi kwa wilaya kufika kwenye familia ya mdaiwa wa mkopo au kufanya mawasiliano na familia yake. iii. Utaratibu huu utasaidia serikali kupitia wilaya kuwa na rekodi [DATA BASE] ya wanafunzi walioko vyuoni kila wilaya na kuandaa utaratibu wa kuwatumia [ajira] watakapohitimu masomo yao chuoni. iv. utaratibu huu wakutumia wilaya utasaidia kuondoa upendeleo, kujuana, rushwa, wizi na ufisadi uliomo ndani ya bodi mikopo [HESLB] nchini kwa kuingiza majina hewa ya wanafunzi kwa kujuana na kupokea rushwa kwa kuwapa mkopo na asilimia kubwa watoto wa vigogo (matajiri) huku wanafunzi wanaotaoka familia maskini wakikosa mkopo (No loan) au kupewa asilimia ambazo hawastahiki. Tumeshuhudia ofisa wa Bodi ya mikopo Esther Budili akifikishwa mbele ya Hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam kwa tuhuma za wizi wa sh. Millioni 90 baada ya kughushi majina ya wanafunzi na watumishi katika vyuo tisa nchini. v. Utaratibu huu utasaidia wanafunzi kutoa na kupeleka malalamiko yao ngazi ya wilaya kama itatokea kupewa asilimia ndogo ya mkopo (%) ambayo haiendani na uhalisia wa familia ya mwanafunzi kiuchumi ili afanyiwe marekebisho ngazi za wilaya na kutumwa Bodi ya mikopo. Maana mara nyingi inatokea ndugu wa familia moja waliosoma shule moja na wamefaulu madaraja sawa. cha ajabu na kushanghaza wanapata asilimia tofauti za mikopo (%) haingii akilini. 10) Mkataba (fomu) uwe wazi kwa mkopoji: mkataba kati ya Bodi ya Mikopo na mwanafunzi wa Elimu ya juu uwe wazi ili ajue vizuri masharti ya mkopo anaokopa Mfano: ni muda gani atatakiwa kurejesha mkopo baada ya kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu na atarejesha kwa nani kupitia njia gani ni muhimu viwekwe kwenye fomu ya kujaza kwa ajiri ya mkopo. 11) Serikali ingie mkataba na Benki hapa nchini ili zitoe mikopo kwa wanafunzi wenye ajira tiari (inservice) chini ya udhamini wa serikali na utaratibu wa mkataba wa Benki na Mwanafunzi utumike mkataba wa Bodi ya mikopo (HESLB) ili kuepuka Riba na usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya serikali kuja na sera ya kutowapatia mikopo kupitia Bodi ya mikopo (HESLB) 12) Serikali ifungue akaunti Maalum ya Bodi ya mikopo kwa ajiri ya wanafunzi wa elimu ya juu kuondoa ukiritimba wa ucheleweshaji wa pesa kutoka Hazina kwenda Bodi ya mikopo. Pia Bodi ya mikopo iingie mkataba na Benki nyingine kama NBC, NMB kuliko kutegemea kupitisha pesa kwenye Benki moja ya (CRDB) pekee na CRDB kusambaza taratibu kwenye Benki nyingine kitendo ambacho hufanya wanafunzi wenye akauti tofauti na CRDB kuchelewa zaidi ya siku 5 hadi 7. kupata pesa zao huku wa CRDB washapata tiari na kuleta vurugu. 13). Tunaiomba serikali kupitia wizara ya Elimu iunde chombo maalum au kupitia (TCU) cha kulatibu ada ya Elimu ya juu vyuo binafsi na shule binafsi ili kuondoa ukilitimba wa kibiashara katika elimu na kutoa fursa kwa jamii maskini nao wapate Elimu. Hivyo tunaiomba serikali iliangalie suala hili kwa jicho la huruma na umakini sana. Kama Serikali iliona umuhimu wa kuundwa vyombo kama Ewura, Sumatra kwenye mafuta,maji gesi, na usafiri ni wakati mwafaka kuundwa chombo kitakachosimamia Elimu na Ada (fees) shuleni hadi vyuo vikuu ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi 14).Tunaiomba Serikali isiingilie Jumuiya na Serikali za wanafunzi pamoja na vyama vya siasa kupandikiza vibaraka wao kupitia uchaguzi wa serikali na jumuiya hizo pia tunaiomba Serikali iziache serikali za wanafunzi zijiendeshe zenyewe kwa mujibu wa katiba zao na sio za Magembe (GN) Serikali iwape itupe uhuru wa kujiongoza wenyewe kwani hakuna Taasisi au Jumuiya za watu ambazo Serikali ilizitungia katiba za kujiongoza. Huu ni unyanyasaji uliovuka mipaka ya haki za binadamu. 15). Kuhusu uhaba na uchache wa hosteli vyuo vikuu hapa nchini. Tunaiomba Serikali iandae mpango mkakati wa ujenzi wa hosteli za kutosha vyuo vyote vya umma na kushinikiza vyuo Binafsi navyo kufanya hivyo katika Bajeti ijayo mwezi wa saba 2012/2013 kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. Pia tunaishauri Serikali ili mpango huu wa ujenzi wa hosteli vyuo vikuu ukamilike kwa haraka na kwa ufanisi ni muhimu Serikali iingie mkataba na Taasisi za hifadhi ya kijamii kama NSSF, PPF, LAPF, GEPF, PSPF. Au Wakala wa nyumba (TBA) na Benki hapa nchini. 16. Tunaiomba Serikali iandae utaratibu wa haraka wa kuboresha na kujenga Miundombinu mpya itakayoendana na ongezeko la wanafunziwa elimu ya juu kama madarasa, kumbi za mihadhara n.k. OUR ADVICE TO THE ADMINISTRATORS OF DODOMA AND DAR ES SALAAM UNIVERSITY Constructive administrative decisions should be applied beyond reasonable doubts by administrators in University when dealing with students demands in their learning process. Its an embarrassing situation seeing Vice Chancellors and their administrative associates failing to give helpful decisions in settling problems facing students. In most cases, their decisions effect students and the country as whole. Since 2008, the University of Dar es Salaam (UDSM AND UDOM) faced riots almost in very year, a situation compelling the public to question what is wrong with the oldest University in the Country. At the end of 2011, students at Mwalimu Nyerere Campus were at demonstration demanding for their right to access loans tuition fees, meals and accommodation allowances. Unfortunately, the UDSM and UDOM administration under the leadership of the vice Chancellors, Prof. Rwekaza Mukandala and prof Idris Kikula targeted only 48 students in udsm and 670 in udom who were reveled that the administration had no proof to substantiate that the expelled students were the real instigators of the strike. Out of the total number of expelled students, some submitted their appeals to be reinstated without fruitful results. To get a true picture of the problem has become difficult since the relevant man to do an assessment is the Vice Chancellors themself, Prof. Rwekaza Mukandala and prof Idris Kikula who has become elusive to give more light to the predicament. It only reffects his negative attitude on people and failure to be accountable to the public members who he sworn to defend and promote. If the VC is such a busy man then he doesn’t qualify to lead such an important institution. No wonder he doesn’t care about students problems thinking that they are a nuisance while in reality are the ones who have made him occupy such a position. The African reporter submitted enquiries to the Vice Chancellor about students matters but the didn’t neither answer the questions nor delegate the responsibility to his assistants! Leaders should learn to delegate power and not moving with office keys in their pockets. Increase team working spirit particularly in educational institutions. Frequent meeting are instrumental tools in running any institution education institutions included. The meetings aim at reviewing and analyzing what the institution have accomplished to be ac-completed and developing plans and strategies for future. It was wonderful as professors sat-down to solve the issue of students loans but they finally came out with the recommendations to expel the students for good. I think they are confused since the decision is arbitrary, excessive and parochial in nature lacking democratic elements and void of compassion. In April 17- 24-2008, UDSM there was a tag of war between the students and the administration following the suspension of some students. The suspension caused students to boycott classes pressing the administration to reinstate the suspended students. At that time DARUSO President Deogratias Daudi said “We held the meeting with the administration to iron out the problem but the administration remained stiff and uncompromising.” Analysts quarry on what is the probem behind UDSM and UDOM students strikes failing to know whether Prof. Mkundala’s administration and Prof Idris Kikula’s administration has failed to run the Universities or is the problem of the students themselves as since 2008 students have not stopped boycotting udsm. And which start udom. Moreover, the field Force Unit (FFU) Kinondoni was deployed under regional Police Commander Jamal Rwambowe said, “we had received the names of 16suspended students as ring leadrs who stared rioting since February 2008 due to water short age”. The 2008 demostration caused the death of one student named Dominic Deogratus due to chaos at the University. UDSM and UDOM leadership needs to learn from other Universities with in and outside the country regarding that Professors are the main advisors of the state. There is a belief that their decisions are above the bar. It could be wise for them if they cant handle students to put down the tools and pave the way for others to take over. It is not good to rule the institution by using your iron hand and out od political dichotomy. In 2008, further demonstrations took place at the some University during the election for DARUSO leaders. One of the contestants for the presidential post Odong Odwar was stoped from contesting by the administration. He was given stiff conditions to prove his legality being at the campus. But how a student’s legality resurfaces during the election. Further in vestigations revealed that it was a political influence. Dr Kenneth Blanchard, Ph.D. and Spencer Johnson, in their book gave tips on management once to seek for advice how to manage the institution. The young man found “a one minute manager” in the office. In the discussion, the manager took the young man to stand at the window looking outside. The young man was asked how many foreign cars were along the road. The young man said “I see more of them every day” The managers asked him why people buy foreign cars. Is it because our country did not make enough cars? Or because the did not make the quality car the public really wanted? The young man said it was a question of quality and quantity. The manager added quality is simply giving people the product or service they really want and need. Productivity is about both quantity and quality. And frankly, the best way to achieve both of these results is through people. The young mans face showed surprise. He had never heard of a One Minute Manager”. Therefore, from this parable, one can imagine, what kind of students do Universities in Tanzania produce. Do universities produce both quality and quantity graduates? What kind of leadership do the learning institutions needs? How could they produce both, if the management, administration and leaders do not clearly show the commitment to give quality and quantity education in the country? Of course we have profession, well respected but we don’t see tangible management examples geared to improve education in the country. Plato advocated about education by insisting that children suitably gifted are to be trained by the state so that they may be qualified to assume the role of a ruling class. The idea or the principle of Plato goes almost differently or against some of the Professors in the Higher learning Institution like UDSM and UDOM that want them to be puppies and men! But obviously the students who were, sent home are the losers since they don’t learn anymore while the Professors are working and getting more salaries. Will the country produce quality and quantified graduate? What do the University of Dar es Salaam and University of Dodoma, the Ministry of education and the state of Tanzania think about this to wards the common tendency of expelling students? For example, it was revealed that students from UDOM this year submitted appeal cases before the dean of the students to be presented to the vice Chancellor for review same to UDSM. Unfortunately, they were kecked out. Jean Piaget the Philosopher placed great value of education in children. He declared in 1934 that, “ only education is able to save our societies from possible collapse, whether violent, or gradual. He described children as little scientists seeing them active. Professors must learn from them from these living examples. These great Philosophers differ in opinion with current Professors at the University of Dar es Salaam and University of Dodoma and other Higher learning Institutions as they fail to capitalize on students potentials buy handling problems hampering smooth learning environment. Professors have read a lot about psychological, administrative, leadership, philosophical books and done researchers how they could discipline the old and the young people in different. So we expect them to be capable of accommodating the situation. Despite having all the required knowledge, they resorted into dismissing students with limited evidences showing their participation in instigating riots. They just “believed that the expelled students were involved in the strike with limited proof. Although they could be found with some mistakes or errors, the Professors had to give alternative punishments including being enrolled in other Universities. I believe that UDSM and UDOM administrators have read about Mason, a British educator who invested her life in improving the quality of children’s education. The problems with most of academicians in Tanzania is that they engage themselves more in political matters, to prepare themselves to feature in to politics after retiring from the public services. In this way, they keep their commitments open and thus ruining the education sector unnoticing. Masons philosophy of education was probably the best. He said “Education is an atmosphere, a discipline, a life” and “Education is the science of relations”. Professors could not teach students educational relationships. That failure indicates that Professors decisions bear some shortfalls. She Mason) believed that children were born persons and should be respected as such; they should also be taught the way of the will and the way of Reason. “I ought, I will”. Therefore, professors should embrace such charisma. Students by laws do not allow expelling any student without watertight evidence. How did they come with the sloppy decision? Locke (1632-1704) had some thoughts concerning education. He expressed the belief that education makes the man. He said “I think I may say that of all the men meet with, nine parts of ten are what they are, good or evil, useful or not, by their education”.It is interesting to note that University Professors are at the forefront to prove to the world the administrative principle lapses and how to run companies, national economy as consultants and advisors of the President! But they miserably fail to solve loan problems for 14,000 students in the country. This is the reason why Locke said “I think a may say that of all the men we meet with, nine parts of ten are what they are, good or evil, usefully or not, by their education”. There is a saying in the philosophy of education which states that Perenialists believe that one should teach the things that one deems to be of everlasting importance to all people everywhere. They believe that the most important topics develop a person. This is what the students need to get from professors. Instead our professors chase the students from colleges. Are the developing the country or destroying it? The same students receiving incomplete education at UDSM and UDOM are the ones who would work at Bank of Tanzania to produce fake and substandard bank notes that are significantly ruining our economy. The government under President Kikwete pledged to provide free education to all primary school pupils and after loans to Higher Education students. But students every year go on rampage demanding their loans while they qualified to join Higher Education institutions. It was received about 14,000 students did not receive loans a reason that triggered for a massive demo. Among the priorities declared by president Jakaya Kikwete after he was elected to become a president was strengthening the education sector. He said “ we will strengthen the higher education students loans Board so that it can offer its services to more people.Some students were quoted as saying “we went on rampage after the Minister for Education and Vocational Training, Dr, Shukuru Kawambwa told us that to loan board had reached its maximum limit of offering loans while majority students were not allocated. The Retired Secretary General of the United Nations Kofi Annan once said “todays real borders are not between nations, but between powerful and powerless, free and the fettered, privileged and the humiliated”. The conflicts that students in particular and the public at large facing right now, is because they are powerless. They are powerless because they are poor, they are poor because they are not educated, and most of them are not educated because they share certain political views. The powerful people in Tanzania are the ones with education, money , or have some connection with an eminent political figure. This is were the border is created between the rich and the poor, educated and uneducated.Poverty is one of the major reasons for the rising crimes rate in may developing countries Tanzania included. There fore the expelled students from UDSM and UDOM will follow track to become rebels if not handled with care because of in-conclusive and not constructive decisions made by the Universities administrators in collaboration with some politicians.It is our hope that the president aware about the expelled students because of demanding loans as per his statement. In that regard we are waiting for his statement on this important matter that would reflect what he said when he was first elected to lead Tanzanians. USHAURI WETU KWA MWESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Sisi kama wasomi (intellectual) tumeona ni vizuri kutumia nafasi hii kukushauri Rais wetu katika harakati za kuongeza kasi ya Maendeleo ya uchumi ili kupunguza umasikini kwa Watanzia. Mheshimiwa Rais Mojawapo ya mambo makubwa katika Awamu ya nne ni msukumo mpya wa kuendeleza kilimo. Tumeshuhudia bajeti ya sekta ya kilimo ikipanda kutoka asilimia 3 ya bajeti kwa mwaka 2001/2002 hadi kufikia asilimia 7.8 mwaka 2010/2011. Pia ruzuku imepanuliwa kutoka kwenye mbolea peke yake hadi kwenye pembejeo zingine kama mbegu na zana za kilimo. Kwa matokeo yake fedha zinazokwenda kwenye ruzuku zimeongezeka kutoka shilingi billion 2 mwaka 2003/04 (sawa na asilimia 1.3 ya bajeti ya kilimo. Mheshimiwa Rais chapisho la mpango huu linaonesha kwamba lengo kuu katika sekta ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa cha kisasa, cha biashara na chenye tija kubwa. Katika andishi la kilimo kwanza imeonyeshwa waziwazi nini kifanyike lini na nani. Wasiwasi uliopo ni kwamba chapisho la kilimo kwanza ni chapisho kama yalivyo machapisho meni hapa nchini yenye lengo la kuendeleza sekta ya kilimo mfano: Dira la Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA, Mini – Tiges Plan, ASDP, AMSDP, MKURABITA, na sera mbalimbali. Kama sio Mwenyeji wa Tanzania ukisoma ahadi zilizomo katika machapisho haya hasa kuhusu kilimo cha wakulima wadogo utadhani nchi itaendelea kesho. Lakini mtu mwenye akili husu akipitia mpango huu kwa makini haraka sana atagundua kwamba hakuna kitu ambacho unaweza kukiita “ubunifu” katika mchakato mzima wa utkelezaji wake ili kuweza kutoafautisha mpango huu na mipango mingi iliyotangulia na kushindwa-maneno, ahadi na mbinu ni zile zile. Kuna mashaka sana kwamba mpango huu utafanikiwa kwa sababu unadai utatekeleza mambo yote kwa miaka mitano ambayo tumeshindwa kuyatekeleza katika kipindi cha miaka 50! Mpango hauelezi tumekuwa tukikosea wapi na umewekwa mkakati gani kukwepa makosa hayo katika kutekeleza mpango huu. Kwa ufupi hakuna ubunifu katika utekelezaji wa mpango huu. Ila ubunifu kidogo unajitokeza katika kutafuta fedha za kugharimia mpango wenyewe. Mheshimiwa Rais ikumbukwe kwamba si kweli kwamba Tanzania haiendelei kwa kukosa mipango mizuri, fedha, wataalam. La hasha. Nchi ina ugonjwa sugu wa kushindwa kutekeleza mipango yake ya dhati kwa sababu mbalimbali kama ubadhilifu na kutowajibika kwa watendaji. Machapisho yanaonyesha kwamba mpango huu utagharimu shilingi trilioni 37.3, kati ya hizo shilingi trilioni 3.8 sawa na karibu asilimia 10.3 ya bajeti yote zitatumika kwenye sekta ya kilimo. Hii ni fedha nyingi sana na ni mfano mzuri wa kulenga mbali tulikoongelea mwanzoni mwa mada hii, na hatuna shaka kwamba fedha hii inaweza kupatikana lakini kwa vile mbinu za utekelezaji zitakuwa zilezile zilizozoeleka na watu ni walewale natabiri (hypothesize). Fedha yote hii itaisha na sekta ya kilimo itakuwa na matatizo yale ya miaka yote, ambayo ni pamoja na : kutegemea huruama za mbingu kuleta mvua; ukosefu wa miundombinu ya kusaidia uzalishaji na usambazaji; mfumo dhaifu wa utafiti na uhgani; matumizi hafifu ya pembejeo na zana za kisasa; kukosa mfumo madhubuti wa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo; mfumo duni wa usambazaji wa pembejeo; matumizi ya mbegu duni za mazao na wanyama; kiwango kidogo cha usindikaji wa mazao ya kilimo; kukosekana kwa mfumo madhubuti wa matumizi ya ardhi; kuathiriwa na hali ya hewa pamoja na soko la uhakika la mazao yao. Mheshimiwa Rais haya ni mapendekezo yetu kuhusu sekta ya kilimo ili kurekebisha makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya ili kuhakikisha Mapinduzi ya kijani Tanzania:- Kwa kuzingatia changamoto na matatizo yanayokwamisha ya serikali yako ya nne ya kilimo kwanza. Tunapendekeza liundwe Baraza la ushauri la kilimo (National Agricultural Advisory council) (NAAC) wajumbe wa baraza hilo wateuliwe bila kujali mwelekeo wao wa kisiasa au kazi zao. Wajumbe wa baraza hilo wawe ni wataalam waliobobea kwenye kilimo ambao historia ya matendo yao (track record) inaonyesha mapenzi na uwezo mkubwa wa kuchambua changamoto zinazokabili sekta ya kilimo. Kuwa na cheo kikubwa serikalini au msomi wa masuala ya kilimo kisiwe kigezo cha kuwa mjumbe wa NAAC. Mjumbe anaweza kuwa mfanyabiashara, mkulima, mfanyakazi wa serikali, mwanasiasa, au mtu binafsi ili mradi awe na uelewa wa kutosha na rekodi inayoweza kuthibitishwa ya uwezo wake wa kuchambua vikwazo vya sekta ya kilimo. Usalama wa Taifa unaweza kusaidia upatikanaji wa wajumbe hao kwa mtindo ule ule ambao wa Mwl. Nyerere alikuwa akitumia kuwapata viongozi. Baraza hilo lipewe jukumu la kufikiria kwa kina, kwa niaba ya watanzania wote, changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo na kupendekeza mipango ya kukabailiana nazo. Ikiwezekana wapewe uhuru zaidi ya kuwa visima vya fikra (think tank) za maendeleo ya sekta ya kilimo. Hapa hatupendekezi kitu kama mabaraza ya ushauri ya mikoa au wilaya (Regional and District consultative councils – RCC and DCC) ambazo ujumbe wa mtu hutegemea cheo cha mtu pale mkoani au wilayani. Kuwa na cheo hakuna uhusiano wa moja kwa moja na uwezo wa kufikiri kwa kina wa mhusika; mara nyingi hutemea uhusiano wa mteuliwa na mteuaji. Bila ya kuwa na chombo kama hiki, maamuzi magumu kuhusu mwelekeo wa sekta ya kilimo yanaachwa mikononi mwa wanasiasa wakiongozwa na mapenzi yao, ambayo mengine yanaweza kuwa yameathiriwa na Rushwa, kujuana, kutowajibika n.k. Mapendekezo ya NAAC yawe yanawekwa hadharani kwa wadau mbalimbali (kwa nkia itakayo kuwa inapendekezwa) ili kujadiliwa na kuwa na umiliki wa mpango wowote utakaotekelezwa. Kwa njia hiyo Tanzania ianweza kuwa na mipango yake mwenyewe kuliko hii ya sasa ya kukata na kubandika kutoka kwa wengine. Kuanzishwa kwa (NAAC) kwende sambamba na kuanzishwa kwa baraza dogo la Mawaziri (Mini Cabinet) ndani ya baraza kubwa la Mawaziri. Mawaziri wa Mini Cabinet wawe ni wale wanaoongoza wizara zinazohusiana na uzalishaji na kukua kwa uchumi. Kwa muundo wa bara la mawaziri la ssa wanaweza kuwa Waziri Mkuu, Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa kilimo usalama wa chakula na ushirika, Waziri wa Maendeleo ya mifugo na uvuvi, Waziri wa fedha na uchumi, Waziri wa ujenzi, Waziri wa viwanda na Biashara, Waziri wa uchukuzi, Waziri wa maji na umwagiliaji, Waziri wa uwezeshaji na uwekezaji na Waziri wa kazi vijana na Ajira. Hawa wanaweza kuwa wanakutana kupokea mapendekezo ya (NAAC) kupanga utekelezaji wa mipango ilipendekezwa na NAAC. Lakini yatosha tu kusema pendekezo la kuundwa kwa Baraza la ushauri la kilimo linaweza kuzaa matunda iwapo kutakuwepo na utashi wa kisiasa wa kweli na mawazo ya kimapinduzi ya kijamii. Mheshimiwa Rais wananchi wako wanateseka na mfumuko wa bei za bidhaa uliofikia asilimia 20 sasa. Watanzania wengi wameshindwa kumudu gharama za maisha huku tukiambiwa uchumi wetu unaendelea kukua. Hivi huku kukua kwa asilimia za uchumi wakati wananchi wengi wanakabiliwa na ugumu wa maisha kuna maana gani. Hivi kipi ni sahihi; kasi ndogo ya kukua kwa uchumi inasababisha walio wengi kuwa masikini au umsikini wa walio wengi kuwa masikini unasababisha uchumi kukua kwa kasi ndogo? Ingawaje swali hili linaonekana kuwa jepesi, lakini ni la msingi mno katika kutafuta suluhisho la kasi ndogo ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Kwa mtu ambaye haelewi maana ya kukua kwa uchumi anaweza kuwa na shida ya kupata jibu la swali hilo. Mheshimiwa Rais tuanze kwa kueleza maana kukua kwa uchumi. Kukua kwa uchumi kunapimwa kwa ongezeko la pato la Taifa, Kiingereza Maarufu kama Gross Domestic Product (GDP) kwa nchi zinazoendelea. Pato la Taifa ni thamani ya bidhaa na huduma mpya zilizozalishwa au kutolewa katika uchumi wan chi kwa kipindi husika. Kipindi hiki kinaweza kuwa mwezi, miezi, miezi mitatu au mwaka. Kwa maana hiyo, iwapo zitazalishwa bidhaa pamoja na huduma nyingi zaidi basi pato la taifa huongezeka. Hivyo hivyo iwapo zitazalishwa bidhaa au huduma ndogo pato la taifa hupungua. Kupungua au kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa au huduma, kwa kiwango kikubwa hutegemea mahitaji ya bidhaa au huduma husika. Iwapo mahitaji yatakuwa makubwa zitazalishwa bidhaa nyingi zaidi, na kama mahitaji yatakuwa madogo bidhaa zitazalishwa kidogo. Mahitaji haya ambayo kwa kingereza yanajulikana kama aggregate demand, kwa mantiki hii ni matumizi ya pesa kununua vitu au huduma. Kwa hiyo uaweza kuona kwamba kumbe kukua au kudorora kwa uchumi kuna uhusiano wa karibu zaidi na ununuzi wa jumla yaani aggregate spending. Hii ina maana matumizi yakiongezeka na pato la taifa huongezeka na kinyume chake ni hivyo hivho pindi matumizi yakipungua. Kama ununuzi ndicho kigezo kikubwa cha kuongezeka au kupungua kwa pato la Taifa ni vizuri tukaangalia ni vitu gani husababisha ununuzi kuongezeka au kupungua. Kitaalamu, vitu hivyo vinawekwa katika makundi manne (4) ambavyo ni Kaya ambapo mtu binafsi au familia inanunua vitu au huduma mbalimbali kama chakula, kodi ya pango, matibabu na vinginevyo. Kundi la pili ni wazalishaji likiwakilisha matumizi ya wazalishaji wanaponunua malighafi za kutengenezea bidhaa nyingine. Kuna serikali kundi la tatu ambayo hununua bidhaa mbalimbali wa ajiri ya kuhudumia jamii kama vile shule, barabara na hospitali. Kundi la mwisho ni la wanunuzi wa nje ambao hununua bidhaa za nchi husika. Lakini kwa hili la mwisho kinachoangaliwa ni tofauti kati ya thamani ya bidhaa zilizonunuliwa na wageni na zile ambazo wageni waliiuzia nchi husika. Iwapo thamani ya bidhaa au huduma iliyonunuliwa kutoka nje itazidi ile ya bidhaa au huduma iliyonunuliwa kutoka nje itazidi ile ya bdihaa au huduma zilizouzwa nje, pato la Taifa litapungua, na litapanda itakapokuwa kinyume chake. Katika pato la Taifa kundi la ununuzi wa kaya ndilo huwa kundi kubwa zaidi na kukua kwa uchumi ambako kunanufaisha sehemu kubwa ya jamii, kunatakiwa kutokane na ongezeko la ununuzi wa kaya. Hii ina maana kwamba kama nchi itakuwa na kaya nyingi ambazo zina uwezo mkubwa wa kununua, basi hata uchumi wake utakuwa mkubwa zaidi kwa vile bidhaa na huduma huhitajika kwa vile bidhaa na huduma huhitajika kwa wingi. Kaya zitahitaji chakula kingi na kizuri zaidi, matibabu bora zaidi, usafiri mzuri, starehe, elimu na mengineyo.Hivyo hivyo, kama nchi ina kaya nyingi zenye uwezo mdogo wa kununua, uchumi wake utakuwa mdogo na utashuka kwa vile kaya zinahitaji bidhaa chache na huduma kidogo tu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba kaya hizi hazina haja na bidhaa au huduma husika, bali kulazimika kuzikosa kwa sababu ya uhaba wa kipato. Lakini fursa ikuruhusu kwa maana ya kipato kuongezeka, mara moja hununua bidhaa hizo kama vile kujitibia vizuri zaidi, kupeleka watoto shule nzuri zaidi, kununua vyombo vya usafiri na mengineyo. Ni kwa sababu hiyo, binafsi tunatilia mashaka mikakati inayoitwa ya kukuza uchumi na kuondoda umasikini katika nchi masikini kama Tanzania. Nafikiri dhana sahihi ingekuwa mikakati ya kuondoa umasikini na kukuza uchumi.Tukishapunguza umasikini wa kipato kwa wananchi walio wengi, hata viwanda vitachangamka kwa vile vitakuwa na soko. Ukifanya utafiti katika viwanda vyetu vingi utagundua kwamba mauzo ya bidhaa zao yamefungamana na shughuli za wakulima. Kiwanda cha urafiki kwa mfano, mauzo ya nguo zake huendana na msimu wa mavuno wakulima wanapovuna na kupata fedha ndipo hunnuua nguo nyingi. Msimu ukiisha tu msimu wa mavuno nguo zinakuwa hazina soko tena. Hivyo hivyo kwa viwanda vya pipi, mafuta ya kula, pombe, sukari, mchele, ujenzi wa nyumba (sementi, mabati, nondo, rangi, misumari,mbao) Tv, Redio, na vinginevyo. Lakini kwa kujua au kutojua viongozi wan chi masikini kama yetu wanaweza kuwa na mikakati ya kukuza pato la Taifa kwa kuongeza ununuzi wa moja ya yale makundi mengine kama vile wazalishaji (ongezeko la wawekezaji) na wageni (ongezeko la mauzo nje ya nchi). Wanaweza kufanikiwa kama ambavyo Tanzania imefanikiwa kupata wawekezaji katika migodi, viwanda, majengo makubwa na mashamba makubwa. Na kutokana na uwekezaji huo wanaweza kufanikiwa kuongeza mauzo nje ya nchi, na kweli pato la Taifa litaongezeka kama ambavyo limekuwa likiongezeka kwa asilimia 6 hadi 7 kwa miaka mitatu iliyopita. Lakini kukua huko kwa uchumi hakutakuwa na manufaa kwa wananchi masikikni walio wengi kwa maana ya kupungua kwa umasikini kwa sababu hata hizo fedha zinapoingia zinaishia mikononi mwa wachache. Kwa kutojua hilo ndio maana viongozi wanashindwa kuelewa kinatokea nini; mbona uchumi unakua vizuri tena kwa kasi lakini watu wanazidi kulalama tu kila kukicha. Kukua uchumi kwa mbinu tunayokwenda nayo kwa sasa Mweshimiwa Rais kutaifanya Tanzania ifanane na nchi kama Kenya na Afrika ya Kusini tunazozipigia mfano na kuzisifu kila mara kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Katika nchi hizi kuna viwanda vingi na uchumi wao ni mkubwa, lakini wananchi walio wengi wamebaki kuwa washangiliaji, huku wakiongelea katika madimbwi ya ufukara. Pamoja na tofauti kubwa baina ya masikini na matajiri, bado Kenya au Afrika Kusini watu wanaishi pamoja hata kama wanamanung’uniko ya chini chini. Mipango ya kueneleza nchi ikiifanya Tanzania ifanane na Kenya au Afrika ksini amani tunayojivunia itatoweka kabisa. Hii ni kwa sababu ya historia tofauti za nchi hizi Kenya na Afrika kusini zimejengwa katika misingi ya kibepari tangu zipate uhuru. Wananchi wameshazoea hali hiyo na wanavumilia. Leo hii Tanzania ina watu wanaokadiriwa kuwa million 42 huku vijana wakiwa asilimia 60 hadi asilimia 70. Lakini wanakabiliwa na tatizo la ajira. Wengi wao hawana Elimu ya kuwawezesha kupata Ajira Rasmi na hata wale wanaohitimu vyuo vikuu wakirudi mtaani wanakumbana na tatizo la Ajira Serikalini wakitaka kijiajiri hawana mitaji (Capita) na mifumo ya ukopeshaji wa kibenki haiangalii mkopaji ana kiwango gani cha Elimu kitakachomuwezesha kukopa na kuzalisha ili arudishe bali benki zinaangalia unamiliki nini (nyumba, Ardhi) ili ukishindwa kurudisha zichukuliwe hizo mali Je,! Hawa vijana wa familia masikini waliobahatika kupata elimu angalau ya vyuo vikuu hawana Ardhi wala nyumba kama mdhamini ili wapate mkopo benki watafanyeje Mweshimiwa Rais wetu? Mheshimiwa Rais ili serikali iweze kutoa huduma za kijamii kwa wananchi kama Elimu, Afya, Maji, umeme, bwawa, mawasiliano ulinzi na usalama wa mali zao inapaswa kukusanya kodi ya kutosha ili kuboresha huduma hizo lakini cha ajabu na kusikitisha suala ambalo ni ugonjwa sugu wa “Rushwa” unaoendelea na kulitafuna Taifa letu na kusababisha kukosa mapato ya kutosha. Mheshimiwa tuna kumbuka “RUSHWA” ni miongoni mwa mambo uliyoahidi kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu kwa kuboresha na kuipa mamlaka taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) lakini Mweshimiwa msaada wa chombo hiki umekuwa ni mdogo au hauonekani kabisa kwa kushindwa kubaini “RUSHWA” inayofanyika mikataba mikubwa ya nchi (Ten percent) mfano Richmond, ununuzi wa Rada, Migodi ya madini na sehemu nyingi za mikataba mikubwa. Nchi yetu Mweshimiwa Rais itaishia mikononi mwa wachache wenye nafasi za uongozi na familia zao huku sisi tukiendelea kuumia na ugumu wa maisha maana huduma za kijamii zote ni ghari kwetu kama Afya, Elimu, Umeme, Maji na mfumuko wa bei ya bidhaa. Kitu ambacho kama serikali ingekuwa inakusanya kodi kama inavyopaswa ingeweza kuzioboresha huduma hizi kwa kuzitengea “RUZUKU” Mfano: TANESCO ili kupunguza na kuondoa taabu wanayopata wananchi pale TANESCO inapopandisha bei za umeme ili shirika hilo liweze kujiendesha lenyewe baada ya kukosa RUZUKU kutoka serikali na kupelekea bidhaa zote zinazotokana na viwanda kupanda mara dufu. Mheshimiwa Rais tunakumbu mwaka 2009 wakati unazindua Jengo la Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika jiji la Dar es Salaam. Ulieleza masikitiko yako wa kusema alilimia 30 ya bajeti ya serikali kila ikipangwa inaishia mifukoni mwa watendaji ukimaanisha TAKUKURU wafanye kazi haswa lakini wapi. Lakini kwa nini Rais wetu ulalamike wewe na sisi wananchi itakuwaje. Rais wawajibishe viongozi wote wenye tuhuma za Rushwa. Mheshimiwa rais ushahidi uko wazi, ripoti za kila mwaka za Mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali (CAG) zinaonesha matumizi mengi yenye kutilia shaka kwa mtindo wa matumizi yasiyoidhinishwa, matumizi yasiyo kwenye vitabu vya mahesabu, malipo yasiyo ya kawaida, malipo yasiyo na viambatanisho, na Halmashauri kupata hati chafu kila mwaka. Kwa mfano: kati ya mwaka 2001 na 2006, fedha kiasi cha shilingi billion 14.5 zilitumiwa vibaya. Pia ripoti ya (CAG) ya Juni 2008 inaonesha kwamba kulikuwepo na mashaka sana juu ya matumizi ya shilingi billion 2.3 katika program ya mbolea ya Ruzuku. Mheshimiwa Rais suala la rushwa, mikataba mibovu (Ten percent), kutowajibika kwa viongozi, ubinafsi vimeendelea kulitafuna taifa na kuwa chanzo cha uchumi wetu kulegalega. Mfano; utafiti uliofanywa na shirika la (Faceit) mwaka 2009 chini ya ufadhili wa serikali ya Denmark ambao uliangali hali ya Rushwa na utawala bora nchini. Taasisi zilizoshika kinara kwa rushwa ni Polisi 76%, Mahakama 71%, Ardhi 64.3%, TRA 54.8%. Mheshimiwa Rais utaona ni namna gani Taifa linakosa mapato ya kutosha ili litoe huduma kwa wananchi kama Elimu, Afya, Umeme, Maji na Barabara kutokana na pato la Taifa kuwa dogo kitu ambacho kinatufanya kuwa tegemezi katika bajeti. Tunaomba serikali imulike, iangaze kwa jicho la kizalendo Rushwa inayofanywa ndani ya jeshi la polisi na namna Taifa linavyokosa mapato, Tunaomba Rais uangalie kwa makini muhimili wa Mahakama kama unatuhumiwa kwa 71% kwa rushwa ni hatari kwa nchi inayojitangaza kuwa na utawala boroa wa kisheria. Ndiyo maana Mafisadi wakipelekwa Mahakamani mwisho wanashinda kesi. Tunaomba kama Rais wetu uangalie kwa makini Sekta ya Ardhi iliyoshika 64.3% kwa rushwa. Tumeshuhudia migogoro vijijini na mijini chanzo cha migogoro hiyo ni Rushwa chonde chonde Rais wetu ingilia kati. Tunaomba Rais wetu kwa Roho ya huruma na moyo wa kizalendo uingalie Mamlaka ya mapato Tanzania iliyoshika 54.8% kwa rushwa hii ni hatari chombo kilichopewa mamlaka ya kukusanya kodi ili Serikali iweze kuwahudumia wananchi wake kinapatikana na hatia ya Rushwa kwa asilimia kubwa namna hii 54.8%. Je? Mheshimiwa nchi yetu kuendelea kuwa tegemezi katika mataifa ya kibeberu kila bajeti yake ya kila mwaka. na serikali kushindwa kuendesha mashirika ya umma kwa kuyapa ruzuku kama (Tanesco), Dawasco ili kupunguza ukali wa maisha na mfumuko wa bidhaa. haya yote na adha hii tutakuwa hatujakosea kama tutatwisha mzigo huu TRA na kubeba mzigo wa dhambi hizo.
1/17/2012. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ilitangaza kwamba Desemba mwaka jana (2011) ilifanya “kufuru” pale waliposema kukusanya kodi kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu kuundwa kwake, zaidi ya miaka 15 iliyopita. Vyombo vya habari vilimnukuu kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA Allan Kiula akisema Desemba, Mamlaka hiyo ilikusanya Sh. 682.5 billioni na kuvuka lengo la Sh. 645 bilioni ambazo hazijawahi kukusanywa kabla. Mheshimiwa Rais kama mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inashika nafasi ya nne kwa Rushwa 54.8% na bado inashangilia eti wamevuka lengo la kukusanya Sh. 645 billioni na wakusanya 682.5 billioni ni dhahiri Rais wetu Serikali yako ikiweka lengo la kukusanya 800 -1000 billioni kwa mwezi inawezekana. Iwapo Rushwa itakomeshwa ndani ya chombo hiki muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. Mheshimiwa Rais ili uweze kutimiza ahadi yao uliowahidi watanzania mwaka 2005 wakati unaomba ridhaa ya kuingia madarakani ya “Maisha Bora kwa kila Mtanzania”. Ni muhimu yafuatayo ushauri wetu ukazingatiwa kwa maslahi ya Taifa letu sote. 1) Serikali yako ipunguze matumizi (ijibane). 2) Mikataba yote (uwekezaji, ubinafsishaji) ipitiwe upya ili ile mikataba iliyofungwa chini ya ushawishi wa Rushwa (Ten percent) ivunjwe kwa maslahi ya Taifa ili lipate mapato stahiki.
3) Serikali iangalie upya Taasisi hizi muhimu hapa nchini TRA na TAKUKURU ili ziisaidie Serikali kukusanya kodi na kusimamia usalama wa kodi za wananchi. Mweshimiwa Rais tunakuwa na mashaka kama Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Usalama wa Taifa kama vijambo hivi vimeshindwa kuisaidia serikali kubaini udanganyifu unaofanywa katika mikataba mbalimbali kama (RICHMOND, UNUNUZI WA RADA) n.k. udanganyifu unaofanywa katika Wizara mbalimbali katika matumizi mabaya ushahidi huu uko wazi ukipitia ripoti zinazowasilishwa na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
4) Mweshimiwa Rais wakati muafaka serikali yako kubadilisha sera ya “Kilimo kwanza” hadi wananchi watakapoelimika na kuja na sera ya “ELIMU KWANZA”. Kwa nini tunakushauri hivyo Mweshimiwa Rais:-
(1) Suala la wanafunzi 9730 kufutiwa matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka jana. (2) Kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika. Shule ya msingi msigani ya Mbezi Kimara Dar es Salaam kushindwa kufunguliwa mwezi januari hadi mwezi machi mwaka huu kwa sababu vyoo vya wanafunzi viliathiriwa na mafuriko ya mwaka jana. Matokeo ya kidato cha nne kuanzia mwaka jana kuonesha zaidi ya nusu kuwa wamefeli. Migomo na maandamano vyuo vikuu iliyosababisha zaidi ya wanafunzi 900 kufukuzwa vyuo na wengine kusimamishwa muda usiojulikana.
5) Mheshimiwa Rais ni wakati muafaka Serikali yako ikapunguza matumizi ili ipate uwezo wa kutoa RUZUKU katika mashirika ya Umma, ili kupunguza gharama wanazozibeba wananchi wa kipato cha chini mfano; Shirika la umeme Tanzania Tanesco likipewa Ruzuku kutoka Serikali itaweza kujiendesha lenyewe jambo ambalo litapelekea Tanesco kupunguza bei ya umeme nchini. Na umeme ukipunguzwa bei ni dhahiri bei za bidhaa nyingi zinazozalishwa viwandani zitapungua. Jambo ambalo litakuwa nafuu na auheni kwa wananchi wa kipato cha chini waweze kuhimiri athari na mfumuko wa bei za bidhaa uliofikia asilimia 20 kwa sasa. Huo ndiyo ushauri wetu Mweshimiwa Rais. Tunaomba kuwasilisha. SHUKRANI Shukrani zetu za dhati zinawendee wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamefanikisha ukamilifu wa waraka huu kwa michango mbalimbali kama ushauri, ushiriki wa moja kwa moja katika kuandaa waraka huu, michango ya watu mbalimbali kwa njia ya makala kupitia Facebook, twiter, Jamii forum, Magazeti, Simu za mkononi, nakala na majarida mbalimbali, michango na mapendekezo ya walimu wetu vyuoni (wahadhiri) lakini shukrani zetu ziwaendee pia wanachi wapenda elimu pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu hapa nchini, pia shukrani zetu ziwafikie viongozi wa Serikali za wanafunzi vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kwa ushirikiano wao katika kufanikisha kazi hii adhimu. Wafuatao tungependa kuwatambulisha kwa majina yao kwa namna moja ama nyingine mchango wao kwa kiasi kikubwa umesaidia ukamilifu wa kazi hii.
DEBORA GABRIEL ( Rais wa chuo Kikuu cha Dodoma) MUSA NDILE (Waziri Mkuu Serikali ya Wanafunzi chuo kikuu cha IFM) MBOYA JAMES (Katibu katika serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha (IFM) DANIEL NAFTAL (Waziri wa mikopo chuo kikuu Cha Dar es Salaam) MRUTA JURIUS (Waziri wa Elimu chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2009/10) LUSAPI, YUDAH (Mwakilishi kamati ya mikopo chuo kikuu cha Arusha) MR. MAKULI (Waziri Mkuu mstaafu Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam) RWEZAULA ROBERT .K. ( waziri mkuu serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha st.John Tawi la DAR ES SALAAM BICHWA SAUL (Waziri serikali ya wanafunzi chuo kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam DUCE ISMAIL MVUNGI (Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Ardhi) MR. SALUM ( Makamu wa Rais serikari ya wanafunzi chuo kikuu Cha Tiba muhimbili) KB OMARI, (Wadau wa Elimu nchini) RANKIM RAMADHANI HUSSENI SUNGURA, (Wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha St. August AMINI RASHIDI Mwanza MUGATA GEOFREY, RUGEMARILA FRENK, (Wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu SELENGIA GEORGE ya Nyerere) HUSSEN RASHID ( Mwanafunzi chuo kikuu cha Tiba IMTU) RICHARD JOHN (Wanafunzi wa chuo kikuu cha tiba Bugando) SADRU MOHAMMED OTHMAN MRISHA, (Wanafunzi chuo kikuu cha Kiislam Morogoro) KURUTHUMU HULEDI Pamoja na wale ambao hatukuwataja humu ndani lakini walitoa mchango wao uliowezesha kufanikisha kazi hii tunatoa shukrani zetu pia kwa walimu wetu mnaotufundisha kwa mioyo ya uzalendo, wazazi na walezi wetu, viongozi wetu wa Dini pamoja na watanzania wote kwa ujumla MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI SEKTA YA ELIMU MASTAWILY FAHAMI MWENYEKITI WA KAMATI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAA 0717262629/0759262629
 
Back
Top Bottom