Mishahara ya SUMATRA kufuru

Mishahara ya SUMATRA kufuru

Ha ha haaa, comments za wadau zimenifurahisha sana!
Kweli 1.53 M nayo ni mshahara mkubwa???. Mwenzetu unataka mishahara ya vibarua nini??
 
hii jf imeharibika sana, watu wanashindwa kufanya tafakuri na kukimbilia matusi badala ya kumuelimisha au kumuelekeza mleta mada, ni ujinga , ni upuuzi...anyway ngoja niseme ni wapuuzi pekee waliomjibu mleta uzi kwa matusi, siwezi kuwaita matahira kwa kuwa sijawapima akili , ila ni wapuuzi.
Mleta mada kaeleza vizuri kuwa katika taasisi za serikali,wengine wanaropoka tu bila kushirikiana na akili zao,twende sawa:
- Wapi katika govt salary scale mtu anapokea dola 25000 kama mchangiaji mmoja alivosema?je uyu aliwahi kusoma hata scale za serikali kweli?anajua high scale ni ipi??au karopoka ?
- Hapa mleta mada kaongelea salary ya mhasibu, akagusia TRA na kwingineko, je mnajua scale za wahasibu hasa new staff kama mleta mada alivosema?mkimbilie matusi,eleza kwa data, dogo mmoja anasema eti atafuatilia mda za mleta uzi ili ajue kama ataamua ambakize kwenye jukwaa ili..vitisho vya nini ?mbona sisi hatujawahi kukufukuza wewe maana haujawahi kupost cha maana isipokuwa kejeli na matusi??
_ Mleta mada hajawa na upeo wa kutosha wa kujua maisha ndo maana kaona slip ya 1point kaogopa, apa si kumtusi, ilibidi kumuelekeza tu kuwa mishahara mikubwa ipo mfano junior meneja wa benki anaweza kuwa na hata 8mil salary ila si kumbeza bila data...jamani tunaishi wapi Tanzania???tunaona kila siku walimu wanagoma kwa mishahara ya lak7, 8 nk wakati manesi wanalipwa chini ya hapo...bado tunamkejeli??
Mleta mada kahamaki labda fani yake mayb mwalimu,sekretary,au ni nesi au mkulima kule Tandahimba,lazma haone ni kubwa, ila tumuelekeze si kumtusi. Mfano, mfanyakazi wa Shirika la Posta ambaye ameanza kazi 28 years ago bado wanalipwa mishahara ya lak4 mpaka 6 wakati vijana tulioanza kazi later than 2007 salary ni five plus time that scale.
Tujifunze kuelimishana na si kutukanana,
I hate wote wanaotukana hata pasipo sababu.
Gsana
 
Unajua mnaweza kumlaumu mtu kumbe yeye hajawahi ona huo mshahara wa mamilion ya fedha, so mnachotakiwa ni kumuelimisha kuwa kuna walio zidi huo na wamo humu humu Tanzania, inawezekana yeye mshahara wake kwa mwezi ni 366,666/= kwa mwezi na hapo hajakatwa kodi, so akiona huo wa milion 1.35, anaona kama ni kumkufuru Mungu.Unajua humu Tanzania kuna wengine wanaishi kama peponi wengine wanajiuliza watapata wapi mlo mmoja kwa siku.
well said Lisa
 
Mtafanya kijana wa watu ajinyonge bure mwacheni tu. Yaani 1.35millioni anaona ni kufuru, hajuai watu wanachukua hadi million 20 na marupurupu lukuki, humu humu Tanzania.

Amesema 1.53 million na siyo 1.35 million
 
Mbona hiyo ni pesa ndogo sana mkuu... umeshawai kujiuliza awa waKenya au waSouth Africa wanaofanya kazi kwenye haya makampuni ya humu wanalipwa kiasi gani???

Utakuta hao "expatriate" wanalipana 20-40mil, alafu waTz hawafiki hata 10... Mkuu ili ni shamba la bibi...
 
Dada punguza pafu!
Wivu wa kike haina maana kwamba mtoa hoja ni mwanamke!
Ila wivu wa aina hiyo, ni tabia za kike, kwamba mwanamke mwenzangu kapendeza zaidi, katengeneza nywele zaidi yangu, na mengine mengi, ambayo ni wivu wa kijinga. Hizo ndio Tabia za Kike

Inategemea mwanamke wa namna gani. Kama unazungumzia mwanamke ambaye hajaenda hata shule ndogo hapo ni sawa. usigeneralise kwa sababu wapo wanawake kama ika Dr Migiro na PROF tibaijuka n.k. ambao sidhani kama wano wivu kama huo.
 
Jamani msimhuzunishe mtoa mada, unapoambiwa wewe umenenepa, inategemea unalinganishwa na nani kujua kuwa umenenepa. Kwa mtoa mada, mjue ni rafiki yake, na kasema ni rafiki yake, Yeye hajasema kipato chake ambacho kalinganisha na huyu wa sumatra. Nadhani ajitafakari kuwa vipato havilingani. Houseboy na Tingo wa Daladala, Wakijilinganisha, houseboy naye atakuja na yake, Matingo wa Bongo mishahara yao Kufuru......
 
Yeah huyu jamaa sio kwamba anaona wivi mimi nimemuelewa kipata hicho nikikubwa sana kwake,na huenda katika mazingira ya kawaida haijatokea kwenye familia yao mtu anayelipwa hivyo,so mngemuelewa na kumsaidia sio kum-accuse
 
hapo bold sasa umeanza matusi,
una uhakika gani kwamba mtoa mada ni mwanamke??
je wewe mama yako alikuwa baba?? na dada yako ni kaka??
mwanao wa kike ni mvulana na mkeo ni mume??

Bora mwalimu gfsonwin umemwambia hivi wivu wa kike na wa kiume ukoje? Yaani wana bore sana watu wengine. Labda hakuzaliwa na mama.
 
Last edited by a moderator:
title yako haioani na ulichoandika mbona??kufuru iko wapi hapo jamani??hujajua maisha yamepanda tu na sio sumatra fanya survey yako uone watu wanavyplipwa kwenye ofisi hizohizo za serikali!JE UMEWAHI KUSIKIA NDUGU MCHECHU WA NHC ANAKUSANYA MKWANJA SAIZ GANI KWA MWEZI??
 
Mtafanya kijana wa watu ajinyonge bure mwacheni tu. Yaani 1.35millioni anaona ni kufuru, hajuai watu wanachukua hadi million 20 na marupurupu lukuki, humu humu Tanzania.
Kweli mkuu, wanamuonea bure kwa kumshambulia. Mie namuona anazo sababu za kuhoji mshahara huo ikizingatiwa taasisi ya umma na muda wa ajira wa huyo jamaa yake.
 
Sijui cape town ni wa kike au ni wa kiume;
unashangaa 1.5m/=
Pole sana; soma na wewe upate maisha bora
kwa kila mtanzania.
 
Last edited by a moderator:
wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
mi nilidhani milioni 153 kumbe milioni 1.53 hivi kwa maisha huo no mshahara wa kufuru? hivi hizo pesa pr Maji Marefu wa STD VII anazikusanya kwa siku ngapi kwa posho tu ya pale Mjengoni?
 
Huyo rafiki yako na wewe wote -------......hakuna kufuru katika mishahara isipokuwa ni wivu wako wa kipuuzi tu. Kwanza mshahara wenyewe mbona bado mdogo au wewe unalipwa na kampuni za maponjoro?
wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
 
Du kama huo ni kufuru ukienda TRA au NSSF unaweza ukazimia.

====================
Ukipata Ujumbe wa Chuki Matusi Futa Delete Kabisa.
====================
 
Huo mshahara ni wa kawaida sana, hautishi kwa lolote. Ila ninachoona ni kwamba, SUMATRA hawana cha maana wanachokifanya katika nchi hii. Kuna umuhimu wa kufanya review ya majukumu ya Taasisi kadhaa hapa nchini. Kwa kweli hii SUMATRA ingeweza tu kufutwa majukumu yake yabandikwe kwenye taasisi zingine.
 
Kuna watu wanafanya kaz BOT kila siku mil 1 tena analalamika anataka mil 2 sasa mshahara wa sumarta mbona mdogo sana.nahis mtoa mada atakuwa mtoto wa mkulima.
 
Kuwa jf sio lazima upost status ndio maana kuna option ya like post zilizofanyiwa utafiti .....tengua kauli
 
wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?

da mkuu acha mbwembwe bana sasa na maisha yalivo juu sasa hivi payee imepanda kila kitu kimepanda unategemea mtu wamlipe sh ngapi??
 
Back
Top Bottom