Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Matokeo ya uharakati wa wanawake feminism, zinapopitishwa sheria za kupendelea wanawake na kukomoa wanaume wanawake wanajisahau na wao watazeeka watoto wao wa kiume au wa kike wakifariki wao wazee hawatapata kitu jasho lao kwa mtoto linaenda kwa mke na ndugu zake tu.
 
Huna mtoto wewe eti mpenzi mtazamaji .
....hta wewe utazeeka na unakuta umefanya effort ila pesa ulilipia ada watoto na wakipata baadae wasikuangalie wewe Uwe mpenzi mtazamaji ni wao na wake zao tu how will you feel?fucking ushauri....
Mzee kubali kataa, kama ulikuwa unapata pesa zote unasomesha means kuna makosa ulifanya, wazazi kulilia mali za mtoto ni aibu
 
“Na huo pia ni utamaduni wetu wa Afrika”.

Umeandika hivyo. Ulimaanisha nini?
Hiyo statement mbona iko wazi kabisa mkuu, na ndio ukweli kuwa ni utamaduni wa watu asili wa Afrika, yawezekana jamii zinabadilika, lakini ukweli hautobadilika. Kama ambavyo kwa utamaduni wetu ni wajibu wa mwanaume kuitunza familia yake.
 
Wakati wa uhai wake waandishi wa habari walienda kwa wazazi wa Kobe na kufanya mahojiano kuhusu maisha ya star huyo na picha za zamani wakawaonesha.
Kobe alikasirika sana na hakuwasamehe wazazi wake mpaka anakufa.

Shikamoo mkuu
 
Binti bado mrembo lazima vijana watapiga tuu na kula mkate wa Kobe.
Kifo ni fumbo sana, ukute mwamba alikuwa anasubiri subiri muda uende aandike mirathi, kifo kikamuwahi.
 
Hata kwenye Ukristo Biblia imesema "Waheshimu Wazazi wako hili.............."hilo neno Waheshimu limebeba Siri kubwa wasioelewa ufikiri ni heshima ya kawaida tu.
Biblia inasema uwaachie urithi wajukuu zako , sio kinyume chake
 
ya wamarekani tuwaachie wenyewe, wana vitu va ajabu sana hawa watu
Na wao wengine wanawaona nyie mna vitu vya ajabu sana kumpa mtoto wajibu wa kumtunza mzazi.

Wanaona that is unnatural, mzazi ndiye anatakiwa kumtunza na kumrithisha mtoto, si mtoto kumtunza na kumrithisha mzazi.

Kuna tangazo moja la biashara la TV Marekani, mtoto kakaa na baba yake wamekula mgahawani, sasa imefikia wakati wa kulipa.

Baba anataka kulipa, lakini mtoto anamkataza kulipa, anasema wewe umestaafu unalipwa pensheni ndogo, fixed income, huwezi ku afford kuitumia ovyo.

Mtoto anataka kulipa.

Mtoto anavyotaka kulipa, baba naye anamkataza kulipa, anasema wewe unafanya kazi bado, una majukumu mengi kuhudumia watoto wako, unatakiwa kujipanga kwenye mafao yako ya uzeeni.

Kila mtu anamfikiria mwenzake.

Nikasema hapa angekuwa Baba wa kibongo angeona kuhudumiwa na mtoto ni sehemu ya "pensheni" yake. Asingemfikiria mtoto.

Tena wengine huwa wanasema kabisa "nakula pensheni".
 
Hiyo statement mbona iko wazi kabisa mkuu, na ndio ukweli kuwa ni utamaduni wa watu asili wa Afrika, yawezekana jamii zinabadilika, lakini ukweli hautobadilika. Kama ambavyo kwa utamaduni wetu ni wajibu wa mwanaume kuitunza familia yake.
Kama ulimaanisha hivyo basi ulikosea namna ya kuandika.

Ulipaswa kuandika ‘Waafrika’ na siyo ‘wa Afrika’.
 
Kulikuwa na shida gani wazazi kuonesha picha kwa waandishi? Au zilionesha "uhalisia" wa familia enzi hizo? Ha ha ha! Ila kama ndio ukweli why akasirike?
PESA mkuu ,wazazi walizitoa Bure kiroho safi kumbe zina thamani ya mabilioni zingefanyiwa biashara kubwa.
Pia walimuanika bila ridhaa yake .
 
Kobe yeye kwa nini hakuwapa ama kuwasaidia wazazi wake akiwa hai?

Mwanaume cha kwanza unachotakiwa kufanya ukifanikiwa ni ku uplift kwanza background yako kabla hujaamua kusimama mwenyewe.

How comes jamaa aliwaacha na kuwatelekez wazazi wake bila kuwainua?

Watu weusi wa ulaya wana malezi mabaya sana. Angalia Ronaldo, amepata pes acha kwanza ni nyumbani, kuinua watu wako, kuinua ndugu zako kisha unaamua kujiinua mwenyewe

Shida ilikua kwa kobe, alikua mtu wa hovyo.
Kwanza ndio leo nasikia habari za mirathi kutoka kwa mtoto kwenda kwa wazazi...
Mzazi mpe maisha ukiwa hai...
Yani kwenye budget yako ya matumizi inabidi uweke kipengele cha wazazi (unless wawe ni watu ambao wanaojiweza lakini bado inabidi uwatumie hata hela ya supu)... tena siku hizi rahisi sana maana kutuma pesa imekua rahisi sababu ya hizi mobile money services..
Otherwise mirathi ni ya spouse na watoto tu..
 
Wamarekani wanamlaumu Kobe Kobe ana makosa ya kutowapa wazazi wake maisha hakuandika wosia kabla hajafa hivyo ni kama alichagua kutojumuisha wazazi wake katika wosia wake hivyo mali zote zimeenda kwa mke wake.

Ukweli wamarekani wana utamaduni wa ajabu sana, how can a person be worth Trillions of Money and his parents are broke? This life is not fair.

Kobe Bryants parents are broke. His dad was forced to auction off the ring Kobe gave him in the year 2000 ili apate hela ya ku survive huku mkewe na Kobe kapewa mirathi ya dola milioni 600 ambazo kobe kaacha bank.


Wazazi wake sio masikini
 
Kabla ya kurukia kuhukumu, inafaa uijue historia ya ugomvi kati ya Kobe na wazazi wake.

Kobe na wazazi wake walikuwa na ugomvi mkubwa Kobe alivyoamua kumuoa Vanessa. Wazazi hawakumtaka Vanessa.

Hata kwenye harusi ya Kobe na Vanessa, wazazi wa Kobe hawakuenda.

Pia, Kobe na baba yake walikuwa na ugomvi kwenye mambo ya kuuza sports memorabilia, baba yake Kobe alikuwa anauza vitu vya Kobe alivyokuwa anatumia utotoni na mwanzo akiwa NBA kama "sports memorabilia" bila kumhusisha Kobe.

Kobe alishawafungulia kesi wazazi wake kuhusu ugomvi huu.

Sasa labda Kobe akaona baba yake aendelee kuuza tu hivyo vitu, na atapata urithi wake kutokana na kuuza hivyo vitu, hatahitaji kupeea urithi wowote kutoka kwake yeye Kobe.

Kama hujui historia ya ugomvi kati ya Kobe na wazazi wake, ni rahisi kutoa hukumu, lakini, ukiichunguza zaidi, unaona historia moja complicated.

 
Back
Top Bottom