Ni kweli baada ya kifo cha baba (mume) kwa asilimia kubwa sana mke, watoto na wazazi wanaingia kwenye mgogoro mkubwa sana

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Suala la mirathi na urithi kwa ujumla linaleta chuki sehemu ambapo upendo ulitawala kwa sababu hakuna utaratibu ambao upo wazi wa kufuata juu ya suala la mirathi. Ni maoni yangu serikali iliwekee sheria na kanuni namna ya kuwawezesha wafiwa kuendelea na maisha mema hata baada ya mpendwa wao kutangulia mbele ya haki.

uzoefu unaonyesha dhahiri familia nyingi zimepasuka vipande vipande kwa kua hakuna muongozo, sheria au kanuni za wazi za kuwasaidia wajane, watoto na wazazi wa kijana/ mwanaume. Ikumbuke mwanamke akifa ni wazi kabisa hakuna mgogoro wa mirathi utakao jitokeza maana kwa utamaduni wa kitanzania na kiafrika kwa asilimia kubwa mali ni za familia chini ya uongozi wa baba kwahiyo sio rahisi mwanamke afariki kuibuke mgogoro wa mirathi.

Mara nyingi mno wazazi wa kijana wamekua wakitengwa na kubaguliwa na kuachwa bila kuthaminiwa kana kwamba walikua sio kitu kwa mwanao badala yake ndugu wa mwanamke wamekua ndio wanufaika wakuu wa mali za marehemu wengi (hapa nazungumzia zaidi marehemu wanaume).

Ikiwepo wazi sheria, kanuni, taratibu pale ambapo hakuna wosia wa marehemu basi watoto, mjane (mwanamke) pamoja na wazazi wa mume (hata wa mke) kwa pamoja wanaweza kupata mwanzo wa kuishi kama ambavyo mpendwa wao alivyo kua hai.

Tizama hapa chini namna ambavyo kifo cha Erasto Msuya kilivyoipasua familia vipande vipande na kupelekea uhai wa watu kupotezwa na mambo mabaya mengi kutokea katika familia hiii kisa mirathi

 
Tumuombe Mungu upendo utawale ndani ya familia zetu kuliko tamaa ya mali aliyotafuta mwingine na kwa jasho la wazazi wake.
 
ni kweli kabisa, yametokea kwenye familia yetu, kama mtoto mkubwa nimeamua kuwaachia madogo wapambanie wenyewe mi nitatafuta zangu.
 
Back
Top Bottom