Dr Wangu wa Muhimbili anasima
"" mgomo hakuna watu wanaendelea na kazi kama kawaida vikao bado vinaendelea"" mwisho wa kunukuu
Sasa tumuamini Doctor wa wapi??? maaana mgomo hakuna:juggle:
Mob psychology ime wa-affect madaktari wetu. Natoa ushauri kila mmoja atafakari ni nini anachogomea hasa kama yeye binafsi bila kutegemea vikao vyao wanavyokaa kupeana molali! Kama ni maslahi yake hayajatekelezwa au ni kuto kujiuzuru kwa mawaziri au vyote viwili. Na ukiangalia dai la kuto kujiuzuri/kutowajibishwa mawaziri imemeza madai yao yote ikiwemo ya masilahi yao. Sasa wawe makini katika madai yao wasije wakawa wanatumiwa na kundi fulani bila kujijua? na hii ndio madhara ya mob psychology. Nawashauri waonane na wataalam wapate ushauri?
Wana JF hivi hatuelewi maana ya Updates. Wekeni updates badala ya kutoa maoni.
Habari za saa ITV zinasema mgomo umeshika kasi, pia wanafunzi wa Muhimbili wameandamana hadi Wizara ya Afya kudai fedha za Chakula.
Kimtizamo unaweza kuona kama madai ya madaktari kutaka kwanza waziri na naibu wake wajiuzulu sio sahihi, ila kimantiki wako sahihi. Mkiwa mnavutana kwenye mambo fulani hasa yale yanayogusa maslahi ya mtu ni vizuri kila upande ukawa na imani na wawakilishi katika majadiliano. Toka mgogoro huu unaanza ilionekana dhahiri kuwa wakuu wa wizara hawakua na nia wala uwezo wa kumaliza tatizo la madaktari. Mara kadhaa wamekuwa wakisema uwongo na kupindisha uhalisia wa chanzo hasa cha mgogoro huo na hatua sahihi za kuumaliza.
Taarifa ya waziri wa afya bungeni kwenye kikao cha mwisho ilijaa upotoshaji na propaganda zisizo na ulazima, hasa zikipambwa na personal attach kwa Dr. Ulimboka. Katika hali kama hii serikali inapanga kukwama kwenye haya majadiliano kwani hata ikitokea imeshindwa kutekeleza baadhi ya madai ya madaktari kwa sababu za msingi kabisa - chini ya mponda na nkya - haitapata imani ya madaktari.
Tafsiri ya kwamba raisi sasa analazimishwa kufanya maamuzi na madaktari haina mashiko. Pamoja na kujifanya eti imemuondoa katibu mkuu kwa tuhuma za uniform na manunuzi ya reagents feki, ukweli unabaki kuwa ni mgomo ndio uliopelekea katibu huyo kuondolewa kwani hayo madai ya mwanzo yamekuwa yakiandikwa muda mrefu tu. Mapendekezo ya madaktari sio amri kwa raisi, lakini katika hali ya kawaida raisi anabaki kuwa na jukumu la kulinda maisha ya watu wake hata kama kwa kufanya hivyo sio tu anatakiwa kufkuza watu kazi bali hata kwa yeye mwenyewe kuachia ngazi pale inapolazimu. The best decision is the one taken timely. Serikali ikubali kuwafukuza sasa waziri na naibu wake au ijiandae kufukuza madaktari na kuweka maisha ya watu rehani
The more they delay to act the worse!
Mponda na Mwenzako, hamkubaliki na madaktari, hivi kwanini hamchukui hatua ya kujiuzulu? mnang'ang'ania nini wizara ya afya?
ifakara hali ni mbaya sana sana sana..........inabidi kipengele kingene kiongezwe cha wazri mkuu akifatiwa na rais waachi ngazi
Hawa madakatari wanatakiwa wauliwe, ni magaidi wanaocheza na roho na maumivu ya watu.
Hauwezi kabisa kila siku ukaja na malalamiko mapya ukae uchekewe tu. Nawaomba sana serikali isiwasikilize kabisa na iwape 2 hours wawepo kwenye kazi zao nje ya hapo, wachukuliwe hatua kali sana ikiwepo na kushtakiwa kwa kila kifo kitachotokea wakati wa mgomo, wakasote jela wakijibu kesi za mauaji.
Madaktari wana akili timamu na wengi wao ni first class material ya high school. Sasa vichwa vyote hivyo vikikutana sidhani kama kweli watashindwa kuanalyse mambo yao ya msingi badala tu ya kuwa pushed kama unavyosema "mob psychology". Kitu cha kujadili hapa nafikiri ni kuangalia kama kweli madai yao ni ya msingi.
Nafiki maswala ya kujadili hapa ni la viongozi wao (mawaziri), vitendea kazi, safety na maslahi yao. Ila binafsi swala la maslahi naona wana push too far ukilinganisha na uwezo wa serikali yetu!! MP alitakiwa awaeleze ukweli halisi ila tatizo naona ni yale malupulupu ya wabunge yalishaiweka serikali njia panda!! Kitu wanachoweza kufanya ni kutoa posho tu kwa madaktari........ Maana wakipandisha mishahara sekta nyingine za serikali nazo zitadai chao!!
Na nani achukuliwe hatua kutokana na vifo vya wagonjwa vinavyotokea kila siku kutokana na uzembe wa watendaji serikalini kwa matumizi mabaya ya fedha (na hivyo kukosa madawa na vifaa muhimu vya kufanyia kazi), kununua madawa yaliyoisha muda wake na mis-allocation of resources?