Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

Kusua sua kwa serikali yenu tukufu ndo kumesababisha yote haya

Wewe unasema ilinyoosha mkono upi?wakati katibumkuu na naibu wake walifukuzwa na pm pinda.lakin cha kushangaza bado wako officen na katika makukubaliano yao kwanza ilikua kuwatimua hawa watu 4 kwanza kabla ya mambo mengine.na pinda aliwatimua hawa pia akadai waziri na naibu wake wako nje ya uwezo wake mwenye jukumu la kuwafukuza ni baba mwanaasha ambaye alikua nje yanch aliporud nchn alitakiwa kuwatimua lakn hajafanya chochote.huon madactar hawa wanasanifiwa na serikali?
 
Si angewaambia kwamba hataki hizo net ili wapewe watu wengine...
Kila mtu alipewa za kumtosha kabisa...afu kwa nini awape watu wengine kitu asichotaka kutumia yeye? Zile net unadhani ni salama kwa afya?
 
Nipo muhimbili,mama mkwe wangu amefariki,aliwekewa mashine ya oxgen usiku baada ya hapo dr hakuja tena,na mama ndo ametutangulia.migomo ina madhara,amefarik saa sita na nusu mchana huu.

poleni sana deo mungu awape faraja na nguvu lakini damu ya mama mkwe wako i juu ya jk, pinda na madaktari kwa upande mwingine.
 
Duh, haya wacha twone magamba wanavyozid kuwapotza watz kwa mi2mbo yao!Manyau kwel hawa gvt ya vasco da gama
 
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.

For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.

Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.
 
Bila kujali maslahi ya upande wowote katika mgogoro huu, naomba mtu anaeunga mkono mgomo huu anijibu swali hili;- wagonjwa, ambao ni haki yao kupata matibabu, na ambao pia sio chanzo cha mgogoro, wana maslahi gani katika mambo yanayoendelea sasa hivi? Istoshe, katika kugoma kwao, ni makosa kusema madaktari wanawakomoa wagonjwa?

Utawezaje kumlalamikia dereva akuwahishe mahali wakati gari halina mafuta. Badala ya kumlaumu aliyemkosesha mafuta unamlaumu anayeendesha sababu tu ndiye unayemuona kikwazo. Chamsingi ni kutatua kiini cha matatizo na si kuangalia wapi pa kutupa lawama. Serikali imajeribu kutufanyia majaribio, sasa wamepata majibu. Tuna sera nzuri sana za mambo ya afya, ila usimamipo hovyo kabisa. Ukiuliza mapungufu yasiyo yalazima yanatokeaje, utaambiwa TUPO KWENYE MCHAKATO. Haya endeleeni na MICHAKATO hiyooo weeeeee.......
 
Mshua hasikii la muazini wala la mnadi swala,anaamua atakalo as long wanaokufa sio wapwa wala shemeji zake yeye kinamuuma nini? hahitaji kura zenu tena,wala hahitaji chochote kutoka kwenu kwa ufupi hana cha kupoteza........hii ndio ccm ya kina Mkama, Nape na Chiligati.*
 
nipo pamoja na madaktari 100%. Kwanini keki ya taifa letu wanufaike watu wachache?

Ama Kweli nimekubali kwamba mafahari wawili wanapogombana zinazoumia ni nyika! Wote sisi tunaoshabikia mnyukano huu Mungu katunusuru tuko wazima. Can you imagine Umegongwa na bodaboda mfupa uko nje unapelekwa Muhimbili unayakuta haya naamini lugha yako itakuwa tofauti! Chonde chonde Tuhurumiane!
 
Hivi Rais anapata faida gani kuendelea kufanya kazi na watu wanaoleta matatizo makubwa kiasi hiki kwenye jamii. Na huyo waziri na naibu wake wanajisikiaje wanapokuwa wanatajwa kila kona ya nchi hii kwa vifo vya watu wasio na hatia, kwa nini wasijiuzulu ili wapishe utekelezaji wa mambo mengine ya kijamii, ama wanahisi kuwa wao ni muhimu sana kwa mustakabali mzima wa wizara na sekta ya afya kwa ujumla.


Kikwete waondoe huyo Mponda na Nkya, usiogope kuambiwa umesalimu amri, ama washauri waende wenyewe ukumbi wa habari maelezo watangaze wenyewe kuwa wameachia ngazi kwa faida ya Taifa
 
Nipo muhimbili,mama mkwe wangu amefariki,aliwekewa mashine ya oxgen usiku baada ya hapo dr hakuja tena,na mama ndo ametutangulia.migomo ina madhara,amefarik saa sita na nusu mchana huu.
Pole sana ndugu!

RIP ma mkwe!
 
Hawa madakatari wanatakiwa wauliwe, ni magaidi wanaocheza na roho na maumivu ya watu.

Hauwezi kabisa kila siku ukaja na malalamiko mapya ukae uchekewe tu. Nawaomba sana serikali isiwasikilize kabisa na iwape 2 hours wawepo kwenye kazi zao nje ya hapo, wachukuliwe hatua kali sana ikiwepo na kushtakiwa kwa kila kifo kitachotokea wakati wa mgomo, wakasote jela wakijibu kesi za mauaji.

masaburi at work.
 
Anguko la serikali sasa ni dhahiri, "that time will tell" is NOW
 
nikweli st francis wamegoma hivi navozungumza wako pale vunja bei bar wanatiririsha valuer tu
 
Kwa jinsi Pinda alivyozungumza kwa busara jana hakika nilitegemea madaktari wangeomba fursa ingine ya kukutana naye tena kuangalia uwezekano wa kutatua vikwazo vilivyojitokeza kuliko kukimbilia kugoma.

Busara ni kumtoa waziri mmoja ili aponeshe mamia ya watu then tuone hawamadaktari kama watagoma. Jambo la msingi ni equality katika kutumia rasilimali za nchi tu ndio sababu tosha. Wanasema inflation ipo juu sana serikali inatakiwa idhibiti sio kuongeza mishahara????????.
 
TANESCO nao wakituhujumu kwenye umme eti tu kudai haki zao...giza nene

TRA wagome kukusanya kodi eti wanadai haki zao.

TBS wagome kuthibitisha ubora wa vyakula eti wanadai haki zao.

Kipepe-100%
 
madoctor waheshimiwe jamani. wale sio walimu ndo maana wanafanya kazi usiku na mchana. hata huyo pinda na mama tunu wote wanamtegemea doctor awapime macho.
 
Wazazi,Raisi ndo kizizi, ila haambiwi tu mi nakufa naye,mtafukuza mawaziri sana kimeo kiko Ikulu?
 
Kidatu ongea na watu vizuri wakueleweshe nini tatizo, hujui majibu waliyotoa hawa mawaziri kwa madaktari mpaka wakafikia hatua hiyo, hakuna mkono wa siasa katika hili zaidi ya mkono wa shetani ccm......hii nchi inahitaji maombi tena si ya kitoto yabidi kukesha na kuomba huku tukiwa tumefunga vinginevyo mpaka 2015 itakuwa kazi.*
 
Back
Top Bottom