Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

Si ajabu gazeti la Uhuru la kesho likasema hakukuwa na mgomo.
 
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.

For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.

Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.

Zipo serikali nyingi katika historia ya dunia hii zilizowahi kudhani kuwa mabavu ni mwalobaini wa kutawala, lakini hazikufanikiwa!!!!
 
Bila kujali maslahi ya upande wowote katika mgogoro huu, naomba mtu anaeunga mkono mgomo huu anijibu swali hili;- wagonjwa, ambao ni haki yao kupata matibabu, na ambao pia sio chanzo cha mgogoro, wana maslahi gani katika mambo yanayoendelea sasa hivi? Istoshe, katika kugoma kwao, ni makosa kusema madaktari wanawakomoa wagonjwa?

labda tuanzie kwenye maswali haya. Hujui kwamba kuna wagonjwa wengi wanakufa kila siku kutokana na ukosefu wa vifaa na dawa? hujawahi ona akina mama wajawazito wakilala wawiliwawili kwenye kitanda kimoja au chini sakafuni kabisa? mambo yako mengi....! in the long run ni wagonjwa wataonufaika zaidi.
 
TANESCO nao wakituhujumu kwenye umme eti tu kudai haki zao...giza nene

TRA wagome kukusanya kodi eti wanadai haki zao.

TBS wagome kuthibitisha ubora wa vyakula eti wanadai haki zao.
Mbona hivyo vyote vilishabinafsishwa na serikali imejitoa kuvisimamia 100%. Sasa wanajitahidi na kubinafsisha huduma ya Afya maana wao tayari wanapata huduma India.
 
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.

For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.

Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.

Sauti yenye mamlaka! "VIWANJA VINA MACHO, VICHAKA VINA MASIKIO"!
 
nipo pamoja na madaktari 100%. Kwanini keki ya taifa letu wanufaike watu wachache?
Kumbd keki tamu!

Nilijua tu Vimon atakuja na update iliyosimama kuliko zile ambazo zinatuchanganya. Kuna mama yangu yuko bugando ngoja nipige simu nione kama kuna huduma ama la.

Kuna dalili za mauaji ya Kimbari hapa.
Madaktari tuoneeni huruma sisi wanyonge.
 
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.

For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.

Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.


Tunapenda kushabikia serikali kutumia BUNDUKI kuulia MENDE. Kwahiyo hili linaweza fanyika haraka kutafutiwa ufumbuzi kuliko tatizo la msingi. Nasisi wananchi hatutakubali kuona kodi zetu zinatumika kiholela namna hiyo. Kama wameshindwa kututumikia kutokana na dhamana tuliyowapa (waliyochakachua), basi waachie ngazi. Haya ndiyo baadhi ya matatizo makubwa yaliyopo kwenye KATIBA yetu ya sasa, kilakitu RAIS. Sasa kama Rais asipokuwa na hekima katika maamuzi, haya ndiyo matunda yake.
 
Hawa madakatari wanatakiwa wauliwe, ni magaidi wanaocheza na roho na maumivu ya watu.

Hauwezi kabisa kila siku ukaja na malalamiko mapya ukae uchekewe tu. Nawaomba sana serikali isiwasikilize kabisa na iwape 2 hours wawepo kwenye kazi zao nje ya hapo, wachukuliwe hatua kali sana ikiwepo na kushtakiwa kwa kila kifo kitachotokea wakati wa mgomo, wakasote jela wakijibu kesi za mauaji.
hivi wewe una akili timamu ama ndio makasuku mliogundua kutumia internet juzi juzi? kabla hujacomment kwenye mitandao ya kiutu uzima uwe unafanya research ya kuendeleza upeo wa akili yako!
hivi unajua katiba imempa nani dhamana ya afya ya mtanzania? kasome katiba ndio uje useme nani anatakiwa kuwajibishwa na vifo vya mtanzania anayetibiwa humu humu (wakiwemo na madaktari wetu) tanzania vitavyotokana na mgomo huu!!! Ebooooo!!!
 
Nipo muhimbili,mama mkwe wangu amefariki,aliwekewa mashine ya oxgen usiku baada ya hapo dr hakuja tena,na mama ndo ametutangulia.migomo ina madhara,amefarik saa sita na nusu mchana huu.
Poleni sana. Nasikitika wenye dhamana na nafasi za maamuzi wamekosa busara ambayo ingetatua mgogoro uliopo..
 
Dr Wangu wa Muhimbili anasima

"" mgomo hakuna watu wanaendelea na kazi kama kawaida vikao bado vinaendelea"" mwisho wa kunukuu

Sasa tumuamini Doctor wa wapi??? maaana mgomo hakuna:juggle:
shushushu mkubwa weee!! na ukome! nimetoka hospitali muhimbili muda sio mrefu, mgomo upo! nyangau weee!
 
...Hawa madakatari wanatakiwa wauliwe, ni magaidi wanaocheza na roho na maumivu ya watu...

We M^^^buri hebu jaribu kuvaa viatu vya madaktari uone starehe yake.
Wanaamshwa usiku wa manane, wanaacha usingizi wao wa mapumziko ili kututibu halafu hawapewi motisha ya kueleweka. Mishahara inachelewa. Vitendeakazi havitoshi n.k., then watu kama wewe mnaotibiwa Apollo wanawabeza, hii si haki. Mbona watendaji wa wizara nyingine hawagomi? Kwa nini? Ushasikia ikulu wamegoma? Na wizara ya fedha je?
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

Wapuuzi ni mawaziri na mkuu wa kaya kilicho baki inatakiwa tugome kulipa kodi mawaziri na jk kodi zetu zinawapa vibuli kwenda kupata matibabu india nk kwa kodi zetu sisi tunapukutika hawajuwi sisi tumewapa hizo kazi hatuwataki kwautendaji mbovu
 
Na mbaya zaidi Waziri wa afya alishapeleka barua ya ku resign tatizo ni JK kampa kiburi

Tatizo siyo Mponda wala Lucy Nkya, bali tatizo lipo Utumishi na Hazina.
Tulianza na Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa wizara tukadhani tumetatua
tatizo kumbe wapi? Sasa tutawafukuza Mponda na Lucy Nkya, kisha tutadhani
tatizo ni Pinda, tutamuondoa na yeye lakini bado tatizo litakuwa palepale na
hatutakuwa tumetatua tatizo kwa kuwa serikali haina hata senti Hazina.
Mishahara ya kuwalipa wafanyakazi wake inakopa kwenye taasisi binafsi,
balozi zetu hazina pesa, wanaishi kwa kuganga njaa kwa kuwa tulichopitisha
kwenye bajeti yetu kilikuwa ni kuchumia tumbo, tuna madini lukuki lakini
yote tunayagawa kwa mikataba isiyo na tija, mibovu kuliko ya enzi za kina
Karl peters, tunasamehe kodi wakati tunategemea misaada ya wahisani!

Waziri Mponda au Lucy Nkya watafanya nini endapo hazina imekataa
kutoa fedha? Watafanya nini wakati Hawa Ghasia (Utumishi) ni tatizo
katika utumishi wa umma? Tafakari, chukua hatua...
ndiye anayesababisha yote haya?
 
Ili mbegu ichipue mbegu nyingine, lazima ife. Kwa hiyo ni lazima watu wajitoe kwa ajili ya maisha ya wengine.
 
Sote tunajua madhara ya mgomo tarajiwa. Serikali yaweza kuepusha madhara kwa jamii pana zaidi kwa kuwaondoa/hamisha hao watu wawili. Hakuna haja ya serikali kukomaa inatakiwa i compromise kwenye hii issue
you are very right Mkuu, Nionavyo the problem hapa ni siasa na taaluma. siasa haina nafasi kwenye taaluma wakati huo huo taaluma in nafasi kwenye siasa '' Sirikali haitaki kukubali hili ''
 
Asante sana madaktari wa Mnazi Mmoja Zanzibar Kwa kuungana na wenzenu wa bara katika mapambano ya ukombozi wa sekta ya afya
 
Back
Top Bottom