Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

Wewe unadhani kwamba unachokifanya sasa hivi ni sahihi kwa sababu ukiwa kama daktari, katika situation iliyopo sasahivi, ni kweli kwamba "umeshika mpini", on the other side, wagonjwa ndio "wameshika makali". Suppose ingekuwa wewe, pamoja na udaktari wako, uko wodini umelazwa, halafu wenzako wanakuja na msimamo kama huu mliokuwa nao sasa hivi, ungekuja hapa jf na statement gani?

Wewe akili yako vipi?? Hivi unafikiri hao madaktari wote ni wazima na hakuna wanaoumwa au waliolazwa mahospitalini?? Hivi unafikiri hao madaktari hawana baba, mama, watoto na ndugu wanaoumwa na wamelazwa?? Madaktari ni watu tu kama wewe na mimi.

Inaelekea wewe unafikiri madaktari siyo wananchi na pia hawana haki ya kudai maslahi yao kama raia wengine!! Kwa ujumla analysis au mawazo yako hayana mshiko kabisa!! Pole Mkuu!!!
 
Bila kujali maslahi ya upande wowote katika mgogoro huu, naomba mtu anaeunga mkono mgomo huu anijibu swali hili;- wagonjwa, ambao ni haki yao kupata matibabu, na ambao pia sio chanzo cha mgogoro, wana maslahi gani katika mambo yanayoendelea sasa hivi? Istoshe, katika kugoma kwao, ni makosa kusema madaktari wanawakomoa wagonjwa?
serikali inawakomoa wagonjwa
 
@Mzito Kabwela, hayo mavifaa ya kivita yaliyonunuliwa kifisadifisadi wala hayana matumizi yoyote...yanasubiri tu siku yataamua kujilipua yenyewe kama vile kule mbagala na gongolamboto...! I wish jamaa wangeinvest kwenye mahospitali kama wanavyofanya kwenye jeshi...!
 
Wameshamaliza kikao chao pale Russian cultural centre....na wamekubaliana kuanza mgomo rasmi wa nchi nzima leo.

Kunavishobikela walikuwa wanashupaa hapa kwamba huu mgomo haupo. Wametoa mapovu weee, sasa utawasikia tupo tayari kukaa meza moja kwa mazungumzo. Sijui kwanini hii serikali haitaki kujifunza ukweli, imezoea ahadi za uongo na kutishia. Serikali ipo pale kutumikia wananchi wake na wala si kuonyesha kuwa inaubavu wa kuamua chochote hata kama hakina maslahi kwa Taifa. Wamejaribu kupiga propaganda ili watu wawachukie madaktari, naona wamesahau kuwa enzi za propaganda zimeshapitwa. Eti wanaogopa wakikubali pendekezo la awali la madaktari na sekta nyingine zitaamua kufanya hivyo. Inamaana inajua sekta nyingi imeweka viongozi dhaifu na wafujaji hivyo inajitahidi kuwalinda. Sidhani kama ingekuwa tishio kama kila wizara ingekuwa inawajibika ipasavyo. Nafikiri huu ndiyo utakuwa mwisho wa uongozi wa kishkaji.
 
Hawa madakatari wanatakiwa wauliwe, ni magaidi wanaocheza na roho na maumivu ya watu.

Hauwezi kabisa kila siku ukaja na malalamiko mapya ukae uchekewe tu. Nawaomba sana serikali isiwasikilize kabisa na iwape 2 hours wawepo kwenye kazi zao nje ya hapo, wachukuliwe hatua kali sana ikiwepo na kushtakiwa kwa kila kifo kitachotokea wakati wa mgomo, wakasote jela wakijibu kesi za mauaji.
Kama ni kweli Sasa ni wakati Muafaka kwa umma kuwafungulia kesi ya mauaji ya kukusudia Madaktari wote kwa kusababisha vifo vya watu wasio na hatia kwa kisingizio cha 'kudai' maslahi bora! ukufika wakati huo wakereketwa wengine, ambao tofauti na akina Kijo bisimba, washauriwe kutembea na kifimbo cheza kuwasaka wauaji hao na kuwaadabisha...hiyo ndiyo nguvu ya Umma!.
 
@Mzito Kabwela, hayo mavifaa ya kivita yaliyonunuliwa kifisadifisadi wala hayana matumizi yoyote...yanasubiri tu siku yataamua kujilipua yenyewe kama vile kule mbagala na gongolamboto...! I wish jamaa wangeinvest kwenye mahospitali kama wanavyofanya kwenye jeshi...!
 
Nafikiri hii ni nafasi pekee ambayo jk amepata kuweza kukumbukwa na labda kufuta mauzauza ya nyuma lakini sidhani kama ataweza kuitumia na kuna msemo usemao "opportunity never come twice"!
 
Nasubiria kuona Uimara wa serikali yetu
Naamini itafanya maamuzi yatakayolinda maslahi ya wananchi wake walio wengi bila kujali umaskini wa uchumi tulionao.
Hii ni sawa kabisa na vita so whether ni kuwafukuza mawaziri au madaktari mi sintojali kama yote hayo yatakua na manufaa kwa wananchi walio wengi.

Mwisho naamini serikali imara haiwezi kuyumbishwa kwa migomo ya makundi namna hii nayo ikaendelea kukubali kufyata mkia........je na keshokutwa jeshi majeshi na sector nyingine zikigoma tutakwenda wapi kama serikali itaruhusu migomo iwe ndo majibu ya matatizo??
 
Mob psychology ime wa-affect madaktari wetu. Natoa ushauri kila mmoja atafakari ni nini anachogomea hasa kama yeye binafsi bila kutegemea vikao vyao wanavyokaa kupeana molali! Kama ni maslahi yake hayajatekelezwa au ni kuto kujiuzuru kwa mawaziri au vyote viwili. Na ukiangalia dai la kuto kujiuzuri/kutowajibishwa mawaziri imemeza madai yao yote ikiwemo ya masilahi yao. Sasa wawe makini katika madai yao wasije wakawa wanatumiwa na kundi fulani bila kujijua? na hii ndio madhara ya mob psychology. Nawashauri waonane na wataalam wapate ushauri?

Madaktari wana akili timamu na wengi wao ni first class material ya high school. Sasa vichwa vyote hivyo vikikutana sidhani kama kweli watashindwa kuanalyse mambo yao ya msingi badala tu ya kuwa pushed kama unavyosema "mob psychology". Kitu cha kujadili hapa nafikiri ni kuangalia kama kweli madai yao ni ya msingi.

Nafiki maswala ya kujadili hapa ni la viongozi wao (mawaziri), vitendea kazi, safety na maslahi yao. Ila binafsi swala la maslahi naona wana push too far ukilinganisha na uwezo wa serikali yetu!! MP alitakiwa awaeleze ukweli halisi ila tatizo naona ni yale malupulupu ya wabunge yalishaiweka serikali njia panda!! Kitu wanachoweza kufanya ni kutoa posho tu kwa madaktari........ Maana wakipandisha mishahara sekta nyingine za serikali nazo zitadai chao!!
 
Binafsi siwalaumu Madaktari kwani walitoa muda wa kutosha kwa Serikali sasa hawajatekelezewa wafanye nini? Najua outcome yake itakuwa sio nzuri lkn siku zote mafanikio hupatikana baada ya wachache kuumia.Please Serikali madhara yatakayopatikana ni makubwa kuliko ata buwabwaga Mponda na Nkya
 
Madaktari Bingwa nao hivi punde wameongeza nguvu na kuwaunga madaktari wengine kwa mgomo usio na kikomo mpaka matakwa yao yatekelezwe. Kikao walichokuwemo kwenye ukumbi wa russian culture kimeisha Punde
Mola tunusuru!!
 
Mponda na Lucy wakiondoka si bado anaweza kuwatafutia ubalozi? waondoke, lengo la madaktari ambalo ni muhimu ni kukomesha ubabe na ulevi wa madaraka, wengine wamepata uhuru kwa kumwaga damu tena nyingi tu. mamlaka ya viongozi yanatoka kwa wananchi, kutii sharti la madaktari ni kutii amri ya mwajiri wako pale unapokosea. namuonea huruma mponda hata hajafaidi bt i kno he wil hv 2 go.
 
Kama ni kweli Sasa ni wakati Muafaka kwa umma kuwafungulia kesi ya mauaji ya kukusudia Madaktari wote kwa kusababisha vifo vya watu wasio na hatia kwa kisingizio cha 'kudai' maslahi bora! ukufika wakati huo wakereketwa wengine, ambao tofauti na akina Kijo bisimba, washauriwe kutembea na kifimbo cheza kuwasaka wauaji hao na kuwaadabisha...hiyo ndiyo nguvu ya Umma!.

Sisi hatupigii kura madaktari, tunapigia kura serikali...na hao serikali ndo wakupeleka mahakamani
 
Wana JF hivi hatuelewi maana ya Updates. Wekeni updates badala ya kutoa maoni.
Habari za saa ITV zinasema mgomo umeshika kasi, pia wanafunzi wa Muhimbili wameandamana hadi Wizara ya Afya kudai fedha za Chakula.
 
Hapa kweli tumuombe Mungu atupe rehema zake. Ila naamini kila hatua ina maana yake.
 
Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.

My take; hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?
Nawasilisha wadau

Wewe na wenzako mnaoshahabikia mgomo wa madaktari ni WAJINGA. Ukiwa na akili timamu huwezi kushahabikia mgomo wa madakari kama ni mtu makini. Fikiria mama, baba au mwanao ni mgonjwa mahututi halafu madaktari wanagoma kumtibia kisa Waziri na Naibu wake wajiuzulu, ungechekelea kama unavyofanya? Kama suala lao la posho limepatiwa majawabu waendelee kuwahudumia Watanzania. Kwa hili siungi mkono ujinga wa madaktari.
 
Kwa hiyo unataka kusema nini? Wanadai maslahi yao na wewe unaleta siasa za viapo uchwara!!

Hakuna serikali yoyote duniani ambayo inaweza kutimizia wananchi wake kila kitu duniani sembuse sisi na umaskini wetu?
Jamani tunaomba madaktari muwe na uzalendo kidogo kwa maana huduma haziwezi kuboreka just kwa siku moja....kumbukeni kwamba pia wafanyakazi wenzenu tunahitaji mishahara kama nyie....sasa bajeti yote kwa sasa ikielekezwa kwenu sector nyingine zitaishije?
 
Back
Top Bottom