chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,553
2,073
Habarini ndugu,

Hivi sasa bei za bidhaa kuanzia bidhaa za majumbani kama sabuni, mafuta na vinginevyo mpaka mbolea ,vifaa vya ujenzi n.k vimepanda bei.

Bei zimekua kubwa sana kiasi mtu wa kawaida kuzimudu inakua shida.

Vifaa vya ujenzi ambavyo vingi tunatengeneza hapa hapa nchini navyo vimepanda bei.hii ni hujuma kwa taifa ,kwa sababu kuna wafanyabiashara wanapandisha bei vitu bila utaratibu maalum na kwa kujitakia tu.

Naomba viongozi mseme neno,hili swala litatuliwe mapema.msisubiri maandamano km yanayotokea nchi za majirani wenzetu wa sudan na kwingineko.

Kinga bora kuliko tiba.nawasilisha
 
Mfumuko wa bei unawahusu CHADEMA na gaidi Mbowe sisi kijani tunatembea kifua mbele maana haituhusu na mwaka 2025 tuna kwenda na Samia" alisikika mlevi mmoja akisema

Maendeleo hayana chama ndugu zangu
 
Wabunge wapo bungeni,

Hakuna anayegusia mfumuko wa bei seriously. Jana nimeshangaa sana kuna ndg yangu ametoka Masasi kwenda Dar nauli 28000/= kutoka 18000-22000 /= hii ni hatari sana.

Wabunge wetu wekeni thamani ya ubunge wenu.

Hakuna amani ya moyo katika maisha ya sasa.
 
Usilete umbea! Katika miezi michache hii, serikali imefanya mambo makubwa kuliko miaka mitano ya serikali iliyopita. Mishahara imepanda, na watu wamepanda madaraja, sasa wewe unalilia nini?
Kumbe ww ndio umepewa kitengo cha kumsifu hangaya? Sawa unafurahia kupanda mishahara harafu pesa yako hiyo hiyo ukienda sokoni haitoshi hata kujaza kapu ssa inafaida gani au nsio unasubiri miaka 60 ule miaez 5 pesa zako ziiishe halafu ujawe na stress UFE?
 
WAbunge wapo bungeni
Hakuna anayegusia mfumuko wa bei seriously.
Jana nimeshangaa sana kuna ndg yangu ametoka Masasi kwenda Dar nauli 28000/= kutoka 18000-22000 /= hii ni hatari sana.


Wabunge wetu wekeni thamani ya ubunge wenu.

Hakuna amani ya moyo katika maisha ya sasa.
Haya ndiyo madhara ya kuwa na bunge la chama kimoja.

Kila mtu anaogopa kuikosoa serikali maana anahofia kuhatarisha kitumbua chake.
 
Usilete umbea! Katika miezi michache hii, serikali imefanya mambo makubwa kuliko miaka mitano ya serikali iliyopita. Mishahara imepanda, na watu wamepanda madaraja, sasa wewe unalilia nini?
Ebu wacha kuchaa chako,
Hivi hujui kuwa sasa hivi mfumuko wa bei upo juu sana?

Kazi ya serikali ni kuwajibika kwa wananchi bila kujali kama imefanya nini jana.
 
Watajadili nini wakati wenzako wapo hadhi za juu! Yeye yupo uchumi wa Kati wewe mwananchi wa kawaida upo uchumi wa chini!!
Hakuna cha kujadili hapo tulieni soko liamue.
 
Back
Top Bottom