USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,666
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema hali ya mfumuko wa bei wa Tanzania ni nafuu ukilinganisha na nchi nyingine Duniani ambazo bei za bidhaa mbalimbali hupanda kila baada ya masaa machache.
Akizungumza wakati wa Vikao vya Bunge Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Watanzania wawe na imani na njia zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kukabiliana na Mfumuko wa bei kwa kuongeza uzalishaji kwenye Sekta mbalimbali.
"Mfumuko wa Bei ni tofauti na bei mfumuko wa bei ni kiwango cha kubadilika kwa bei, mfumuko wa bei Tanzania si kama nchi nyingine ambazo kila saa unabadilika, na huo ndiyo mfumuko wa bei ambao ni tatizo kubwa kwenye uchumi" Amesema Waziri Mwigulu Nchemba
Aidha Waziri Mwiguli Lameck Nchemba ameongeza kuwa kwenye kukabiliana na mfumuko wa bei Rais Samia ameagiza kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali ikiwemo uongezaji wa uzalishaji kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo Kilimo kwa kutoa ruzuku ya mbolea
"Kama tatizo ni kupanda kwa bei zinatatuliwa kwa hatua ambazo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amezichukua hasa kwa kuongeza uzalishaji" Ameongeza Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba