Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Inanikumbusha sakata la Mengi na waziri Masilingi miaka ya awamu ya III kuhusu uuzwaji wa Kilimanjaro Hotel, sijui iliishaje.

Nadhani JK ana kazi kubwa sana kwa baraza hili la Mawaziri, wengi naamini hawana uwezo na busara katika maamuzi yao naona kama wanakurupukaga tu. Namhurumia JK, Mungu amsaidie.

Mungu humsaidia anaejisaidia muungwana hajaonesha kujisaidia baada ya kulundika maswahiba kwenye nyazifa nyeti bila kujali ufanisi! ikumbukwe kwenye hotuba baada ya kuunyakua alisema hatawasahau wote waliomfikisha hapo nikajua tumekwisha! maana muda wa malipo ya fadhila kwa gharama za watanzania ulikua umewadia! kazi kwelikweli!
 
Lawrence Kego Masha



Partner
Admitted to the Bar, 1996.

Practice Areas:

Natural Resource Law; Banking & Finance; Privatization; Corporate Restructuring; Securities; Conveyancing.

Brief biography:

Born in Sengerema , Tanzania , March 11, 1970.

Education:

University of Dar es Salaam (LL.B., Hons., 1991);
Georgetown University (LL.M., 1993).


Work experience:

State Attorney, 1991;
Company Secretary and Managing Director, Tanzania Oxygen Limited, 1996-1997;
Council Member, Dar Es Salaam Stock Exchange.

Member:

Tanganyika Law Society
East African Law Society

Languages:

English and Swahili.

Email: masha@immma.co.tz

(NB: Mr. Masha is currently on sabbatical leave following his appointment as Deputy Minister in Tanzania’s Fourth Phase Government. Mr. Masha, who was initially appointed Deputy Minister of Energy and Minerals, is currently the Deputy Minister of Home Affairs in the Government of the United Republic of Tanzania

Masha kazaliwa 1970 na kamaliza LLB (UD) 1991...ina maana aliingia UD akiwa 17 yrs old?

Mwenzangu,

hilo la Masha kuingia chuo kimaajabu liliongelewa sana hapa wakati fulani. Kumbuka pia wakati huo ilikuwa lazima mtu upite JKT kabla ya kwenda chuoni.

Skandali hiyo iko servers za JF.... ni suala la muda.

Mzee Mengi sikubaliani naye kwenye mambo mengi lakini kwenye hili, nitakuwa naye mpaka Masha akome kuwalinda mafisadi ambao wanatakiwa kuwa keko au segerea sasa hivi
 
Kichuguu,

Ni raha na amani moyoni kuwa na walimu kama wewe hapa jamvini.

Masha akisoma hii post yako na kisha akavuta pummmmm ....vuta pumzi, atajua ukubwa na madhara ya alichokifanya.

Asante sana.

wakati mwingine hwua naanza kuhisi kama wewe ni mchaga bai haujadiliki.Sioni mantiki ya watu kumtete a Mtu kama Mengi.Mtu ambaye anadaiwa na wafanyaki wake pesa ya fidia.

Iko wapi maana ya kutoa million 100 wakati unadaiwa?
 
- Kama nilivyosema jana, kwenye hili Mengi ameenda nje ya mstari hawezi kuanzisha serikali yake ndani ya serikali ya jamhuri, ameanzisha mwenyewe wakati kuna njia nchungu nzima angeweza kuzitumia kutatuta tatizo lake, mara mashehe mara waziri kesho itakua rais, it has to be stopped tena now.

- Taifa tunaongozwa na sheria, sio uhuni uhuni wa kukusanya habari za walevi mitaani na kuzigeuza dhana za kutishia walevi, mimi sinyiwi pombe na nina marafiki 75% wanaolewa kila siku, sasa nikijali maneno yao ya ulevi sitakua na rafiki hata mmoja. Kwenye kesi yake against Manji nilikuwa mmoja wa waliomtetea sana Mengi kwa wahusika wa uamuaji ile kesi kuwa anaonewa lakini not this time, kwa sababu this one yuko nje ya mstari tena out na ninaunga mkono kwa 100% any response kwa wale wote aliohusika na kuwarecord au kuwapiga video na picha wakiwa kwenye ulevi, kama ndio sababu ya claims zake against viongozi wa serikali.

- Priviledge ya kumiliki media au kuwa na uwezo wa kuandika kwenye vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti na mitandao haiwezi kuwa sababu ya wale wenye hizo access kuchafua majina ya wengine kuwa ni mafisadi na the rest of the story bila sababu wala ushahidi, hapa ndipo tunapomheshimu sana Dr. Slaaa, kwa kuweka mambo yote ya ufisadi kwa kalamu na ushahidi usiopingika.

- Masha hana sababu ya kujiuzulu kwa kusimamia kiapo chake kwa jamhuri, yaani kulilinda taifa kwa njia zote zilizopo chini ya uwezo wake kisheria, ni wajibu wa waziri wa ndani kuhakikisha kua wananchi hawabughudhiwi na viongozi au wananchi wengine, na wale wanaobughudhiwa ni wajibu wao kufikisha matatizo yao kwenye vyombo vya dola kwa ufumbuzi wa kisheria iwapo wanao ushahidi wa kisheria, kama sheria yetu inavyosema. Sasa anapotokea mwananchi yoyote mwenye kuamua kwenda kinyume na sheria zetu, regardless ya who he is serikali ni lazima isiamie sheria tena kwa nguvu zote ilizonazo.

- Ninarudia tena kwamba ni wajibu wa waziri wa ndani kusimamia mambo ya ndani bila ya kujali ni waziri gani anayetajwa au asiyetajwa, Mengi ni lazima afikishwe kwenye sheria na atoe ushahidi wake uliopatikana kisheria ili kuiridhisha sheria ya jamhuri, ambayo waziri wa sasa wa ndani amekula kiapo kuilinda kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote. Tunaishi kwa kuongozwa na sheria sio uhuni uhuni wa kukurupuka kwenye public na tuhuma nzito kwa viongozi wetu wa juu kwenye media, ni kujaribu kuwatisha ili wasifanye kazi zao walizopewa na na sisi wananchi kwa mujibu wa sheria. Hata US sheria iko wazi kuwa ukilia moto kwenye sehemu kama ya cinema wakati moto hakuna, unachukuliwa hatua za kisheria tena kali sana, sasa hapa ni wajibu wa serikali yetu ya jamhuri ikiongozwa na waziri wa ndani ambaye ndiye kisheria mhusika mkuu kuhakikisha kuwa Mengi anapewa haki yake so is waziri aliyetajwa pia akipewa haki yake na pia kutulinda sisi wananchi wengine wa kawaida na viongozi in the future na this kind of Mengi's accusations, hakuna anayekataa haki za Mengi kulindwa na sheria, lakini ni lazima huheshimu sheria za jamhuri na utaratibu wetu wa kisheria.

- Ninamuunga mkono kwa 100% kitendo cha waziri wa ndani kumpa Mengi muda wa kutoa ushahidi wake kwa serikali, na pia kumpa waziri anayehusishwa nafasi ya kusema pia mbele ya sheria, na sheria iamue nani mwenye makosa kisheria na nani hana, lakini the important ishu ni kuhakikisha kua next time Mengi anakwenda kwenye vyombo vya sheria bdala ya media, hawezi kusema kua haviamini kwani vimewahi kumpa nafasi ya kujitetea na akashinda kesi, tena against waziri wa jamhuri, ni lazima Mengi ajifunze kupeleka malalamiko yake kwenye sheria, kama sheria inavyotaka.

- Wote sisi ni wananchi wa Tanzania, na hili taifa ni letu sasa tusitishane na hizi tabia mpya za kujifanya wanamapinduzi, kwa kutaka kulazimisha kwa nguvu hoja za kuwaita walioko kwenye power tuliowachagua kisheria kuwa ni mafisadi just because hatuwataki au tuna chuki zetu za binafsi, dawa ni kudai tu kwa nguvu kuwa ni mafisadi kwa sababu ni wimbo unaokubalika kirahisi na wananchi bila hata ushahidi ulio wazi, hili sio taifa la walevi au wajinga wajinga, tunazo sheria na ni lazima zitekelezwe kwa nguvu zote.

Hatuwapendi mafisadi, lakini ni lazima kuwa na ukweli juu ya uifisadi wao, na ni wajibu wa waziri wa jamhuri kulinda sheria, bila kujali kama ni Mengi au anybody.

Mungu Aibariki Tanzania.

Mkuu toka hii habari imezuka umeng'ang'ania habari imetoka ulevini! vp hapa? ulikuwepo kwenye huo ulevi? au una maana suala hili zima limekaa kilevi?
 
Mimi naona ni upuuzi, utoto, upumbavu, na ukuku (uoga) tu unaoendelea hapa. Huyo Mengi kama ana uhakika na ushahidi alionao, kama ana chembe ya ujasiri, kama anaongozwa na kanuni, basi amtaje kwa jina tu huyo waziri. The burden of proof is on him. Asipofanya hivyo, sakata zima litakuwa reduced to uzushi. Unatoa tuhumu halafu huwezi kuthibitisha madai yako...what the hell....?!!?!?!?!? Aseme tu huyo waziri ni nani. Kwani kuna ugumu gani?
 
Ila ukiangalia hii kitu katika angle nyingine Mengi ametoa hii taarifa kwa kujilinda zaidi hasa baada ya kusema amemsamehe huyo waziri....sasa akigoma kumtaja kwa chini ya mwamvuli wa "nimeshamsaheme sitaki tena kuzungumzia hili swala" tutamlazimisha?

Akigoma kumtaja mimi nitahitimisha huyu mzee kaanza kupoteza marbles zake au ni mwongo asiyeweza kujizuia kuongopa. Huwezi ukachafua sifa ya mtu hivi hivi kwa kutoa tuhuma nzito (kama alivyofanya Kuhani kwa dk. Masau--ingawa alifanya hivyo anonymously) huku huna ushahidi unaounga mkono madai yako. If Mengi refuses to name that person then that is very small of him.
 
Hivi lile sakata lake na kile kiwanda cha hakuna matata limeishia wapi nasikia alikopa pesa benki kiwanda kikafa kauza mitambo ile kwa viwanda kama tbl kwa bei chee wafanyakazi wake wengi walihamia viwanda vingine na siri moyoni

mengi una mengi ya kutuambia sasa hivi bwana
 
Umakini unatakiwa wakati wa kujibu hoja! Inawezekana kweli Mh. Masha anataka kumsaidia Bw. Mengi katika hili. Ni sahihi, Mengi kama mwanajamii atoe uthibitisho maana yake aseme nani anamfanyia hizo ghiliba ili sheria ifuate mkondo wake. Kisura you are right!
 
Mimi natabiri hamna chochote cha maana kitakachotokea. Mengi hatataja jina. Siku saba za Masha zitapita na yeye hatafanya lolote. Na kufikia Jumatatu ya wiki ijayo hii mada itakuwa haina mvuto kama iliyo nayo sasa hivi.
 
Mimi natabiri hamna chochote cha maana kitakachotokea. Mengi hatataja jina. Siku saba za Masha zitapita na yeye hatafanya lolote. Na kufikia Jumatatu ya wiki ijayo hii mada itakuwa haina mvuto kama iliyo nayo sasa hivi.

Cynical as always but sadly true!
 
1.Mengi vs Masilingi 2. Mengi vs Malima 3. Mengi vs Manji 4. Mengi vs Masha who will be next?
 
Hili swala limeishakuwa complicated tayari. Kitendo cha Mh. Masha kumuagiza Mengi athibitishe tuhuma zake, kunanifanya nipate mashaka kweli kama Jeshi la Polisi litafanya kazi yake ipasavyo.

Turudi nyuma kidogo tu, Mzee Six - Spika wa Bunge (Mzee wa Kujiridhisha kwanza kama ilivyo jadi ya wanasheria) pamoja na Katibu wa Bunge walipeleka tuhuma za mkanda wa kideo kwenye Jeshi hilo hilo la Polisi wakimtuhumu Mbunge mmoja ambaye alionekana ndani ya ukumbi wa Bunge na senior officer wa Bunge wakiranda randa. Baadaye Jeshi la Polisi walikuja kusema kwamba kwenye huo mkanda hakukuwa na picha yoyote, the video was empty!

Ajabu ni kwamba Mzee wa Vijisenti alishatishia kumshitaki Six kwa kumchafulia jina. Nadhani kama kweli the video was empty, ilikuwa ni right time ya Mzee wa Vijisenti kupeleka kesi mahakamani na kudai fidia na ni kitu ambacho kingemng'oa Six kwenye kiti cha enzi. Lakini baada ya tamko la Polisi kwamba mkanda ulikuwa hauna kitu, Vijisenti alikaa kimya na Mzee Six nae akakaa kimya, mambo yakaisha kimya kimya.

Je, leo hii Mengi ni nani apeleke ushahidi Jeshi la Polisi within 7 days na awe na uhakika kwamba ushahidi huo utafanyiwa kazi. Je, wakifanya ule usanii wa mkanda kuwa hauna kitu?

Mtikila alisema ana ushahidi wa watu waliomuua Marehemu Chacha Wangwe, hatukusikia Masha akitoa tamko la siku 7 kwa issue nzito kama hiyo ambayo ilivuruga amani ya Tanzania na hasa Tarime. Lakini leo baada ya kusikia Waziri Kijana na tena wa Wizara Nyeti, Masha kakimbilia TBC1 kwenda kutoa siku 7 hata kabla hajaandika barua. Hivi yeye ndio ana wajibu wa kushughulikia hayo mambo?

Dr. Slaa alipotoa list of shame sikusikia Waziri wa Mambo ya Ndani akitoa tamko lolote, bali watuhumiwa ndio waliojibu mapigo kwa kutishia kwenda mahakamani na mpaka leo Mzee Slaa anadunda mtaani na documents za siri za serikali akiwa nazo na alishasema hata Bungeni mbele ya Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani kwamba ana documents nyeti za serikali, mbona hakupewa siku 7 kuzisalimisha mikononi mwa serikali?

Huu ni usanii, na Mengi asipokuwa makini ategemee kwamba yale yaliyotokea Mjengoni (ya empty video) yanaweza kumkuta yeye pia kwa kuwa Jeshi la Polisi halifanyi kazi yake ipasavyo na hasa kama mtuhumiwa ni Boss wao!
 
Cynical as always but sadly true!

I call it keeping it real. You wait coz at the end of the day I'm going to be right!!!!

Mnaona sasa hivi hatuwazungumzii tena Mramba na Yona.....heheheheheeeeee
 
Mimi natabiri hamna chochote cha maana kitakachotokea. Mengi hatataja jina. Siku saba za Masha zitapita na yeye hatafanya lolote. Na kufikia Jumatatu ya wiki ijayo hii mada itakuwa haina mvuto kama iliyo nayo sasa hivi.

...mind you NN, it is seven working days, i.e minus weekend, Eid etc etc...

i wonder muheshimiwa gani mwingine naye atajitokeza next kuchukua 'ujiko' wa front pages zama hizi za EPA na mafisadi.

Funika kombe mwanaharamu apite, na wapiganapo mafahari, nyasi ndio huumia...
 
1.Mengi vs Masilingi 2. Mengi vs Malima 3. Mengi vs Manji 4. Mengi vs Masha who will be next?

Wote anaogombana nao majina yao yanaanzia na MA,au masharti ya mganga hahahaha (msinitoe roho jokes tu.....!!!!!!)
 
1.Mengi vs Masilingi 2. Mengi vs Malima 3. Mengi vs Manji 4. Mengi vs Masha who will be next?

4. Mengi vs Mkapa. 5. Mengi vs Lowasa. 6. Mengi vs Kikwete. 7. Mengi vs Wananchi (ambao watakuwa wamechoka naye na kushindwa kumwonea huruma)
 
4. Mengi vs Mkapa. 5. Mengi vs Lowasa. 6. Mengi vs Kikwete. 7. Mengi vs Wananchi (ambao watakuwa wamechoka naye na kushindwa kumwonea huruma)

Naona umekose kidogo barabara yako tunaelekea Mbagala , huko uendako GongolamBoto

Never underestimate this guy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom