Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,103
- 43,356
- Thread starter
- #261
Mkuu hapa unamanisha kwamba Masha (the learned friend) 'kakurupuka' kuitetea serikali na ni ishara kwamba anajitetea mwenyewe?
absolutely:
a. Aliyetuhumiwa kutoa vitisho ni "Waziri"
b. Anayetoa siku saba kutolewa ushahidi ni "Waziri"
c. Sasa itakuwaje kama "Waziri" aliyetuhumiwa ndiyo "Waziri" aliyetoa siku saba?
d. Kwa yeye kutoa siku saba amejitangaza kuwa yeye siyo "Waziri" aliyetuhumiwa kwani mzee Mengi ataweza tena kusema kuwa "Waziri" aliyemnua ni Masha bila kuonekana analipiza kisasi?
e. Msemaji wa haki ambaye alitakiwa kutoa wito kwa Mengi ni adha Mwanasheria Mkuu, IGP, au DPP au hata RPC
f. Masha ametoa maelekezo ya wapi Mengi aende kutoa taarifa kwenye kituo gani cha Polisi
g. Masha ndiye WAziri mwenye dhamana ya Jeshi la Polisi na asikuambie mtu ana madaraka makubwa sana ya uendeshaji wa jeshi hilo hata kutoa maagizo kwa niaba ya Rais.
h. Mengi akienda kutoa taarifa kwenye hicho kitua na Masha akiwa Waziri akaagiza kuwa "Taarifa hizo nataka nipatiwe mara moja ili tumshughulikie Waziri huyo au niweze kumpatia taarifa Rais" itakuwaje?
I. Kwa kujitokeza hadharani na kudai ushahidi wa kutaka "Waziri" atajwe, Masha ameingilia kati kupatikana kwa haki na haiwezekani kamwe Mengi kutendewa haki.
Ndio maana nimeandika mojawapo ya tahariri kali nilizowahi kuandika, hawa watu wasichezee madaraka wakifikiri wao ni miungu watu!