Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Je kama Mengi akiweza kuthibitisha hiyo kauli yake kama alivyotakiwa na uthibitisho huo ukawa wa kweli kabisa itakuwaje? Sidhani kama Mtu mwenye akili zake anaweza kukurupuka na kutamka maneno kama haya bila ya kuwa na ushahidi wa aina fulani tena unaojitosheleza.
 
sasa katika umakini wake timamu akaamua kwenda kusema Mengi amtaje Waziri huyo wakati akijua ni yeye mwenyewe au kwamba yeye ametajwa kwenye JF kuwa ndiye aliyekusudiwa? Inanifanya nihoji kama ningeenda shule ningekuwa na faida ya aina fulani..

check on you.
Eti masha naye msomi tena mwanasheria................sasa sirikali ya danganyika hao ndio viongozi wetu.
Rushwa inaua elimu kuliko ugonjwa wowote ule duniani, kwani rushwa inashambulia hata wale waliosoma tayari na kuuwa ubongo wa kufikiri na ikikomaa inakuwa gonjwa sugu ufisadi.
 
Ukweli ni kuwa, kwa Masha kusema alichosema ameshamfanya Mengi kushindwa. There is no way kwa Mengi kushinda.

a. Akikataa kumtaja Waziri ataitwa Muongo

b. Akimtaja kuwa ni "x" ataambiwa atoe ushahidi

c. Akisema ni "Masha" ataambiwa anamlipizia kisasi

d. Akikaa kimya anaweza kubambikizwa mashtaka ya uchochezi (kufanya watu waichukie serikali) kama ya MwanaHalisi

so, the only way to settle ni kwa hawa wawili kwenda Ngurdoto or somewhere exotic and have a good chat just the two of them; no polisi and no reporters. Wazungumze hadi wafikie mwisho. na Wakimaliza waniombe niwaandikie press statement!!!!
 
Mzee Hii kitu usiianzishe!! yatakua yale yale ya NSSF

Ningekua ninaheshimu sura za watu au kuogopa majina yao ningekuwa nimeacha haya siku nyingi kweli. SImpigii magoti mwanadamu yeyote, fisadi ni fisadi tu! awe na digrii asiwe nayo, awe na mali asiwe na mali, awe CCM au upinzani, awe mfungwa au jaji! So worry not.
 
kwa hiyo BAKHRESSA yuko kimya kwa sababu hajaenda shule?

makubwa haya!

.game ....aliyesema bakhresa ..hajaenda shule ndio maana halalamiki amekosea...kwanza alitakiwa kujuwa kuwa bakhressa pamoja na kuwa hajaenda shule ...ana biashara stable sana na ni mmoja wa wazawa wa kujivunia....kampuni yake inaheshimika sana.,

pili bakhressa ameajiri wataalamu hadi wenye phd ....kuendesha biashara,ambalo ndio jukumu kuu la mfanyabiashara ,kumiliki timu nzuri ya wafanyakazi wenye ujuzi[mtaji mkuu huu]..

tatu bakhressa watoto wake wana elimu kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika sana ..so kitaalamu tutasema kuwa bakhressa has the best SUCCESSION PLAN in his business empire....

pia bakhressa hata akilalamika ...hutaweza kujuwa kwani hana media ya kuzipa uzito complains zake....lakini kuna wanaokumbuka hapa kuna wakati unga wake na mahindi tani kwa tani ....ulichomwa moto kwa makosa.....alilalamika.....mfanyabiashara yoyote hakosi malalamiko..ila wengi huandikiana tu barua na vyombo husika......thats is a routine in business....
 
Ukweli ni kuwa, kwa Masha kusema alichosema ameshamfanya Mengi kushindwa. There is no way kwa Mengi kushinda.

a. Akikataa kumtaja Waziri ataitwa Muongo

b. Akimtaja kuwa ni "x" ataambiwa atoe ushahidi

c. Akisema ni "Masha" ataambiwa anamlipizia kisasi

d. Akikaa kimya anaweza kubambikizwa mashtaka ya uchochezi (kufanya watu waichukie serikali) kama ya MwanaHalisi

so, the only way to settle ni kwa hawa wawili kwenda Ngurdoto or somewhere exotic and have a good chat just the two of them; no polisi and no reporters. Wazungumze hadi wafikie mwisho. na Wakimaliza waniombe niwaandikie press statement!!!!

Ila kama kweli Mengi anajina na ushahidi amtaje huyo waziri, lakini kama naye alinusishwa habari na nyoka wake kazi kweli.

hata hivyo kwa jinsi alivyoongea Mengi, Serikali haiwezi kumbana, ila hapa kuna something behind this.
Mengi alisha sema kama mbaya mbaya tu.
 
Ningekua ninaheshimu sura za watu au kuogopa majina yao ningekuwa nimeacha haya siku nyingi kweli. SImpigii magoti mwanadamu yeyote, fisadi ni fisadi tu! awe na digrii asiwe nayo, awe na mali asiwe na mali, awe CCM au upinzani, awe mfungwa au jaji! So worry not.

Asante kwa kuonesha msimamo wako katika mapambano haya.Swali langu ni rahisi tu.. Je Kujiuzulu ndio njia pekee ambayo Masha anaweza kuichukua katika suala hili?(maana umeiweka ya kwanza) na hata kama sio ya pekee lakini kwa kuiweka kwako ya kwanza je ina funika kabisa njia nyingine zinazowezekana kutumika katika kutatua suala hili?
 
Hakuna njia nyingine ya kuruhusu haki kuonekana. Unless kuna uwezekano wa yeye "kujitoa" kwa muda kutokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani? Ukicheza chess utaweza kuona all possible moves way ahead. In this case, there is only one way and that is the removal of Masha as the Minister of Internal affairs either voluntarily au kwa uteuzi wake kutenguliwa na Rais.
 
Ila ukiangalia hii kitu katika angle nyingine Mengi ametoa hii taarifa kwa kujilinda zaidi hasa baada ya kusema amemsamehe huyo waziri....sasa akigoma kumtaja kwa chini ya mwamvuli wa "nimeshamsaheme sitaki tena kuzungumzia hili swala" tutamlazimisha?
 
Ilipofikia serikiali hii ya JK ni dalili za wazi kuwa kuna siku moja inaweza kuanguka ama kuangushwa.

Waziri huyu naye kaamua kuiga staili ya waziri mwenzie wa mambo ya Ndani Agustine Mrema ya kutoa siku saba , je? huu ndio utaratibu wa mawaziri wa mambo ya ndani?

Masha , alipaswa kuwa makini zaidi kwanbi kwa yeye kujitokeza na kujibu huku waziri aliyetuhumiwa akisemekana ni kijana basi inamfanya watanzania waanze kumhisi kuwa lazima ni yeye, hata kama wizara yake ilipaswa kusema angelimpa jukumu hilo naibu wake ambaye ni mzee.
 
so, the only way to settle ni kwa hawa wawili kwenda Ngurdoto or somewhere exotic and have a good chat just the two of them; no polisi and no reporters. Wazungumze hadi wafikie mwisho. na Wakimaliza waniombe niwaandikie press statement!!!!

haha ha
This is why i like Mwanakijiji!Unapenda kufanya kile wengine ambacho hawawezi kukifanya
 
Kama Mengi kaishutumu serikali kwa nini Masha aisemee serikali? Kwani Masha ni msemaji wa serikali? Na kwa nini Mengi athibitishe kauli yake kwa Masha? Kwani Masha ni mahakama au ni mkuu wa polisi? Au ukishakuwa waziri wa mambo ya ndani basi wewe ndo kila kitu!!

Masha amesema Mengi akishindwa kuthibitisha kauli yake hatua zitachukuliwa dhidi yake. 1. Ni hatua gani/zipi zitakazochukuliwa?
2. Na zitatolewa na nani?, na Masha, mahakama au nani?

Kwa kweli kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya kauli za huyu waziri kijana na msomi!
 
Mwanakijiji si alishamtaja Masha ..?Naona Masha kaamua kujibu sasa!

I love this Game

kumbe serikali inatoa habari zake kwa mwanakijiji ,so funy........tell me this is a joke

Then hata ikiwa hivyo yeye ndiye mtuhumiwa haki itaendeka akiwa yeye bado waziri.He need to step down kama ushahidi anautaka .
 
Masha kama Waziri anayehusika na mambo ya ndani ana kila haki ya kuuliza hilo. Hapa hautishiwi usalama wa mtu mwingine bali Mengi mwenyewe. Mengi ana kila sababu ya kutaja jina la huyo waziri aliyemtuhumu kwa vitisho.
 
Ukweli ni kuwa, kwa Masha kusema alichosema ameshamfanya Mengi kushindwa. There is no way kwa Mengi kushinda.

a. Akikataa kumtaja Waziri ataitwa Muongo

b. Akimtaja kuwa ni "x" ataambiwa atoe ushahidi

c. Akisema ni "Masha" ataambiwa anamlipizia kisasi

d. Akikaa kimya anaweza kubambikizwa mashtaka ya uchochezi (kufanya watu waichukie serikali) kama ya MwanaHalisi

so, the only way to settle ni kwa hawa wawili kwenda Ngurdoto or somewhere exotic and have a good chat just the two of them; no polisi and no reporters. Wazungumze hadi wafikie mwisho. na Wakimaliza waniombe niwaandikie press statement!!!!

I like this.
kila kwenye migogoro tunapaswa kuangalia nasisi namna ya kuishi. kwikwikwikwi tehe tehe
 
It's a big mistake for Mr Masha to come up illogically that early! This has no any other interpretation than FOOLISH SHOWDOWN! Hakuna busara yoyote iliyoonyeshwa na Masha ukilinganisha elimu yake na wadhifa wake. His emotional posture ilikuwa inamsuta machoni pake wakati anaelezea mambo ya Mengi TBC1 leo asbh. He was unnecessarilly too emotional when explaining his stance on the said issue.

Kuhusu elimu yake, natilia shaka uelewa wake wa philosophy of law (Jurisprudence). Kama alifaulu, in which case najua alifaulu kidogo lakini ni kuwa alikariri tu. Kamwe hutamuona mwanafalsafa yeyote akikurupuka kama alivyo jihusisha na kujibu tuhuma za Mengi.

By implication (other things being equal) hii inaonyesha kuwa yeye ndiye aliyetuhumiwa na Mengi. SHAME ON HIM. He is not the state. Hata kesho asubuhi anaweza kuwa derailed na wizara ikaendelea tu!

Na hii ndio psychology of money and power kwa WATOTO! Wakipata vijisenti kiasi fulani na wakijua BABA nawapenda huwa inakuwa taabu kwelikweli! Hata shuleni hapakaliki.

By the way, ni kwanini aende TBC1 mapema kiasi hicho kutoa vitisho, HANA SUBIRA HATA CHEMBE. Na hii inaonyesha jinsi hafai kuwa kiongozi.

NATABIRI, Masha will be derailed soon!

Mkuu hapa naona nawewe una jazba kama ilivyo kwa Mengi na Masha. Hili suala huenda lisingekuwa kubwa kiasi hiki kama kila mtu angeacha sheria ichukue mkondo wake
 
- Kama nilivyosema jana, kwenye hili Mengi ameenda nje ya mstari hawezi kuanzisha serikali yake ndani ya serikali ya jamhuri, ameanzisha mwenyewe wakati kuna njia nchungu nzima angeweza kuzitumia kutatuta tatizo lake, mara mashehe mara waziri kesho itakua rais, it has to be stopped tena now.

- Taifa tunaongozwa na sheria, sio uhuni uhuni wa kukusanya habari za walevi mitaani na kuzigeuza dhana za kutishia walevi, mimi sinyiwi pombe na nina marafiki 75% wanaolewa kila siku, sasa nikijali maneno yao ya ulevi sitakua na rafiki hata mmoja. Kwenye kesi yake against Manji nilikuwa mmoja wa waliomtetea sana Mengi kwa wahusika wa uamuaji ile kesi kuwa anaonewa lakini not this time, kwa sababu this one yuko nje ya mstari tena out na ninaunga mkono kwa 100% any response kwa wale wote aliohusika na kuwarecord au kuwapiga video na picha wakiwa kwenye ulevi, kama ndio sababu ya claims zake against viongozi wa serikali.

- Priviledge ya kumiliki media au kuwa na uwezo wa kuandika kwenye vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti na mitandao haiwezi kuwa sababu ya wale wenye hizo access kuchafua majina ya wengine kuwa ni mafisadi na the rest of the story bila sababu wala ushahidi, hapa ndipo tunapomheshimu sana Dr. Slaaa, kwa kuweka mambo yote ya ufisadi kwa kalamu na ushahidi usiopingika.

- Masha hana sababu ya kujiuzulu kwa kusimamia kiapo chake kwa jamhuri, yaani kulilinda taifa kwa njia zote zilizopo chini ya uwezo wake kisheria, ni wajibu wa waziri wa ndani kuhakikisha kua wananchi hawabughudhiwi na viongozi au wananchi wengine, na wale wanaobughudhiwa ni wajibu wao kufikisha matatizo yao kwenye vyombo vya dola kwa ufumbuzi wa kisheria iwapo wanao ushahidi wa kisheria, kama sheria yetu inavyosema. Sasa anapotokea mwananchi yoyote mwenye kuamua kwenda kinyume na sheria zetu, regardless ya who he is serikali ni lazima isiamie sheria tena kwa nguvu zote ilizonazo.

- Ninarudia tena kwamba ni wajibu wa waziri wa ndani kusimamia mambo ya ndani bila ya kujali ni waziri gani anayetajwa au asiyetajwa, Mengi ni lazima afikishwe kwenye sheria na atoe ushahidi wake uliopatikana kisheria ili kuiridhisha sheria ya jamhuri, ambayo waziri wa sasa wa ndani amekula kiapo kuilinda kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote. Tunaishi kwa kuongozwa na sheria sio uhuni uhuni wa kukurupuka kwenye public na tuhuma nzito kwa viongozi wetu wa juu kwenye media, ni kujaribu kuwatisha ili wasifanye kazi zao walizopewa na na sisi wananchi kwa mujibu wa sheria. Hata US sheria iko wazi kuwa ukilia moto kwenye sehemu kama ya cinema wakati moto hakuna, unachukuliwa hatua za kisheria tena kali sana, sasa hapa ni wajibu wa serikali yetu ya jamhuri ikiongozwa na waziri wa ndani ambaye ndiye kisheria mhusika mkuu kuhakikisha kuwa Mengi anapewa haki yake so is waziri aliyetajwa pia akipewa haki yake na pia kutulinda sisi wananchi wengine wa kawaida na viongozi in the future na this kind of Mengi's accusations, hakuna anayekataa haki za Mengi kulindwa na sheria, lakini ni lazima huheshimu sheria za jamhuri na utaratibu wetu wa kisheria.

- Ninamuunga mkono kwa 100% kitendo cha waziri wa ndani kumpa Mengi muda wa kutoa ushahidi wake kwa serikali, na pia kumpa waziri anayehusishwa nafasi ya kusema pia mbele ya sheria, na sheria iamue nani mwenye makosa kisheria na nani hana, lakini the important ishu ni kuhakikisha kua next time Mengi anakwenda kwenye vyombo vya sheria bdala ya media, hawezi kusema kua haviamini kwani vimewahi kumpa nafasi ya kujitetea na akashinda kesi, tena against waziri wa jamhuri, ni lazima Mengi ajifunze kupeleka malalamiko yake kwenye sheria, kama sheria inavyotaka.

- Wote sisi ni wananchi wa Tanzania, na hili taifa ni letu sasa tusitishane na hizi tabia mpya za kujifanya wanamapinduzi, kwa kutaka kulazimisha kwa nguvu hoja za kuwaita walioko kwenye power tuliowachagua kisheria kuwa ni mafisadi just because hatuwataki au tuna chuki zetu za binafsi, dawa ni kudai tu kwa nguvu kuwa ni mafisadi kwa sababu ni wimbo unaokubalika kirahisi na wananchi bila hata ushahidi ulio wazi, hili sio taifa la walevi au wajinga wajinga, tunazo sheria na ni lazima zitekelezwe kwa nguvu zote.

Hatuwapendi mafisadi, lakini ni lazima kuwa na ukweli juu ya uifisadi wao, na ni wajibu wa waziri wa jamhuri kulinda sheria, bila kujali kama ni Mengi au anybody.

Mungu Aibariki Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom