Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Kwa kuwa ndiye anaye kipa Chama cha Mapinduzi ushindi na kuipa Serikali ya JK nguvu kupituia media zake .
 
Mimi nadhani muuliza swali ana majibu, kwa kuwa swali halina mashiko. Lakini kuna swali ambalo pengine katika ile makala iliyoonekana kama ya kufumba fumba, kuna hoja kwamba Yusuf Manji yuko juu ya sheria, ni zaidi hata ya Rais, Waziri Mkuu, IGP, Mkuu wa Usalama, Mkuu wa Majeshi na kadhalika. Swali hapa ni kwamba, NI KWANINI YM (Yusuf Manji) anaogopewa kuliko Rais? Hapo utakua nahoja. Nadhani ama umekosea ama umefanya kwa makusudi kwani hoja zote ziko wazi.

Hoja ni kwamba kuna kesi nyingi dhidi yake, achilia mbali zinazoandikwa katika magazeti lakini zipo zilizopo na zilizowahi kuwapo katika vyombo vya dola.
Hapa nitaanza kumnukuu mtu mmoja yeye alisema, "Nikisikia Lowasa anafikishwa mahakamani sitashangaa, lakini nikisikia Yusuf Manji anashitakiwa nitashangaa sana, na ninaamini hilo halipo."

++ Ukisoma Mwananchi Jumapili Januari 28 ukurasa wa pili habari inayotoka ukurasa wa kwanza kolamu ya kwanza aya (para)ya tatu, "Harakati hizi (za PCB) zinaweza kugonga mwamba kufuatia baadhi ya ambao mafaili yao yako PCB wanahusishwa na shughuli mbalimbali za kuchangia CCM kama vile viongozi wa chama hicho hawana habari ya wafanyabiashara wanaochunguzwa"
---- Aya hiyo inarejea habari ya awali katika gazeti hilo ya Januari 25, 2007, "Mfanyabiashara maarufu kumfuata Balozi Mahalu" mwishoni mwa habari katika The East African la wiki hii, inarejea pia habari hiyo.

Kwa ufupi habari hiyo inarejea taarifa sahihi toka ofisi ya DPP kuwa kuna jalada ambalo linashughulikia na taasisi mbili yaani PCB na DPP. Habari hiyo ilikua na mapungufu ya kitaaluma, lakini jambo la msingi ni kuwa mfanyabiashara anayetajwa (HABARI ZA UHAKIKA) ni Yusuf Manji, na kesi husika si ya jana wala juzi, kabla hata ya huo unafiki unaoitwa ugovi wa MENGI NA MANJI kuanza. Kesi hiyo iko PCB tokea mwaka 2004na ilipelekwa kwa DPP mwishoni mwa 2004 na kurudishwa PCB mwanzoni mwa 2005, lakini hadi leo MANJI alilindwa na serikali ya Ben Mkapa, na cha ajabu sasa kwa sababu waliomlinda hawakuwa wanampenda, walipenda pesa na sasa wako pia wanaopenda pesa. Hapo ndipo unapaswa kuuliza swali, KWANINI MANJI ANAOGOPWA KULIKO JK? Ukiwa na hoja.

Kesi nyingine nyingi na za zenye ushahidi wa kutosha, zinaelezwa kuwa zinachunguzwa na vyombo husika vinathibitisha tena kwa maandishi. Aliyekuwa Waziri wa Kazi, Prof, J. Magembe alitamka wazi kuwa kesi ya NSSF na Manji iko katika uchunguzi wa PCB. Uliza swali ukiwa na ushahidi usiburuzwe na hisia binafsi ama kusukumwa na propaganda kama za kina Mahalu na ZOmbe kushitaki magazeti na wako waliowaamini kwa dhati. TUSIKUBALI KUBADILISHWA KWA PROPAGANDA< TUIPENDE NCHI YETU< TUMSAIDIE RAIS WETU ILI AKISHINDWA TUMSUTE, SIO KUKATISHA TAMAA JUHUDI ZA WAPIGA FILIMBI
 
Jamani!
Wananchama na wapenzi wa Jambo Forum kwanza ningependa kujitambulisha mimi binafsi ni Bw. Kiona na ubin wangu ni Mbali, hivyo unaweza kutamka jina langu kamili ni Bw.Kiona Mbali.

Lengo la kuingia katika hii forum ni kuweka mtazamo wa kesho kitatokea nini? wakati wengi wetu humu ndani tunaangalia yaliyotokea jana na ndiyo maana tumekuwa tukiona mambo mbalimbali yaliyotokea huko nyuma, lakini mimi nipo na mtazamo tofauti wa kuangalia yanayotarajia kufanyika kesho, wiki ijayo, mwezi ujao na mwaka ujao hadi miaka.

Hii itatoa changamoto kubwa kwa wanachama wa Jambo forum nao kuchangia mawazo yao na siyo hadi tuone jambo limeaharibika na kuanza kukimbilia kulaumu, ni jukumu letu pia kutoa tahadhari na pengine kuweka msimamo wa pamoja kutokana na maoni mbalimbali tutakayoyapata.

Jambo moja ambalo mimi naliona na liko mbele yetu ni jinsi mfanyabishara maarufu wa hapa Tanzania, Bw. Reginald Mengi akiwa katika mbio za kukimbiza kijiti anachoshikilia Bw. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kiona Mbali nimegundua kuwa mazoezi anayofanya Bw. Mengi kukikimbiza kijiti hicho ni cha kasi kubwa na tofauti na matarajio ya wengi.

Nina sababu kadhaa kuthibitisha ukweli wangu.

1. Bw. Mengi amekuwa akitumia baadhi ya wabunge kueneza sera zake ambazo zitampa nafasi ya yeye kugombea nafasi hiyo, na hivi sasa amekuwa akimtumia mmoja wa wabunge kutoka mkoa wa mmoja maarufu, kwenye masuala ya madawa ya kulevya na mbunge huyo amekuwa kutumiwa na mfanyabishara huyo bila mwenyewe kujua au ni mipango yao.

Hiyo ni kuhakikisha kwanza kuwachafua baadhi ya wabunge waliopo mkoa wa Dar es Salaam, baadhi ya wafanyabiashara, mawaziri na viongozi na watu maarufu kwa madai ya kuhusika na madawa ya kulevya.

Bw. Mengi pia anadaiwa kuwa amemuahidi mbunge huyo kuchagua jimbo lolote la mkoa huo, ili uchaguzi ujao aweze kuingia katika kinyang'anyiro hicho kwa gharama yoyote ile.Sasa hivi mbunge huyo ameingia bungeni kupitia mgongo wa jumuiya moja.

Tayari mbunge huyo amekuwa hana mahusinao mazuri na wabunge wenzake kutoka katika mkoa huo kwa jeuri ya Mh Mengi.

Hivi karibuni Mengi alimshauri mbunge huyo kuiomba serikali impatie ulinzi kama alivyofanya yeye (mengi) mwaka 1994 kwa madai kuwa anataka kuuliwa na baadhi ya wafanyabishara wa kiasia.

2. Mengi alikuwa akitoa support kubwa kwa kiongozi wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji, Cristopher Mtikira na agenda yake ya kutaka katiba ya Tanzania ibadilishwe na kuwe na mgombea binafsi.

Mtikira alisisima kidedea katika kesi hiyo hadi alishinda, lakini yeye (Mtikira) alikuwa boya tu, mwenye kesi mwenye ni Mheshimiwa Mengi.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1995, Bw. Mengi alikuwa akifanya jitihada kubwa za kuhakikisha kunakuwa na sheria ya mgombea binafsi, lakini kutokana na msimamo mkali wa hayati baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere suala hilo lilipingwa na kuondolewa kabisa kwa madai kuwa nchi yetu haina mabepari hadi kufikia kugombea bila ya kuwa na chama.Hizo pesa watapata wapi kama si kuuza nchi kwa wafadhiri? Mwalimu aliuliza?

3. Lengo kubwa la kuanzisha kwa vyombo vyake vya habari lilikuwa si kufanya biashara, lakini lilikuwa ni kujiweka sawa na kuanza kujitangaza a ndiyo maana hadi leo kama alivyozungumza, mbunge wa Mkuranga, Bw. Adam Malima kuwa TV yake amekuwa akichukua muda mwingi kwa jambo lisilo la msingi na taarifa za Rais na mambo mbalimbali ya serikali yakipewa uzito mdogo.

4. Amekuwa akijitahidi kuwa karibu na jamii, tofauti na wafanyabishara wenzake ili kuonekana kuwa ana mapenzi ya dhati na watu wa hali ya chini na kufikia eti kula chakura na vilema, mazeruzeru na viziwi na baadae kupigwa picha.

Sasa Mheshimiwa anawasadia watu kwa chakura harafu anawapiga picha kutolewa kwenye ma TV, magazeti yake na pengine kuoneshwa kwa wafadhiri na nyie mliokuwa Uingereza mnaweza siku moja mkaona mikanda hiyo, kwamba yeye anakubalika kwa lengo la kupata mapesa ili aweza kuichukua nchi.

Jamani Tanzania tuna matajiri wengi tu, lakini ambao hawapendi makuu, tena wana mapesa mengi na mfano halisi ni Bw.Said Salim Bakhresa, huyu jamaa kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana mwaka jana mwezi wa nne kutoka TRA, Bw. Bakhresa ndio alikuwa akishika namba moja, lakini kikubwa kwambak kuna watu Tanzania hawamjui huyu bwana na badala yake wanaojulikana zaidi ni watoto wake.

Huyu mzee ana uwezo wa kufanya jambo lolote lile, kuwa na TV,kutoa misaada ya mamilioni ya shilingi, lakini amekuwa kimya na biashara zake na kwenda msikitini.Hivi kwa nini huyu mengi hasiwe kama huyu jamaa.

5. Bw. Mengi amekuwa akijifanya kama kiongozi furani mkubwa, kwani amekuwa akiwaalika mabalozi wa nchi mbalimbali ofisini kwake na kufanya nao mazungumzo na taarifa zake kupatikana katika magazeti yake na TV kanakwamba ni Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.

Amekuwa akitumia 'super power money' kwa kujifanya anaweza kusema lolote kwa serikali na kumsikiliza na amekuwa akiogopewa sana si kwa viongozi wa mashirika ya umma, hata mawaziri ambao wamekuwa wkimpta taarifa za kila siku katika Serikali na hata kikao cha baraza la mawaziri.

6. Ili kuweka mambo yake ya biashara safi, Bw. Mengi amekuwa akifanya jitihada za kuhakikisha kuwa wakuu ya mashirika na taasisi za umma , wote wapo kwenye himaya yake na yule ambae ataonekana kwenye kinyume, basi atafanyiwa ufisadi na vyombo vyake vya habari ili aweze kuondolewa hapo.

Tumeshuhudia hivi karibuni, alipoanza kumsakama Mkurugenzi wa NSSF, Bw. Ramadhani Dau kuhusu ununuzi wa maghara ya Quality Group.

Lengo lake yeye anachotaka pale wawepo kina Kimaro, Tesha, Massawe.

7.B Mengi amekuwa akikitumia CHADEMA kama mgongo wa kutaka kujiweka safi kisiasa na ndiyo maana katika uchaguzi uliopita aliweza kusaidia mamilioni ya shilingi kuhakikisha chama hicho kinafanya vizuri pamoja na mgombea wake wa Urais, Bw. Freeman Mbowe.

Mengi amekuwa na urafiki wa karibu na Mh: Mbowe na inadaiwa kuwa kama hatafanikiwa kuingia kama mgombea binafsi, basi mwaka 2010 chama hicho kinamsimamisha Bw. Riginald Abraham Mengi.

8. Hivi sasa ameanza katika harakati zake za kuipiga vita serikali ya Jakaya kikwete baada ya kuona viongozi wote wawili, Rais na Waziri Mkuu wakimpita kama yai bovu, baada ya viongozi hao kugundua janja yake na kutaka kuzidi kujenga jina lake kupitia katika uongozi wao.

JK alionana na Bw. Mengi katika kuchagia njaa ambapo alitoa milioni 25 na magunia ya mahindi na picha kupigwa sana, lakini baada ya hapo Kikwete amekuwa akimpungia na hata pale alipohitaji kuonana nae, jamaa yuko busy na kuwaletea Watanzania maisha bora.

Baada ya hapo alimgeukia Lowassa, huyu ni afadhari ya JK ambae anaweza kuongea nae huku akicheka jamaa yuko makini, hakumpata kaibsa nafasi na matokeo yake amemtumia mbunge wa Chadema bw. Ndesamburo kutka kumchafua Wazuri Mkuu, lakini kutokana na mheshimiwa Lowassa kujua janja yake hakujibu hoja zake kwani yupo busy na Watanzania wake zadi ya miloni 35 wakioangalia anvyochapa kazi kuwaletea maendeleo.

Ndugu zangu,wananchi wenzangu, hayo ni machache kati ya mengi niliyokuwa nayo kuhusu huyu Bw. mengi naomba kuwasilisha hoja kwenu,

Hakuna matusi wala jaza naomba zijibiwe hoja!KARIBUNI
 
Kiona Mbali,

Mengi anataka kugombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya CHADEMA au binafsi; UNA USHAHIDI ZAIDI YA HAYO MANENO?
 
wewe toa hoja, acha kuleta maneno, eleza yale unayoyajua na siyo kunieleza mimi ninayoyafahamu
 
Kiona Mbali,
Nijuavyo mimi Mengi ni CCM dam dam. Hata kama wanatoka kumoja na Mbowe. Pia nijuavyo mimi Mbowe alimfuata Mengi kuomba mkopo/msaada wakati wa kampeni zake za 2005 Mengi alikataa. Sasa sijui huu ni urafiki wa aina gani.
 
Kiona mbali pengine yeye mwenyewe ndio Mengi. Kazi imeanza kampeni hiyo 2010.
 
Baada ya kusoma maelezo yako marefu maana hayana hoja ni maelezo mepesi nimehitimisha kwamba wewe si Kiona Mbali nali ni Kiona Karibu ama Mpika Majungu dhidi ya Mengi

Nimeshangaa umeweza kumtaja Mengi na kumnanga namna hii lakini umeacha kutaja majina kibao .Je unataka tukuamini kwamba una hoja ama hadithi za mitaani ?Hapa Mengi huwa anapigwa mawe sana lakini akiwa na jambo la kumpigia mawe.

Yaani unaona karibu kiasi kwamba Mgombea binafsi unaogopa asiwepo kama vile JK anavyo weweseka usiku akiogopa Mgombea Binafsi ?

Yaani kwa akili yako unasema Mengi kamtumia Mtikila unaweza kusema maneno haya mbele ya Mtikila ? Ile kesi ya Mtikila na zingine kama Richmond, Rada nk zinaweza kufunguliwa na mwanchi yeyote na zikasikilizwa wewe unaona mbali wapi usiweze kuona hili ?

Umeendelea na mahubiri ambayo hayana kichwa wala miguu na kupoteza muda wa watu kujadili hoja za maana na hata kusema Mengi anawatumia je wewe unatumiwa na nani ?
Umetumwa na JK ? Lowasa ? Manji ?ana Malima ?

Kweli waswahili walisema angalia akili za watu but we are not foolish .Unasema JK yuko busy kuwaletea Watanzania maisha una uhakika na hili ? Mengi awe Chadema leo kwelo huoni hata maandishi ya magazeti yake na TV zake ? Mbona juzi wameandama hatukuona TV kwenye eneo lile hata magazeti kuandika ? Unaogopa Mengi kugombea urais ? Sasa nani anafaa ? Manji ? Malima ? Lowasa ama wewe Kiona ukingoni ?

Nani kakutuma wewe na ukadhani kwamba sisi JF ni wapuuzi wa mawazo ?
 
Kionambali,
Umeomba ujibiwe hoja bila jazba na matusi, hoja zenyewe ziko wapi? Ni rahisi mno kujua kuwa umeendelea na tabia yako ya kuingia kwenye forum hii kwa majina lukuki ili kutema sumu zako dhidi ya watu fulani. Labda la kukumbusha tu humu mtu fulani anapojadiliwa hajadiliwi kwa kabila lake au dini yake au rangi yake bali kwa mchango wake hasi au chanya kwa maendeleo ya nchi. Wewe kama una chuki na mtu kuwa Mchaga hilo ni tatizo lako.
 
Miaka mingi sijaingia humu japo ni mwanachama wa siku nyingi, ila huwa nawasoma sana, leo hii mikono imeniwasha kweli kweli nahapa nilipo natetemeka, moyo unanidunda, saa yoyote naweza nikafuatwa na AMBULENSI, baada ya kusoma eti Viongozi wa ngazi za juu wa tanzania wapo busy kuwaletea watanzania maendeleo hii -should be a Joke!!! wewe kiona UKINGONI hebu tueleze huo ubize kwaza upo wapi? na wa nini? Usije ukawa unamsifia jongoo kuwa ana miguu mingi kumbe mwendo wake ni taratibu, Ubize wa viongozi hao uliowataja ni sawasawa na mwanamme kuoa mke mzuri lakini hata kupika hajui, kuchota maji kwa ndoo hawezi, sasa wa nini? wa kazi gani mke ambaye hata kitandani hana maana yoyote, mke anayejiremba kutwa nzima mume ukirudi chakula hakuna. ndugu chunga vidole vyako unapoandika tena kuwa muangalifu sana haswa unapoandika jambo la kisiasa linaloihusu Tanzania. Serikali ya JK ni serikali inayojirembaremba tu kwamba inataka kuwaletea maendeleo watanzania, lakini si kweli, Serikali hiyo ikishajiremba kupitia vyombo vya habari huwa haitosheki bado inatumia mamluki kama nyinyi mje kuandika vioja humu, tena serikali hiyo inafikiria watanzania wa leo hawana upeo wa kuelewa,kuchanganua, na kuona muelekeo wa mambo na ndio sababu inawatumieni watu kama KIONA KARIBU, sasa rudisha salamu kwa Serikali Ya JK Mwaambie hivi, WATANZANIA WA LEO ASIWAFANANISHE KABISA NA WATANZANIA WA TANU YOUTH LEAGUE Wa miaka ya 70, sisi ni watu wengine kabisa na karne yetu tunajua mambo.
Sasa nataka utueleze hayo maendeleo aliyoyaleta JK au anayotegemea kuyaleta ni yapi?
Nchi ilikuwa na matatizo makubwa sana ya umeme, na matatizo yaliyojitokeza kuhusu kampuni ya RICHMONDS yanajulikana, lakini Ili JK atufunike blangeti la mbao muda mfupi kabla ya mvua za vuli kupamba moto, eti akatutangazia tatizo la umeme linakaribia kwisha, au kupungua, yaani JK anadiriki kututangazia kumalizika kwa tatizo la umeme kwa kutumia vipimo vya hali ya hewa? Hivi haya ni maendeleo jamani au anaturudisha nyuma miaka kibao? sasa mimi binafsi mpaka sasa sishawishiki kabisa na serikali ya JK kwamba itatuletea maendeleo, serikali ya JK haina muelekeo wowote si wa maendeleo wala chochote, zaidi ya kubeba wimbi la wafanyabiashara, kuwatembeza dunia nzima kwa pesa za walala hoi, eti anawatambulisha au anafanya uhusiano au sijui ana maana gani, Kwani wafanya biashara hao waliwezaje kufanya biashara bila ya kujua soko la bidhaa zao, ilikuwaje wafanye biashara bila ya soko, mimi sio mchumi lakini kwa kutumia akili yangu tu siwezi kuanza kufanya biashara bila ya kutafuta soko, na kutafuta contacts na wafanya biashara wa nje na ndani ya nchi, huu ni upuuzi.

Ndugu,naomba ueleze maendeleo ya nchi tangu JK aingie na kundi lake serikalini.

Ukiwa kama mtanzania unashabikia na kusema eti JK au Lowasa hawakumpatiliza Bw Mengi kwa kuwa wamegundua Janja yake, utakuwa unauonyesha UMAMLUKI wako dhahiri, na Umamluki ukiwa hadharani kiasi hiki basi tutauita UMAMLUKI THABITI ambao ndio uliosababisha Rwanda na Burundi kuchinjana. Be carefull!!!!!!!!!
Mengi anasaidia watu kivyovyote vile, akiwa anatolewa katika vyombo vya habari au la, lakini msaada umefika na umesaidia. so sioni point hapo ya msingi.
Kiona karibu kusema Vyombo vya habari havitilii mkazo kuonyesha maswala ya serikali na zinamuonyesha Mengi Peke yake, hili bado sio kosa kwani yeye ndio anamiliki vyombo hivyo, na anatangaza biashara yake na anajitangaza yeye mwenyewe na atagombea nafasi yoyote ile ya serikali kwa mujibu wa katiba na sio kwa mujibu wa kiona karibu. Na jambo la kuonyesha ktk TV zake kuwa anakula na vilema, au amesaidia walemavu hili ni jambo kubwa sana hata katka seriakali kwa sababu serikali ndio ina walemavu ndani ya Taifa, Na kwahili Mengi atakuwa ameisaidia sana serikali maana serikali haiwezi kula na vilema Serikali ya JK inakula na wakina MANJI na RICHMONDS Na RADA Tena inakula na watu MIJIZI KWELI KWELI Inakula nao bila hata Kunawa.
JK mwezi wa Ramdhani alikula na vikundi malimbali na hii nayo unaiitaje?
sasa siku nyingine uje na hoja za maana, na kama ungekuwa karibu yangu hapa ningekunasa kibao.
usomaji mwema
 
Sina mengi yakuogea hapa Bw.kiona mbali unatumiwa na manji kumchafua Mengi simnajua huyu muheshimia aliomba asiletwe kwenye mahakama ya JF sasa mnamleta ya nini huku,

mwacheni mengi kumwandika huku kwa mabaya andikeni na mazuri basi muheshimiwa Mengi jibu mashambulizi sasa.......
 
Less than two weeks after President Kikwete returned from London, portraying Tanzania as a safe place for British Investment, British investors Stewart Middleton and Sarah Hermitage are once again placed under threat by the conduct of Benjamin Mengi and his wife Millie Mengi.

Few in Tanzania are unaware of the issues surrounding the conduct of Benjamin Mengi against the British couple and the continuing harassment and intimidation that they have faced on a daily basis for the last three years because of Benjamin Mengi’s attempt to re-gain the lease to Silverdale & Mbono Farms.

http://archive.wn.com/2006/10/11/1400/litigationuk/

http://www.onlypunjab.com/investments/fullstory-insight-investments+stocks-newsID-3988.html

The couple returned from a month’s holiday in January to face further abuse of law, violence and intimidation from Benjamin Mengi, his wife Millie Mengi, Mengi’s employee Anold Kimaro and members of Mengi’s staff conduct being openly facilitated by Police Inspector Janet of the Moshi Police the officer securing Mr. Middleton’s committal to Moshi prison in July 2006 on allegedly ‘trumped up’ charges later withdrawn by the Republic.

Having failed to secure the investors departure from Tanzania by intimidation, and harassment together with, a vile campaign of alleged defamation by IPP Media, (http://www.pressmethod.com/releasestorage/10987.htm) the chief executive officer of which is Reginald Mengi, Benjamin Mengi’s brother, attention and abuse is now focused against Mr. Middleton’s wife Sarah Hermitage and the destruction of commercial crops grown by Mr. Middleton’s company Silverdale Tanzania on Silverdale Farm for export to the U.K.

During the week commencing 17th January, Benjamin Mengi and Anold Kimaro opened four ‘trumped up’ criminal charges against Mr. Middleton’s wife Sarah Hermitage. Once again, police Inspector Janet from the Moshi Police was placed in charge of the investigations.

On or around the 25th January, Inspector Janet telephoned an employee of Mr. Middleton’s in the presence of Mengi and stated that Mengi’s staff, ‘…….would now carry a bow and arrow on the farm in order to protect himself against Ms. Hermitage and that she should be careful what she does’. This was a very clear threat, from a senior Moshi police officer against Ms. Hermitage in that, not only was Inspector Janet not going apply the rule of law but that she was participating in its abuse. (www.pressmethod.com/releasestorage/10939.htm)

Ms. Hermitage, an ex Metropolitan and Kent police officer and non practicing Solicitor admitted to the Supreme Court of England and Wales states, ‘I have not been spoken to by any police officer, have no idea of the content of the allegations and cannot, comment on them’.

This continued harassment and intimidation is facilitated by the fact that Mrs. Millie Mengi refuses to remove a herd of some sixty cattle and goats from Silverdale Farm, which constitutes a continuing act of Criminal Trespass upon which the police refuse to act. In June 2006, Mrs. Mengi opened civil and criminal cases against Mr. Middleton alleging that he was killing and stealing her cattle and accusing him of forging a quarantine order placed on her animals in May 2006 by Zonal Veterinary Officer, Dr. Swai. (http://www.pressmethod.com/releasestorage/10937.htm).

Mrs. Mengi obtained, allegedly through abuse of due process, an ex-parte court order allowing her and her associates unfettered access to Silverdale Farm. The order has never been heard inte-partes and was issued prior to the actual hearing stated on the order. The High Court has so far failed to Review the order under an application filed under a Certificate of Urgency in November 2006 by Mr. Middleton’s lawyer. Seven other allegedly vexatious Plaints have been issued by Mr. Mengi and his wife against Mr. Middleton and his company Silverdale Farm. None of the Plaints discloses a cause of action; none have been dealt with by the courts in Moshi or dismissed. British M.P. for Thanet North, Mr. Roger Gale has placed a White paper before the British parliament asking for the suspension of aid to Tanzania until the Middleton’s land tenure is secured and Benjamin Mengi is brought to justice.

http://www.topix.net/content/prweb/2494816393037995317807769455903198687432

In early 2006, Mr. Middleton and his wife had to suffer the appalling sight of Mengi’s cattle dying from neglect and Foot & Foot Mouth disease where infected carcasses were, on the instructions of Mr. and Mrs. Mengi, deliberately left unburied around the area of the couple’s house. Mr. and Mrs. Mengi and their staff, continue to use the animals as a means of harassment and intimidation and as a means of destroying Mr. Middleton’s commercial interests in Tanzania.

The latest destruction of crops by the Mengi’s took place on the 31st January 2007 when Mrs. Mengi's adult cattle herd was driven into a two-acre plot of commercial Baby Corn by Mengi’s employee Mr. Salem. Salem has been banned from entering the farm on four occasions due to his persistent acts of perjury against Mr. Middleton and his wife. When approached by Mr. Middleton’s staff Salem attacked Mr. Able Ngoja, Mr. Middleton's Technical Farm Manager with a Machete and threatened to kill him.


Commenting on the incident, Mr. Middleton states, ‘on the 31st January 2007, an employee of Mr. Benjamin Mengi was found on my property having deliberately driven a herd of some forty adult cattle into a two acre Baby Corn plot grown for export to the U.K. The crop was destroyed. When approached by my staff the man threatened to kill my Technical manager Able Ngoja and came at him wielding a Machete. The man was apprehended and hand cuffed in full compliance with laws of Tanzania. The police were called but failed to attend for four hours. Mr. Salem was handed over to Inspector Janet from the Moshi Police who eventually attended the farm with Benjamin Mengi. She examined the damaged property and took Mr. Salem into custody. He was then released by Inspector Janet and allowed to go to the District Police Station and open criminal charges of assault against my staff. Mr. Benjamin Mengi was not present at the scene stated to reporters from IPP Media yesterday, one Jackson Kimambo that I had incited his staff to beat Mr. Salem. Once again IPP Media have reported the facts in a defamatory manner and have given me no right of reply’.

Mr. Mengi, not present at any stage of the incident stated to police that evening that the Masungu ‘foreigners’ should go back to South Africa where they belonged claiming that they were responsible for abusing Tanzanian Citizens. He further incited IPP journalist Jackson Kimambo to print defamatory material regarding the incident with the clear intention of inciting racial hatred against Mr. Middleton. Clearly, attempting to gain ‘political capital’ from the events he did not witness, Benjamin Mengi and his wife Millie Mengi, ultimately responsible for the acts of their staff simply appear, to be above the law in Tanzania.

For the second time, IPP media, the Chief Executive Officer of which is Reginald Mengi, is for the second time engaging in a defamatory campaign against British Investors in Tanzania. Radio 1, IPP Radio Network, announced on the evening of 3 February 2007 that British Investor Stewart Middleton’s staff had beaten up an employee of Mr. Benjamin Mengi brother of IPP Media’s CEO Reginald Mengi, on Silverdale Farm. The Radio did no site a case number, the issue of destruction of crops or, the fact that Mr. Salem was lawfully detained under the Penal Code of Tanzania or the fact that none of Mr. Middleton’s staff had been charged with any offence. Further IPP Media’s newspapers The Guardia and The Nipashe, reported similar articles paying no regard to the laws of defamation and stating that Mr. Middleton stood by and watched and incited his staff beat up Mr. Habib. A clearly cowardly act on the part of Jackson Kimambo, the journalist, the Managing Editor of the Guardian and IPP’s CEO Reginald Mengi who was placed on notice of the defamatory attack on Mr. Middleton by the former British High Commissioner to Tanzania Andrew Pocock in December 2005.

The question must surely be asked, why is there such reluctance on the part of the Tanzanian authorities to apply the rule of law to this situation and the continued abuse being vented against Mr. Middleton and his wife being, in the words of Dr. J. Ngasongwa, Minister for Investment and Empowerment in Tanzania, ‘bona fide investors in all respects with the full support’ of the Ministry of Investment. The Commissioner of lands for Tanzania refuses to rectify the Land Register to reflect their lawful ownership of their equitable lease holding of the farms and refuses to address correspondence sent to him by both the investors and, their Moshi Lawyer My Lymambo.

Mr. Middleton and his wife are not the only investors facing serious difficulties in the Kilimanjaro Region of Tanzania. It has been revealed this week by Paul Bebbington, Managing Director of Mufindi Tea Company, one of the largest agricultural investors in Tanzania and, the largest in the Kilimanjaro region, that Mufundi are closing their operations in the Kilimanjaro region in March 2007. Mr. Bebbington states that the company is closing its operations due to the problems the company are facing with the Co-operative Societies, (head lessors of their six commercial coffee farms) by which their land tenure has been rendered insecure.

A further blow to investor confidence was the suspension last week of the operations of the TPC Sugar Estates in the Kilimanjaro area due to worker unrest and violence.


Janet Lever
1st February 2007.
 
[

Tumeshuhudia hivi karibuni, alipoanza kumsakama Mkurugenzi wa NSSF, Bw. Ramadhani Dau kuhusu ununuzi wa maghara ya Quality Group.

Lengo lake yeye anachotaka pale wawepo kina Kimaro, Tesha, Massawe.

7.B Mengi amekuwa akikitumia CHADEMA kama mgongo wa kutaka kujiweka safi kisiasa na ndiyo maana katika uchaguzi uliopita aliweza kusaidia mamilioni ya shilingi kuhakikisha chama hicho kinafanya vizuri pamoja na mgombea wake wa Urais, Bw. Freeman Mbowe.

Mengi amekuwa na urafiki wa karibu na Mh: Mbowe na inadaiwa kuwa kama hatafanikiwa kuingia kama mgombea binafsi, basi mwaka 2010 chama hicho kinamsimamisha Bw. Riginald Abraham Mengi.

8. Hivi sasa ameanza katika harakati zake za kuipiga vita serikali ya Jakaya kikwete baada ya kuona viongozi wote wawili, Rais na Waziri Mkuu wakimpita kama yai bovu, baada ya viongozi hao kugundua janja yake na kutaka kuzidi kujenga jina lake kupitia katika uongozi wao.

bwana kiona pua,
naona umeamua kuadopt jina la marehemu conrad dastan"kiona mbali" aka mzee wa kiraracha ..anyway jamaa alikuwa kichwa hakuwa mwepesi kama wewe...kwenye hii post yako ya 5 ,ulikuja kutuambia hili au umekuja na jina jipya..
mimi binafsi kuna mambo mengi ambayo mengi simkubali...lakini nasikitika GARI LAKO SIPANDI especially hasa inapoonekana hoja yako ni ya kikabila zaidi ....LET US NOT TAKEN FOR A RIDE..
 
Msimamo mkali wa Mwalimu ulipinga mgombea binafsi? Rejea hotuba ya Mwalimu siku ya mei mosi aliyoitoa Mbeya 1995.
 
Kiona Mbali,

Hii makala yako ni UPUPU mtupu sasa unataka tujadili nini?
 
Mheshimiwa/Afande/Bwana/Mtukufu/Chief/Boss/Mhariri KIONAMBALI,
Nimekuita majina yote hayo hapo juu nikiwa na imani kwamba umewasilisha mawazo ya KUNDI la watu wanaofanana na hizo nyadhifa.

Kwanza nasikitika sana kwa wewe kutumia jina la mwenzetu Merehemu Kiona Mbali (Conrad Dustan) Mungu ampe nafuu huko aliko.

Nilichoona katika maelezo yako kwa kiasi kikubwa yanaakisi mawazo ya watu wanaotetea uhalifu na umechanganya hoja zote wanazozitumia ambazo naamini kwamba huziamini ila unaziwasilisha.
 
Waacheni watu waseme . Hapa kuna wanao jua sakata hili vyema . Kuficha ama kufuta haisaidii . Naupongeza uamuzi huu wa kurudisha hii thread . Safi sana .Sauti zetu wanyonge zimesikika . Hapa Mengi atatetewa na kupondwa . Mleta thread anaonekana kama yuko uchi mbele za umma uwanja wa Taifa . Tuendelee kukata issue hakuna kuogopa . Anaye tumiwa ataonekana maana wana JF si wajinga .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom