Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Kwa mtu anayemfahamu Mengi na biashara zake ukweli uko wazi kwamba kwa kipindi cha 1995 mpaka 2005 amekuwa kinyume kabisa na upinzani nchini. Vyombo vya habari vya Mengi particularly ITV vina nguvu sana-kama angeunga mkono CHADEMA mambo yangekuwa tofauti sana. Lakini ilikuwa kinyume chake.

CHADEMA bado haijaamua mgombea urais wake, kusema kwamba Mengi ni mgombea wa CHADEMA wakati hata sio mwanachama ni kutokututendea haki.

Baadhi mmeunganisha msimamo wa CHADEMA kuhusu pesa za NSSF ama shutuma za ndesamburo na Mengi na uchaga. Huku nako ni kutukosea haki na kuhamisha mjadala wa msingi. CHADEMA tumesimamia mambo mengi ya kitaifa na tunaendelea kuyasimamia. Wakati tunapinga ununuzi wa ndege ya rais sikusikia mtu akisema anayepingwa ni Mramba Mchaga. Wakati tunapinga ununuzi wa RADA haya hayajitokeza. Wakati tunamshambulia Lowasa kuhusu Richmond sijasikia yoyote hapa akisema kwamba huo ni UKASKAZINI.

Bottomline, hapa kuna watu wanataka kututoa kwenye kujadili masuala ya vyanzo(source issues)- kwenye suala la NSSF/PSPF-suala la msingi ni je, bilioni 83 za michango ya walipakodi ziliwekezwa vizuri au zilizochotwa kutokana na ufisadi? NSSF/PSPF/Manji nk wanawajibu wa kujibu?

Ndesamburo ameweka bayana madai ya rushwa na amesema chanzo ni nini, Mengi na Lowasa. Lowasa ni kiongozi wa umma, hajajitokeza kujibu. Rais amesema serikali haitajibu. Kuna nini hapa kinafichwa? Hili ni suala hapa! Tulijadili na kuhoji

Ya Mengi na Manji tuwaachie wenyewe wameshapelekana mahakamani kwa tuhuma za kukashifiana. Tusiingilie uhuru wa mahakama.

Lakini haya matumizi ya pesa za walipa kodi na tuhuma za rushwa; ni ya kwetu haya, tuyajadili kweli kweli...

CHADEMA si chama cha wachaga: rejea tamko rasmi la chama kuhusu suala hili http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php

Kwa hiyo mtanzania yoyote ana haki ya kuwa ndoto ya kugombea urais kupitia CHADEMA 2010: awe msukuma, awe mhaya, awe mchaga, awe mjita:wote karibuni ili mradi tu uendani na misingi ya falsafa ya nguvu ya umma http://www.chadema.net/nyaraka/falsafa.php na itikadi ya mrengo wa kati http://www.chadema.net/nyaraka/itikadi.php

JJ
 
very well said Mnyika .Lakini hatutatoka kwenye line kamwe . Tutabaki kusimamia issues
 
Hi JMnyika**
Unaposema UKASKAZINI unamaanisha nini, pliz define it!!
 
Maamuzi ya spika: Zito kasamehewa, Cheyo inabidi aombe msamaha kwa kumwambia Mh. Shibuda muongo. Mbona kesi ya Malima na Mengi imeharishwa kutolewa uamuzi hata baada ya ripoti kukamilika?
 
Ukaskazini ni dhana iliyoanzishwa humu kwenye JF ikimaanisha kanda ya Kaskazini ikibeba dhima ya ubaguzi, ukabila na upendeleo.

Ni hoja mufilisi ambayo ilizuka baada ya wajumbe kadhaa kushindwa hoja ya msingi na kuamua kudandia kitu tofauti. Awali walianzisha hoja kwamba CHADEMA ni chama cha WACHAGA, wakakosa ushahidi kwa kuwa wachaga ni wachache kwa ujumla katika CHADEMA ukilinganisha na makabila mengine(rejea http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php )Wakabili hoja na kusema CHADEMA ni chama cha watu wa Kilimanjaro napo wakakosa ushahidi wa kuthibitisha madai yao. Baada ya kushindwa hapo wakaja na hoja mpya kabisa kwamba CHADEMA ni chama wa watu wa kanda ya kaskazini. Hapo ndipo dhana ya UKASKAZINI ilipoanza kujadiliwa. Lakini neno kanda ya kaskazini lilikuwepo hata wakati wa mkoloni.

I just used in the context ya Lowasa na Richmond. Soma vizuri post yangu utajua kwa nini niliandika hivyo.

Turejee kwenye masuala ya msingi ya hii thread, hili litatutoa kwenye mstari.

JJ
 
Kwanza Nikupongeze Kijana Wangu Mnyika Kwa Uwezo Wako Wa Kutetea Hoja. Hakika U-mwanasiasa Japo Kuna Huyu Lunyungu Nahisi Yeye Ni Bendera Inayofuata Upepo.

Mengi Yamezungumzwa Lakini Nataka Kutoa Mwanga Katika Suala Moja. Unajua Enzi Zetu Sisi Siasa Ilikuwa Ni Ya Watu Ambao Kwa Kweli Wana Uchungu Sana Na Hii Nchi Na Sio Kama Ile Nji Ya Mrema.

Wanangu Mmekuja Katika Kipindi Kibaya. Taifa Limekumbwa Na Majambazi Wa Siasa. Watu Walio Amua Ima Kwa Wao Kushiriki Au Kwa Kuwatumbukiza Watu Kwenye Siasa Ili Wao Wafadike Kwa Namna Moja Au Nyengine. Hili Limeonekana Na Linaonekana..japo Kama Chief Mwenye Busara Nisingependa Kulisema Hapa.....majina Tunayo.

Sasa Basi Nirudi Kwenye Mada...katika Yaliyosemwa Ni Lazima Mkumbuke Kwamba Wako Wengi Sana Ambao Waliingia Kwenye Vyama Dakika Ya Mwisho Wakapewa Vyeo. Kuna Watu Waliingia Hata Kwenye Vyama Ili Wapate Ubunge. Ninaposema Muda Namaanisha Miaka Kama Mmoja Hadi Miwili Na Hata Mnyika Anawajua.

Watu Hawa Wapo Kila Sehemu Toka Cuf, Chadema Hata Ndani Ya Baba Yetu Ccm.hii Ni Siasa.mwanangu Mnyika Usikatae Yasemwayo Labda Kama Wewe Ni Msemaji Wa Chama Au Umepewa Ruhusa Na Chama Kuzungumza Hili.

Kwa Kumaliza Ningependa Kunukuu Kauli Ya Mmoja Wa Wachangiaji Kwamba Ni Vyema Mkaweka Interest Za Watanzania Kwanza, Huku Mwanza Hawa Wadogo Zako Wanaweza Potea Mkifanya Mchezo.

Wenu,
Chief Masanja.
 
Jamani!

Nina sababu kadhaa kuthibitisha ukweli wangu.

4. Amekuwa akijitahidi kuwa karibu na jamii, tofauti na wafanyabishara wenzake ili kuonekana kuwa ana mapenzi ya dhati na watu wa hali ya chini na kufikia eti kula chakura na vilema, mazeruzeru na viziwi na baadae kupigwa picha.

Sasa Mheshimiwa anawasadia watu kwa chakura harafu anawapiga picha kutolewa kwenye ma TV, magazeti yake na pengine kuoneshwa kwa wafadhiri na nyie mliokuwa Uingereza mnaweza siku moja mkaona mikanda hiyo, kwamba yeye anakubalika kwa lengo la kupata mapesa ili aweza kuichukua nchi.

Jamani Tanzania tuna matajiri wengi tu, lakini ambao hawapendi makuu, tena wana mapesa mengi na mfano halisi ni Bw.Said Salim Bakhresa, huyu jamaa kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana mwaka jana mwezi wa nne kutoka TRA, Bw. Bakhresa ndio alikuwa akishika namba moja, lakini kikubwa kwambak kuna watu Tanzania hawamjui huyu bwana na badala yake wanaojulikana zaidi ni watoto wake.

Huyu mzee ana uwezo wa kufanya jambo lolote lile, kuwa na TV,kutoa misaada ya mamilioni ya shilingi, lakini amekuwa kimya na biashara zake na kwenda msikitini. Hivi kwa nini huyu mengi hasiwe kama huyu jamaa.



Nimeonesha kwa red color, kukuthibitishia jinsi ulivyo na ufahamu finyu tena mfupi kuliko hata wa PIMBI wa magazeti ya sani!

Yaani umedraw attention ya watu kwa heading nzuri lakini ndanimo ni udadu tena ufukunyuku mtupu!

Umebadili jina, kwani ungetumia lakwako la sikuzote Mswahili, ulihofunini ilhali ujumbe ni uleule wa kuthibitisha umekwenda shule za vichochoroni?

Unadiriki kujifunua nguo kutuonesha uchi wako hapa....Eti watanzania matajiri wamwiige huyo bosi wako kupeleka pesa msikitini(si umeandika mwenyewe) unatufundisha ualkaida kufadhili ulipuaji mabomu?

Wafikiri kuwa tajiri then kuweka hela kwenye mifuko makalioni ndo busara, huyo Mengi kazitumi akuwafariji hao maskini,....wewe unataka azipeleke kanisani(kama ilivyoainisha) HUONI KWAMBA WEWE UNA CHEMBEHAI ZA UDINI TENA UKABILA NDANI YAKO?

Amakweli ukistaajabu ya ........utaona ya ..........! U'r Lost Onto The Bush!
 
Hizi ndiyo faida za kuacha threads bila ya kuzifuta wala kuleta maneno mengi . Watu wanasema na kutoa Elimu hapa , safi sana na mimi naendelea kuwasoma .Tuendelee kwa kweli .Ila huyu jamaa na mada yake nadhani katumwa si bure kabisa .
 
Miaka mingi sijaingia humu japo ni mwanachama wa siku nyingi, ila huwa nawasoma sana, leo hii mikono imeniwasha kweli kweli nahapa nilipo natetemeka, moyo unanidunda, saa yoyote naweza nikafuatwa na AMBULENSI, baada ya kusoma eti Viongozi wa ngazi za juu wa tanzania wapo busy kuwaletea watanzania maendeleo hii -should be a Joke!!! wewe kiona UKINGONI hebu tueleze huo ubize kwaza upo wapi? na wa nini? Usije ukawa unamsifia jongoo kuwa ana miguu mingi kumbe mwendo wake ni taratibu, Ubize wa viongozi hao uliowataja ni sawasawa na mwanamme kuoa mke mzuri lakini hata kupika hajui, kuchota maji kwa ndoo hawezi, sasa wa nini? wa kazi gani mke ambaye hata kitandani hana maana yoyote, mke anayejiremba kutwa nzima mume ukirudi chakula hakuna. ndugu chunga vidole vyako unapoandika tena kuwa muangalifu sana haswa unapoandika jambo la kisiasa linaloihusu Tanzania. Serikali ya JK ni serikali inayojirembaremba tu kwamba inataka kuwaletea maendeleo watanzania, lakini si kweli, Serikali hiyo ikishajiremba kupitia vyombo vya habari huwa haitosheki bado inatumia mamluki kama nyinyi mje kuandika vioja humu, tena serikali hiyo inafikiria watanzania wa leo hawana upeo wa kuelewa,kuchanganua, na kuona muelekeo wa mambo na ndio sababu inawatumieni watu kama KIONA KARIBU, sasa rudisha salamu kwa Serikali Ya JK Mwaambie hivi, WATANZANIA WA LEO ASIWAFANANISHE KABISA NA WATANZANIA WA TANU YOUTH LEAGUE Wa miaka ya 70, sisi ni watu wengine kabisa na karne yetu tunajua mambo.
Sasa nataka utueleze hayo maendeleo aliyoyaleta JK au anayotegemea kuyaleta ni yapi?
Nchi ilikuwa na matatizo makubwa sana ya umeme, na matatizo yaliyojitokeza kuhusu kampuni ya RICHMONDS yanajulikana, lakini Ili JK atufunike blangeti la mbao muda mfupi kabla ya mvua za vuli kupamba moto, eti akatutangazia tatizo la umeme linakaribia kwisha, au kupungua, yaani JK anadiriki kututangazia kumalizika kwa tatizo la umeme kwa kutumia vipimo vya hali ya hewa? Hivi haya ni maendeleo jamani au anaturudisha nyuma miaka kibao? sasa mimi binafsi mpaka sasa sishawishiki kabisa na serikali ya JK kwamba itatuletea maendeleo, serikali ya JK haina muelekeo wowote si wa maendeleo wala chochote, zaidi ya kubeba wimbi la wafanyabiashara, kuwatembeza dunia nzima kwa pesa za walala hoi, eti anawatambulisha au anafanya uhusiano au sijui ana maana gani, Kwani wafanya biashara hao waliwezaje kufanya biashara bila ya kujua soko la bidhaa zao, ilikuwaje wafanye biashara bila ya soko, mimi sio mchumi lakini kwa kutumia akili yangu tu siwezi kuanza kufanya biashara bila ya kutafuta soko, na kutafuta contacts na wafanya biashara wa nje na ndani ya nchi, huu ni upuuzi.

Ndugu,naomba ueleze maendeleo ya nchi tangu JK aingie na kundi lake serikalini.

Ukiwa kama mtanzania unashabikia na kusema eti JK au Lowasa hawakumpatiliza Bw Mengi kwa kuwa wamegundua Janja yake, utakuwa unauonyesha UMAMLUKI wako dhahiri, na Umamluki ukiwa hadharani kiasi hiki basi tutauita UMAMLUKI THABITI ambao ndio uliosababisha Rwanda na Burundi kuchinjana. Be carefull!!!!!!!!!
Mengi anasaidia watu kivyovyote vile, akiwa anatolewa katika vyombo vya habari au la, lakini msaada umefika na umesaidia. so sioni point hapo ya msingi.
Kiona karibu kusema Vyombo vya habari havitilii mkazo kuonyesha maswala ya serikali na zinamuonyesha Mengi Peke yake, hili bado sio kosa kwani yeye ndio anamiliki vyombo hivyo, na anatangaza biashara yake na anajitangaza yeye mwenyewe na atagombea nafasi yoyote ile ya serikali kwa mujibu wa katiba na sio kwa mujibu wa kiona karibu. Na jambo la kuonyesha ktk TV zake kuwa anakula na vilema, au amesaidia walemavu hili ni jambo kubwa sana hata katka seriakali kwa sababu serikali ndio ina walemavu ndani ya Taifa, Na kwahili Mengi atakuwa ameisaidia sana serikali maana serikali haiwezi kula na vilema Serikali ya JK inakula na wakina MANJI na RICHMONDS Na RADA Tena inakula na watu MIJIZI KWELI KWELI Inakula nao bila hata Kunawa.
JK mwezi wa Ramdhani alikula na vikundi malimbali na hii nayo unaiitaje?
sasa siku nyingine uje na hoja za maana, na kama ungekuwa karibu yangu hapa ningekunasa kibao.
usomaji mwema
Kamua baba mpe vidonge vyake huyo
 
Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa tumekuwa tukiona magazeti ya bwana Mengi yakichukua a dramatic twist katika story zake:

Mfano amekuwa akimuandama sana Yusuph Manji kwa kurudia stori hiyo hiyo kupitia gazeti la THIS DAY akidai ni crook business man ambae ana shaddy deals na mamlaka kadhaa.

Amekuwa akiiandama sana taasisi ya NSSF kwa kuwa na the same story kila siku tangu gazeti lilipoanza akizungumzia kitu kimoja tu cha ubungo plaza akidai limenunuliwa na NSSF kimakosa.

Ameiandama sana hii kampuni ya madini inayodaiwa kuwa na link na ccm. Sasa kumekuwepo na malalamiko mengi kuwa amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kujijengea himaya ya kuogofya watendaji wa serikali huku wengine wakidai ana misuse his media outlets to serve his personal benefits.

Mimi binafsi nikiangalia naona alianza vizuri na vyombo vyake ila siku kuna changes nyingi katika operations zake manake sawa mfanyabiashara haanzishi mavyombo mengi kama yale bila kuwa na personal benefits lakini anakwenda to the extreme kwa sasa.

Hii ni kesi ya tatu kuisikia ambayo Bwana Mengi ameshitakiwa manake ya kwanza ni ile ya YUSUPH MANJI anaedai bilioni moja na pesa nyingine kadhaa, ya pili ni ile ya mhariri wa daily news mkumbwa Ally ambae nae ameshitaki kwa kudai kukashifiwa na sasa hii kwa hiyo unaona kama wote wakifanikiwa mengi kwisha!

Mimi naungana na Bw. Kiona mbali kwamba huyu bwana personal benefits zake ni kuhakikisha kuwa anaukwaa urais katika miaka ijayo.

kwani ameanza kujijenga na kuichafua serikali pamoja na taasisi zake kupitia magazeti yake ya udaku kwa lengo na kujifanya anafanya investgation reporting.

Lakini akumbuke bw mengi kushindana na serikali iliyoko madarakani ni sawa na kuchezea makala ya kisu wakati mwenzako ameshika mpini.Hakuna mfanyabiashara atakaeqweza kufanikiwa kwa kushindana na serikali,.

Lakini kikubwa ambacho rafiki yangu mengi anachohitaji ni kuabudiwa kama sultani, jambo ambalo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mawaziri wale wanaotoka kanda ya kaskazini, lakini wale ambao wanatoka kanda nyingine wamekuwa wakimuona kama cocroch.

Nadhani watu wa chadema wanampotosha bw. mengi, lakini ukweli unabaki pale pale huyu bwana aiche serikali ifanye mambo yake a yeye afanye biashara zake, kamwe hawezi kuongoza nchi ya Tanzania kama hukuchaguliwa na wananchi, kamwe ikulu ya nchi haiwezi kuwa haidery plazza gorofa ya tano.

Pia ikumbukwe bw mengi anamshumu bw. manji kwa kuchota mapesa ya nssf, je yeye mengi uchafu wake wa kuchukua pesa za serikali ukitajwa hapa nyie chadema na vibaraka wake mtakimbia.

Hivi karibuni alijipatia mabilioni ya pesa za madini kwa kisingizio cha CCM, nyie mnafahamu, mwamibie aingie humu atoe maelezo na siyo kumtolea maelezo.

We nyika jitahidi nadhani unataka akusaidie kukupatia pesa ya kuwania tena ubunge, jitahidi kujipendekeza kwake.

Lakini all in all, huyu jamaa ni bepari mkubwa kuliko huyo manji.
 
Mazungumzo ya Mengi kwa waandishi wa habari katika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam tarehe 32 Machi 2006,alisema kuwa hana ugomvi wala hakuwahi kuwa na ugomvi au uhusiano wa kibiashara na Manji au Quality Group Limited.

"Hivi karibuni vyombo vya habari vimeandika kuhusu suala la mikataba ya mauzo ya maghala ya Quality Group kwa NSSF kama linavyoandikwa na This Day na Kulikoni (magazeti ya Mengi)".

"Baadhi ya watu na viongozi kadhaa wamedai kuwa suala hili ni ugomvi na malumbano binafsi ya kibiashara kati yangu na Manji, lakini hawajaweka bayana ni ugomvi gani huo".

"Nakubali vyombo vyangu vya habari (This Day na Kulikoni) vimendika habari kuhusu uhusiano kati ya Quality Group na NSSF, lakini mimi ni mmiliki na si mwandishi wa habari wala mhariri wa vyombo hivyo."

"Magazeti hayo ni ya habari za uchunguzi wa mabaya na mazuri, kazi yangu ni kuyapa sera za utendaji kwa ujumla na si maagizo kuhusu waandike nini au kuhusu nini."

"Sihudhurii mikutano ya uandishi au uhariri na ninasoma magazeti hayo baada ya kuchapishwa kama wafanyavyo watu wengine. Kama mmiliki, lingekuwa ni jambo la kuwadhalilisha waandishi iwapo ingewaingilia katika shughuli zao."

"Pamoja na hayo, mimi ni mmiliki wa magazeti mengi na vituo vya televisheni na redio. Ninazo shughuli nyingi za kibiashara. Hata ingekuwa hizi shughuli nyingine hazipo, nisingeweza kupata muda wa kushughulikia uhariri na uandishi wa vyombo vya habari ninavyomiliki hata kama ningependa kufanya hivyo."

"Hivi vinaongozwa na wahariri watendaji. Vyombo vya habari ninavyomiliki siviingilii. Ni vyombo huru."

"Baada ya kusoma magazeti hayo ninachoona mimi ni vita baina ya Quality Group na wanyonge wafanyakazi wa Tanzania wanaofunga mikanda yao kwa miaka mingi na wengine wao wakidhoofika kiasi cha kukuta kilichobaki cha kufunga ni uti wa mgongo tu, wakati wachache wanalegeza mikanda yao."

"Kila mwezi mishahara yao inakatwa kwa ajili ya mafao yao ya uzeeni, lakini sasa wana wasiwasi wa kuyapata wakati ufikapo kwa sababu kulingana na taarifa zilizopo fedha zilizolipwa kutoka NSSF ni zaidi ya sh bilioni 47.5 kiasi ambacho kwa vyovyote vile ni kikubwa sana."

"Suala la kujiuliza ni je viongozi wanaodai kuwa suala hili ni ugomvi binafsi wa kibiashara kati ya Mengi na Manji wapo madarakani kwa maslahi ya mtu mmoja au maslahi ya Watanzania wote hasa wengine wa Tanzania?"

"Na je, inakuwaje waandishi wanaojitahidi kuwafahamisha Watanzania masuala yenye utata washawishiwe kinyume na maadili kuacha kufanya hivyo na kutishiwa usalama wao? Haya yametokea. Usalama wangu na waandishi wa magazeti hayo umetishiwa na taarifa zimekwishatolewa Polisi," alisema Mengi.

Swali la kujiuliza Je yeye hakuna pesa yoyote aliyochukua kutoka Serikalini na kwenye makampuni ya madini? ambayo ni jamsho la wananchi na wengine wanafia katika mashimno kule melerani?
Natoa ukumbi ndugu zangu, huyu ambae hasemi maneno mawili bila ya kutaja jina la mungu, lakini ni msaliti mkubwa wa wananchi wa Tanzania, tena anakura hadi pesa za walemavu anazopewa msaada kutoka nje, je hili mnalijua nyie?
------------------
 
SEHEMU YA UAMUZI WA SPIKA SAMUEL SITTA

8.0 TUHUMA KWA WABUNGE KUPEWA RUSHWA
8.1 Kabla ya Kamati kuwasilisha taarifa yake kwangu, mjumbe wa Kamati Mhe. Ndesamburo alielezea mkasa ambao ulihusisha suala la rushwa.

8.2 Kwa bahati mbaya, katika suala hilo, Mhe. Ndesamburo katika nyakati mbalimbali, amelitolea kauli ambazo zinakinzana. Kwanza aliieleza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa Bw. Mengi alimlalamikia kwa njia ya simu kwamba:-

"anaamini Bw. Mengi Kamati hiyo haingemtendea haki Bw. Mengi, kwa kuwa kulikuwa na vitendo vilivyoashiria maamuzi ya Kamati kuingiliwa na Serikali, na pia alikuwa na taarifa na ushahidi kuwa Bw. Mengi aliitwa na Waziri Mkuu ambaye alimshauri ajitoe katika ‘kesi' hiyo, kwa kuwa Wabunge wamehongwa na Bw. Manji, hivyo hatashinda."

8.3 Alipokuja kuniona ofisini Dar es Salaam, Mhe. Ndesamburo akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Nh'unga na Makamu Mhe. Masilingi, tarehe 10 Januari, 2007 mimi nikiwa na Naibu Spika, alitueleza nia yake ya kujiuzulu ujumbe wa Kamati ikiwa Kamati haitawahoji Bw. Mengi na Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nilimjibu kuwa, ikiwa tuhuma ni dhidi ya Wabunge wengi au dhidi ya Kamati, isingewezekana Wabunge waitwe na kuwahoji, kama mashahidi wakati wao wenyewe Wabunge ndiyo watuhumiwa. Isitoshe kwa nini aamini mazungumzo ya simu kwa jambo zito kama hilo?

8.4 Hata hivyo siku hiyo hiyo akaniletea barua yake ya kujiuzulu ujumbe wa Kamati ambamo alidai umetokana na:

"(a) kuwepo kwa madai kwamba Wabunge wamepewa rushwa na Manji na Kamati kutofuatilia suala hilo kujua ukweli wa mambo kabla ya kesi ya msigni kuamuliwa."

"(b) kuwepo kwa mazingira ya Mhimili wa Utawala (Executive) kuingilia Mhimili wa Bunge (Legislature) ambayo ni kinyume na utawala bora na mgawanyo wa madaraka."

8.5 Lakini taarifa za vyombo vya habari tarehe 11 Januari, 2007 vikinukuu aliyoyasema kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana yake zilidai kuwa, Mhe. Ndesamburo alieleza kuwa, wenye kutiliwa mashaka ya kula rushwa ni wanakamati wenzie na siyo Wabunge "wengi" kama alivyonieleza ofisini au "wabunge" bila kubainisha kama alivyoniandikia. Pia alielekea kusema kuwa alikutana na Bw. Mengi kuyapata maneno na siyo kwa simu tu kama alivyotamka awali.

8.6 Kwa hiyo, ili kuondoa utata, nilimwandikia barua aweke bayana zaidi tuhuma zake, ili niweze kuamua hatua za kuchukua. Ikiwa ni wajumbe wa Kamati ndiyo watuhumiwa wa rushwa nilikuwa na uwezo wa kuagiza utaratibu wa Kibunge utumike katika kuchunguza. Lakini ikiwa ni "Wabunge wengi" au "Wabunge" kwa idadi isiyo wazi isingewezekana kutumia utaratibu wa Bunge. Hii ni kwa sababu ya msingi kwamba, Bunge/Wabunge wasingeweza, wao wenyewe wakiwa ni watuhumiwa, kujichunguza na kujisafisha au kujihukumu.

8.7 Barua ya Mhe. Ndesamburo aliyonijibu tarehe 24 Januari, 2007 bado imeendeleza utata kwa kudai kwamba, wanaohisiwa kula rushwa ni Wabunge kwa ujumla. Habainishi kwamba, ni Wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, au Wabunge wengineo nje ya Kamati hiyo. Wakati wote huu suala hili la tuhuma za Mhe. Ndesamburo kuhusu rushwa limeendelea kuchukuliwa kisiasa na chama chake cha CHADEMA ambao wamenukuliwa na vyombo vya habari wakisema kwamba wamepeleka barua kwa Mhe. Waziri Mkuu. Aidha, wamekuwa wakizungumzia uvumi kwenye mikutano mbalimbali ya wananchi.

8.8 Taarifa za karibuni zinaelezea kwamba, Mhe. Ndesamburo sasa anachapisha kitabu kuelezea jinsi suala la Bw. Mengi na Mhe. Malima lilivyoshughulikiwa vibaya na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

8.9 Katika hali inayozidi kukanganya katika barua yake ya tarehe 24/1/2007, Mhe. Ndesamburo akinijibu kuainisha tuhuma amedai kwamba:
"Na hata katika barua yangu sijamtaja Yusufu Maji aliyenitukana magazetini. Mini nilimtaja MANJI tu ambaye anamjua Bwana Mengi na huenda siyo Yusufu Manji."

8.10 Tuhuma za "Wabunge kupewa rushwa" ni nzito na ukizingatia kuwa zimetolewa na Mbunge mtu mzima na mzoefu, haziwezi kupuuzwa hata kidogo. Kutokana na sababu hiyo, na kwa kuzingatia ukweli kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi;

8.11 Na kwa kuwa, kwa kosa la jinai Wabunge hatuna kinga yoyote, na kwa kuwa kuna chombo mahsusi cha kisheria cha kushughulikia uchunguzi wa rushwa, niliamua kumwagiza Katibu wa Bunge awasiliane kwa maandishi, na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Rushwa (TAKURU) ili uchunguzi ufanywe kubaini ukweli, na hatimaye kuachia sheria ichukue mkondo wake.

8.12 Katibu wa Bunge aliandika barua tarehe 26 Januari, 2007 kukabidhi suala hili kwa TAKURU. Aidha, kwa nakala ya barua hiyo, Mhe. Ndesamburo amehimizwa kutoa ushirikiano kwa TAKURU, ili ukweli kamili ufahamike.

8.13 Aidha, nimemwagiza Katibu wa Bunge anipatie ushauri kamili wa uhalali au vinginevyo, wa Mhe. Ndesamburo akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge, kufanya mawasiliano yasiyo rasmi na mmoja wa wanaochunguzwa wakati uchunguzi unaendelea.

8.14 Ingewezekana kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatilia jambo hili, lakini nimeona si hekima kufanya hivyo kwa sasa. Nachelea kuchukua hatua zozote ambazo zitaonekana kumwekea vipingamizi Mhe. Ndesamburo, hasa kwa sababau tuhuma za rushwa anazielekeza kwa Waheshimiwa Wabunge wenzake.

9.0 UAMUZI (RULING)
9.1 Kwa kuzingatia matokeo ya uchunguzi na ushauri wa Kamati ya Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, na pia kwa kuzingatia ushauri wa wajumbe wawili wa Kamati hiyo waliotoa mawazo tofauti na pia uchambuzi na ufafanuzi nilioutoa hapo juu, na vile vile na kwa kuzingatia mwenendo wa suala lenyewe na yote yaliyojitokeza wakati Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikifanya uchunguzi wake;

9.2 Na kwa kuzingatia uzito wa tuhuma za Mhe. Malima dhidi ya Bw. Mengi zimemuathiri Bw. Mengi zenye athari ya kumgonganisha na viongozi wakuu wa nchi;

9.3 Na kwa kuwa, kitendo cha Bw. Mengi cha kukosea utaratibu kwa kutumia lugha ya kuudhi kukanusha matamshi ya Mhe. Malima kupitia vyombo vya habari na kuwa pia imemuathiri Mhe. Malima;

9.4 Na kwa kuwa, itakuwa ni kwa manufaa ya wahusika, ambao ni watu maarufu kwamba, suala hili limalizwe na kufikia mwisho wake;

9.5 Na kwa kuwa, linapotokea suala lolote Bungeni au kwenye Kamati ya Bunge, suala hilo linapaswa liamuliwe kwa mujibu wa utaratibu za Kibunge (Parliamentary usage and practice);

9.6 Na kwa kuzingatia kuwa, malalamiko husika hayakuwa ni ‘kesi' kati ya Mhe. Malima na Bw. Mengi, bali ni malalamiko ya wote wawili, kila mmoja akimlalamikia mwenzake, yaliyowasilishwa kwangu kwa utatuzi;

9.7 Na kwa kuwa, busara zangu zinanituma kwamba, njia nzuri na iliyo bora ya kuyashughulikia na kuyamaliza malalamiko ya watu hawa wawili, ni kwa usuluhishi (reconciliation) kati yao; kwa hiyo basi, ili kuleta suluhu hiyo, naelekeza kwamba:

(i) Katibu wa Bunge awasiliane na wahusika ili tukutane ofisini kwangu Dar es Salaam, kwa siku nitakayopanga na iliyo muafaka kwao tuweze kuongea pamoja kwa madhumuni ya kukubaliana nami, utaratibu muafaka, utakaojenga suluhu endelevu baina yao na kuepuka hatari ya suala hili kushamirisha makundi yaliyochomoza ambayo yameonekana kuibua masuala ya udini, rangi na tofauti za vipato katika jamii.



Uamuzi huu nimeutoa Dodoma leo tarehe 08 Februari, 2007.



Mhe. Samuel J. Sitta (Mb.)
SPIKA WA BUNGE
 
Mtetezi,
Hivi mengi huyu ni mwandishi wa habari au mhariri wa magazeti ya This day na Kulikoni? Hebu tueleweshe kwanza uhusiano wa Mengi na habari zinazoandikwa na magazeti hayo.
 
Mtetezi,
Hivi mengi huyu ni mwandishi wa habari au mhariri wa magazeti ya This day na Kulikoni? Hebu tueleweshe kwanza uhusiano wa Mengi na habari zinazoandikwa na magazeti hayo.

ahaha mjukuu wangu,

habari za jioni kama si asubuhi kama huko kwa bush mjukuu wangu.mie ni mzee wako chief masanja wa majebele.umenifurahisha sana ulipouliza suala kaa huyu bwana ni muhariri au ni muandishi.

nakupa mambo mawili ya maana mjukuu wangu kama sio mwanangu.mengi ni anakaa katika vyeo vyote japo sio kimwili. habari zote zinazoandikwa humo kwa upande mmoja au mwengine zinahusiana moja kwa moja na yeye. kwani mambo yote yanatokana na yeye pia kutaka yajulikani.

nirejee maneno yaliyosemwa na kijana mmoja jina limenitoka , kwamba bwana mengi anania ya kugombea uraisi na akitetea hoja hiyo kwa maneno kama yako. unajua kuna watu wanashindwa tofautisha art yao ya kuandika na maneno ya maboss zao na ndiyo maana mjukuu wangu mmoja anaitwa maulid wa kitenge inasemekana alifukuzwa kwenye chombo baada ya kumsifia mmoja wa mahasimu wakubwa wa huyu bwana. sitaki kusema kwamba alifukuzwa kwa kuwa mengi na manji wana tatizo lakini hapa bwana mkubwa alivaa viatu vya uwariri na kusahau kwamba bwana kitenge ni mwandishi wa habari.

hili pia nimelisikia kwenye tanzania daima pia , wakati fgualani likiwa taraji kutokea baada ya waandishi fulani wa gazeti hili kushukiwa kwamba wana ......ndani yao. hili limesababisha hadi muandishi mmoja mahili mwenye sifa ya kweli ya kuondoka akiwa anaona mazingira magumu ya kufanya kazi.

hivyo basi, swali lako ni zuri.laweza kuwa na ukweli kimaelelzo kama mimi nilivyoangalia nguvu ya hoja au laweza kuwa na uongo kwa kuangalia kwa mtazamo wa ndani.lakini mengi si muandishi wala muhariri wa gazeti hili.

mzee wenu,

chief masanja wa majebele
 
Majebele Masanja Chief ama Chef magazet ya This day ba kulikoni si ya Mengi ni mali ya Mtandao wa JK an EL . Sasa kazi kwako .Nia ya haya ni kuwabomoa wasio wana mtandao na Mengi ni carrier pekee ili kuwazuga washinda hoi .
 
kampuni ya IPP MEDIA ambayo mwenyekiti mtendaji wake ni Bw. R. Mengi ya anza kampeni kwa kutumia vyombo vyake vya habari kwa kuanzisha kipi kinachoitwa ''Mpaka Kieleweke'' RADIO ONE naneno yanayo tumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw. freeman Mbowe CHADEMA ''chama cha demokrasia na maendeleo''

Maneno hayo yana ashiria nini kwa mtizamo wa wengi nikama uanzishe kipindi kinachoitwa ARI MPYA, KASI MPYA, NA NGUVU MPYA wewe ni CCM 100%

Bw. Mengi huanzisha kwanza vipindi vyake kwenye Radio kupima Joto alafu kuweka kwenye TV

Ebu wachambuzi wa mambo liangalieni hii kwa unandani mkilinganisha na tuhuma zilizoshatoka kuhusu Mengi na Mbowe.

Naomba kutoa hoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom