Mchungaji Shayo: Michango ya harusi ni ushamba; usitoe mchango wowote

Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.

Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.

View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
​
Yupo sahihi kabisa
 
Pia, sadaka ni jambo la kijamii, mnatoa kwa a common goal, kuendesha kanisa, kueneza dini, yenu wote, pamoja, jambo la jumuiya hiyo nzima, si sawa na harusi, jambo la mtu binafsi.
Kwani michango ta harusi inatolewa bila malengo mkuu?
 
Naunga mkono hoja
ghalama za harusi zinawahusu waowaji na waozaji tu:
Wengine wanaweza kutaarifiwa na kama kuchangia kuwe kwa matakwa Yao:
Majirani wanakuletewa kadi lukuki huku hata mwoaji humjui:
mpaka sasa Nina kadi zaidi ya Kumi na Tano za majirani Ndugu na marafiki na wafanyakazi wenzangu:

Nikiwa fare inabidi nitumie milioni sio zaidi ya mbili kwa michango tu kwa Mwezi mmoja;
Tena mwingine unasalimiana tu naye barabarani utakuta anakuambia, Naona wiki ijayo nitakulelea kadi ya mchango wa harusi yangu au mdogo wangu nk.
Imekuwa usumbufu na ghalama juu:
Alika watu wako wa karibu na kadiria sherehe yako:
Watu Nyakati hizi tuna mambo mengi sana yanayo hitaji pesa
 
Kwani michango ta harusi inatolewa bila malengo mkuu?
Kwani wapi nimesema lolote linafanyika bila malengo?

Kutoa sadaka kanisani ni sawa na kulima kwenye shamba la kijiji vha ujamaa, unachangia jambo lenu wote pamoja.

Mchango wa harusi ni kuchangia jambo la mtu mmoja.

Huelewi wapi?
 
Bila ya ku endorse mfumo wowote wa kuchangiana, nataka kuijua jamii yetu zaidi tu.

Wabongo wengi mbona wanachangia sana harusi, lakini sioni watu kuchangiana sana kwenye suala la kusoma?

Ina maana jamii yetu inathamini sana harusi kuliko kusoma?

Kuna kijana kutoka familia isiyojiweza kiuchumi amepata scholarship kusoma nje ya Tanzania, this is a big deal for him, anaenda kubadilisha maisha yake na anaweza kuwa na mchango mkubwa sana kwa jamii, anahitaji msaada kidogo tu nauli na pesa ndogo ya kuanzia, lakini anapata tabu sana kufikisha lengo.

Nimemchangia kama $1,500 lakini watu wengine ni kama wamempotezea na siku za safari zinakaribia.

Huu ungekuwa mchango wa harusi angepata watu wengi zaidi.

Tatizo liko wapi?
Mfumo tuliokuta kwa wenzetu waliotutangalia pengine ndiyo imeathiri mambo mengi

Kwenye upande wa huyo kijana jamii ya kibongo kawaida tuu kuna ubinafsi, na umimi linapokuja suala la maendeleo ya mtu mwingine ikiwa mtu kuomba ada, matibabu, ama kuinuana kiuchumi

Jamii itajenga maswali kwamba huyo mtoto wake nikimsaidia je fadhila zitarud vipi ??

Jamii hiyo hiyo inajenga swali angekuwa mwanangu angesaidiwa ?

Jamii hiyo hiyo itajenga maswali kuhusu tabia za huyo kijana na wazazi hata watangulizi wao ili tuu wapate kushinda wasichangie

Badala yake tumekuta mfumo ya kuwa changia harusi kwa sababu mwanao nae ataoa hivyo jamii itakutenga usipofanya hivyo

ama mtu kafariki mtu anatokea huko ama kikundi na kusimamia kila kitu ilihali walishindwa fanikisha matibabu yake

Hivyo mm nasema kuwa jamii yetu ili ikusaidie inataka kuona msaada huo utarudi vipi kwamba hawatoi kama sadaka ama bure kuna mazingira ya uwekezaji ya kuja kurudisha fadhila waliyokupa
 
Kifupi ni jamii yenye amana ndogo, no social trust.

Wananchi hawawaamini viongozi, viongozi hawawaamini wananchi. Wananchi hawaaminiani wao kwa wao, viongozi hawaaminiani wao kwa wao.

Kwanza kumsaidia mtu si lazima akurudishie. Yani mtu hajisikii vizuri kuona tu pale kasaidia mpaka arudishiwe na yeye? Umasikini gani huu wa mawazo?

Pia hii ni jamii yenye unafiki mwingi sana. Ni jamii inayoweza kuwa na methali kama "Tenda wema uende zako, usingoje shukurani" bila kuitekeleza.

Halafu ni jamii yenye poverty mindset, poverty anxiety. Yani inawezekana kabisa tukawa na mtu mwenye potential nzuri kabisa ya kutusaidia huko baadaye, hata kama tunasaidia kibinafsi, kijana anaweza kwenda nje akatengeneza michongo ya kusaidia nchi, kutusanua mambo mengi, lakini tukamzibia kijinga kwa sababu hatuoni mbali zaidi ya pua zetu tu.

Tunang'ang'ania sana sherehe za kumaliza mamilioni kwa siku moja kama harusi, halafu sehemu za kuongeza human potential zenye real Return on Investment watu wakasome kuijua dunia na kufungua milango wengine wengi zaidi waende, hatuchangiani kila mtu anapambana kivyake.

Halafu tunashangaa kwa nini umasikini unazidi.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.

Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.

View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
​
Ana hoja ,asikilizwe.

Mchango wa kuoa? Je kuendesha familia utahitaji tena michango? Maana mimi naona harusi ni very simple sana kuirun maana unaweza ukajipanga kukudunduliza hata miaka mitatu ila kuendesha familia ndiyo NTITI hapo hamna hamna si chini ya miaka 18.
 
Kwa hiyo wewe unashauri nini kifanyike mkuu?
 
Kuna mtu anaweza kumpinga huyo mchungaji kwa hiyo statement aliyoitoa

Lakini nyuma ya keyboard, ana kadi 3 za harusi na zote anatakiwa achangie 250,000 Kila moja 🙌

Ni ukweli uliowazi, michango ya harusi imekuwa kero nyakati hizi
 
Kifupi ni jamii yenye amana ndogo, no social trust.

Wananchi hawawaamini viongozi, viongozi hawawaamini wananchi. Wananchi hawaaminiani wao kwa wao, viongozi hawaaminiani wao kwa wao.

Kwanza kumsaidia mtu si lazima akurudishie. Yani mtu hajisikii vizuri kuona tu pale kasaidia mpaka arudishiwe na yeye? Umasikini gani huu wa mawazo?

Pia hii ni jamii yenye unafiki mwingi sana. Ni jamii inayoweza kuwa na methali kama "Tenda wema uende zako, usingoje shukurani" bila kuitekeleza.

Halafu ni jamii yenye poverty mindset, poverty anxiety. Yani inawezekana kabisa tukawa na mtu mwenye potential nzuri kabisa ya kutusaidia huko baadaye, hata kama tunasaidia kibinafsi, kijana anaweza kwenda nje akatengeneza michongo ya kusaidia nchi, kutusanua mambo mengi, lakini tukamzibia kijinga kwa sababu hatuoni mbali zaidi ya pua zetu tu.

Tunang'ang'ania sana sherehe za kumaliza mamilioni kwa siku moja kama harusi, halafu sehemu za kuonheza human potential zenye real Return on Investment watu wakasome kuijua dunia na kugungua milango wengine wengi zaidi waende, hatuchangiani kila mtu anapambana kivyake.

Halafu tunashangaa kwa nini umasikini unazidi.
Umemaliza kila kitu mkuu ndiyo jamii tuliyo nayo
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.

Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.

View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
​
Hapo kwenye maoni yako mkuu umenikosha! Ameshiba sadaka huyu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom