Mchungaji Shayo: Michango ya harusi ni ushamba; usitoe mchango wowote

Mchungaji Shayo: Michango ya harusi ni ushamba; usitoe mchango wowote

Siwezi kuchangia harusi hata awe anaoa mdogo wangu wa kuzaliwa.

Hadi anataka kuoa maana yake ameshajipanga na yupo tayari kubeba majukumu kama kiongozi wa familia.

Tutasaidiana kwenye shida za kawaida za maisha lakini sio harusi.

Mwanaume mzima huoni aibu kuchangisha michango ya harusi maana yake unatudhihirishia kwamba huna uwezo wa kujisimamia mambo yako hata huko kwenye ndoa.
 
Huoni utaenda kinyume na utamaduni wa kiafrika wa kushirikiana kijamii? Na sio kwamba kila anayekuomba mchango hana fedha za kuendesha sherehe yake bali anataka ushirikishwaji wa ndugu na jamaa. Na baadhi ya ndugu na jamaa ukiandaa harusi peke yako bila kuwachangisha, hawawezi kuhudhuria. Watadhani umewatega.
 
Kijana oa, tualike tuje kugonga menyu, si unataka sifa? Ila usiombe tukuchangie, mpaka umeamua kuoa ina maana we unajitosheleza, huo ndio uanaume wenyewe. La sivyo aoa kimyakimya hatutashangaa
 
Kijana oa, tualike tuje kugonga menyu, si unataka sifa? Ila usiombe tukuchangie, mpaka umeamua kuoa ina maana we unajitosheleza, huo ndio uanaume wenyewe. La sivyo aoa kimyakimya hatutashangaa
Sasa akioa kimyakimya mkanda wa video utatokaje mkuu? Nani atatazama huo mkanda? Matukio ya harusi ni kama movie.

Kwa waswahili harusi ni FILAMU. Ndio maana hadi watu wanalipia king'amuzi cha TV kuangalia kipindi cha sherehe (CHEREKO). Kwa mnaotazama TBC, hivi hiki kipindi cha chereko bado kipo?😅🤣😂
 
Huoni utaenda kinyume na utamaduni wa kiafrika wa kushirikiana kijamii? Na sio kwamba kila anayekuomba mchango hana fedha za kuendesha sherehe yake bali anataka ushirikishwaji wa ndugu na jamaa. Na baadhi ya ndugu na jamaa ukiandaa harusi peke yako bila kuwachangisha, hawawezi kuhudhuria. Watadhani umewatega.
Ushirikishwaji sio lazima uwe kukamuana fedha. Unaweza kumshirikisha mtu kwa kumpa mwaliko aje ahudhurie sherehe yako inatosha.
 
Haya mambo ya michango wakati mwingine ni wazazi ndio huyashadidia wenyewe, wanataka wachangiwe waonekane kijana wao kapitia njia sahihi kuoa. Wanawatwisha mzigo marafiki zao wawachangie, wazazi wanakuwa kimbelembele kubeba harusi ya kijana wao. Kule kwa binti nako wazazi wake wanatwisha mizigo marafiki zao michango ya send off. Wazazi ndio vimbelembele sana kwenye harakati za harusi za watoto wao
 
Sasa akioa kimyakimya mkanda wa video utatokaje mkuu? Nani atatazama huo mkanda? Matukio ya harusi ni kama movie.
Nimeishia kusoma hapa. Yaani kuoa ni hadi kuwe na mkanda wa video?

Mungu hahitaji ushahidi wa video kubariki ndoa bali utaratibu wa kiimani ukitimizwa inatosha.
 
Kwani bila michango ya harusi watu hawataoana? Ndoa hazitafungwa? Cha msingi ni kulipia zile document za ndoa kwa msajili unaenda kwa padri/mchungaji, sheikh au bomani, kimila sijui aliyeidhinishwa kufungisha ndoa ni nani, au unasogeza tu njoo tuishi, na maisha yanaendelea, shida iko wapi? Mambo ni simple tu
 
Hakika yaani kwanza unachangiaje wazinifu maana wengi wao walishagatombana...so nikabariki uzinzi wao kwa hela yangu....nope
20260520_161225.jpg
 
Hakuna ubaya kuchangia harusi ili mradi iendane na hali ya maharusi. Sio maharusi ni makapuku halafu wanataka mambo makubwa.

Harusi = sherehe ya kuhalalisha watu wawili wa jinsia tofauti kudinyana.
 
Hakuna ubaya kuchangia harusi ili mradi iendane na hali ya maharusi. Sio maharusi ni makapuku halafu wanataka mambo makubwa.

Harusi = sherehe ya kuhalalisha watu wawili wa jinsia tofauti kudinyana.
Kwani sherehe ni lazima mkuu? Kwanini watu wasifunge ndoa kisha warudi nyumbani kuendelea na maisha yao?
 
Kwa hiyo anataka kuwapangia watu maisha mkuu?
Mchungaji anatoa ushauri kwa jamii.
Kuachana na desturi hiyo mpya inayoshika kasi.
Kuomba omba michango ni kitu kilicho kwenye udhalili.
Jamii ijinasue na hilo.
Tubaki na michango ya dharula kama misiba na majanga kama moto, vimbunga, mafuriko nk
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom