Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,000
- 153,679
Kuna Mbongo Mnyamwezi wangu mmoja alitoka zake US, karudi Bongo, mchumba wake naye Mbongo katoka US, wamerudi kufunga ndoa na kuishi nyumbani Tanzania.Nawashauri vijana ,wakitaka kuona wajipange kudunduliza FUBA wao wenyewe na wala siwachangishe michango kuwalazimisha watu ,michango iwe ni optional lakini 99% ya gharama zitoke kwa bwanaharusi na bibi harusi.
Watoto wa Oysterbay long time hawana shida ndogo maisha haya.
Basi Mnyamwezi akawa anawapeleka Wabongo ile Kinyamwezi Nyamwezi mpaka kwenye harusi yake.
Watu wakawa wanataka kumchangia, akawaambia harusi yangu haipokei mchango. Tutafanya kila kitu wenyewe. Ila tuna charity cause huko Umasaini, kuna kijiji kinahitaji maji, kama unataka kuchangia, changia huko kwenye cause yetu kupeleka maji Umasaini kijijini.
Wabongo wengine waliguna sana, wakasema huyu jamaa kukaa Marekani anajiona sana, anaona hataki mchango wa mtu.
Nikasema Wabongo wengine hawana jema, ukiwachangisha lawama, usipowachangisha lawama 😂😂😂