Twilumba
Platinum Member
- Dec 5, 2010
- 13,468
- 16,168
Taarifa zilizotufiukia hivi punde katika chumba chetu cha habari, zinaeleza kuwa mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Emmanuel Mathias almaarufu MC Pilipili, amefariki dunia ghafla mchana leo, Novemba 16, 2025.
Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikwa na mauti.
Global TV imezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.
Source: Global TV Online