Polisi: Uchunguzi kifo cha MC Pilipili bado unaendelea

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,717
Reaction score
2,746
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeeleza kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa msanii maarufu wa vichekesho na mshereheshaji, Emanuel Mathias, maarufu MC Pilipili kilichotokea mkoani Dodoma.

Akizungumza mapema leo Desemba 22,2025 jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gallus Hyera amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na Jeshi la Polisi linakusanya taarifa muhimu ili kubaini chanzo na mazingira ya kifo hicho.

Hyera ameeleza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, watatangaza hadharani matokeo ya uchunguzi huo ili umma upate taarifa sahihi kuhusu tukio hilo.

Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuepuka kutoa taarifa zisizo sahihi na kuwataka kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi huo.

Chanzo Mwanachi
 
View attachment 3519108
Chanzo Mwanachi
Yaleyale ya tume za uchunguzi wa matukio yakitokea. Yani hapa ni kama wanasema tulieni nyinyi, huu ndo mwisho wa hiyo storii...mtasahau tu
 
Hakuna jeshi hapo, ni genge la wezi tuu na materorist wanaojiita polisi, hao na TISS ndio watekaji na wauaji wa watanzania
 
Back
Top Bottom