Tetesi: Mbunge Shangazi ana ubia na Kampuni ya DP World

Na wewe ndivyo ufanyavyo?

Sio Shujaa wewe, sijakubaliana na mawazo yako kabisa 😂

Siyo lazima unifuate mimi...

Mbowe amesema ataitisha maandamano ya nchi nzima.

Nategemea kukuona mstari wa mbele kabisa yakiiva...

Nchi hii inahitaji mashujaa kama wewe. Wenye makovu ya risasi kama akina Tundu Lissu

Kila la heri ng'wanangwa!
 
MBUNGE, Rashid Shangazi anatajwa kuwa ndiye Dalali wa Kampuni ya DP World inayotaka kuuziwa bandari zote Tanzania isipokuwa za Zanzibar tu, Shangazi alianza kuipigia debe na baadaye kuwaleta nchini na kukamilisha hiyo dili ambalo limezua mgogoro mkubwa Tanzania.

Ushahidi wa ni SWALI NA 58 LA TAREHE 4 NOVEMBA, 2022 ambapo kwa mujibu wa Tovuti ya Bunge, Mbunge huyo aliuliza

"58. MHESHIMIWA RASHID ABDALLAH SHANGAZI (MLALO) :Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi: Je, ni lini utekelezaji wa Mkataba wa Kibiashara kati ya Serikali na Kampuni ya Dubai World utaanza"
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi( ATUPELE MWAKIBETE ALIJIBU NAKUU)

United Republic of Tanzania

Primary Questions
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, ni lini utekelezaji wa Mkataba wa kibiashara kati ya Serikali na Kampuni ya Dubai World utaanza?

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2022 Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilisaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Dubai Port World (DP-World) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, kuhusu uwekezaji katika maeneo ya bandari nchini. Aidha, tarehe 25 Oktoba, 2022 Serikali ilisaini makubaliano na Serikali ya Dubai (Inter-Governmental Agreement - IGA).

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba wa kibiashara unakwenda katika hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ni mkataba kati ya nchi na nchi (Intergovernmental Agreement - IGA) ambao tayari umesainiwa. Mkataba huo unaweka msingi wa Serikali za pande mbili kuanza majadiliano kuhusu maeneo ya uwekezaji.

Baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, majadiliano yataendelea kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuhakikisha kwamba uwekezaji huo unakuwa na tija kwa nchi. Matarajio ya Serikali ni kuwa majadiliano hayo yatafikia tamati mwishoni mwa mwezi Desemba, 2022.

Mwisho wa Kunukuu.

Hivyo basi Watanzania tusimtafute mchawi wa suala hili kwani aliyeileta kampuni hii na kuipenyeza serikalini ni Mhe. Shangazi ambaye ni Katibu wa Wabunge wa CCM ambaye ametumia ushawishi wake alionao ndani ya Chama na Serikali kuileta kampuni hii na kumchafua Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Shangazi ni Mbunge wa Mkoa wa Tanga amepigia debe ili bandari zote ziuzwe kwa kampuni hiyo ambayo inasemekana yeye wadau wake wamepewa donge nono kuhakikisha kampuni hiyo inanunua bandari zote na kuendesha kwa miaka isiyojulikana.

View attachment 2649962
Rashid Shangazi- Mbunge wa Mlalo
Katika hili hakuna jinsi ya kutomuhusisha rais katika ufisadi huu wa karne
 
Mambo ya kumezeshwa pini ujisaidie mlingoti wa umeme wa msongo wa high tension ndio haya.

Hii suala la kukodisha/kuuza bandari zote za Tanganyika ni muhimu Watanganyika wenyewe wajiongeze na waende mbali zaidi. Watanue wigo wao wa kuyatafakari mambo.

Na ikumbukwe wakati wa maoni ya mchakato wa Katiba mpya ya Mh Jaji Warioba Mbunge na PM mzitafu kulitokea mabishano ya ama serikali 3, 2 au 1. Watanganyika wenye msimamo wa 3 wakatishiwa eti mipaka ya nchi ya Zanzibar wakati wa sultani ilikuwa inaingia mwambao wa pwani ya Tanganyika hadi maili 50 za nchi kavu kuanzia kaskazini hadi kusini. Na eti sultani alilinunua hilo eneo kwa Wajerumani, kumbuka si kutoka kwa Watanganyika.

Maadamu anayekodishwa Bandari zote za Tanganyika ni mwarabu na yako madai ya aina hiyo. Inawezekana huu ni mwanzo tu wa mkakati wa masafa marefu wa kujaribu kuanza kurudisha hiyo mipaka ya Zanzibar ya Sutanese. Kwa nini Mwarabu, Kwa nini bandari zote za Tanganyika, kwa nini bandari za Zanzibar haziguswi acha tu kufikiriwa na huu mkataba??? Na waliombele kwenye huu mkataba wanaongozwa na Waziri Mzanzibari. Huyu Mbunge Mh Shangazi naye niwa Tanga pengine asili yake ni sehemu ya huo mwambao tajwa.
 
Kuna ubaya gani kuileta kampuni ya DPworld Tanganyika?

Mkataba ufanyiwe marekebisho.

Hii ni Dubai 1960 bandari yao ilikuwa ya Mitumbwi na Majahazi wakati huo sisi tulikuwa tumeachiwa Bandari kubwa na Mkoloni
View attachment 2650033
Warekebishe nini wakati hata uliosainiwa sasa ni siri, tatizo sio private company kama DP World kuendesha port yetu na tunajua ni biashara na ni jambo la kawaida sana duniani na nchi nyingi zinafanya hivyo, tatizo tuna experience mbaya sana na wapigaji waliotuingiza mikataba ambayo hatujawahi kupata faida na kuishia kulipa mabilioni kila mwaka, sio kwa serikali hii ya CCM acha tuu tuendeshe bandari mpaka watu makini waje wa kutuingiza kwenye mikataba inayoeleweka
 
Watanzania tumfuate huyu Mbunge anaitwa Rashid Shangazi kutoka Tanga ndio anao mchongo mzima wa namna Kampuni ya DP World ilivyopatikana hadi kuzusha mgogoro mkubwa kitaifa wa kuuza bandari za Tanganyika
View attachment 2649975

Aende akauze za kwao Zanzibar maana inaonyesha huyu sio Mtanganyika. Kama anataka basi ziuzwe bandari zote za Jamhuri ya Muungano Tanzania (THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA). Au anaogopa serikali ya Zanzibar?
 
Muulize mwakibete alisema utekelezaji unaanza mwishoni mwa 2022
wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi katika
Bandari Tanzania (The Intergovernmental Agreement Between the United Republic
of Tanzania and the Emirate of Dubai Concerning Economic and Social
Partnership for the Development and Improving Performance of Sea and Lake
Ports in Tanzania).
 
Aliyepo juu ni wa imani yake
Na aliyetajwa hapa pia ni wa imani yake.

Huyu bibi hanaga akili linapokuja suala linalomgusa mwenzake kiimani na anasikia raha zaidi anaposikia waliokabidhiwa hii rasilimali muhimu kwa taifa ni mwarabu aliyemrithisha dini hapo anazidi kuamini kuwa dini yake imezidi kuwa ya haki.
 
Mambo ya kumezeshwa pini ujisaidie mlingoti wa umeme wa msongo wa high tension ndio haya.

Hii suala la kukodisha/kuuza bandari zote za Tanganyika ni muhimu Watanganyika wenyewe wajiongeze na waende mbali zaidi. Watanue wigo wao wa kuyatafakari mambo.

Na ikumbukwe wakati wa maoni ya mchakato wa Katiba mpya ya Mh Jaji Warioba Mbunge na PM mzitafu kulitokea mabishano ya ama serikali 3, 2 au 1. Watanganyika wenye msimamo wa 3 wakatishiwa eti mipaka ya nchi ya Zanzibar wakati wa sultani ilikuwa inaingia mwambao wa pwani ya Tanganyika hadi maili 50 za nchi kavu kuanzia kaskazini hadi kusini. Na eti sultani alilinunua hilo eneo kwa Wajerumani, kumbuka si kutoka kwa Watanganyika.

Maadamu anayekodishwa Bandari zote za Tanganyika ni mwarabu na yako madai ya aina hiyo. Inawezekana huu ni mwanzo tu wa mkakati wa maasfa marefu wa kujaribu kuanza kurudisha hiyo mipaka ya Zanzibar. Kwa nini Mwarabu, Kwa nini bandari zote za Tanganyika, kwa nini bandari za Zanzibar haziguswi acha tu kufikiriwa na huu mkataba??? Na waliombele kwenye huu mkataba wanaongozwa na Waziri Mzanzibari. Huyu Mbunge Mh Shangszi naye niwa Tanga pengine asili yake ni sehemu ya huo mwambao tajwa.
Wanapewa halafu mkataba haturuhusiwi kuvunja.
 
Warekebishe nini wakati hata uliosainiwa sasa ni siri, tatizo sio private company kama DP World kuendesha port yetu na tunajua ni biashara na ni jambo la kawaida sana duniani na nchi nyingi zinafanya hivyo, tatizo tuna experience mbaya sana na wapigaji waliotuingiza mikataba ambayo hatujawahi kupata faida na kuishia kulipa mabilioni kila mwaka, sio kwa serikali hii ya CCM acha tuu tuendeshe bandari mpaka watu makini waje wa kutuingiza kwenye mikataba inayoeleweka
Mimi huwa najali ajira tu na nimesha Apply kazi.

Look, nimeshuhudia Magufuli akifunga migodi huko kanda ya Ziwa tulioathirika ni sisi Wafanyakazi so I don't care serikali inapata nini ninachojali ni kupata ajira.
 
Siyo lazima unifuate mimi...

Mbowe amesema ataitisha maandamano ya nchi nzima.

Nategemea kukuona mstari wa mbele kabisa yakiiva...

Nchi hii inahitaji mashujaa kama wewe. Wenye makovu ya risasi kama akina Tundu Lissu

Kila la heri ng'wanangwa!
Mie siandamani bali nitapiga goti kumuomba Jehova ashughurike na hao wezi, imani yangu inao uwezo wa kuhamisha milima.
 
Aende akauze za kwao Zanzibar maana inaonyesha huyu sio Mtanganyika. Kama anataka basi ziuzwe bandari zote za Jamhuri ya Muungano Tanzania (THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA). Au anaogopa serikali ya Zanzibar?
Unataka arogwe atupe hijabu.
 
Back
Top Bottom