Zitto ashauri iundwe kampuni ya ubia kati ya DP World na Tanzania kuendesha bandari

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,090
49,791
Ni mara elfu Zito Kabwe na ACT Huwa wanakuja na alternative solution na wako optimistic kuliko Machadema Huwa ni Majinga na Yasiyo na Suluhisho..

Chadema ni chama Cha hovyo sana eti nao wanataka Wapewe madaraka wakati hawajawahi kuwa na suluhisho.

Kazi wanayoweza Chadema ni kutukana,kulaumu,kupinga Kila kitu,ulalamishi,kujisifu huko Twitter,kuonesha picha za nyomi na ujinga mwingine..

Chadema ni Moja ya chama Cha hovyo na kimejaa wasalatonge ,njaa tupu.😁😁

Chadema mna Mengi ya kujifunza Kwa Zito na ACT Wazalebdo..

----
Chama cha ACT- Wazalendo kimetoa mapendekezo kwa serikali kuhusu suala la mkataba wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai juu ya usimamizi wa shughuli za bandari ambapo kimetaka wawekezaji hao kuanzisha kampuni ya uendeshaji wa bandari nchini ambayo itakuwa na umiliki wa asilimia 50 kwa 50 kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya DP World.

Akizungumza Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kampuni hiyo inaweza kuitwa Tanzania-Dubai Ports Limited (TDPL) ambayo uwepo wake utasaidia kuondoa hofu kwa wananchi pamoja na Tanzania kuwa na udhibiti wa kila kitu katika uwekezaji huo.

Pendekezo la pili, imetaka mkataba wa uendeshaji wa bandari uingiwe kati ya TPA na Kampuni hiyo ya Ubia (TDPL) ambayo itatoa asilimia 50 kwa 50 ili kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa.

“Tunataka asilimia 50 katika kampuni ya uendeshaji, tunataka makubaliano yote ambayo nchi yetu itaingia na wawekezaji yapitie hiyo kampuni ambayo TPA ina asilimia 50 na mwekezaji ana asilimia 50. Mwekezaji analeta hela na teknolojia, sisi tunatoa bandari yetu na ardhi yetu, 50 kwa 50 wawekeze tuongeze ufanisi ambao unatakiwa katika nchi yetu,” amesema.

Chama hicho pia kimependekeza kampuni ya DP World isifanye uwekezaji wowote kwenye bandari shindani na bandari za Tanzania hususani bandari za nchi jirani bila kujadiliana na Serikali ya Tanzania (exclusivity).

Credit: SwahiliTimes
 
Yawezekana una hoja lkn umeonyesha zaid chuki kuliko facts!! Kama ni ushauri hao CDM washatoa san mapendekezo na nn cha kufanya.

But waliishia kuzomewa na kutolewa nje ya bunge!! Mi naomba niulize jambo.. kulingana na siasa za Nchi hii CHADEMA wanasemwa san kwann wasifanye hivi au vile, but wakija na solution aidha wananyooshewa kidole hawaitakii mema au aman nchi yetu.

Mwanzo CHADEMA walikua hawataki affiliation na CCM kwa namna ya kujadiliana kuhusu mustakabali wa changamoto za kisiasa zilizopo lkn haohao CHADEMA walilaumiwa san kua ni kama hawataki aman wanataka vurugu na maandamano.

Imagine wameangalia njia ya maridhiano kisiasa kama baadhi ya watu walivyoshaur mwanzo lkn now wanaitwa walamba asali, wengine humu wanasema CHADEMA hawakupaswa kufanya maridhiano!! Sasa hivi hawa CHADEMA ni kipi walitakiwa wafanye?

NB; mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" lkn mnyonge huyu ananyongwa na haki hapewi!
 
Tuunde kampuni ya ubia kwani bandari ya nani?

Hao DP World wana kipi cha maana kutulazimisha sisi kuunda kampuni ya ubia nao, na isiwe mwingine?

Ule mkataba ni batili, hawa mawakala wa shetani wanaogopa kusema kweli wasimuudhi bosi wao msaliti.
 
Yawezekana una hoja lkn umeonyesha zaid chuki kuliko facts!! Kama ni ushauri hao CDM washatoa san mapendekezo na nn cha kufanya. But waliishia kuzomewa na kutolewa nje ya bunge!! Mi naomba niulize jambo.. kulingana na siasa za Nchi hii CDM wanasemwa san kwann wasifanye hivi au vile, but wakija na solution aidha wananyooshewa kidole hawaitakii mema au aman nchi yetu. Mwanzo CDM walikua hawataki affiliation na CCM kwa namna ya kujadiliana kuhusu mustakabali wa changamoto za kisiasa zilizopo lkn haohao CDM walilaumiwa san kua ni kama hawataki aman wanataka vurugu na maandamano. Imagine wameangalia njia ya maridhiano kisiasa kama baadhi ya watu walivyoshaur mwanzo lkn now wanaitwa walamba asali, wengine humu wanasema CDM hawakupaswa kufanya maridhiano!! Sasa hivi hawa CDM ni kipi walitakiwa wafanye? NB; mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" lkn mnyonge huyu ananyongwa na haki hapewi!!!
Cdm imewahi toa mapendekezo yapi unayoyajua wewe?

Au Kuna Chadema nyingine tofauti na hii ya walalamishi wasio na suluhisho? Nitajie mapendekezo Yao ya kuhoresha Ufanisi wa Bandari
 
Tuunde kampuni ya ubia kwani bandari ya nani?

Hao DP World wana kipi cha maana kutulazimisha sisi kuunda kampuni ya ubia nao, na isiwe mwingine?

Ule mkataba ni batili, hawa mawakala wa shetani wanaogopa kusema kweli wasimuudhi bosi wao msaliti.
Bandari ibayo underperform Ina faida gani?
 
Cdm imewahi toa mapendekezo yapi unayoyajua wewe?

Au Kuna Chadema nyingine tofauti na hii ya walalamishi wasio na suluhisho? Nitajie mapendekezo Yao ya kuhoresha Ufanisi wa Bandari
Wee kumbe bado hujui kitu yawezekana hata kipind wapinzani wapo bungeni wakipinga miswada mbalimbali na kutoa suluhisho ww ulikua bado kijijin huko unalima ngogwe!!
 
Tuunde kampuni ya ubia kwani bandari ya nani?

Hao DP World wana kipi cha maana kutulazimisha sisi kuunda kampuni ya ubia nao, na isiwe mwingine?

Ule mkataba ni batili, hawa mawakala wa shetani wanaogopa kusema kweli wasimuudhi bosi wao msaliti.
Tena bora wasiwepo kabisa
 
Waambie hatuhitaji bandari zetu kuwekwa mikononi mwa hao maharamia kama serikali iwekeze hapo bandarini kwa kiwango hichohicho hao wawekazaji wanachotaka kuwekeza hata ikiwa ni kwa gharama ya kuwekewa tozo kwa kila sahani ya chipsi au kilo ya unga ili mradi tu bandari ibaki yetu
 
Wee kumbe bado hujui kitu yawezekana hata kipind wapinzani wapo bungeni wakipinga miswada mbalimbali na kutoa suluhisho ww ulikua bado kijijin huko unalima ngogwe!!
Acha utoto wewe,nimesema leta mapendekezo ya Chadema au leta hapa sera zenu mbadala za kuleta Ufanisi..

Mumefikia mahala mnadanganywa watu eti Katiba Mpya ndio muarobaini wa Umaskini wakati mnajua kabisa huu ni utapeli.
 
Upuuzwe huna akili
Huna hoja na hoja yangu itasimama pale pale kwamba Chadomo ni chama Cha matapeli na walalamishi..

Toka nimeanza kuwafuatilia the only section mko vizuri ni kwenye wanasheria , kwenye uchumi na Biashara ni weupe na makopo tuu,na Zito ndio alikuwaga ananwabeba those days.
 
Zitto anazungumzia YAFUATAYO, sisi tunazungumzia YALIYOPO.

Zitto anazungumza mazungumzo baada ya habari, Sisi tunazungumza Taarifa ya habari yenyewe.

Kiufupi sisi tunazungumzia mkataba mama, Zitto anazungumza vimikataba vidogo vijavyo.

MKATABA MAMA una shida, tena shida kubwa sana, inabidi urekebishwe kabla ya kwenda hatua nyingine ya kuingia hivyo vimikataba vidogovidogo.

1. Mkataba hauna kikomo
2. Mkataba scope yake haieleweki
3. Mkataba unatengeneza monopoly kwa kampuni moja
4. Mkataba unaenda kushape sheria zetu za bandari zitii mkataba huu
5. Mkataba hauspecify share zetu zisipungue ngapi
6. Mkataba hautaji chochote kuhusu haki za binadamu
7. Mkataba unatupa sisi masharti tu lakini huoni ukimwambia mwekezaji kuwa hiki na kile ni no go zone
8. Mkataba unakataza sisi kujitoa hata kama jamaa watafadhili vikundi vya waasi, au hata kuhatarisha uwepo wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
9. Mkataba unataka eti sisi tukitaka kuvutia uwekezaji katika mambo haya ya bandari tukawaambie wao kwanza. Wao ni akina nani?

Sasa mkataba wa kijinga namna hii unataka tuukubali?

Hebu waende wakerekebisha vifungu halafu waulete tena kabla ya kuingia hiyo mikataba ya HGA.
 
Ni mara elfu Zito Kabwe na ACT Huwa wanakuja na alternative solution na wako optimistic kuliko Machadema Huwa ni Majinga na Yasiyo na Suluhisho..

Chadema ni chama Cha hovyo sana eti nao wanataka Wapewe madaraka wakati hawajawahi kuwa na suluhisho.

Kazi wanayoweza Chadema ni kutukana,kulaumu,kupinga Kila kitu,ulalamishi,kujisifu huko Twitter,kuonesha picha za nyomi na ujinga mwingine..

Chadema ni Moja ya chama Cha hovyo na kimejaa wasalatonge ,njaa tupu.😁😁

Chadema mna Mengi ya kujifunza Kwa Zito na ACT Wazalebdo..

----
Chama cha ACT- Wazalendo kimetoa mapendekezo kwa serikali kuhusu suala la mkataba wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai juu ya usimamizi wa shughuli za bandari ambapo kimetaka wawekezaji hao kuanzisha kampuni ya uendeshaji wa bandari nchini ambayo itakuwa na umiliki wa asilimia 50 kwa 50 kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya DP World.

Akizungumza Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kampuni hiyo inaweza kuitwa Tanzania-Dubai Ports Limited (TDPL) ambayo uwepo wake utasaidia kuondoa hofu kwa wananchi pamoja na Tanzania kuwa na udhibiti wa kila kitu katika uwekezaji huo.

Pendekezo la pili, imetaka mkataba wa uendeshaji wa bandari uingiwe kati ya TPA na Kampuni hiyo ya Ubia (TDPL) ambayo itatoa asilimia 50 kwa 50 ili kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa.

“Tunataka asilimia 50 katika kampuni ya uendeshaji, tunataka makubaliano yote ambayo nchi yetu itaingia na wawekezaji yapitie hiyo kampuni ambayo TPA ina asilimia 50 na mwekezaji ana asilimia 50. Mwekezaji analeta hela na teknolojia, sisi tunatoa bandari yetu na ardhi yetu, 50 kwa 50 wawekeze tuongeze ufanisi ambao unatakiwa katika nchi yetu,” amesema.

Chama hicho pia kimependekeza kampuni ya DP World isifanye uwekezaji wowote kwenye bandari shindani na bandari za Tanzania hususani bandari za nchi jirani bila kujadiliana na Serikali ya Tanzania (exclusivity).

Credit: SwahiliTimes
Bandari zetu ziendelee chini ya TPA Zito kama anapenda sana DP akamuzie bandari zake hii za Taniania haziuzwi.
 
Huo ndio ushauri wa hovyo kweli yaani Tanzania iwape DPW 50% ya bandari.

Kitu serikali inachoenda fanya ni kama BTO (Build, Tranfer, Operate) contract. Wanatoa hela zao kufanya uwekezaji, mali inakuwa ya TPA.

DPW wanapewa muda wa ku-operate kuongeza ufanisi na kurudisha hela yao taratibu huku serikali ikuchukua percentage ya hayo mapato ya upande wao ikitaka. Hela ya uwekezaji ikirudi na mkataba unaisha, kwenda mbele baada ya hapo wakiongezewa muda hela yote inayokusanywa inakuwa ya serikali wao wanalipwa managing fees tu.

Sasa ukawepa 50% ya shares wavune, halafu kuwatoa ununue tena hizo shares; hiyo ndio akili gani.
 
Back
Top Bottom