Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Pauline Philipo Gekul, mbunge wa Babati Mjini (CCM) amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Holili, Rombo, Kilimanjaro. Hii ni nia OVU. Jambazi Pauline aliwateka Hashimu na Michael, kuwatesa na kuwawekea chupa makalioni.

====

20231126_222242.jpg

Pauline Gekul akiwa kituo cha polisi​

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kufuatia sakata la vijana wawili wanaodaiwa kufanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji na aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul anayedaiwa kuwatendea vitendo hivyo tarehe 11.11.2023.

ACP Katabazi ameongeza kuwa wanaendelea na uchunguzi wa suala hili na mahojiano yamefanyika na yuko nje kwa dhamana (Mbunge wa Manyara Mhe. Pauline Philipo Gekul) hivyo bado tunaendelea na uchunguzi wa suala hili"

Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini anatuhumiwa kumfanyia unyanyasaji vijana wawili ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine waliwadhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa ili wakiri kutumwa kufanya uhalifu.

Saa chache baada ya habari kusambaa kuwa Pauline Gekul amefanya uhalifu, Rais Samia alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, lakini barua ya Ikulu haikuelezea sababu ya utenguzi wake.

Baada ya Pauline Gekul kutenguliwa, wanaJF walisema asiishie hatua hiyo bali anatakiwa kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani.

Zaidi soma:

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul
 
With a rotten system, Mwisho wa movie lazima ataachiwa huru tu. Manakumbuka Kigwangala aliwahi kutuhumiwa kumpiga mtu risasi ya mguu? Nini kiliendelea? Bashite na Sabaya wapo uraiani na kulikuwa na evidence za uhalifu hadi footage za CCTV camera. Msitarajie jipya hapo, baada ya Wiki moja hili sakata litasahaulika
 
Pauline Philipo Gekul, mbunge wa Babati Mjini (CCM) amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Holili, Rombo, Kilimanjaro. Hii ni nia OVU. Jambazi Pauline aliwateka Hashimu na Michael, kuwatesa na kuwawekea chupa makalioni.
Dunia hii ni ya ajabu sana sisi tunapigania chakula kwa familia zetu kuna wengine wana kila kitu ila kiburi tu kinawaponza angejua wenzake tunavyotamani alivyokuwa navyo angetulia na kumshukuru mungu, kaibiwa vitu vya thamani ndogo tu nina uhakika angeweza kumuachia mungu akatoa sadaka au aache sheria ichukue mkondo wake matokeo yake unapoteza kila kitu kisa kiburi
 
Pauline Philipo Gekul, mbunge wa Babati Mjini (CCM) amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Holili, Rombo, Kilimanjaro. Hii ni nia OVU. Jambazi Pauline aliwateka Hashimu na Michael, kuwatesa na kuwawekea chupa makalioni.
Zamu yake ya kuwekewa chupa imefika , Malipo ni hapahapa

Usaliti ni laana
 
Back
Top Bottom