Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Mahakama ya Wilaya ya Babati imemtumia wito Mbunge Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo Disemba 27, 2023 kujibu kesi inayomkabili.

Mahakama hiyo imemtaka kufika pasipo kukosa.
IMG_9319.jpeg


Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.

Wito huo uliotolewa leo Jumatatu, Desemba 11, 2023 na Mahakama ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara baada ya wakili Peter Madeleka kumfungulia kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu.

Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tumeiona), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa.

Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul.

Akizungumzia wito huo, wakili wa mlalamikaji, Madeleka amesema umekuja baada ya kufungua kesi ya jinai ya shambulio la kudhuru mwili. "Kwa wito huo kesi itaanza kusikilizwa Desemba 27."

Alipotafutwa kuthibitisha iwapo amepokea wito huo, Gekul amesema hakuona wala kuupokea.

"Sijaona, sijapokea wala sifahamu chochote kuhusu hilo," amesema Gekul ambaye Novemba 25 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewasilisha jadala la tuhuma zake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ili apate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo.

Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa za kishirikina katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula.

Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye makalio.

Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya tuhuma za mbunge wake na akithibitika kuhusika achukuliwe hatua za kisheria.

Pia soma:

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis
 
Ngoja tusubiri haki itendeke
Hii issue ilivyoshughulikiwa, mimi sitegemei sana kuwa haki itatendeka. Nadhani kule kutumbuliwa uwaziri ''wenye nchi'' wanadhani inatosha. Nasema hivi kwa sababu makosa anayotuhumiwa ni makubwa na yako dhahiri kiasi ambacho angekuwa ''kamchape'' ungekuta alishafikishwa mahakamani siku nyingi na kunyimwa dhamana na kesi kuahirishwa mpaka ndama watakapoota meno ya juu.
 
Hii issue ilivyoshughulikiwa, mimi sitegemei sana kuwa haki itatendeka. Nadhani kule kutumbuliwa uwaziri ''wenye nchi'' wanadhani inatosha. Nasema hivi kwa sababu makosa anayotuhumiwa ni makubwa na yako dhahiri kiasi ambacho angekuwa ''kamchape'' ungekuta alishafikishwa mahakamani siku nyingi na kunyimwa dhamana na kesi kuahirishwa mpaka ndama watakapoota meno ya juu.
Mkuu hadi hakiza binadamu wamesimama nayo kazianayooo
 
Back
Top Bottom