Rufaa ya Pauline Gekul (Mbunge Babati Mjini) yapigwa kalenda

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara, imeahirisha rufaa ya jinai iliyokatwa na Hashim Ally dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya mjibu rufaa huyo kutopewa wito wa kuitwa mahakamani.

Leo Jumatatu Machi 18,2024 Mahakama hiyo ilipanga kusikiliza rufaa hiyo namba 577/2024, mbele ya Jaji Devotha Kamuzora, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya wadaawa (mrufani na mrufaniwa), shauri hilo limeahirishwa hadi Machi 21,2024.
Wakili wa mrufani, Peter Madeleka amesema mahakama haijapeleka hati za wito wala nyaraka za rufaa kwa mjibu rufani.

Katika rufaa hiyo, Ally anapinga maamuzi yaliyofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Desemba 27,2023 ya kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Leo Pauline hukuweza kufika mahakamani ambapo Wakili Ephraim Kisanga anayemwakilisha, ameeleza kuwa siyo mteja wao wala wao(mawakili) hawakuwa wamepokea nyaraka zozote za rufaa na badala yake wamesikia taarifa za rufaa hiyo kupitia vyombo vya habari.

Gekul alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Ally Novemba 11,2023 kinyume cha kifungu cha 41 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya 2022.

Pia Soma:

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi
Ya Gekul hayajaisha, Wakili Madeleka kukata rufaa

DPP: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi ya Jinai dhidi ya Pauline Gekul
 
Back
Top Bottom