Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,027
144,382
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Martin Maranja Masese kupitia mtandao wa X, habari ikimuhusu Pauline Gekul.

Kaandika hivi:

"Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul kadhaminiwa polisi Babati, karudi nyumbani kwake kupumzika baada ya kuhojiwa, lakini anasema anahofia usalama wake.. kwani Gekul anatakaje? Tumpelekee chupa za Coca-Cola zimlinde?"

1701063435045.jpeg
Kabla ya hapo aliandika...
"PAULINE GEKUL hadi muda huu saa 20:50 usiku EAT, anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Manyara, pichani akiwa ofisi za RCO - Manyara.

"Kamanda wa polisi Manyara, GEORGE KATABANZI amegoma kutoa maelezo ya ziada ya kwanini anashikiliwa, amesisitiza ni taratibu za upelelezi. Taarifa nyingine ni kwamba katibu wa Pauline Gekul anayeitwa HUSSEIN S. ABRIMA na vijana wawili walioshiriki utesaji ule, wanashikiliwa polisi.

"Taarifa tulizonazo ni kwamba jalada lililofunguliwa polisi ni malalamiko ya Pauline Gekul kutaka kuuwawa na siyo malalamiko ya Hashimu Philemon.Afande George Katabanzi, tunataka kuona haki ya Hashimu inapatikana polisi. Watanzania tupo tayari kuchanga fedha akapimwe hospitali za kisasa.

"Tunakwenda kumpima kupata ushahidi wa kitabibu wa kumuingizia chupa makalioni Hashimu. Mnachelewesha ili ku-buy time eeh? Tumeshtuka.Tutafungua kesi mbili kama hamtaki kumshtaki Pauline GEKUL.

"Tutafungua kesi ya jinai, madai na kikatiba na tutaomba tafsiri ya mahakama kuu.Tunao mawakili wa kutosha. Jopo linaongozwa Manyara na Wakili Thadei, Wakili Madeleka na mawakili wengine. Hatutaki kona-kona katika hili."

Pia soma >>>


Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya
 
Mara nyingi huwa tunasikia fulani kahojiwa na kabakishwa polisi ili kulinda usalama wake tena hata huwa hawaogopi wenyewe, sasa yeye ambae anahofia kabisa usalama wake kwann wamemrudisha nyumbani baada ya kumuhoji
Hii nchi ina mstari mkubwa sana kwenye kutoa haki kati ya raia na watawala, na sehemu kubwa katika mahakama zetu na polisi inategemea nguvu ya watu walio nyuma yako.
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Martin Maranja Masese kupitia mtandao wa X, habari ikimuhusu Pauline Gekul.

Kaandika hivi:

"Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul kadhaminiwa polisi Babati, karudi nyumbani kwake kupumzika baada ya kuhojiwa, lakini anasema anahofia usalama wake.. kwani Gekul anatakaje? Tumpelekee chupa za Coca-Cola zimlinde?"
Dhamana ni haki ya mtuhumiwa!.
P
 
Gekul akubali tu, hiyo ndio imeenda.

Unaibu waziri amepoteza. Ubunge ndio unakwenda kufikia tamati 2025, na harudi tena bungeni. Biashara zake ndio mwanzo wa kufilisika. Hadhi na heshima yake kijamii ndio imekwenda milele.
"usinene ukamala", subiri uchaguzi wa 2025.

usije ukaja kupigwa na kitu kizito pale sisiemu itakapokufanyia surprise, utashangaa anarudi bungeni na kuzawadiwa uwaziri.
 
Back
Top Bottom