Mbunge Martha Festo Aibana Wizara ya Maji Kupeleka Maji katika Mji wa Mpanda na Mkoa wa Katavi, Kigoma na Rukwa Kutoka Ziwa Tanganyika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE MARTHA FESTO AIBANA WIZARA YA MAJI KUPELEKA MAJI MPANDA NA KATAVI KUTOKA ZIWA TANGANYIKA

"Sisi Wananchi wa Mji wa Mpanda, Mkoa wa Katavi tuna changamoto kubwa sana ya Maji ukizingatia Mji wa Mpanda ni Mji unaokua kwa kasi na kuwa na ongezeko kubwa sana la watu. Mji wa Mpanda Serikali imefanya uwekezaji wa Bandari lakini changamoto ya Maji bado ni kubwa sana" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Muarobaini wa kutatua changamoto ya Maji Mpanda na Katavi ni kutoa Maji kutoka Ziwa Tanganyika. Mradi huu muhimu utakwenda kuikomboa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa. Waziri miaka tuna takribani miaka 3 umekuwa ukituchenga kwenye huu mradi, uje utueleze ni lini mradi huu utatekelezwa ili wananchi waondokane na kadhia kubwa wanayoipata ya kupata Maji yasiyo Safi na Salama" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Serikali imekuwa ikileta pesa nyingi sana katika Mkoa wa Katavi lakini pesa hizo zimekuwa hazileti matunda kwa sababu miradi mnayoenda kuelekeza siyo miradi endelevu" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mwaka 2021 tulikuambia Waziri wa Maji, mradi wa milala usitekelezwe ili pesa ielekezwe kwenye mradi wa kutoa Maji Ziwa Tanganyika ambapo ni takriban kilomita 100 mpaka Mji wa Mpanda, lakini jambo hilo limekuwa kimya" - Mhe. Martha Festo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Waziri wa Maji uje utueleze mradi huu utawezekana au hautawezekana. Ikiwa imewezekana kuleta Maji ya Ziwa Victoria na kuleta Mkoa wa Tabora, Shinyanga na Dodoma. Nini kinashindikana katika Mkoa wa Katavi, Kigoma na Rukwa"? - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mkoa wa Katavi kuna wakandarasi chechefu, wamekuwa wakikwamisha mama zetu. Wakandarasi wengi hawakamilishi miradi kwa wakati. Mfano, Mradi wa Maji Mishamo-Ifumbula anaitwa HAMWA Constructions ana mradi wa Milioni 886. Mkandarasi ametelekeza vibarua bila kuwalipa" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mkandarasi HAMATEK mwenye mradi wa zaidi ya Milioni 480 katika Kata ya Katuma Wilaya ya Tanganyika. Makamu wa Rais alisema Mkandarasi huyu achukuliwe hatua na mpaka sasa hivi hajachukuliwa hatua na wananchi hawajapata Maji. Waziri na Naibu Waziri mje mtueleze nini kinakwamisha kumchukulia hatua Mkandarasi huyu" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mkandarasi anayekamikisha mradi eneo la Milala Mji wa Mpanda, Mkandarasi yule zoezi limesimama na hamna kinachoendelea pale (Site). Mheshimiwa Waziri naomba ushughulike na wakandarasi hawa wanaokuwekea doa" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Wananchi wa Mkoa wa Katavi Jimbo la Kavuu katika Kata ya Majimoto. Mji wa Majimoto unakua sana kutokana na kilimo cha Mpunga na watu ni wengi wanaokwenda kununua mazao. Tunakuomba utupatie Kisima kimoja kiweze kukaa Kata ya Majimoto na Kata ya Chamaland" - Mhe. Martha Festo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-11 at 15.25.00.mp4
    28.4 MB
  • WhatsApp Image 2023-05-11 at 16.55.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-11 at 16.55.25.jpeg
    131.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom