Mbunge Martha Mariki Ataja Muarobaini wa Kumtua Mama Ndoo Kichwani Katika Ziara ya Chongolo Mkoa wa Katavi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MBUNGE MARTHA MARIKI ATAJA MUAROBAINI WA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI MKOA WA KATAVI KATIKA ZIARA YA CHONGOLO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki ameshiriki katika ziara ya Katibu Mkuu CCM, Ndugu Daniel Chongolo katika Mkoa wa Katavi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi na Wabunge akiwemo Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki

"Muarobaini wa kumtua Mama Ndoo kichwani katika Mkoa wa Katavi ni kuyatoa Maji ya Ziwa Tanganyika na kuyapeleka katika Mji wa Mpanda" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Kina Mama wa Mkoa wa Katavi tupo imara na tumejipanga kukisimamia Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha kwamba tunakwenda kushinda katika uchaguzi mkuu 2025 na 2024 kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi tunashika maeneo yote. Kina Mama wamejipanga kwenda kushika fomu na kushika nafasi hizo" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nilifanikiwa kufanya ziara katika Mkoa wa Katavi kwenye Kata zote 58, nilikutana na changamoto ndogo katika Kata ya Ilunde. Ilunde wanaishukuru Serikali kwa ujenzi wa kituo cha Afya cha Ilunde, vifaa tiba vimefika lakini hatuna Umeme kwaajili ya shughuli za upasuaji hususani wamama wanapojifungua" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

Katika ziara, Ndugu Daniel Chongolo amekagua miradi ya Maji, Umeme, Barabara, Kilimo na Ardhi na kutoa maelekezo kwa Mawaziri wanaohusika kufika na kutatua changamoto zilizojikita ili wananchi waweze kupata huduma kwani ni wajibu wa viongozi kuwatumikia Wananchi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-10-06 at 14.46.02.mp4
    17.9 MB
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 11.43.55(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 11.43.55(2).jpeg
    72.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-07 at 11.43.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-07 at 11.43.53.jpeg
    33.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom