Mbunge Martha Festo Mariki Ahitimisha Ziara na kugawa Milioni 29 Katika Kata Zote 58 za Mkoa wa Katavi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MBUNGE MARTHA FESTO MARIKI AHITIMISHA ZIARA NA KUGAWA MILIONI 29 KATIKA KATA ZOTE 58 MKOA WA KATAVI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki amehitimisha ziara yake ya kutembelea Kata 58 za Mkoa wa Katavi katika Kata ya Majimoto na Kasansa zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambayo ilianza tarehe 03 Julai, 2023 hadi tarehe 06 Agosti, 2023.

Mbunge, Mhe. Martha Festo Mariki amefanya ziara katika Mkoa wa Katavi kwa muda wa mwezi mmoja na wiki moja (tarehe 30 Julai, 2023 mpaka tarehe 06 Agosti, 2023) ambapo ameweza kuzunguka katika Kata 58 na kugawa Shilingi Milioni 29 ambayo ni sawa na Shilingi Laki Tano (500,000) kwa kila Kata.

Ziara ya Mbunge Martha Festo Mariki ilijikita kusaidia vikundi ujasiriamali vya Wanawake wa UWT Kata 58 za Mkoa wa Katavi kwa lengo la kuwasaidia na kuwawezesha Shilingi Milioni 29 sawa na Shilingi Laki Tano (500,000) kwa kila Kata.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki katika ziara yake aliweza kufanya mambo yafuatayo;

✅ Kugawa Mtaji wa Shilingi Milioni 29 kwa Kata 58 (Laki Tano Kwa Kila Kata) kwaajili ya Kusaaidia vikundi vya wanawake wajasiriamali UWT

✅ Kugawa Kadi 2,000 kwaajili ya kuongeza idadi ya wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Katavi

✅ Ugawaji wa GRR 120 (Vitabu vya risiti za ulipaji wa Ada za uanachama) kwaajili ya ulipaji wa Ada

✅ Kuchangia Ujenzi wa Zahanati, Kituo cha Afya cha Ilangu Wilaya ya Tanganyika Shilingi Milioni Moja (1,000,000)

✅ Kuchangia Ujenzi wa Zahanati ya Kajeje Wilaya ya Mpanda Jimbo la Nsimbo Kata ya Kanoge Shilingi Milioni Tano (5,000,000) jengo la Mama na Mtoto

✅ Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Shanwe iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi Shilingi Laki Tatu (300,000) katika Wilaya ya Mpanda

✅ Kuchangia Kikundi cha Bodaboda Shilingi Laki Mbili (200,000) kilichopo Kata ya Kibaoni Jimbo la Mlele

✅ Kuchangi Ujenzi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya; Mifuko 50 ya Saruji Wilaya ya Tanganyika na Mifuko 50 ya Saruji Wilaya ya Mlele; Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) kwaajili ya ukarabati Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda sawa na Shilingi Milioni 4,300,000 katika Ofisi za CCM Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi.

✅ Kutembelea Miradi mikubwa ya kimaendeleo ndani ya Mkoa wa Katavi iliyoletwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
  • Mradi wa Bandari, Wilaya ya Tanganyika
  • Mradi wa Maji Kata Mwamkulu Wilaya ya Mpanda
  • Mradi Mkubwa wa Bwawa la maji wa zaidi ya Shilingi Bilioni 4.2 katika Kata ya Senkwa Jimbo la Katavi utakaonufaisha Kata 5 na Vijiji.
  • Mradi wa Daraja la Msadiya uwekezaji wa Shilingi Bilioni 4.2 linalounganisha Kata ya Chamalendi na Mwamapuli.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki katika ziara yake alizungumzia mbalimbali ikiwemo; Kukemea vikali vitendo vya Ukatili wa kijinsia; Masuala ya Mmomonyoko wa Maadili; Uchumi kuhusiana na VICOBA vya akina Mama; Mkundi ya Vijana; Masuala ya Watu wenye ulemavu; Utoro Mashuleni na kukemea Wazazi ambao wamekuwa wakiwaozesha watoto wao katika umri mdogo.

Mwisho, Mhe. Martha Festo Mariki amewashukuru viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM, UWT, Wazazi, UVCCM), Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha ziara huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha za miradi mbalimbali ya Afya, Elimu, Maji na Miundombinu katika Mkoa wa Katavi na Mhe. Martha Mariki ameahidi kuendelea kutoka ushirikiano kwa viongozi na wananchi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.11.52(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.11.52(2).jpeg
    104.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.07.26(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.07.26(2).jpeg
    131.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.52(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.52(2).jpeg
    66 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.47.jpeg
    138.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.41(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.41(1).jpeg
    154.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.40(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.40(1).jpeg
    139.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.43(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.43(1).jpeg
    129.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.44(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.04.44(2).jpeg
    165 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.50.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.50.jpeg
    125.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.47(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-07 at 17.09.47(1).jpeg
    158.8 KB · Views: 1
Wajinga ndio waliwao, amehonga million 29 ambazo ni mshahara wake wa miezi miwili tu ili 2025 wampitishe tena vitu maalum.

Ccm kumejaa mazezeta kwelikweli, hapo pesa yake ya pensheni bunge likivunjwa haiguswi karibu million 400.
 
Katumia ngapi katika ugawaji huo ?

Kama kweli anatoa na kutaka kusaidia si angewatumia mpesa tu au asaidie kwenye mradi wowote au awalipie wote Tozo za miezi sita wanazochukua wenzake through miamala....

1691948540731.png
 
Wajinga ndio waliwao, amehonga million 29 ambazo ni mshahara wake wa miezi miwili tu ili 2025 wampitishe tena vitu maalum.

Ccm kumejaa mazezeta kwelikweli, hapo pesa yake ya pensheni bunge likivunjwa haiguswi karibu million 400.
Huyubangefaa kupigwa mawe fvcken kabisa
 
Kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi, kuwasemea matatizo yao kwa serikali na kamwe siyo kutumia pesa zake kutatua matatizo hayo.
Siyo lazima mbunge mzuri awe tajiri.
Fikra za kutumia fedha binafsi zinachochea rushwa kwenye uchaguzi na ufisadi kwa kuwa wabunge hawataweza kuishauri , kuisimamia na kuiwajibisha serikali inapoenda kinyume na matarajio ya wananchi.
 
Back
Top Bottom