Katavi: Mkandarasi akwamisha mradi wa maji wa Miji 28

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,068
12,503

Wakati Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji hapa nchini ili wananchi waweze kusogezewa huduma ya maji hasa kwa kumtua mama ndoo kichwani, imeeleza kuwa bado baadhi ya wakandarasi wanashindwa kutekeleza miradi hiyi kwa wakati ambapo mradi wa maji unaotekelezwa katika bwawa la Milala manispaa ya Mpanda mkoani Katavi unasuasua.

Mradi huo unaojulikana kwa jina la Miji 28 ni moja ya mradi ambao endapo utakamilika utaondoa kero ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Mpanda ambapo mhandisi kutoka mamlaka ya maji mjini MUWASA amesema gharama za mradi huo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 22 na utazalisha maji Lita Milioni 12 kwa siku na kunufaisha manispaa nzima.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusufu amesema amesikitishwa mkandarasi kuendelea kusuasua licha ya mara kadha kutembelea na kukagua mradi huo ambapo amekuwa akitoa maelekezo ya Serikali lakini bado utekelezaji wake hauridhishi huku Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko akimtaka mkandarasi kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa haraka na kwa kufuata maelekezo ya serikali ili mradi huo wa maji wa mini 28 uanze kuwafikia wananchi wa Manispaa ya Mpanda.

Mradi huo wa maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Manispaa ya Mpanda ulianza kutekelezwa Aprili 2023 na unatarajiwa kukamilika 2025 lakini hadi mwanzoni mwa Februari 2024 mkandarasi anasuasua.
 
Back
Top Bottom