Mbowe: Tunanyimwa haki ya kupata mlo wa mchana na maji kwa miezi mitano sasa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mhe. Mbowe amenyoosha MKONO na kumwaleza Mhe. Jaji kwamba Wana miezi mitano bila kula chakula cha Mchana kwa maana nyingine kauli Hii inaonyesha watuhumiwa hawa wamekuwa wakishinda na kulala bila kula Kwa siku zote wanazoletwa mahakani huku mahakama ikishindwa japo kupitisha mchana bila kula

" Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tkitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote.. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.."

--
Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji naomba kuleta Kwenye Mahakama yako kuwa tumekosa haki ya kula chakula mchana kwa Miezi 5, Wakati nyie Mna' break kwenda kula sisi hatupati chakula wala maji kwa miezi Yote 5

Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tukitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.

Jaji: sasa nyie Kibatala mnatoa uwakilishi gani hapa Mahakamani kama wateja wenu hawali miezi mitano?

Kibatala: Sisi tulifikisha kwa Officer wa Magereza, Suluhu aliyotoa ndiyo hiyo asubuhi watoke na chakula Kutoka Jela Kitu ambacho tulibishana na hatukufikia Muafaka kwa sababu haiwezekani. Nafikiri hata Msajili Wa Mahakama analijua hilo, sitaki kumsemea.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu Wa Jambo lililoletwa naomba Tubreak Kidogo tuweze Kuishauri Vyema Mahakama. Imekuwa ghafla sana.

Jaji: Basi nawaita Mawakili kuwakilisha Watu wote Ofisini Kwangu, Tuweze Kujadili
 
Katika kesi yake inayoendelea, Freeman Mbowe ameieleza mahakama kuhusu kunyimwa haki ya kupata mlo wa mchana wanapohudhuria mahakamani, kitendo ambacho kimefanyika kwa miezi mitano mpaka sasa.

Hapa chini ni sehemu ya alichokisema:

Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji naomba kuleta Kwenye Mahakama yako kuwa tumekosa haki ya kula chakula mchana kwa Miezi 5, Wakati nyie Mna' break kwenda kula sisi hatupati chakula wala maji kwa miezi Yote 5

Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tkitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote.. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.

Jaji: sasa nyie Kibatala mnatoa uwakilishi gani hapa Mahakamani kama wateja wenu hawali miezi mitano?

Kibatala: sisi tulifkisha kwa Officer wa Magereza, Suluhu aliyotoa ndiyo hiyo Asubuhi Watoke na Chakula Kutoka Jela Kitu ambacho tulibishana na hatukufikia Muafaka kwa sababu haiwezekani.. Nafikiri hata Msajili Wa Mahakama analijua hilo, sutaki kumsemea.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu Wa Jambo lililo letwa naomba Tubreak Kidogo tuweze Kuishauri Vyema Mahakama.. Imekuwa ghafla sana..

Jaji: basi nawaita Mawakili Kuwakilisha Watu wote Ofisini Kwangu, Tuweze Kujadili
 
Da chadema wana roho mbaya sana yaani mbwembwe zote zile kuwa Kila siku kunawasamalia wanaleta chakula mahakamani kume wanakul mashabuki tu atuhumiwa hawapewi? Mara walete keki yaani wana zambi sana wakiambiwa wmtoe wanakataa eti mwacheni tu mbwakabisa hawa
 
kwa akili yako unaweza ukampelekea mtu aliyejera chakula akiwa mahakamani ?
 
Da chadema wana roho mbaya sana yaani mbwembwe zote zile kuwa Kila siku kunawasamalia wanaleta chakula mahakamani kume wanakul mashabuki tu atuhumiwa hawapewi? Mara walete keki yaani wana zambi sana wakiambiwa wmtoe wanakataa eti mwacheni tu mbwakabisa hawa
Mkuu uliishia darasa la ngapi?

Mm nimeishia la pili B lakn nafahamu taratibu za magereza

Elimu elimu elimu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Da chadema wana roho mbaya sana yaani mbwembwe zote zile kuwa Kila siku kunawasamalia wanaleta chakula mahakamani kume wanakul mashabuki tu atuhumiwa hawapewi? Mara walete keki yaani wana zambi sana wakiambiwa wmtoe wanakataa eti mwacheni tu mbwakabisa hawa
Akili zako zimechukuliwa na pepo mchafu wa St. Valentine, je hujui ukiwa chini ya ulinzi wa magerrza unakula chakula cha jela tu?
 
Back
Top Bottom